Mkopo:Ujenzi wa Kulijengea Kaburi
Ujenzi wa Kulijengea Kaburi: humaanisha kusimamisha aina yoyote ile ya jengo juu ya kaburi, iwe ni kuba (kijimnara), dharih (kiunzi au jengo la heshima linalolizunguka kaburi), au hata msikiti. Kwa mujibu wa wengi wa maoni ya wanazuoni wa Kiislamu wa madhehebu mbalimbali n i kwamba; hakuna tatizo lolote lile kuhusiana na kulijengea makaburi, ni jambo linaloruhusiwa na lenye uhalali kamili wa kisheria. Hoja ya wanazuoni hawa imeegemea juu ya ushahidi wa kihistoria na kifiqhi, wakirejea mwenendo (sira) wa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), Maswahaba na Tabiʿina. Hata hivyo, kwa mtazamo wa wafuasi wa mkondo wa Kiwahabi (Wahhabism), ujenzi juu ya makaburi unachukuliwa kuwa ni bidʿa (uzushi katika dini) na hata kuhesabiwa miongoni mwa aina za shirki. Kwa msingi huo, wanazuoni wa mkondo huo wametoa fatwa zinazoruhusu au kuhimiza kubomolewa kwa majengo yaliyojengwa juu ya makaburi. Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, wafuasi wa mrengo wa Kiwahabi (Wahhabism) katika vipindi mbalimbali walionekana kubomoa baadhi ya majengo yaliyojengwa juu ya makaburi ya Maimamu wa Kishia na wanazuoni wa dini. Miongoni mwa mifano inayotajwa ni kubomolewa kwa majengo katika eneo la Jannat al-Baqi huko Madina, ambako kulikuwa na majengo juu ya makaburi ya Ahlul-Bait (a.s) pamoja na Maswahaba mbalimbali. Tukio jengine muhimu ni lile la mwaka 1216 Hijria (1802 Miladia), ambapo vikosi vinavyohusishwa na harakati hiyo vilivamia mji wa Karbala nchini Iraq na kubomoa sehemu za haram ya Imamu Hussein bin Ali na ya Al-Abbas ibn Ali, na kupora mali zilizokuwamo ndani yake. Ufafanuzi wa Dhana na Nafasi ya Ujenzi wa Kujengea Makaburi Kinachokusudiwa hapa kuhusiana na ujenzi wa kujengea makaburi, ni aina yoyote ile ya ujenzi unaosimamishwa juu ya eneo la kaburi, kama vile kuba, baraza au kijiuwanja, nyumba, dharih (jengo lenye muundo wa uzio), msikiti na mfano wa hayo. [1] Kujenga juu ya makaburi — hasa makaburi ya Manabii, watu wema na mawalii — ni miongoni mwa masuala yaliozua mijada katika karne ya kumi na tano Hijria, ambapo wafuasi wa Kiwahabi wameonyesha msimamo mkali dhidi yake na kuwakosoa Waislamu wengine, wakiwemo Mashia, waliokuwa na tamaduni za kutekeleza jambo hilo. [2] Kutokana na kwamba jambo hili limezua maswali mengi ya kimsingi na kisheria, watafiti wameamua kujikita katika kuchambua uhalali wa kisheria juu ya ujenzi huo, ili kubaini usahihi wake ndani ya misingi sheria za Kiislamu. [3] Tathmini ya Kihistoria ya Usanifu wa Makaburi katika Uislamu Inaelezwa kuwa tangu alfajiri ya Uislamu, usanifu wa maeneo ya makaburi au kuyajengea makaburi, imekuwa ni desturi na ni sehemu za utamadu unaoakisika ndani ya historia ya Waislamu. Jambo ambalo lilonekana kufanyioka bila kupingwa na Mtume (s.a.w.w) wala wafuasi wake waminifu. [4] Ingawa nyakati zimepita, ila bado kumbukumbu za wanahistoria zinatukumbusha kuwa, hata Mtume mwenyewe (s.a.w.w) alimstiri Fatima bint Asad ndani ya msikiti, na kufanya mahali hapo kuwa nembo ya kihistoria. [5] Aidha, katika kipindi cha mwanzo wa Uislamu, sambamba na tukio la Sulhu ya Hudaybiyya, jengo au msikiti wa kwanza kabisa ulijengwa juu ya kaburi kaburi la Abu Basir Utbah ibn Asid kupita Abu Jandal ibn Suhayl. Tendo ambalo lilitendeka katika zama za bwana Mtume (s.a.w.w), na wala hakuna andiko lililodhihiri katika katika kukaripia tendo hilo la Abu Jandal. [6] Pia mwili wa bwana Mtume (s.a.w.w) nao ulizikwa ndani ya nyumba yake mwenyewe, na huku Waislamu wakionekana kulitunzwa na kulilinda jengo la nyumba hiyo tangu miaka ya mwanzoni mwa kufariki kwake, kupitia juhudi za Waislamu na makhalifa mabalimbali. [7] Utaratibu huu uliendelea pia baada ya kipindi cha bwana Mtume, hadi kufikia katika zama za Masahaba na Tabiʿina. Jambo hili linaonesha kwamba, kujenga juu ya makaburi kulikuwa ni jambo lililozoeleka miongoni mwa Waislamu. Kwa mfano, imenukuliwa ya kwamba; Aqil ibn Abi Talib alichimba kisima ndani ya nyumba yake, na katika kuchimba huko aligonga jiwe ambalo baadaye ilibainika kuwa ni kaburi la Habiba bint Sakhr bin Harb. Kisha akalifukia tena kwa udongo na akajenga chumba juu yake. [8] Al-Samhudi (aliyefariki 911 H), ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wa Kishafiʿi kutokea Misri, amenukuu habari isemayo kwamba; juu ya kaburi la Hamza ibn Abd al-Muttalib kulikuwepo kuba (mnara) zuri na imara lenye mlango wa chuma, ambalo lilikuwa limejengwa katika kipindi cha ukhalifa wa Al-Nasir li-Din Allah.[9] Imeelezwa kwamba hata juu ya makaburi ya viongozi wa madhehebu za fiqhi za Ahl al-Sunna kulikuwepo makuba, au kusanifiwa kwa mfumo maalumu na kujengewa majengo juu yake. Kwa mujibu wa nukuu za wanahistoria, kaburi la Abu Hanifa (aliyefariki 150 H), ambaye ni kiongozi wa madhehebu ya Kihanafi huko Baghdad, lilikuwa na kuba pamoja na jengo la heshima lililojengwa katika karne ya nne na ya tano Hijria. [10] Vilevile, juu ya makaburi ya Malik ibn Anas (aliyefariki 179 H), kiongozi wa madhehebu ya Malikiyya lililoko katika eneo la Jannat al-Baqi, [11] kaburi la Muhammad ibn Idris al-Shafi'i, kiongozi wa Shafiʿiyya lililoko nchini Misri, [12] na kaburi la Ahmad ibn Hanbal (aliyefariki 241 H), kiongozi wa Hanbaliyya lililoko huko Baghdad, [13] yamejengewa kuba juu yake. Kwa mujibu wa maelezo ya Ja'far Subhani, [14] licha ya mifano hiyo ya kihistoria, mtu wa kwanz kabisa katika historia ya Uislamu ambapo aliyejitokeza kupinga ujengeaji wa makaburi, alikuwa ni Ibn Taymiyyah pamoja na mwanafunzi wake Ibn Qayyim al-Jawziyyah. Wao ndiwo walioonekana kutoa fatwa za kuharamisha jambo hilo na pia wakasisitiza wajibu wa kuyabomoa majengo yaliyojengwa juu yake. [15] Mtazamo wa Wanazuoni wa Kiislamu Tukiachana na wafwasi wa mrengo wa Kiwahabi, Wanazuoni wa wamechukulia ujenzi wa kujengea makaburi kuwa ni jambo linaloruhusiwa kisheria. Ili kuthibitisha uhalali huo, wameitoa dalili na hoja zifuatazo: • Kwa mujibu wa ufafanuzi unaopatikana katika Aya ya 21 ya Suratu al-Kahf ni kwamba; baada ya siri ya watu wa As-habu al-Kahfkufichuka na kuonekana miili yao iliyomo pangoni, kundi la washirikina lilipendekeza pango hilo lifungwe, ili kuficha na kusahaulisha tukio hilo ambalo ni dalili ya kuthibiti ufufuo wa wafu. Hata hivyo, kundi la Waumini lilipogundua jambo hilo, lilipendekeza pajengwe msikiti juu ya mahali hapo, ili kuifanya kumbukumbu yao isifutike na sehemu hiyo iwe ni mahali pa ibada. [16] Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wametegemea Aya hii kama ni dalili ya kuonesha uhalali wa kujenga juu ya makaburi. [17] • Pamoja na kwamba Ujenzi na wa kujengea na kusanifu makaburi ya Mitume na mawalii wa Mwenyezi Mungu, ni uhifadhi wa makaburi hayo dhidi ya uharibifu, pia suala hili hutazamwa kama miongoni mwa mifano halisi ya kutukuza alama za Mwenye Ezi Mungu (Ta'adhim Sha'airi Llahi). Jambo ambalo limesisitizwa katika Qur'ani kupitia aya isemayo: “وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ” (Na anayetukuza alama za Mwenye Ezi Mungu, basi hakika jambo hilo ni katika uchamungu wa nyoyo). [18] • Sira na mwenendo wa kivitendo wa bwana Mtume (s.a.w.w) na Waislamu tangu mwanzoni mwa Uislamu na kuendelea, ni kibali tosha kitoashiria uhalali na ruhusa ya kisheria ya ujenzi juu ya makaburi. Al-Hakim al-Nishapuri, katika kazi yake iitwayo al-Mustadrak 'ala al-Sahihain, akifafanua Riwaya zinazokataza ujenzi huo, anabainisha kwa kusema kwamba; Riwaya hizo (zinazokataza jambo hili) haziweze kufanyiwi kazi kivitendo. Hii ni kwa sababu ya suala la ujenzi juu ya makaburi ni jambo ambalo liliandaliwa na kutekelezwa na viongozi wa mwanzo wa Kiislamu, na wasomi wa baadaye nao wakafuata nyenendo hizo za kisheria na kijamii. [20] • Baadhi ya wanazuoni pia wamedai kwamba uhalali na kujuzu kwa ujenzi juu ya makaburi ni jambo lililothibitishwa kwa msingi wa ijmaa (makubaliano ya wanazuoni wa Kiislamu). [21] • Katika vyanzo vya riwaya vya Shia, kua Riwaya kadhaa zinazoashiria juu ya uhalali wa kujenga majengo juu ya makaburi, hasa makaburi ya Mitume na Mawalii wa Mungu. Kwa mfano, katika moja Riwaya imeelezwa kuwa, Imamu Sadiq (a.s.) alitoa kiasi fulani cha pesa kwa mmoja wa masahaba zake aitwaye Safwan al-Jammal ili akarabati kaburi la Imamu Ali (a.s.). [22] Mtazamo wa Kiwahabi Wahabi, wakifuata nyayo za Ibn Taymiyyah, [23] wanahesabiwa kuwa ndio wapinzani wakuu dhidi ya ujenzi wa majengo juu ya makaburi, [24] wao huchukulia kitendo hicho kuwa ni uzushi (bidaa) na ushirikina. Katika kutetea itikadi yao hii, wameegemea kwenye riwaya zinaeleza kuwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alikataza kujenga misikiti juu ya makaburi. [25] Katika kujibu hoja hiyo, imeelezwa kwamba Riwaya zinazotajwa hazioneshi uharamu wala ubidaa (uzushi) wa kujenga juu ya makaburi; bali kiwango cha juu kinachoweza kufahamika humo, ni kuwa kitendo hicho ni makruhu (kisichopendeza), na si haramu kama walivyofamu wao. [26] Kwa msingi huo, mafakihi wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu wametoa fatwa ya ukaraha tu, na wala hawakuharamisha jambo hilo. Aidha, wengi wao wameondoa makaburi ya Manabii, mawalii na mawasii wa Mwenye Ezi Mungu katika hukumu ya ukaraha. [27] Baadhi yao hata hawakuona kuwepo kwa umakuruhu fulani kuhusiana na kujenga juu ya makaburi ya wanazuoni. [28] Uharibifu wa Majengo ya Makaburi wa Mawahabi Makala zinazohusiana: Uharibifu wa Baqii, Yaumu al-Hadmi, Shambulio la Mawahabi dhidi ya Karbala, Uharibifu wa Haram ya Imamu Hussein (a.s), na Uharibifu wa Haram ya Askariyyain Wanazuoni wa Kiwahabi hawakuishia tu katika kuharamisha ujenzi na usanifu wa makaburi na kuuhesabu kuwa ni bidaa, bali pia walitoa fatwa ya kubomoa majengo yaliyokuwa yamejengwa juu yake na wakalitekeleza hilo kwa vitendo. Mara ya kwanza mnamo mwaka 1220 H, walibomoa makaburi ya Jannat al-Baqi, [29] na tena wakaripi tendo hilo mnamo mwezi 8 Shawwal mwaka 1344 H. Katika mashambulizi hayo mawili, yalibomolewa makuba yaliyokuwa yakinasibishwa na bibi Fatimah bint Muhammad — yaliyojulikana kama Bait al-Ahzaan — pamoja na athari zote za kihistoria za makaburi ya Baqii, zikiwemo kumbi zliliyokuwapo ndani yake. Aidha, kuliripotiwa uharibifu kadhaa uliofanywa katika eneo la Al-Masjid an-Nabawi. [30] Wafuasi wa Kiwahabi pia walivamia mji wa Karbala mnamo mwaka 1216 H, tukio lilitokea ndani ya siku ya Iddi ya Ghadir. [31] Mawahabi hao walichukuwa hatua ya kuharibu haram ya Imamu Husayn ibn Ali na ya Al-Abbas ibnu Ali, pamoja na kupora mali, hazina na vitu vya thamani vilivyokuwamo ndani yake. [32] Aidha, katika miaka ya 2006 na 2008 Miladia, magaidi wa kitakfiri wenye itikadi inayonasibishwa na mkondo huo, walifanya mashambulizi ya mabomu katika haram ya Al-Askari na kusababisha uharibifu wa mfuniko wa matofali na pambo la nakshi za dhahabu za kuba la haram (shrine) hiyo, mapambo ya vigae vya kuta, pamoja na minara ya ya jengo hilo. [33]