Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Uislamu wa Kirehema au Uislamu Rehemevu

Kutoka wikishia

Uislamu wa Kirehema au Uislamu Rehemevu: ni dhana inayojadili msimamo wa kitafakuri unaoisoma na kuifasiri dini ya Kiislamu kwa kuzingatia msingi wa rehema, huruma na upendo, huku ukikataa misimamo ya vurugu na misimamo mikali isiyovumilia tofauti. Kwa mujibu wa watetezi wa mkabala huu, Uislamu katika asili yake hukabiliana na fikra kinzani kwa njia ya uvumilivu na unyumbufu, kwa kuyapa kipaumbele mazungumzo, kuheshimu uhuru wa mawazo, na kujiepusha na ubinafsi wa kimamlaka, ukiritimba wa kifikra, huku ukijitenga na msimamo wa kufungamana na tafsiri sugu isiyoruhusu mjadala. Hata hivyo, miongoni mwa wanaounga mkono mtazamo huu kumekuwapo na mjadala kuhusu iwapo sifa ya urehemevu ni sehemu ya kiini cha Uislamu tangu asili yake au ni tafsiri iliyoibuka katika mazingira ya kihistoria ya baadaye. Vilevile, kuna tofauti za maoni kuhusu iwapo mkabala huu unaweza kuafikiana kikamilifu na dhana ya dola ya Kiislamu au la. Miongoni mwa wanaotambulika kama watetezi wa dhana ya Uislamu wa Rehema ni Mohsin Kadivar na Abd al-Karim Soroush, ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika mijadala ya kisasa kuhusu ufasiri wa dini katika ulimwengu wa leo. Kwa mtazamo wa Sayyid Ali Khamenei, ambaye ni Marjaa Taqlidi (Mujtahidi mwenye hadhi wa kufuatwa) wa Kishia na Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, dhana ya “Uislamu wa Rehema” ni mkabala wa kiitikadi wenye mwelekeo wa wigo uathiriwa na misingi ya kiliberali na fikra za nje ya turathi asilia za Kiislamu. Katika kujibu mtazamo huo pamoja na tafsiri zinazohamasisha misimamo mikali au matumizi ya mabavu, yeye sambamba na Abdullah Javadi Amoli wanapendekeza dhana ya “Uislamu Halisi”. Kwa ufafanuzi wao, huu ni Uislamu unaojengwa juu ya misingi uelewa wa kina wa kielimu; unaosisitiza matumizi ya mantiki (aql), msimamo thabiti dhidi ya uadui na dhuluma, na wakati huo huo unakataa vikali siasa ya mabavu pamoja na mwenendo wa ukufurishaji (takfīr). Aidha, kwa mujibu wa wakosoaji wa dhana ya “Uislamu wa Rehema”, mkabala huu unaweza kuishia kwenye dhana ya kuifunga dini katika wigo wa masuala ya Akhera peke yake, na hivyo kuipokonya nafasi yake katika uongozi wa maisha ya kijamii na kisiasa. Pia wanasema kuwa, mwelekeo huu huweza kusababisha ulegevu katika utekelezaji wa sheria za dini na kusahilisha utendaji wa mambo yaliyokatazwa. Mtazamo wa “Uislamu wa Rehema” umejitokeza miongoni mwa baadhi ya wanafikra wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu. Hata hivyo, imeelezwa kuwa kutokana na kuundwa na kuimarika kwa mfumo wa kisiasa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, fikra hii imepata uwanja mpana zaidi wa kujadiliwa ndani ya mazingira ya Iran na maeneo ya Washia. Kwa mujibu wa baadhi ya wachambuzi, historia ya kujitokeza kwa dhana hii kama mkondo wa kielimu na kijamii imeanza tagu mwishoni mwa muongo wa mwaka1980 Miladia. Tafsiri ya Urahmanu ya Uislamu Uislamu wa Rehema au Uislamu Rehemevu: ni jina linalotumika kuelezea mtazamo fulani wa mafundisho ya Kiislamu ambao, kwa mujibu wa wana‑nadharia wake, mtazamo huu ni wenye kunasisitiza mazungumzo, kuwepo kwa mitazamo tofauti, uhuru, na uvumilivu katika kuisha na wanaotofautiana (tunaotofautiana nao). Wafuasi wa mtazamo huu huona kwamba, baadhi ya tafsiri nyingine za Uislamu zimeelekea katika umonopoli (ukiritimba) wa ukweli, ukakamavu na usugu wa fikra, pamoja na mtazamo finyu. Watafiti hawa wanakosoa mitazamo mingi ya kiislamu ambayo, kwa maoni yao, imegeuka kuwa ni ya vurugu na ya msimamo mkali. [1] Kwa mujibu wa maoni ya Mohsen Kadivar, Uislamu Rehemevu unapingana na kile anachokiita Uislamu wa Kifashisti, Uislamu wa Kitalibani, Uislamu wa Umawiyya, na Uislamu mweusi wenye ukakamaa kwenye fikra mgando. [2] Kiini cha Uislamu Rehemevu Kulingana na itikadi ya Mohsen Kadivar, mmoja wa wana‑nadharia wakuu wa dhana ya Uislamu Rehemevu, Uislamu kiasili una tabia ya urehemevu. Hata hivyo, kutokana na kupita muda mrefu, na kuingia kwa desturi ngumu (za kimabavu) za kijahili pamoja na kupuuzwa kwa roho na malengo ya msingi ya dini, Uislamu ulianza kupoteza baadhi ya sura zake za kiurehemevu. [3] Pia imedokezwa kwamba, katika kauli za baadhi ya watu kama vile; Akbar Hashemi Rafsanjani, Sayyid Muhammad Khatami, na Hassan Rouhani, kuna ishara zinazoonyesha mtazamo usemao kwamba, msingi wa urehemevu ni kiini cha Uislamu. [4] Kwa upande mwingine, Abdulkarim Soroush, anadai kuwa Uislamu haukuzaliwa ukiwa na sura ya kiurehemevu, bali kutokana na mabadiliko ya fikra yaliyotokea miongoni mwa wanafikra wa Kiislamu kadiri karne zilivyopita, vipengele vya kiurehemevu vilianza kujitokeza hatua kwa hatua. Katika nadharia yake ya Dini na Mamlaka, Soroush alielezea nadharia yake kwa kutegemea misingi ya nadharia mbili; Upanukaji wa Uzoefu wa Kiutume na Mfinyo na Mpanuko wa Nadharia ya Sheria. [5] Uislamu Rehemevu Mkabala na Uislamu wa Kihistoria Katika mjadala huu, wafuasi wa dhana ya Uislamu wa Urehemevu huugawa Uislamu katika viwango viwili vya uelewa, navyo ni: Uislamu wa kihistoria na Uislamu wa kiroho (kiurehemevu). Kwa mujibu wa mtazamo huo, Uislamu wa kihistoria hufungamana na muktadha wa wakati, mazingira ya kijamii, na hali mahususi za kihistoria zilizoambatana na kushuka kwa wahyi na utekelezaji wa awali wa sheria. Kinyume chake, Uislamu wa kiurehemevu hujengwa juu ya kanuni za msingi na makusudio ya jumla ya dini (maqasid), bila kuzifanya zitegemee mabadiliko ya nyakati au hali za kijamii. [6] Kwa maoni ya Mohsin Kadivar, ili kuifikia hakika ya dini na kuelewa madhumuni sahihi wa Uislamu asili, yabidi kujitenga na usomaji unaoifunga dini ndani ya fremu ya kihistoria peke yake, na badala yake kuutazama kwa misingi ya akili na mantiki. [7] Kwa mujibu wa mtazamo wa Sayyid Muhammad Ali Ayazi nikwamba, katika usomaji wa Uislamu wa Kirahmani (Kirehemevu), misingi na kanuni kuu za dini pamoja na sehemu kubwa ya hukumu za ibada na miamala zinaendelea kuwa na uhalali na mamlaka yake ya kisheria bila kutetereka. Hata hivyo, baadhi ya sheria na taratibu ambazo zilifasiriwa au kutekelezwa ndani ya muktadha maalumu wa kihistoria, tofauti na mazingira ya asili ya kushuka kwa Qur’ani, zinaweza kuwa zimejitenga na ilie roho ya kirahmani. Kwa sababu hiyo, kwa mtazamo wake, hukumu hizo zinahitaji usomaji na tafsiri mpya ya kifikra na kimantiki, ili kurejeshwa katika mkondo wa malengo na maadili ya msingi ya dini yenye asili ya urehemevu. [8] Sifa Kuu za Uislamu wa Rehemevu Misingi ya Ufahamu wa Dini katika Nadharia ya Uislamu Rehemevu Mbali na radhi na rehema za Mungu, ambazo Mohsen Kadivar anaziona kuwa ndiyo msingi mkuu wa nadharia ya Uislamu wa Urehemevu, pia yeye anasisitiza mno suala la kutegemea mamlaka ya akili katika kuufahamu Uislamu. Yeye anaamini kwamba, hakuna kauli ya kidini inayopingana na mantiki inayoweza kukubalika, na kwamba kila hukumu ya kidini ni lazima iendane na akili timamu. [9] Kadivar pia anasisitiza umuhimu wa kuitumia elimu na maarifa katika welewa wa kufahamu na kuufasiri Uislamu. Aidha anaona kwamba, sayansi za kisasa za binadamu, zikishirikiana na sayansi za Kiislamu, zinaweza kutoa ufahamu mpana na sahihi zaidi kuhusu Uislamu. [10] Uadilifu, Maadili, na Haki za Binadamu katika Uislamu wa Kirahmani (Kirehemevu) Imeelezwa kwamba katika mtazamo wa Uislamu wa Urehemevu, haki na maadili huhisabiwa kama misingi muhimu ya kuufahamu Uislamu. Kwa mujibu wa mtazamo huu, kila fatwa au hukumu ya kidini inayopingana na haki ya kijamii haina uzito wa kuweza kuzingatiwa; [11] vivyo hivyo, ni lazima kila hukumu au fatwa iendane na kanuni za maadili. [12] Kwa msingi huo, Uislamu wa Urehemevu umejengwa juu ya uhuru na hiari ya mwanadamu, na zaidi ya hayo, aisha inasemwa kwamba Uislamu unathamini uhifadhi wa uhai, mali, heshima na uhuru wa kila mwanadamu, bila kujali dini au madhehebu yao. [13] Vilivile, aina yoyote ile ya ulazimishaji au kushurutisha katika mambo ya kidini chini ya mtazamo huu wa kidini. [14] Uhusiano wa Dini na Siasa katika Uislamu wa Urahmanu Wana‑nadharia wa Uislamu wa Urehemevu wanaamini kwamba katika masuala ya utawala na siasa, demokrasia ndiyo njia bora zaidi ya kuendesha jamii. Kwa mtazamo wao, katika jamii ya kidemokrasia, mamlaka ni ya wananchi wenyewe, na serikali inapaswa kuundwa kwa mujibu wa matakwa ya watu. [15] Kadivar anasema kwamba; uhuru wa taasisi ya dini dhidi ya taasisi ya siasa kuwa ni miongoni mwa nguzo kuu za Uislamu wa Urehemevu. Yeye anaamini kwamba; aina yoyote ile ya kuingilia kwa serikali katika masuala ya kidini ni batili. Kwa mujibu wa mtazamo wake, taasisi ya dini na taasisi ya siasa zinapaswa kufanya kazi kwa kujitegemea, bila kutegemeana katika mamlaka au maamuzi yao. [16] Hata hivyo, katika baadhi ya tafsiri nyingine za Uislamu wa Urehemevu imesemwa kwamba; si lazima na wala hakuna haja ya kunganishwa taasisi ya dini na siasa. Kwa mujibu wa ufahamu uliotolewa kutoka katika kauli za ya wanatafakuri wa mambo ya kisiasa, kama vile Akbar Hashimi Rafsanjani, Sayyid Muhammad Khatami na Hassan Rouhani, Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu yamejengwa juu ya kanuni za kiurehemevu, na yanapinga vurugu na ukakamavu sugu wa fikra. [17] Aidha, imedaiwa kwamba; kuutambulisha Uislamu wa asili katika sura ya kiurehemevu kunasaidia katika kutoa ufahamu sahihi wa Uislamu kwa jamii za kimataifa, na pia kunaweza kuwa na athari chanya katika kufanikisha malengo ya Jamhuri ya Kiislamu katika uhusiano wake wa kimataifa. [18] Historia na Maendeleo ya Nadharia ya Uislamu Rehemevu Ingawa, kwa upande mmoja, dhana ya Uislamu wa Kirahmani (Uislamu Rehemevu) imesambaa miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu tofauti duniani; [19] ila tafiti zinaonesha kuwa, muktadha wa kisiasa na kijamii wa Iran wa baada ya mapinduzi Kiislamu, ndio uliotoa mazingira wezeshaji kwa ajili ya kuchipuka na kukua kwa fikra hii. [20] Ni dhahiri kuwa, kuanzia mwishoni mwa Muongo wa 1982 Miladia, na mwanzoni mwa muongo wa 1992, nadharia ya Uislamu Rehemevu ulijitokeza kama msukumo mpya wa kielimu unaojipambanua kama mfumo maalumu wa kielimu na kijamii. [21] Ijapokuwa ishara za mwanzo za tafsiri ya Uislamu kiurehemevu zinatajwa kuonekana katika kauli za Mehdi Bazargan, Ali Golzadeh Ghafury, Sayyid Hussein Nasri, Akbar Hashimi Rafsanjani, Muhammad Mujtahid Shabistari, Abdulkarim Surush, Mustafa Malikian, Sayyid Muhammad Khatami, Muhsin Kodivar na Hassan Ruhani, [22] ila ni muhimu kutambua kuwa; Mohsin Kadivar ndiye mtu wa kwanza aliyebeba dhima ya kipekee katika uenezaji wa dhana hii. [23] Kadivar ndiye aliyejitolea kuitangaza kama dhana huru kabisa, huku akikiri kwamba, fikra hii si zao lake binafsi bali aliathiriwa na fikra za Fazlur Rahma ambaye ni Mmarekani wa Kipakistani. [24] Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya watafiti, miongoni mwa usomaji muhimu zaidi wa Uislamu wa Kirahmani (kirehemevu) ni fikra ya Uislamu wa kijamii ya Fethullah Gülen nchini Uturuki, inayojulikana kama Uislamu wa Anatolia. Inasemekana kuwa mkabala huu umeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mielekeo ya Kisufi. Kwa kusisitiza dhamira kama vile mapenzi, huruma na mshikamano wa kijamii, Gülen anautambulisha Uislamu kama dini isiyo na misingi ya vurugu, na inayoweza kuafikiana na hali ya kisasa (modernity) pamoja na mfumo wa usekula (secularism). [25] Kauli ya Sayyid Ali Khamenei "Wakati mwingine kauli mbiu fulani hutolewa, kauli mbiu ambazo kwa dhahiri ni za Kiislamu lakini kwa batini si za Kiislamu; ikiwemo... 'Uislamu wa Kirehemevu'; Sawa, ni neno lenye kuvutia, Uislamu wake ni mzuri, na Urehemevu wake ni mzuri; lakini lina maana gani? ... Huu Uislamu wa Kirahmani ni neno-funguo (keyword) kwa ajili ya maarifa yanayotokana na Uliberali…. [26] Mtazamo wa Wakosoaji Dhidi ya Uislamu wa Kirehemevu Kwa mujibu wa wakosoaji wa tafsiri inayoitwa “Uislamu wa Kirahmani au Kirehemevu” ni kwamba; mkabala ni hatua maalumu lenye lengo la kupunguza upeo na mamlaka ya Sheria za Kiislamu (Fiqhi), kwa kuibana dini ndani ya fremu za usekula, uhuru usio na mipaka, na dhana ya uvumilivu uliopindukia mipaka. Wakosoaji hao wanadai kwamba; Uislamu wa Kirehemevu ni tafsiri ya "kisomi-mamboleo" ambayo, kwa kisingizio cha kupunguza chuki na vurugu, hatima yake imekuja kupuuza sehemu ya hukumu na sheria msingi za kidini. [27] Aidha, imeelezwa kuwa kwa kiasi fulani dhana hii imeathiriwa na muktadha wa Uprotestanti uliopo ndani ya Ukristo, ambao unalenga jitihada za kuisoma upya dini kulingana na mazingira ya kisasa. [28] Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kuhusiana na mtazamo wa Sayyid Ali Khamenei, imeelezwa kwamba; yeye anaamini kuwa dhana ya Uislamu wa Kirehemevu ni mkabala uliondwa kwa kuchanganya vipengele visivyo na uhusiano wa kimsingi. Sababu ni kwamba mkabala huu umeathiriwa na mtazamo wa itikadi zisizo sahihi, na misingi ya kumweka mwanadamu kuwa ndiyo kitovu (anthropocentrism) na kuachana na nadharia ya tawhidi. Na hatimaye kupelekea itikadi ya kukubali wingi wa dini kwa namna ya kipluralisti, kuthamini zaidi maisha ya dunia, na kuuwekea dini mipaka kwa kuifungamanisha na masuala ya akhera peke yake. Kwa msingi huo, kwa mujibu wa mtazamo wa Sayyid Ali Khamenei, usomaji sahihi wa Uislamu ni ule unaopelekea kuufahamu Uislamu kamili, ambao ni jumuishi na wenye utoshelevu wa ndani. Uislamu huo, kwa mujibu wake, hauhitaji kukamilishwa au kuongezewa misingi kutoka katika mifumo mingine ya kifalsafa au kiitikadi, bali unawajibisha uaminifu na utiifu kwa jumla ya maarifa na mafundisho yake bila kuyapunguza au kuyachagua kwa upendeleo fulani. [29] Imeelezwa kuwa hata ile dhana ya Uislamu wa Kirehemevu inayotambulishwa na Mohsen Kadivar pia nayo inakumbana na changamoto juu ya suala la haki ya uadilifu; kwa kuwa Kadivar anasema kwamba; ili kuelewa uadilifu wa kweli ni lazima kurejea katika desturi za kijamii (mazoea ya kijamii), ilhali akili ya pamoja haiwezi kuchukua nafasi ya wahyi. Vilevile, heshima ya utu wa binadamu katika Uislamu wa Kirehemevu, ambayo msingi wake ni ubinadamu, inaingia katika mgongano na haki za Mwenyezi Mungu, jambo ambalo si sahihi. [30] Aidha, katika moja ya makala imeelezwa kuwa; kuna mgawanyi wa wazi kabisa inayojitokeza katika namna ya kushikamana na kuufanyia kazi Uislamu wa kisiasa. Kwani upande mmoja kuna watetezi wa Uislamu wa Kirehemevu, na upande mwingine ni tafsiri za kitakfiri na zenye kutumia nguvu ambazo pia hujulikana kama ufurutu ada wa Kiislamu. Kati ya mitazamo hii miwili, Sayyid Ali Khamenei na Abdullah Jawadi Amuli wanapendekeza mtazamo mwengine wa tatu unaokabiliana na ulegevu na upindukiaji mipaka. Mtazamo huu ndio uleule wa Imamu Khomeini kuhusiana na Uislamu wa kisiasa. Misingi mikuu ya mtazamo huu, matumizi ya akili, umakini na kutokusalimu amri mbele ya maadui, sambamba na kukataa aina yoyote ile ya mapambano yasiyo ya kiakili na yenye kutegemea nguvu na ukafirishaji. [31] Mada Zenye Kuhusiana • Uislamu Halisi • Uislamu wa Kimarekani