Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Nadharia au imani ya “Tanasukh” (Reincarnation)

Kutoka wikishia

Nadharia au imani ya “Tanasukh” (reincarnation): ni nadharia inayorejelea imani na itikati ya kuhamia kwa roho ya binadamu kutoka mwili mmoja hadi mwingine baada ya kifo cha mwnadamu huyo. Kwa mujibu wa itikadi za Kishia, itaikadi ianhisabiwa kuwa ni miongoni mwa itikadi zinazopingana za misingi mikuu ya itikadi za Kiislamu. Na kwa kuwa imani hii ni ni yenye kwenda kinyume na imani ya “maad” (ufufuo), hivyo basi, imani ya Tanasukh inahisabiwa kuwa ni miongoni mwa imani za kufuru. Maimamu wa Kishia (a.s) wamekanusha na kuipinga vikali imani hiyo katika Riwaya zao, huku wanatheolojia wa Kishia wakionekana kutoa hoja mbali mbali za kielimu na za kiakili katika kuthibitisha ubatili wake.

Kwa mujibu wa watafiti, imani kuhusu tanasukhi (yaani uhamaji wa roho kutoka mwili mmoja hadi mwingine) haijawahi kuwa sehemu ya itikadi ya Waislamu wengi. Hata hivyo, baadhi ya Waislamu, walipokutana na tamaduni na dini nyingine, walivutiwa na dhana hiyo. Wafuasi wa ghulat (waliopita mipaka katika imani juu ya viongozi wa dini) wanatajwa kuwa miongoni mwa waumini wa awali wa tanasukhi. Ingawa imeelezwa kuwa baadhi ya makundi miongoni mwao waliamini kuwa roho ya Mwenyezi Mungu imeingia katika roho za Maimamu wa Kishia (A.S.), mitazamo hiyo ilihesabiwa kwa upole kuwa sawa na tanasukhi na wataalamu wa madhehebu. Baadhi ya wanazuoni wa Ahl al-Sunna wamefanisha tanasukhi na imani ya rajaʿa (kurudi kwa baadhi ya waja kabla ya Siku ya Kiyama) katika itikadi ya Kishia. Hata hivyo, wanazuoni wa Kishia wanafafanua kwamba rajaʿa ni tofauti kabisa na tanasukhi, kwani rajaʿa haimaanishi kuwa nafsi moja itakuwa na miili mingi.

Watafiti wanaohusiana na msuala ya dini wanakubali kwamba, kiuhalisia, imani ya Tanasukh yenye maana ya kuzaliwa upya kwa roho ya mwnadamu katika mwili mwingine baada ya kifo, haijawahi hata mara moja kushika mizizi na kuwa ni miongoni mwa itikadi za Waislamu walio wengi ulimwengu. Hata hivyo, baadhi ya Waislamu, kutokana na kuchanganika kwao na tamaduni za dini nyengine, walijikuta wakivutwa na kutumbikia ndani imani hii. Vikundi vya kwanza kabisa kutajwa na kuhusishwa na imani ya Tanasukh ni vikundi vinavyojulikana kwa jina la Ghulat (vikundi vya wenye imani za kupindukia mipa). Ingawa, yasemekana kwamba: Baadhi ya wataalamu wa masuala itikiadi walichanganya na hawakutofautisha baina ya imani ya Mguhulat ya juu Hulul (kuingia kwa roho ya Kiungu katika miili ya Maimamu wa Kishia) na imani ya Tanasukh. Kwa lugha nyengine, walitazama mambo mawili haya kwa mtazamo mmoja, na hivyo kuyahisabu kuwa ni kitu kimoja. Pia, baadhi ya wanazuoni wa upande wa Ahlu al-Sunna wamejaribu kuifananisha itikadi ya Tanasukh na imani ya Raj'a (kurejea kwa baadhi ya watu duniani kabla ya Siku ya Kiyama) iliyopo miongoni mwa Mashia. Lakini wanazuoni wa Shia wanafafanua na kusisitiza kwamba; Raja na Tanasukh ni imani mbili zisizokutana katika msingi mmoja. Tofauti kuu baina yake ni kwamba: imani ya Raja hairuhusu roho moja kuwa na miili mingi kwa wakati mmoja, kama inavyodaiwa kwenye imani ya Tanasukh. Kifupi, kwa mtazamo wa itikadi za Shia, imani ya kurejea ulimwenguni haiendani sawa na itikadi ya kuzaliwa upya.

Muhammad bin Zakariya al-Razi anachukuliwa kuwa ndiye mwanafalsafa wa kwanza kabisa wa Kiislamu wa aliyeambatana na itikadi ya Tanasukh. Kinyume chake, Ibn Sina (Avicenna) anatajwa kuwa ndiye mwanafalsafa wa mwanzo aliyechukuwa hatua za kubatilisha itikadi ya Tanasukh kwa marefu na mapana. Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya watafiti, Mulla Sadra, akitumia msingi wa nadharia yake ya Harakatu Al-jawhariyyah (harakati ya kimsingi/kidhati), ameweza kujenga msingi imara kabisa unaofafanua na kuthibitisha uhai na uendelevu wa nafsi ya mwanadamu, msingi ambao umekuja kufunga na kujenga ukuta imara kabisa dhidi ya nadharia inayojaribu kutoa uthibitisho wa dhana ya Tanasukh.

Baadhi ya wanazuoni wanaamini kwamba; misingi ya irfani (unyoofu wa kiroho), inayojumuisha shauku ya mwanarifani (mshikamanifu wa unyoofu wa kiroho) ya kuachana kikamilifu na maisha ya kidunia, haiwezi kuendana na dhana ya Tanasukh. Hii ni baada ya kizingatia kwamba; itikadi ya Tanasukh inawakilisha dhana ya urejeo wa roho katika kiwiliwili cha duniani. Aidha masufi na wanairfani wote wa Kiislamu ni kushikamana na itikadi ya Maad (ufufuo wa mwisho), jambo ambalo linapingana mojawapo na misingi ya imani ya tanasukhi. Hata hivyo, kuna ripoti zinazoeleza kwamba; moja ya sababu zilizopelekea kutuhumiwa kwa wanairfani na kunasibishwa na imani ya Tanasukh, ni ile itikadi baadhi yao ya kuamini Hulul (kuingia kwa roho ya Kiungu katika miili ya baadhi ya wanadamu), pamoja na kushikamana kwana na itikadi ya Tajalli (kujidhihirisha kwa Mungu kupitia viumbe wake).


Itikadi ya kuhama kwa roho (Tanasukh) au dhana ya kuzaliwa upya hufafanuliwa kama kitendo cha kuhama kwa nafsi ya mtu kutoka katika mwili mmoja na kuingia katika mwili mwingine. [1] Aidha, kuna maelezo yanayoonyesha kuwa historia ya maisha ya mtu aliyekufa ndiyo inayochora mfumo au hali ya mwili mpya ambao roho yake itaelekea. [2] Kiini hasa cha dhana hii ni msisitizo wake juu ya nafsi kubaki katika ulimwengu wa kimwili hata baada ya kifo cha mwanadamu kiachopelekea kubomoka na kuharibika kwa mwili wake. Dhana ya Tanasukh ni miongoni mwa dhana zilizoshughulikiwa na kuchanganuliwa kupitia mitazamo na mifumo mbali mbali ya kidini na kifalsafa. [3]


Itikadi ya tanasukhi inatajwa kuwa ni mojawapo ya imani msingi na ilionea zaidi katika Dini za wanadamu mbali mbali ulimwenguni humu, ikianzia kwenye mizizi ya dini za mwanzo hadi zile zilipo katika zama za hivi sasa [4]. Dhana ya Tanasukh inahisabiwa kuwa ni miongoni mwa imani isio na utangamano na baadhi ya itikadi za Dini za Kiibrahimu (Ukristo, Uyahudi na Uislamu), hasa kuhusiana na itikadi ya Maad (ufufuo) [5].

Kwa mujibu wa makubaliano ya wanazuoni wote wa Kiislamu, ni kwamba; dhana ya tanasukhi ni moja wapo ya imani batili ziendazo kinyume na misingi ya kisheria pamoja na itikadi za Kiislam.  Hivyo basi, kuamini na kushikamana na itikadi hii, kunachukuliwa kuwa ni moja aina za kufuru, zinayopingana na misingi ya tauhidi na imani ya Akhera. [6].

Baadhi ya watafiti wamebainisha wakisema kwamba; itikadi ya uazaliyyah (umilele na utangu) wa roho, ugumu wa kutoa tafsiri inayokubalika juu mateso ya kidunia, jitihada za kuoanisha baina ya shari zilizomo duniani na uadilifu wa Mungu, pamoja na uhalali wa vitendo vya kulipiza kisasi, ndiyo sababu za kuibuka kwa imani ya Tanasukh miongoni watu mbali mbali. [7]

Aina za Tanasukhi

·        Tanasukh Nazuliy (Tanasukh ya Kushuka Daraja): Hii inafafanuliwa kwa maana ya uhawilishwaji wa ruh ghair kamil (roho isiyo kamilifu) kwenda kwenye daraja ya chini zaidi. Roho hii isiyokamifu inaweza kuelekea kwenye daraja ya chini zaidi ya kibinadamu, kuhawilishwa na kuwekwa kwenye mwili wa wanyama, kuwekwa kwenye mwili wa mimea, ua pia kuteremshwa daraja ya chini zaidi na kuwekwa kwenye vitu visivyo hai. [8]

·        Tanasukh Su’udi (Tanasukh ya Kupanda Daraja): Hii inahusiana na uhawilishwaji wa roho kutoka daraja ya chini ya kibinadamu, ya wanyama, ya kimmea, na kutoka katika vitu visivyo hai, na kuelekea kwenye daraja ya juu zaidi. [9]

uhusiano na kiini pekee kinachoziunganisha aina hizi za Tanasukh, ni itikadi ya kuhamishwa kwa roho kutoka kiwiliwili kimoja kwenda chengine. [10]

Kimsingi, dhana ya Tanasukh, ambayo inajikita katika itikadi ya uhawilishwaji wa roho kutoka chombo kimoja cha kimwili hadi chengine, inatofautiana kabisa na nadharia ya Maskh, ambayo inafafanuliwa kama metamofosisi (mabadiliko) ya umbo la nje la kiumbe fulani. [11] Katika muktadha wa Tanasukh, kuna uhamaji kamili wa roho, ambapo nafsi huondoka katika hali yake ya awali na kuingia katika hali mpya, ikiwa imejumuisha athari za maisha yaliyotangulia. Kinyume chake, Maskh inahusisha kuimarika kwa roho ndani ya mwili wake asilia, huku umbo la mwili huo likibadilishwa kama adhabu ya Mungu. [12]

Imamu Ali bin Musa ar-Ridha (a.s) anasema:

“مَنْ قَالَ بِالتَّنَاسُخِ فَهُوَ کافِرٌ بِاللَّهِ الْعَظِیمِ مُکذِّبٌ بِالْجَنَّةِ وَ النَّارِ”

“Yeyote yule anayeshikilia imani ya kuhama kwa roho (Tanasukh) huhisabiwa kuwa ni kafiri aliyemkana Mwenye Ezi Mungu Mtukufu, na atakuwa tayari ameshakanusha ukweli wa kuwepo kwa Pepo na Moto wa Jahannam.” [13]

Ukafiri na Ubatilifu wa Dhana ya Tanasukh katika Fikra za Kishia

Kulingana na mafundisho ya Shia, itikadi ya Tanasukh, inahisabiwa kuwa ni miongoni mwa itikadi za kikafiri. Hii ni kutokana na kupingana kwake na msingi wa Maad (Ufufuo) na itikadi ya kuamini siku ya malipo (Akhera). [14] Kuna vyanzo kadhaa vya Hadith vinavyonukuu kauli za Maimamu wa Kishia (a.s.) zinazokana dhana hiyo potofu. [15] Kupitia moja ya tawqi ‘at (barua rasmi) za Imamu Mahdi (a.f), imethibitika kwamba; Imamu Mahdi (a.f) alijitenga na makundi fulani ya Kishia yaliyokuwa na mwelekeo wa kuamini itikadi Tanasukh. [16] Aidha, Hadith zinabainisha kwamba; sababu ya msingi ya kuhesabu imani hiyo kuwa ya kikafiri, ni kukanusha kwake imani ya uwepo wa Pepo na Moto wa Akhera. [17] Wanazuoni kadhaa wa ‘ilm al-Rijal (elimu inayohusiana na utafiti wa juu ya maisha na nasaba za wapokezi wa Hadithi), wametumia kalamu zao katika kuakisi udhaifu wa wale wapokezi wa Hadithi waliohusishwa au walioshikamana na imani ya Tanasukh. [18]

Wafasiri wa Shia, wakiegemea kwenye Aya kadhaa za Qur’ani zinazofafanua itikadi ya Maad (Ufufuo), wamekataa na kupinga katakata nadharia ya Tanasukh. [19] Wao wakuonekana wakitoshea na kitendo cha kuikataa itikadi hiyo, bali pia wameonekana kuichambua na kukosoa hoja za wafuasi wa imani hii potofu waliokuwa wakijaribu kutumia Aya za Qur’ani kwa ajili ya kutafuta uhalali wa imani yao. [20] Aidha, wanateolojia wa Kishia wametoa hoja kadhaa za kiakili na kimantiki dhidi ya itikadi ya Tanasukh, [21] na wali hawakuaacho kujibu hoja zilizokuwa zikitolewa na upande unaoshikamana na dhana hiyo. [22] Mfano muhimu wa wanazuoni waliotumia kalamu zao katika uwanja huo, ni Sheikh al-Tusi, aliyesimama katika kujibu kisingizio cha matumizi ya mateso ya dunia kama ni hoja ya kuthibitisha Tanasukh. Akijibu dai hilo alisisitiza akisema kwamba; utesekaji wa binadamu duniani humu, haufai kuhisabiwa kama ni aina fulani ya adhabu, na kwa njia hii, aliweza kubatilisha hoja ya wanaoamini kwamba; mateso ya wasio na hatia ni matokeo na natija ya dhambi walizotenda katika maisha yao ya awali. [23]

Je, Kweli “Raj ‘a” ni sawa na “Tanasukhi”?

Baadhi ya wanazuoni waupande wa madhehebu ya Ahlu al-Sunna wameonekana kuifasiri imani ya raj‘a ilioko katika mafundisho ya Kishia kwa maana ile ile ya dhana ya Tanasukh. [24] Hatua ambayo imepelekea kuwahesabu Mashia miongoni mwa wale wanaoamini itikadi ya kuhama kwa roho kutoka mwili mmoja hadi mwingine. [25]

Hata hivyo, wanateolojia wa Kishia wamepinga tuhuma hiyo kwa kutoa ufafanuzi wa kina kabisa juu ya tofauti msingi zilizopo kati ya nadharia ya raj‘a na itikadi ya Tanasukh. Miongoni mwa wanazuoni mashuhuri waliotumia upanga wa kalamu katika kupambana na tuhuma hizo, ni Ja‘afar Subhani. Katika jitihada zake za kufafanua tofauti ya itikadi mbili hizo anaeleza akisema; Raj‘a haiwezi kuchanganywa na itikadi ya Tanasukh, kwani dhana ya Tanasukh hubatilika kupitia sifa mbili kuu nazo ni: kurudi kwa roho kutoka ngazi ya juu ya ubinadamu na kutumbukia kwenye daraja chini kabisa ya viumbe visivyo na akili; pili, nadharia ya Tanasukh inaamini uwepo wa miili mingi kwa kwa ajili ya roho moja. Ila tukirudi kwenye nadharia ya Raj’a, tuikuta nadharia hiyo imeepukana na nguzo mbili hizo zilizoifanya nadharia ya Tanasukh kubatilika na kukosa thamani mbele ya wachambuzi mbali mbali wa masuala ya kiitikadi. [26]

Kwa mujibu wa Subhani, Raj‘a ni tukio la kimiujiza la kufufuliwa kwa wanadamu, ambapo roho mwnadamu fulani hurejea katika mwili wake wa awali bila kupoteza hadhi ya kimaumbile ya mwanadamu huyo. [27] Bwana Ja’afar Subhani akiendelea na uchambuzi wake, anaifananisha nadharia ya Raj‘a na muujiza wa Nabii Isa (a.s) wa kufufua wafu, muujiza ambao katu haujawahi kuchukuliwa kuwa ni moja ya aina za tanasukhi. Wala hakujatokea Muislamu au Mkristo yeyote yule aliyewahi kuuingiza muujiza huo kwenye fungu la nadharia ya Tanasukh. [28]

Kuna maandiko kadhaa yaliyoandikwa kuhusu dhana ya Tanasukh, ukosoaji wake, na pia kutoa ufafanuzi wa maelezo yanayotofautisha kati ya nadharia hiyo na itikadi ya Raj‘a. Miongoni mwa kazi andishi zilizoshughulikia nyanja hizo ni kitabu kiitwacho “Tanasukh Gozashteh wa Imruz” (Tanasukh Katika  Zama Zilizopita na za Leo) kilichochapishwa na Chuo Kikuu cha Adyani wa Madhahib, [29] chengine ni kitabu kiitwacho “Tanasukh” kilichoandikwa kwa lugha ya Kiajemi na kutolewa na Taasisi ya Utafiti wa Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Baqir al-Ulum (a.s). Kitabu cha tatu katika uwanja huu, ni kitabu kiitwacho “Tanasukh dar Andisheye Islami” (Tanasukhi katika Fikra za Kiislamu) kilichoandikwa kwa lugha ya Kiajemi na bwana Ali Ridhai Birjandi. [31]

Sababu Zilizowafanya Baadhi ya Waislamu Kuamini Tanasukh

Uchambuzi wa kihistoria unaonesha kwamba kuenea kwa itikadi ya Tanasukh katika baadhi ya vikundi vya Kiislamu, kulichangiwa na vigezo mbalimbali vya kijamii na kidini.

Sababu ya kwanza inayotajwa inayotajwa kuhusiana na jambo hili, ni mwingiliano wa Waislamu na tamaduni za kigeni, ikiwemo Dini za Wabudha, wafuasi wa Mani (Manichaean), falsafa za Kigiriki (au dini za Wagiriki), na imani za Wamazdakiyyah (Mazdakians). [32] Sababu ya pili ni ufahamu wao mbaya kuhusiana na dhana ya Maskh (metamorphosis, au mageuzi ya umbo) iliyopo ndani ya theolojia ya Dini za Kiibrahimu (Ukiristo, Uyahudi na Uislamu). Dhana hii ni miongoni vivukio vilivyotumiwa na baadhi ya Waislamu katika kutumbukia kwenye dhana ya Tanasukh. [33] Zaidi ya hayo, pia kuna rekodi zinazothibitisha kuwepo kwa dalili za itikadi ya Tanasukh katika jamii ya Waarabu kabla ya kipindi cha Kiislamu. [34]

Baadhi ya watafiti wa masuala kiitikadi, humtaja Abdullah bin Harith [35] na Abdullah bin Saba, [36] kama ndiwo waumini wa kwanza kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu walioanza kutumbukia kwenye bonde la itikadi ya Tanasukh. Kwa upande wa makundi na madhehebu mbali mbali, Maghulat ndio kundi la kwanza linalotuhumiwa kushikamana na imani ya Tanasukh. [37] Watafiti wameeleza wakisema kwamba; baadhi ya wanazuoni wa taaluma ya madhehebu ya Kiislamu walichanganya mambo, na hatimaye wakaifasiri imani ya Tanasukh na imani ya Hulul ilioko katika baadhi ya madhehebu ya Kishia (Kaysaniyyah). [38] Kulingana na maelezo ya watafiti mbali mbali, sababu msingi iliyopelekea tafsiri hiyo, ni kuwepo kwa baadhi ya mifanano kati ya dhana mbili hizo, pamoja na ulaini (upuruziaji kamba) wa kalamu za wanazuoni na watafiti hao uliotumika katika kufafnanua istilahahi mbili hizo. [39] Hali kadhalika, Isma'iliyyah walihesabiwa kuwa ni miongoni mwa waamini wa nadharia ya Tanasukh, hii ni kutokana na uwepo wa mitazamo yao inayokaribiana na itikadi hiyo. [40]

Pia kuna orodha nyengine ilikuja kuwajumuisha baadhi ya watu fulani na kuwatambua kuwa ni miongoni mwa waamini wa itikadi ya Tanasukh. Orodhahiyo inawajumuisha watu kadhaa ndani yake, akiwemo: Ibn Abi al-'Awjaa’, [41] baadhi ya wanazuoni wa Mu’utazilah, [42] Nusayriyyah, [43] Druziyya, [44] Ahl al-Haqq, [45] Rawandiyyah, [46] Sepidjamegan “Al-Mubyaddhah” (Wafwasi mtu aitwaye Al-Muqanniya), [47] Khurramdiniyyah, [48] na baadhi ya madhehebu ya mchanganyiko (syncretic) kama vile Yazidiyyah, Azar Kaiwaniyan, Nuqtawiyyah, na Pasikhaniyan. [49]

Tanasukh Katika Misingi ya Falsafa ya Kiislamu

Makala kuu: Tanasukh Ndani ya Falsafa na Ir’fani

Kuna baadhi ya watafiti wanaosema kwamba; katika muktadha wa historia ya falsafa ya Kiislamu, kuna ushahidi unaoonesha kwua, kule kuibuka kwa wanafalasifa waliokubali au kuonesha mielekeo ya kukubali nadharia ya Tanasukh, ndiko kulikosababisha kutanuka na kuimarishwa kwa hoja zote za wanazounga mkono dhana hiyo. Jambalo pia lilipelekea kuibuka kwa hoja madhubuti zaidi zitokazo kwa wapinzani waliosimama dhidi ya mkondo huo. [50]

Abu Bakar Muhammad ibn Zakara al-Razi (aliyeishi baina ya mawaka 251 na 313 H), [51] ambaye ni daktari na mwanafalsafa mashuhuri, hutajwa kama ndiye mwanafalsafa mkuu wa Kiislamu aliyeamini waziwazi itikadi ya Tanasukh. [52] Vilevile, maandishi ya wanafalsafa wa Ikhwan al-Safa (Brethren of Purity) na pamoja na Al-Farabi yanatuhumiwa kuwa na uhusiano fulani na dhana ya Tanasukh. [53]

Nafasi ya Ibn Sina Katika Mjadala wa Tanasukh

Katika uwanja wa fikra na falsafa ya Kiislamu, Ibn Sina ndiye mwanafalsafa wa mwanzo kabisa aliyesimama na kuchambua na kujadili kwa undani zaidi itikadi ya Tanasukh. [54] Wanafalsafa wa Kiislamu, wakiongozwa na Ibn Sina na wafuasi wake, ndiwo watafiti wa kwanza kabisa waliobaini kwamba; imani ya Tanasukh imejengwa juu ya msingi wa dhana inayoamini kwamba nafsi ya mwanadamu ni ya kiumbe kinye maisha ya utangu wa milele, bila ya kutegemea chanzo fulani. Kwa mantiki hiyo, juhudi zao ziliilenga kuipinga fikra hiyo kwa kutima hoja madhubuti zenye kuthibitisha kwamba; nafsi ni kitu kilichoumbwa na muumba maalumu, na si cha tangu ya kale na kale. [55]

Katika hoja zake za kifalsafa, Ibn Sina alieleza kwamba; kuikubali nadharia ya Tanasukh kunamaanisha kuna uwezekano wa nafsi mbili kuhusiana na mwili mmoja, jambo ambalo haliwezekani kimantiki. Kwa kutumia hoja hiyo, mwanafalsafa huyu aliweza kuthibitisha ubatili wa nadharia ya Tanasukh. [56] Kulingana na maelezo ya baadhi ya watafiti, hojo hii madhubuti ya Ibn Sina, imeonekana kupokelewa kwa mikono miwili na wanafalsafa wa mtazamo wa Mashaa’iyyun (wanafalsafa wanaofuata mfumo wa Aristotelian), ambayo pia imeonekana kutumiwa na wanafalsafa hao katika maandiko yao ya baadaye, ikitumiwa kama hoja kuu ya kukataa dhana ya uhamaji wa roho (Tanasukh). [57]

Msimamo wa Sheikh al-Ishraq Kuhusiana na Tanasukh

Sheikh al-Ishraq (Suhrawardi) hakuonekana kuwa na msimamo wa wazi katika kuijadili dhana ya Tanasukh, jambo lililowaweka njia panda wanazuoni wa wanafalsafa wa Kiislamu.  Baada ya wanazuoni kurejea maandiko yake mbali mbali, yakiwemo Partawnama, Al-Mutarahat, na Alwah-i Imadiyyah, wameibuka na kauli isemayo kwamba; Suhrawardi anonekana kufuata misingi ya wanafalsafa wa shule ya Mashsha’i (wanafalsafa wanaofuata mfumo wa Aristotelian), hii ni kutokan na upinzani wake dhidi ya imani ya Tanasukh iliomo ndani ya maandiko yake hayo. [59] Hata hivyo, katika moja ya vitabu vyake maarufu kiitwacho Hikmat al-Ishraq, Suhrawardi anaonekana kuwa na mashaka juu ya baadhi ya hoja zilizotolewa dhidi ya nadharia ya Tanasukh, huku akizihisabu hoja kuwa dhaifu zisizo na uzito wa kutosha katika kupinga nadharia hiyo, jambo lililomsukuma kuonesha mwelekeo wa kukubali baadhi ya vipengele vya dhana hiyo, ingawa pia hakuonekana kutoa uamuzi wala hitimisho maalumu lililo wazi juu ya msimamo wake. [60]


Mulla Sadra na Kupinga Tanasukh Kupitia Nadharia ya Mwendo wa Kiasili

Baadhi ya watafiti wanasema kuwa Mulla Sadra, kwa kutumia nadharia yake ya Harakati al-Jawhariyya (Mwendo wa Kiasili wa Kiini), aliweza kuelezea kwa ustadi mkubwa mno, namna ya roho inavyoumbwa na kuendelea na uwepo wake, na hivyo kuupiku uthibitisho wa dhana ya Tanasukh kuufana kuwa ni kitu kisichowezekana. [61]

Kulingana na nadharia hiyo, mwanzoni mwa kuumbwa kwao, roho na mwili ni vitu viwili vyenye uwezo wa kuingia katika hatua mbali mbali, huku vikiwa bado havijamiliki chochote miongoni mwa hatua hizo (bilquwwah), huku vikiwa na mwendo wa kiasili wa ndani (wa kiini). [62] Vitu viwili hivi, kwa kupitia maisha ya kawaida, huanza kuachana hali yake ya awali ya kiuwezekano na hatimaye huingia katika hali ya utendekaji (bilfi’l), utendekaji ambao ima huwa ni wa kiustawi au uporomoja. [63]

Kwa mujibu wa mtazamo wa Mulla Sadra, Tanasukh ni sawa na kiumbe kurejea nyuma akitoka katika hali ya ukamilifu na utendaji (fi’liyyah) na kurudi tena kwenye hali yake ya mwanzo ya kutomili kitu ambayo ni hali kuwepo kwa uwezekano kuingia katika hatua za baadaye (quwwah), yenye sifa ya hali fiche. Jambo ambalo kamwe haliwezekani kukubali, si kiakili wala kifalsafa (muhal). [64]

Tanasukh Katika Irfan ya Kiislamu

Makala kuu: Tanasukh Katika Irfani (Tasawwuf)

Baadhi ya watafiti wanaamini na kusisisitiza kwamba; misingi ya misingi ya Irfan ya Kiislamu, inayomfanya mwnairfani kujiepusha na ulimwengu wa kidunia na kushikamana na Fana fi Llahi, haitoi nafasi wala mwanya wa kuweza kuhalalisha dhana ya Tanasukh. [65] Hii ni kwa kuwa Tanasukh inaashiria kurudi tena kwa roho ya mwandamu katika ulimwengu wa kimwili, jambo linalopingana na lengo la kiroho la wanairfani la kuachana na maisha ya kidunia. [66] Aidha, msingi wa imani ya Ma‘ad katika mafundisho ya wanairfani wa Kiislamu, unaosisitiza ufufuo wa kiroho na kuhukumiwa kwa kupewa adhabu au thawabu baada ya kifo, umekuwa ndiyo msingi kuu ya kukataliwa dhana ya Tanasukh mbele ya wanazuoni wa tasawwuf. [67] Si hayo tu, bali kuna wanairfani na Masufi kadha mashuhuri waliosimama na kupambana dhidi ya nadharia ya Tanasukh huku wakionekana kusimamisha hoja na dalili mbali mbali katika kukabilia na imani hiyo. Miongoni mwa wanairfani hao ni pamoja na; Abu Nasr al-Sarraj, [68] Ibn ‘Arabi, [69] Sheikh Mahmud Shabistari, [70] na ‘Ala’ al-Dawla Simnani. [71] Kwa mfano Shabistari, akifafanua itikadi ya Tanasukh, aliihisabu imani hiyo kuwa ni matokeo ya mtazamo finyu katika welewa wa mfumo wa uumbaji, [72] mtazamo ambao, kwa mujibu wa wafasiri wa kitabu kiitwacho Gulshani Raz, umezaliwa kutokana na kutoutambua na kutoamini uwepo wa mwili wa Kibarzakh. Jambo ambalo limepelekea kufikiria kwamba; mwili wa kimaada ndio mwili pekee unaohusiana na roho, hata baada ya kifo mwanadamu. [73]

Sababu nyingine iliyochangia wanairfani na Masufi kuliangalia kwa makini zaidi dhana ya Tanasukh, ni uwepo wa imani ya Hulul miongoni mwa baadhi ya makundi yao. Kwa bahati mbaya, kwa kuwa baadhi ya wasomi wa Kiislamu walichanganya mambo, hii ilipelekea kuiweka dhana ya Tanasukh sambamba na dhana ya Hulul, na kuzifasiri dhana mbili hizi kwa maana moja. Na Hii ndiyo sababu msingi iliyopelekea wanairfani na Masufi wa Kiislamu kutuhumiwa kwa imani ya Tanasukh. [74] Zaidi ya hayo, hata ile imani katika dhana ya Tajallī (dhihiriko la Mungu kupitia viumbe vyake) inayoshikiliwa na wanairfani, pia nayo hutajwa kama miongoni mwa sababu nyengine iliyopelekea kutumiwa na imani ya Tanasukh. [75] Tuhuma hii iliwafanya baadhi ya Maarif waliokuwa na elemu ya kina katika tafiti mbali mbali kusimama na kutumia uwezo wa kalamu zao kwa ajili ya kujibu tuhuma hii, pamoja na kukosoa vikali dhana ya Tanasukh. Mafahali hao wa Kiirfani walifafanua wazi tofauti lilizopo kati ya nadharia mbali mbali, ikiwemo dhana ya Tajalli na Tanasukh. [76]