Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Mvinyo au Khamr

Kutoka wikishia

Mvinyo au Khamr: Neno Khamr kimsingi linamaanisha pombe itokanayo na zabibu (divai ya zabibu), ambayo unywaji wake ni haramu. Ila katika maandiko ya kisheria (fikihi), kanuni hii inapanuka na kujumuisha vileo vyote (intoxicants). Wanazuoni wanashikilia kuwa uharamu wake ni suala la mwafaka miongoni mwa Waislamu, na ni miongoni mwa misingi ya lazima ya dini hiyo. Hivyo basi, anayehalalisha aina yoyote ile ya kileo huhisabiwa kuwa amekufuru. Maandiko ya Qur'ani yanatoa taswira ya kamili ya kijamii na kisaikolojia, yakibainisha kuwa khamr (divai ya zabibu) ni chombo cha Shetani cha kueneza uhasama na kumpotosha mwanadamu, anachokitumia kwa ajili kumuondoa mwanadamu kwenye dhikri na Sala. Kitaaluma, kuna utofauti mkubwa kati ya divai ya kidunia yenye sifa ya kupotea kwa akili, na divai ya Akhera inayoelezwa kuwa ni yenye ladha maalumu kwa wanywaji wake bila kuleta madhara ya kifiziolojia au kimaadili. Kwa mujibu wa fatwa za mafaqihi wa Kiislamu, pombe inachukuliwa kuwa ni najisi, na hivyo muamala au biashara yake yoyote ile ni batili kisheria. Aidha, ni haramu na batili kununua au kuuza zabibu na tende kwa lengo mahususi la kutengeneza pombe. Pia hairuhusiwi kutumia kileo kama dawa, isipokuwa katika mazingira ya dharura kubwa iliyopindukia mipaka. Kwa upande wa adhabu, mtu yeyote anayekunywa pombe hukabiliwa na adhabu ya kisheria ya viboko themanini. Maana ya Khamr na Nafasi Yake Unyaji Pombe Kilugha, neno Khamr linamaanisha pombe inayotokana na zabibu, [1] na ndilo neno lililotumiwa ndani ya Qur'ani kurejelea vinywaji vyote vya kulevya. [2] Ingawa baadhi ya vitabu vya fikihi vinabaki na maana hiyo finyu, [3] ila kamusi nyingi na mafaqihi wakuu wametanua dhana hiyo ikijumuisha kioevu chochote kile chenye asili (sifa) ya kulevya. [4] Aidha baadhi ya wanazuoni wamekiingiza kila kitu chenye kulevya kwenye orodha ya ulevi, iwe ni cha maji maji au kilavu. [5] Katika Uislamu, unywaji pombe si tu ni haramu, [6] bali ni miongoni mwa madhambi makuu. [7] Uharamu huu ni suala lenye mwafaka wa kijumla miongoni mwa Waislamu wote duniani, na ni sehemu ya mambo yanayolazimiana na dini (dharuriyyat al-din), kiasi kwamba mtu anayeihalalisha pombe huhesabiwa kuwa ni kafiri. [8] Neno Khamr Kama Lilivyokuja Ndani ya Qur’ani Ndani ya Qur'ani Tukufu, neno Khamr (pombe) limetajwa mara kadhaa kwa kutumia misemo tofauti inayobainisha sifa zake hasi. [9] Miongoni mwa sifa zake zilizotajwa ndani Qur’ani ni ile sifa yake ya kulevya [10] inayosababisha maumivu ya kichwa, [11] sifa ya kuchochea madhambi, [12] na kupelekea kupotea kwa akili. [13] Aidha, Qur'ani inaifafanua pombe kama jambo chafu [14] na kazi (nyenzo) ya Shetani [15] inayolenga kupandikiza mbegu za uadui na chuki miongoni mwa wanadamu, [16] huku ikiwazuia kumkumbuka Mwenye Ezi Mungu na kuwatenga na utekelezaji Sala. [17] Hata hivyo, Qur'ani inatoa taswira tofauti kuhusu divai ya Peponi; inaeleza kuwa huko Peponi kuna mito ya divai itiririrkayo, [18] ambayo ni tamu na yenye ladha nzuri mno, [19] lakini haina madhara yoyote kama vile ilivyo kwenye ulevi wa kidunia. Mvinyo wa huo hulevyi, [20] hauleti maumivu ya kichwa, [21] huuchochezi kutenda maasi [22] wala hausababishi kudhoofika wa utambuzi (akili). [23] Unywaji Pombe Makala Asili: Unywaji Pombe Unywaji wa pombe hufafanuliwa kwa maana ya utumiaji wa kioevu chochote kile chenye sifa ya kulevya. [24] Katika mfumo wa Kiislamu, ni haramu mtu kutumia aina yoyote ile ya kileo, [24] bila ya kujali asili yake, iwe kimetokana na zabibu, tende, zabibu kavu (kismish), au malighafi nyingine yoyote. [26] Kwa mujibu wa vyanzo vya fatwa, mnywa pombe anachukuliwa kuwa ni fasiqi (mtenda dhambi), hali inayopelekea kukataliwa kwa ushahidi wake mahakamani. [27] Sheria ya Kiislamu imeweka adhabu ya haddi [28] ya viboko themanini kwa kosa hili. [29] Hata hivyo, sheria inatoa nafasi ya rehema maalumu juu ya kosa hili. Rehema hii ni kwamba; mhusika anaepushiwa adhabu ya viboko iwapo atatubu kabla ya mashahidi kutoa ushahidi wao dhidi yake. [30] Mchakato wa Kuharamishwa kwa Pombe katika Uislamu Makala Kuu: Kuharamishwa kwa Pombe Ingawa Waislamu wote wanakubaliana moja kwa moja juu ya uharamu wa kunywa pombe, [31] ila kuna nadharia mbili tofauti zinazotolewa na watafiti mbalimbali kuhusianana na kuharamishwa kwa pombe ndani ya Uislamu: Nadharia ya Uharamu wa Mara Moja na Nadharia ya Uharamu wa Hatua kwa Hatua. Tofauti ya kimsingi kati ya mitazamo miwili hii ni namna ya nama ya kuzielewa Aya za zilizokuja kuharamisha kinyaji hichi; kwamba je Aya hizo ni Aya zilizoshuka Makka [32] au Madina. [33] Wale wanaounga mkono uharamu wa hatua moja, wanaamini kuwa pombe ilipigwa marufuku kwa mkupuo mmoja tangu kipindi cha Makka na kabla Waislamu hawajahamia Madina. [34] Kwa upande mwingine, mtazamo wa wa pili (ulioenea zaidi miongoni mwa Ahlu al-Sunna na baadhi ya wasomi wa Kishia) unaaminia kuwa hapo mwanzo pombe ilikuwa ni halali, na uharamu wake ulikuja taratibu kupitia hatua mbalimbali za kisheria. [35] Licha ya tofauti hizi za kihistoria, leo hii uharamu wake ni suala la mwafaka wa kijumla miongoni mwa Waislamu wote ulimwenguni. [36] Unajisi wa Pombe Mafaqihi na wafasiri wengi wa Qur'ani, wakitegemea Aya ya 90 na 91 ya Suratu al-Ma'idah [37] pamoja na Riwaya zinazohusiana na mvinyo, [38] wametoa hukumu ya unajisi wa mvinyo (pombe). Wanazuoni wakubwa wa zama hizi akiwemo Imam Khomeini [39] na Sayyid Abu al-Qasim al-Khui [40] pia nao katika maandiko yao wamesisitiza hukumu hii. Allamah Hilli, mwanazuoni mashuhuri wa karne ya 8 Hijiria, alibainisha akisema kuwa kuna mwafaka wa jumla (ijmai) miongoni mwa mafaqihi juu ya unajisi wa pombe, akidai kuwa hata uharamu wa kuinywa unatokana na asili ya maada hiyo kuwa ni najisi. [41] Aidha, alinukuu kutoka kwa Sayyid Murtadha na Sheikh Tusi kuwa hapakuwa na hitilafu yoyote ile miongoni mwa Waislamu juu ya unajisi huo. [42] Licha ya mwafaka huo mkubwa, vyanzo vinaonyesha kuwa baadhi ya wanazuoni wa kale walikuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na unajisi huo. Kwa mfano, Sheikh Saduq na Muqaddas Ardabili waliwahi kuwasilisha au kuelekea kwenye nadharia isemayo kuwa pombe ni maada tohara (safi). [43] Hukumu Zinazohusiana na Pombe Baadhi ya hukumu za kisheria kuhusiana na pombe ni kama ifuatavyo: • Kwanza, pombe haina thamani ya mali kisheria; kwa hiyo, ni batili kuuza au kununua maada hiyo, [44] isipokuwa pale inapohusiana na watu wa dhimma au pale pombe hiyo inapowekwa kwa nia ya kuandaa siki. [45] • Pili, ni haramu kuuza zabibu, tende au vitu vingine kwa dhamira ya kutengeneza pombe, na muamala huo ni batili kisheria; hata hivyo, wanazuoni hawana kauli moja (ya haramu au umakruhu) juu ya hukumu ya kumuuzia vitu hivyo mtu anayejulikana kuwa kazi yake ni kutengeneza pombe—bila ya muuzaji huyo kuwa na nia ya kumuuzia kwa ajili ya kutengeneza pombe. [47] • Tatu, kwa mtazamo wa madhehebu mengi ya Kiislamu, hairuhusiwi (ni haramu) kutumia pombe kwa ajili ya tiba, iwe kwa kunywa au kwa njia nyingine, , isipokuwa tu katika hali za dharura (isiyoepukika kirahisi). [48]