Mkopo:Mauaji yanayofanana na ya makusudi
Mauaji yanayofanana na ya makusudi (shibhu-amdi): ni aina ya mauaji maalumu ambapo mhusika wa tendo hili huwa hana dhamira ya kuua katika utendaji wake. Pia aghalabu tendo husika huwa si lenye kuangamiza na kusababisha kifo, huku mhusika wake akiwa amelitekeleza tendo hilo kwa hiari ya yake. Mfano wake ni pale tabibu fulani anapoamua kufanya utaratibu wa kimatibabu ambao bila baadaye hupelekea mauti ya mgonjwa anayemtibu. Aina hii ya mauaji inasimama mkabala na mauaji ya makusudi pamoja na mauaji yasiyo ya makusudi (ghairi-amdi); ambapo katika kategoria ya kwanza, muaji anakuwa na nia thabiti ya kuua, ilhali katika kategoria ya pili, muaji huwa hana nia ya kuua wala hakudhamiria kutekeleza kitendo kilichosababisha mauti dhidi ya mhusika aliyemuua. Kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni wa sheria za Kiislamu ni kwamba, mauaji yanayofanana na ya makusudi (shibhu-amdi) hayastahili adhabu ya kulipiza kisasi, ila mhusika wa kitendo hicho hulazimika kulipa fidia kamili ya damu aliyoimwaga sambamba na kutoa kafara ya kisheria. Utaratibu wa kafara hiyo ni kufunga saumu ya miezi miwili mfululizo, na asipoweza kufanya hivyo atatakiwa kulisha mafukara sitini kamambadala wa kafara ya saumu. Kanuni za Adhabu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimefafanua vigezo mbalimbali kuhusiana na mauaji yafananayo na mauaji ya makusudi, huku zikibainisha kwamba mauaji yanayojiri kupitia hali ya kutojua (un-awareness), yanaingia moja kwa moja katika kategoria ya mauaji yafananayo na ya makusudi. Mauaji yanayoshabihiana na ya makusudi, ni mojawapo ya aina mbalimbali za mauaji. [1] Wanazuoni wa sheria za fiqhi wameizungumzia anwani hii kwenye milango maalumu inayohisiana na masuala ya kisasi pamoja na dia (malipo ya fidia), na wakatoa ufafanuzi kamili kuainsiha hukumu za tendo hilo vitabuni mwao. [2] Aidha, kuna mlango wenye anwani hii unaopatikana katika baadhi ya vyanzo mbalimbali vya Hadithi. [3] Aya ya 92 ya Suratu An-Nisa ni Aya maalumu inayohusiana na tendo la hili, ambayo imelitaja tendo hilo pamoja na kuanisha sheria ya malipo ya fidia kwa mwenye kutokezewa na tendo kama hilo. [4] Ufafanuzi wa Dhana Mauaji yanayofanana na ya makusudi (nusu makusudi), humaanisha tukio la kifo linalotokana na kitendo kilichofanywa kwa makusudi bila ya mtendaji wake kuwa na nia ya kuua, na ambacho kwa kawaida si miongoni mwa vitendo vinavyosababisha mauti. [5] Miongoni mwa mifano yake hai, ni hatua za kitabibu zinazopelekea mgonjwa fulani kufariki dunia bila ya tabibu wake kuwa na makusudio ya kumuua mgojwa huyo. [6] Mfano wengine ni adhabu ya kawaida iliyotolewa kwa lengo la kumlea mtoto fulani ambayo imebabisha kifo chake bila bila ya makusudio. [7] Kifiqhi, mauaji haya hutofautishwa na yale ya kukusudia na mauaji yasiyo ya kukusudia ambayo hayana sura ya mauaji ya kukusudia. [8] Mizani na kipimo cha mauaji ya kukusudia ni kuwepo kwa muungano thabiti kati ya dhamira ya mhusika na utekelezaji wa kitendo chenyewe. Ama kigezo kikuu cha mauaji yasiyo ya kukusudia ni kuwepo kwa utelezi kwenye utekelezaji kitendo fulani, huku nia ikiwa na malengo tofauti. Mfano wake ni kama pale mhusika anapokusudia kumlenga mnyama fulani, ila kwa bahati mbaya risasi yake ikamsibu mwanadamu fulani. [9] Kipimo cha mauaji ya yanayofanana na ya makusudi ni kuwepo kwa dhamira ya utendaji wa kitendo fulani, bila ya kuambatana na nia ya mauaji ya atendewaye kitendo hicho. [10] Wakati mwingine huwa ni vigumu kwa manasheria kuyatambua mauaji yafananayo na ya makusudi. Hali inatokana na kule dhana hii kuchanganyika na mseto wa aina mbili za mauaji: ya makusudi na ya kosa la moja kwa moja lisiloshabihiana na mauaji yeney sura ya makusudi. [11] Hii ni kwa sababu ya kwamba, kwa upande mmoja, yanafanana na mauaji ya makusudi, kwani muaji wake huwa amekesudia kutenda kitendo kilichsababisha mauti, lakini kwa upande mwingine, yanafanana na mauaji ya kosa tupu, kwa sababu mtendaji huyo hakuwa na nia ya kumuua mhanga huyo. [12] Wakati mwengine hutokea khitilafu katika maamuzi ya kisheria miongoni mwa wanazuoni mbalimbali. Kwa mfano, wanazuoni wameonekana kutoa fatwa tofauti kuhusiana na mtu atakayemdhuru mwingine na kumsababishia ugonjwa ambao baadaye utapelekea kifo chake. [13] Hukumu ya Mauaji Yafananayo na ya Makusudu Kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni wa fiqhi zilizofafanuliwa katika fiqhi ya jina, mauaji ya mauaji yanayofanana na ya makusudi hayamwajibishi mwanasheria kumhukumu mtendaji wake kwa kumpa adhabu ya kulipiza kisasi (qisās); badala yake, muuaji huyo analazimika kulipa fidia (diya) ya damu aliyoimwaga. [14] Muda wa kulipa fidia ya kosa la mauaji yafananayo na ya makusudi ni miaka miwili, na fidia hiyo inatakiwa kulipwa kutoka katika mali ya muuaji mwenyewe. [15] Katika vitabu vya fiqhi imeelezwa kuwa, katika baadhi ya hali fulani, wajibu wa kulipa fidia unaweza kuondolewa kwa kusamehewa moja kwa moja iwapo mwenye haki ya kudai fidia atamuondolea dhima muuaji huyo. Pia wajibu wa huo huondoka moja kwa moja iwapo muuaji anayanasibishwa na tendo hilo atakuwa amejiondolea dhama kabla kutokea kifo cha muhanga huyo. Mfano wa hali hii, ni kama pale daktari fulani atapomweleza mgonjwa wake wazi wazi kuhusiana na hali ya kifo inayoweza kutokea huku akikataa tokea mwanzo kubeba jukumu la kulipa fidia iwapo tukio hilo litamfika mgonjwa huyo. Kisha mgonjwa au mlezi wake akakubali sharti la daktari huyo, huku daktari huyo alikwa ametekeleza wajibu wake bila ya kufanya uzembe wa kimatibabu. Kwa mujibu wa maoni mashuhuri, endapo mgonjwa atafariki, daktari huyo halazimiki kulipa fidia ktokana na kifo hicho. [16] Kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni wa fiqhi, katika mauaji yafananayo na ya makusudi, pamoja na fidia, pia mtendaji wa tendo hilo huwajibu kutoa kafara kutokana na tendo hilo adhimu. [17] Kulingana na mtazamo unaokubalika zaidi mbele ya wanazuoni mbali mbali, [18] kafara hiyo hulipwa kwa mpangilio ufuatao: kwanza kabisa anatakiwa kumuacha huru mtumwa; iwapo hilo haliwezekani, basi atatakikwa kufunga miezi miwili mfululizo; na iwapo haya yote hayatawezekana, hapo atapaswa kulisha maskini sitini. [19] Mauaji ya Yafananayo na ya Makusudu katika Sheria za Iran na Mataifa Mengine
Nchini Iran, Sheria ya Kiraia ya Kijanai iliyopitishwa mwaka 1304 SH na marekebisho yake ya mwaka 1352 SH, inainisha mauaji katika makundi mawili: mauaji ya makusudi na mauaji yasiyo ya makusudi. Hata hivyo, katika sheria za adhabu za makosa zilizopitishwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1357 SH, kama vile Sheria ya Adhabu kulingana na sheria za Kiislamu ya mwaka 1370 SH na Sheria ya Fidia (Dia) na Adhabu ya mwaka 1392 SH, zilifafanuliwa kosa la mauaji na kuliweka kategoria katika vichwa kuu vitatu: mauaji ya makusudi, mauaji ya nusu-makusudi (yafananayo na ya makusudi), na mauaji ya kosa lisilo na shaka ndani yake. [20] Ibara ya 291 ya Sheria ya Adhabu ya Kiislamu imetaja mifano maalumu ya mauaji yafananayo na ya makusudi, ambapo mauaji yanayotokana na hali ya kutofahamu yameainishwa kuwa miongoni mwa makosa na nusu-makusudi. Mfano wa mauaji hayo ni mwindaji anayemfyatulia risasi binadamu kwa kudhania ni mnyama, na kumsababishia mauti. [21] Katika baadhi ya mifumo ya kisheria isiyo ya Kiislamu, kama vile ya Ufaransa, mauaji yamegawanywa katika makundi mawili peke yake; ya makusudi na yasiyo ya makusudi, bila kuwepo kwa dhana ya mauaji ya nusu-makusudi ndani yake. [22]