Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Mauaji ya Ayatullahi Khamenei

Kutoka wikishia

Mauaji ya Ayatullahi Khamenei ni tukio muhimu linalorejelea kuuawa kishahidi kwa Ayatullahi Sayyid Ali Khamenei ambaye alikuwa ni kiongozi mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Tukio hili la kibeberu lilijiri mnamo mwezi 10 Ramadhani mwaka 1447 Hijiria kupitia shambulio za kombora. Shambulio lililotekelezwa na Wazayuni wakishirikiana Wamarekani. Shambulio hili lilijiri pale baadhi ya viongozi wakiwa pamoja naye walipokuwa katika shughuli zao za kiserikali ndani ya jengo lijulikanalo kwa jina la Bait Rahbariy (Jengo la Uongozi) lililopo mjini Tehran. Habari za tukio hili zilitangazwa alfajiri ya mwezi 11 Ramadhan mwaka 1447 Hijiria.

Shambulio hili lililotekelezwa kwa ushirikiano wa Wazayuni na Wamarekani lilisababisha vifo vya viongozi kadhaa wa serikali. Miongoni mwa waliopoteza roho zao baaya kujiri kwake ni pamoja na viongozi wakuu wa kijeshi akiwemo; Sayyid Abdurrahim Musawi (kamanda mkuu wa vitengo vyote kijeshi), Muhammad Pakpur (kamanda mkuu wa kikosi cha Sepah Pasdaran) na Ali Shamkhani (msimamizi mkuu wa Kamati ya Shura Kuu ya Ulinzi). Mwengine ambaye ni miongoni mwa watu muhimu waliopoteza roho zao, ni waziri wa ulinzi (Aziz Nasirzadeh).

Lengo kuula lililokusudiwa na wahalifu wawili hawa katika hujuma hii, ni kuvunja na kuvuruga umoja na mshikamano wa dola pamoja na wananchi wake. Pia miongoni mwa malengo mengine yaliotajwa, ni dhamira ya Wazayuni ya katika kuitia mkononi ardhi ya nchi ya Irani pamoja na kubadili mfumo wa uongozi wa nchi hiyo.

Kwa Nini na ni kwa Namna Gani Hujuma Hii Imeweza Kukamilika

Ayatullahi Sayyid Ali Khamenei alikuwa kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuanzia mwaka 1990 hadi 2026 Miladia. Uongozi wake ulifikia mwisho baada ya shambulio la makombora lililodaiwa kufanywa kwa ushirikiano wa Israel na Marekani. Kiongoni huyu shupavu alishikilia na nafasi hiyo akiwa ni kiongozi mkuu wa Iran pamoja Mashia waishowo ndani ya nchi mbalimbali ulimwenguni. Ila mnamo mwezi 10 Ramadhani 1447 Miladia sawa na tarehe 28 Februari mwaka 2026, uongozi ulihitimishwa kupitia shambulio mseto la Wazayuni na Wamarekani. Tukio ambalo lilipelekea kufa kishahidi yeye pamoja na jopo la viongozi wakuu waliokuwa ndani ya Jengo la Makao Makuu ya Uongozi. [1]

Dondoo Kutoka Hutuba ya Mwisho ya Ayatullahi Khamenei

Wananchi wa Irani wanayafahamu fika mafunzo ya Uislamu na Ushia, wanaelewa vyema nini cha kufanya. Imamu Hussein (a.s) anasema: “«مِثلی لا یُبایِعُ مِثلَ یَزید؛” (Mtu kama mimi hawezi kumuunga mkono mtu kama Yazid). Wairani nao pia wanasema: “Watu kama sisi, wakiwa na tamaduni, wakiwa na tarehe ing’aayo, wakiwa na uelewa wa juu, katu hawawezi kuwaunga mkono na kukubaliana na mafasiki wa kilimwengu kama wale waongozao Amerika”. [2] Lengo la kumua kiongozi mkuu wa Irani ni kuvunja umoja na mshikamano wa wananchi wa nchi hiyo, madhumuni yakiwa ni kuitia mkononi ardhi ya nchi hiyo [3] pamoja na kubadilisha mfumo wa uongozi unaotawala nchini humo. Aidha imeelezwa kwamba; kisingizio cha jinai hii ya Wazayuni na Wamarekani, iliyopelekea kuuawa kwa kiongozi mkuu wa Irani pamoja na wananchi kadhaa wa Irani, eti ni kwa lengo la kuzuia mradi wa upanuzi wa silaha za nyukilia wa Irani. [4] Shambulio mseto la Wazayuni na Wamarekeani limepelekea kuuawa kwa baadhi wanafamila wa kiongoni mkuu wa Irani pamoja viongozi wakuu kadhaa wa serikali. Viongozi wakuu hao ni pamoja na; Sayyid Abdurrahim Musawi (kamanda mkuu wa vitengo vyote kijeshi), Muhammad Pakpur (kamanda mkuu wa kikosi cha Sepah Pasdaaraan) na Ali Shamkhani (msimamizi mkuu wa Kamati ya Shura Kuu ya Ulinzi). Mwengine ambaye ni miongoni mwa watu muhimu waliopoteza roho zao, ni waziri wa ulinzi (Aziz Nasirzadeh).

Kiongozi mkuu wa Irani na Juhudi Zake za Kutetea Mhimili wa Upinzani

Sayyid Ali Akhamenei alijulikana kama kiongozi mkuu wa Mhimili wa Upinzani, akiwa ni mtetezi wa daima wa mhimili huo. Yeye ni mwanaharaki mkuu dhidi ya utakaliaji wa kimbavu wa Wazayuni katika ardhi mbalimbali, pia ni mpizani mkuu wa unyemeleaji wa Wamarekani, hasa katika maeneo ya Magharibi mwa Asia.

Matishio Mbalimbali ya Kumuua Kiongozi Mkuu wa Irani

Kabla ya kuuawa kwake kupitia shambulio mseto la Wazayuni na Wamarekani, kiongozi mkuu wa Irani alikabiliwa na vitisho mbalimbali vya kumuua. Miongoni mwavyo ni vili vilivyotolewa na Wamarekani wakishirikiana na Wazayuni katika kipindi cha vita siku 12. Katika vita hivi vilivyofuatiwa na vita vya hivi sasa (Februari mwaka 2026), mara kadhaa kiongozi huyu alionekeana kutishiwa maisha yake kupitia mabeberu wawili hao. Miongoni mwa waliomtishia mauti ni raisi wa Marekani akishirikiana na viongozi wakuu wa Israel, akiwemo waziri mkuu wa nchi hiyo. [5] Mafaqihi wakuu wa Hauza ya Najaf pamoja na Qom, wakishirikiana na wanazuoni mbalimbali pamoja na taasisi za kidini, hawakulaani vitisho hivyo bali pia walionekana kumuunga mkono bila ya pingamizi kiongozi huyu shupavu. [6] Miongoni mwa yaliosemwa kutoka kwa wanazuoni wa Qom na Najaf, ni ile kaule yao iliosema; Sayyid Ali Khamenei ni nembo ya msimamo, fakhari na umoja wa umma wa Kiislamu, hivyo basi aina yoyote ile ya kumkabili kwa hatari, ni sawa na kutangaza vita dhidi ya umma mzima Kiislamu, na ni khiana ya wazi kabisa dhidi ya nyenzo za thamani za utamaduni wa kumwabudu Mungu Mmoja. [7] Kwa upande mwengine pia kulikuwa na wanazuoni walitoa maonyo makali zaidi ya hayo, miongoni mwao ni Ayatullahi Makarim Shirazi [8] na Ayatullahi Nuri Hamadani. [9] Wanazuoni hawa walisimama wakisema kwamba; Aina yoyote ile ya hujuma dhidi ya Ayatullahi Khamenei, kutaambatana na tangazo la kumbambua mhusika wake kama ni kafiri aliyetangaza vita dhidi ya Uislamu (Muhaarib).

Kosa la Jinai na Kidini Kisiana

Kulingana na sheria za Umoja wa Mtaifa, ni haramu na ni kosa kubwa kisheria kuua viongozi wa kisiasa wa nchi fulani. [10] Hivyo basi, kumuua kiongozi mkuu wa Irani na Mashia kwa ujumla, ni kosa lililopitiliza mipaka ya jinai za kisiasa, kwani yeye hakuwa ni kiongozi wa nchi fulani bali anatambulikana na kiongozi mkuu wa Mashia duniani. [11]

Radiamali

Kufuatia kifo cha kishahidi cha Ayatullahi Khamenei, kulimiminika salamu za rambirambi kutoka pande mbalimbali. Miongoni mwa wanazuoni waliowasilisha samamu hizo ni pamoja na; Sayyid Ali Sistani, Wahid Khurasani, [12] Nasir Makarim Shirazi, Hussein Nuri Hamadani, Jafar Subhani, Jawadi Amuli na mkuu wa vyo vya Kiislamu vya Qum. Salamu za rambirambi zilizotolewa na Nuri Hamadani zilibeba ujumbe usemao; Ni wajibu kwa kila Muislamu duniani kusimama kwa ajili ya kulipiza kisasi dhidi ya mauaji ya kiongozi wake muadhamu. Kwa upande wake Makarim Shirazi, ameliona tukio hili kama ni utangulizi wa kujwa kwa mwokozi (Imamu Mahdi) (a.s).

Aidha viongozi mbalimbali wa serikali waliwasilisha rambirambi zao kufutia tukio hili. Miongoni mwao ni; viongozi wa nguvu kuu tatu za serikali, maraisi wa nchi mbalimbali kama vile; Urusi, Tajikistani, Uzbakistani, Iraq, waziri mkuu wa Malaisia [13] pamoja na spika wa bunge la Lebanoni. Putin Raisi wa Urusi, amelitaja tukio la mauaji haya kuwa ni hujuma na jinai iliokosa haya, pia amesema kwamba; tukio hili ni tukio lililokiuka mipaka yote ya kimaadili pamoja na kunja sheria za Umoja wa Mataifa Duniani. Viongozi wa Mhimili wa Upinzani (Muqawamah), pia nao wameonekana kuwasilisha rambirambi zao mbele ya Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Miongoni mwao ni pamoja na; kiongozi mkuu wa Hizbullahi ya Lebanoni, kiongozi wa kikosi cha Ansaru Al-Llahi ya Yemen, mkuu wa kikundi cha Hikmat Milli cha Iraq, Kikosi cha Hamas, Kikosi cha Mujahidina cha Palestina pamoja Muqtada Sadri ambaye ni kiongozi wa wanajihadi wa Iraq. [14] Baadhi ya viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali pia nao waliakisi hisia zao kwa kutoa salamu zao za rambairambi kufuatia tukio hili la jinai. Miongoni mwao ni kiongozi mkuu wa madhehebu ya Orthodox wa nchini Urusi. [15] Vyombo kadhaa vya habari viliakisi tukio hili hatari kupitia idhaa zao mbalimbali. Kufuatia mauaji haya, Irani ilitangaza siku saba za mapumziko pamoja na siku 40 za kuomboleza msiba huu adhimu. [16] Iraq ilitangaza siku tatu za msiba na huzuni, huku mikoa ya Karbala na Najaf ikitangaza kusitisha kazi za mikoa miwili hiyo kwa muda wa siku moja. Mashia wanaishi katika mikoa mbalimbali ya Irani wakishirikiana na wenzao wanaoishi nje ya nchi hiyo ikiwemo; Iraq, Pakistani, India, Lebanoni, Yemen, Australia, Nigeria na nchi nyengine kadhaa ulimwenguni, wameonesha hisia zao kwa kushiriki maandamano ya kuadhimisha msiba pamoja na vikao mbalimbali vilivyojiri wakilaani jinai hiyo pamoja na kuakisi ukubwa wa huzini zao kuhusiana na msiba huo. Mashia katika miji ya Beirut, Baghdad na Karachi waliandaa maandamano makubwa ya kulaani tukio hilo. Katika baadhi ya maeneo, maandamano hayo yalielekea karibu na balozi za Marekani kama ishara ya hasira na kupinga tukio hilo. Kiasi cha watu 34 waliuliwa mjini Karachi kufuatia hatua hiyo, mauaji hayo yalijiri baada ya walinzi waliomo ubalozini kuwafyetulia risasi waandamaji hao wenye hasira. Aidha nchini Kishmir pia kumeripotiwa kutokea vurugu baina ya waandamanaji na askari polisi waliokuwa wakijaribu kuwazuia waandamanaji hao. Pia bendera ilioko katika haram ya Imamu Ridha huko Mash’had ilishushwa na kuwekwa bendera ya msiba, kufuatia kifo cha kishahidi cha Ayatulahi Khamenei. Aidha bendera nyekundu yenye maandishi yasemayo: “یا لثارات الحسین” (Enyi walipizaji wa damu ya Hussein) ilianza kupepea ndani eneo la msikiti mkuu wa Jamkarini, ikiashiria hali ya vita na kutaka kulipiza kisasi. Ili Mashia wa mji wa Kadhimain waooneshe kikamilifu hisia zao, wao waliamua kutengeneza mazishi pandia kama ni kioo kinachoashiria hali walizokuwa nazo kufuatia msiba huo.

Matokeo na Mwitikio wa Baada ya Tukio

Kufuatia tukio hilo liumizao moyo ambalo lililodaiwa kufanywa na Israel na United States, Islamic Revolutionary Guard Corps (Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu), waliamua kujibu shambulio hilo kwa kuanzisha operesheni iliyopewa jina la “Wa’adi Saadiq 4”. Katika operesheni hiyo, mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones) yalielekezwa dhidi ya maeneo ya ardhi zilizokaliwa kwa mabavu, pamoja na vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyopo katika eneo la Asia Magharibi.

Matokeo na Mwitikio wa Makundi ya Upinzani

Katika muktadha wa tukio hilo, Hezbollah ya Lebanon ilitoa taarifa rasmi ya kutangaza kujiunga na Iran katika mapambano dhidi ya Israel. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, chama hicho kilianzisha mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel, kikisema hatua hiyo ni sehemu ya kulipiza kisasi cha kuuawa kwa kiongozi wa Iran na kuonyesha mshikamano wao na Tehran. Aidha, baadhi ya makundi ya upinzani ya Iraq pia nayo yalitangaza kushiriki katika mapambano hayo. Miongoni mwao ni kundi la Saraya Awliya al-Dam, ambalo lilitangaza kuanza mashambulizi yake dhidi ya United States na Israel. Vilevile, kundi linalojulikana kama Hezbollah Kurdistan pia nalo lilitangaza jihad dhidi ya Marekani na Israel, likieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono kile wanachokiita mhimili wa upinzani (Axis of Resistance) katika eneo hilo.

Maudhui Zinazofungamana

  • Kuuawa kwa Sayyid Hassana Nasrullah
  • Kuuawa kwa Qasim Suleimani