Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Majosho ya wajibu

Kutoka wikishia

Majosho ya wajibu: Katika istilahi za sheria ya Kiislamu, majosho ya wajibu ni yale yenye sifa ya kutoharisha hadathi kuu (uchafu mkuu wa kiwiliwili na kiroho), sambamba na ile iliyofaradhishwa kwa sababu ya uwekaji wa nadhiri, kiapo, na mambo yanayofanana na hayo. Utekelezaji wa majosho haya sita ni sharti la msingi kwa ajili ya kusihi na kukubalika kwa baadhi ya ibada, ikiwemo ibada ya Sala. Orodha ya majosho hayo inajumuisha josho la janaba, josho la maiti, josho la kugusa maiti (massu al-mayyit), na majosho matatu mahususi kwa ajili ya wanawake; ambayo ni josho la hedhi, nifasi, na istihadha. Kwa mujibu wa fatwa za Mafakihi, ni kwamba; hakuna ulazima au wajibu wa mtu kujitoharisha na kutekeleza majasho hayo. Ila wajibu huu unakuja kutokana na ibada iliyoshurutishwa kuitekeleza huku mja akiwa ni mwenye tohara kamili. Majosho yatokanayo na nadhiri, ahadi, na kiapo, yamehesabiwa kuwa ni wajibu kwa muktadha wa ulazima wa kutimiza ahadi na makubaliano ya kisheria pekee, na wala hayako katika jumla ya masharti ya kusihi kwa ibada fulani. Wanazuoni wengi wa Kishia wanashikilia msimamo usemamo kwamba; ikiwa mtu anawajibikiwa na majosho kadhaa (josho zaidi ya moja kwa wakati mmoja), anaweza kuoga josho moja tu huku akiweka nia ya kujitoharisha na majosho yote yalioko katika dhima yake. Wanazuoni wote wa Kishia wanakubaliana kuwa baada ya josho la janaba, hakuna haja tena ya mtu kutia udhu (yaani anaweza kusali au kufanya ibada nyengine bila ya kuhitaji udhu); na wengi wao wamethibitisha kuwepo kwa mwafaka (ijmai) katika suala hilo. Hata hivyo, kuna tofauti za kimaoni kuhusu majosho mingine ya wajibu, ya kwamba jee hivi mtu anaweza kuyategea katika kutohitaji udhu baada yake.

Katika sheria za kifiqhi, josho la faradhi hufafanuliwa kuwa ni josho linalomwajibikia mukallaf kutokana na kule yeye kuingia katika hali ya kupata hadathi kuu (uchafu mkuu), na kulitekeleza josho hilo ndiko kunakompatia na kumrudishia hali yake ya tohara na kumruhusu kufnaya ibada bila ya kikwazo. Uzito wa kifiqhi wa aina hii ya majosho unatokana na ile kauli ya wanazuoni isemayo kwamba—ukiondoa josho la nadhiri, ahadi na kiapo—kusihi kwa baadhi ya ibada muhimu, kama vile Sala, Saumu na sehemu ya manasiki ya Hija, (amali za Hija) kuko chini dhamana ya utekelezwaji wa majosho ya wajibu. Kadhalika, ni haramu kwa mwenye majosho hayo (asiyejitoharisha na kupitia majosho hayo) kuingia misikitini, kuzuru maeneo matukufu ya Maimamu wa Shia, au kugusa maandishi ya Qur’ani. Vilevile, kwa mujibu wa kauli mashuhuri ya wanazuoni ni kwamba; hairuhusiwi (haijuzu) kufanya tendo la ndoa kabla ya mwanamke kujitoharisha na majosho ya kike yanayomkabili (hedhi, nifasi na istihadha). Aina za Miyosho ya Wajibu Kwa mujibu wa fiqhi ya Shia, [1] hukumu ya wajibu inahusu miyosho sita ya kisheria pamoja na josho la nadhiri na kiapo. Miyosho hiyo sita ni: • Josho la janaba • Josho la kugusa maiti (mas al-mayyit), • Josho la maiti • Majosho matatu mahsusi ya wanawake inayotokana na damu tatu za kifiqhi, ambazo ni hedhi, nifasi na istihadha. Katika fiqhi imeelezwa kuwa josho linaweza kuwajibika kwa nadhiri, ahadi au kiapo, kama ilivyo kwa mtu anayejilazimisha kwa nadhiri kufanya josho kwa ajili ya ziara. [2] Kwa mujibu wa rai za wanazuoni mashuhuri, josho la maiti na josho la nadhiri na ahadi, ndiyo majosho pekee yenye hukumu ya wajibu binafsi. Majosho mingine ya faradhi yaliobakia huhesabiwa kuwa na wajibu ghairi (usio binafsi), kwa maana kwamba hayajawajibika kwa dhati yake yenyewe, bali huwajibika kwa ajili ya ibada ambazo utekelezaji wake umefungamana na tohara. [3]

Hukumu za Majosho ya Wajibu Katika maandiko ya sheria za kifiqhi ya Kishia, hukumu za majosho ya wajibu zimebainishwa kama ifuatavyo: • Kuna njia mbili za kutekeleza majosho ya wajibu; njia ya utaratibu wa kuosha mwili hatua kwa hatua (Tartibu) au kwa kuzama majini (Irtimasi). [4] • Muda wa kuoga kwa ajili ya majosho ambayo ni sharti la ibada (kama vile josho la janaba) hutegemea wakati wa ibada husika. Kwa mfano, mtu anayekusudia kufunga ni lazima aoge kabla ya kuchomoza kwa alfajiri; [5] au ikiwa ni kwa ajili ya Sala, basi josho huwa ni wajibu pale tu unapowadia wakati wa kusali sala fulani. [6] Hukumu za Udhu Baada ya Mtu Kujitoharisha na Majosho Mbalimbali Katika fiqhi ya Shia, kumeripotiwa ijmaa [7] isemayo kwamba, josho la janaba linachukua nafasi ya udhu. Aidha kulingana na rai mashuhuri ya wanazuoni wa Kishia, ni kwamba haijuzu kuchukua udhu baada ya kukoga janaba. [8] Ila Sheikh Tusi ameona kuwa ni, mustahabu mtu kutia udhu baada ya josho lake la kujitoharisha na janaba (yaani ni vyema mtu kutia udhu kabla ya Sala baada ya josho la janaba). [9] Na kuna khitilafu miongoni mwa wanazuoni kuhusia na na uwezo wa majosho mingine ya wajibu kuchukua nafasi ya udhu; ila rai mashuhuri inaona kuwa, majosho hayo hayawezi kuchukuwa na fasi ya udhu. [10] Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni wa fiqhi wa karne ya kumi na nne na ya kumi na tano Hijria, miongoni mwao Khui, Sistani pamo na Shubari Zanjani, wanaona kuwa kwa majosho yote ya wajibu yanachukua nafasi ya udhu, isipokuwa josho la istihadha ya wastani.

Utekelezaji wa Josho Moja kwa Niaba ya Majosho Kadhaa Maandiko ya fiqhi yanaelezaa kwamba; iwapo mtu anapaswa kutekeleza majosho kadhaa—iwe ya wajibu, ya sunna, au ya mchanganyiko wa hali zote mbili—kisha akatia nia ya kuyatekeleza kutekeleza josho moja kwa niaba ya majosho hayo, basi josho hilo litahesabiwa kuwa ni josho sahihi na lenye kutosheleza. [11] Kulingana na rai ya wanazuoni walio wengi, hukumu hii inatumika bila kubagua, iwe majosho yake ni ya sunna peke yake, ya wajibu pekee, au ni yenye mchanganyiko wa wajibu na sunna. [12] Tafiti Zenye Mafungamano na Tafiti Hii • Majosho ya Mustahabbu