Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Kudharau Sala

Kutoka wikishia

Kudharau Sala (Istikhfafu al-Salati): ni kutoipa sala nafasi na hadhi yake stahiki. Hali hii inaweza kujitokeza kwa kuacha sala ipite bila kuisali kwa wakati, nakuilipa (qadhā) baadaye, au kwa kutotekeleza kikamilifu wajibu shati zake za msingi. Kuna tofauti ya maoni kuhusu mifano halisi ya tabia hii. Baadhi ya wanazuoni wamehesabu kuchelewesha sala bila udhuru, kutokuwa makini au kukosa khushuuʿ (unyenyekevu wa moyo) kuwa ni miongoni mwa vielelezo vya kukumbwa na tabia hiyo. Hata hivyo, wengine wanaona kuwa mifano hiyo haipatani kikamilifu na maana ya “kudharau sala” kama ilivyotajwa katika Riwaya zinazoambatana na onyo la adhabu ya Mwenye Ezi Mungu. Mafakihi wa Kishia wamelihukumu tendo kudharau sala kuwa ni haramu. Kuna madhara na athari kadhaa zilizotajwa ndani ya riwaya kuhusiana na tabia hii, miongoni mwazo: kunyimwa uombezi wa Ahlul-Bait, kutokubaliwa kwa sala, kupunguziwa umri, kufa katika hali ya fedheha, na kupata adhabu ya kaburi. Umuhimu wa Dhana Turaihi katika kazi yake andishi iitwayo Majma’u al-Bahrain, anaifafanua dhana ya kudharau sala kama ni kitendo cha kuivunjia heshima sala na kuidhalilisha kupitia kitendo cha kukanusha au kuipinga. [1] Hata hivyo, baadhi ya wachunguzi wanaamini kwamba, tafsiri hii ya Turaihi inahusiana na ukanushaji wa nafasi na umuhimu wa sala katika maisha ya kidini, na siyo kukanusha uhalali wa kisheria wa ibada yenyewe. [2] Kuna Riwaya kadhaa zililizokuja kuwataka waumini kutojihusisha na dhambi ya kudharau sala. [3] Aidha tukirudi katika kitabu cha Wasailu al-Shia tutaktana na mlango maalumu kitabuni humo uliokusanya Riwaya hizo. [4] Katika dini ya Kiislamu, Sala imefafanuliwa kama alama kuu ya Uislamu, na kutojali sala kunatafsiriwa kama kutojali sharia nzima. Kwa mtazamo huu, baadhi ya wanazuoni wameeleza kwamba; tahadhari na vitisho vilivyotolewa kuhusiana na kudharau sala vina uhusiano wa moja kwa moja na nafasi ya sala kama kiashirio cha dini. [5] Wanazuoni wa Kishia wote kwa pamoja wamekubaliana kwamba kudharau sala ni haramu. [6] Murtadha Mutahhari amesema; mtu anayepuuza sala anaingia katika orodha ya wale waliotajwa katika Aya isemayo: «قالوا لَمْ نَکُ مِنَ الْمُصَلِّین» “Walisema: Hatukuwa miongoni mwa wanaosali.” [7] Kudhalilisha na kutojali sala humtoa mtu katika nafasi na kundi la wasalihina Siku ya Kiyama. [8] Mifano ya Uachaji Sala Kuna mifano mingi kuhusiana na tabia ya uachaji sala, miongoni mwa mifano muhimu ilitajwa na wanazuoni ni: kusalia kwa qadhaa (kusali kwa mfumo wa kulipa) kutokana na uzembe, [9] kuacha sala bila udhuru wa kisheria, kutotekeleza kwa umakini vipengele vya wajibu katika sala, [10] kutohudhuria sala ya jamaa kwa sababu ya kuiona haina thamani, [11] kuchelewesha sala bila sababu halali na kutoisla katika wakati wake wa mwanzo, [12] kutojali kujifunza hukumu na masharti ya sala, pamoja na kufanya haraka na kutokuwa makini katika kutamka dhikri za sala, kiasi cha kuacha dhikri za rukuu na sajda bila ukamilifu. [13] Baadhi ya watafiti, wakiegemea kwenye vitisho vya Akhera na uharamu wa kitendo hiki vilivyopo ndani ya Riwaya mbalimbali, wanaamini kwamba mifano ya kudharau sala inahusiana tu na vipengele msingi vya wajibu katika sala, na wala haihusishi vipengele vya sunna. [14] Kinyume chake, wengine wanaona kwamba kuna daraja mbalimbali za kudharau sala, na kuacha sunna za sala kupitia watu waliokaribiana na Mwenyezi Mungu huweza kuchukuliwa kama ni moja ya aina za kupuuza sala. [15] Athari za Kudharau Swala Miongoni mwa athari zilizotajwa kuhusiana na kudharau sala ni kama ifuatavyo: • Kutokubaliwa kwa swala. [16] • Kunyimwa uombezi wa Ahlul-Bait: [17] Imenukuliwa kwamba pale Imamu Jafar al-Sadiq (a.s) alipokuwa katika hali ya sakarat al-maut aliwaita jamaa zake na kuwambia: “Uombezi wetu haumfikii yule anayelidharau swala.” [18] Sayyid Ridha Muayyid (aliyefariki 1401 Shamsia), ambaye ni mshairi wa mashairi ya kidini, aliielezea Hadithi hii kwa kwa mtindo wa kishairi akisema: Naisema kutoka kwa Imam Sadiq hadithi hii adhimu, Ili mfuasi wake aiandike kwenye ubao wa moyo wake. Alisema (Imamu Jafar al-Sadiq): Hatafikiwa na uombezi wetu, yule anayelidharau sala na kuliona ni kitu holela. [19] • Madhara yaliyotajwa katika riwaya kuhusiana na jambo hili ni:

Kunyimwa bahati ya kukutana na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kando ya Haudh al-Kauthar (hodhi au chemuchemu ya maji) siku ya Kiyama. [20]

• Kupatwa na tabia au kuandamwa na adhabu kumi na tano, kwa mujibu wa riwaya iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume akimsimulia bibi Fatimah bint Muhammad (a.s). [21] Tabia au adhabu hizo zimeorodheshwa kama ifuatavyo: [22] 1. Kukosa baraka katika umri wake. 2. Kukosa baraka katika mali yake. 3. Kunyimwa nuru usoni mwake. 4. Kutokubaliwa kwa matendo yake. 5. Kutopokelewa dua zake. 6. Kunyimwa dua za watu wema. 7. Kufa katika hali ya fedheha. 8. Kufa njaa. 9. Kufa na kiu, kiasi ya kwamba hata akinywa maji hayamuondolea kiu yake. 10. Kupata giza la kaburi. 11. Kuadhibiwa kaburini mwake. 12. Kuburuzwa kifudifudi siku ya Kiyama mbele ya hadhara ya watu. 13. Kufanyiwa hisabu ngumu siku ya Kiyama. 14. Kuadhibiwa kwa adhabu chungu ya Akhera. 15. Kunyimwa mtazamo wa rehema ya Mwenyezi Mungu.