Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Kitabu cha "Ensane 250 Sale" (Mwanadamu wa Miaka 250)

Kutoka wikishia

Kitabu cha "Ensane 250 Sale" (Mwanadamu wa Miaka 250): ni kazi inayokusanya dondoo za hotuba za Ayatullah Khamenei (Aliyekuwa kiongozi mkuu wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran), kuhusu maisha ya kisiasa ya Maimamu wa Kishia (a.s). Licha ya kuwepo tofauti dhahiri za kizama na kimazingira, ila kitabu hichi kimewatizama Maimamu hawa kama ni mtu mmoja aliyeishi maisha enedelevu ya miaka 250. Maisha ya mwanadamu huyu yalianza tu baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), hadi mwaka wa 260 Hijiria, kipindia ambacho kilirefuka na kufikia miaka 250, huku Maimamu hawa wakiwa kaqtika harakati za kujenga serikali ya Kiislamu. Maudhui ya kitabu hichi yamechaguliwa kwa uangalifu kutoka katika hotuba za Ayatullah Ali Khamenei, aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, zilizotolewa kati ya Mei 1980 na Machi 2011. Muda mfupi baada ya kuchapishwa toleo la kwanza, maudhui hayo yalifanyiwa uhariri na kwa kuyapanga upya katika makundi kadhaa ya kimaudhui kisha kuongezwa sehemu nyingine zilizochopolewa kutoka katika hotuba zake. Hatimaye, mkusanyo huo ulichapishwa upya katika mfumo wa mfululizo wa vitabu unaojulikana kama Mviringo wa Kwanza (Halkaye Avval) na Mviringo wa Tatu (Halka-ye Sevvom). Kitabu "Ensane 250 Sale" (Mwanadamu wa Miaka 250 kimeandikwa kwa lugha ya Kifarsi, na kuchapishaji upya zaidi ya mara themanini na tano. Zaidi ya hayo, kutokana na umaarufu wake, kitabu hichi kimetafsiriwa katika lugha mbalimbali duniani, na hivyo kukifanya kiwe miongoni mwa kazi zinazosomeka katika lugha tauti za kimataifa.

Hadhi na Umuhimu wa Kitabu Kitabu cha "Mwanadamu wa Miaka 250" kinajumuisha mkusanyiko wa hotuba za Ayatullah Khamenei, ambaye alikuwa ni Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mmoja wa marejeo makuu aliyekuwa akirejewa katika masuala ya kisheria (Marja' al-Taqlid) na Washia mbalimbali ulimwenguni. Maudhui ya kitabu hichi yanahusiana na nadharia ya "mwanadamu wa miaka 250", maudhui ambayo inatokana na hotuba za mwanazuoni huyu zilitolewa katika miaka ya kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, hususan wakati wa harakati za mapambano ya wananchi dhidi ya utawala wa Pahlavi. [1] Kutokana na umuhimu wake, kitabu hichi kimechapishwa upya mara kadhaa kwa lugha ya Kiajemi, na hatimaye kutafsiriwa katika lugha zaidi ya kumi ulimwenguni. [2] Hali kadhalika, nchini Iran kuna utaratibu madhubuti wa kuendesha kozi maalumu za mafunzo [3] kupitia mashindano [4] mbalimbali yanayozingatia maudhui ya kazi hii. Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Hassan Ali al-Imad, ambaye ni Katibu Mkuu wa harakati ya Tandhi Mustaqbal al-’Adalah nchini Yemen, kitabu hiki kimeleta mageuzi makubwa katika mtazamo na fikra za Washia wa Yemen kuhusu dhana ya jihadi na mapambano nchini hyumo. [5] Chimbuko la Anwani ya Jina la Kitabu Anwani ya kitabu "Mwanadamu wa Miaka 250" inarejea kipindi cha karne mbili na nusu cha uongozi wa Maimamu wa Kishia. Kipindi ambacho ni kuanzia wakati wa kifo cha bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) kilichojiri mwaka wa 11 Hijiria, hadi kuanza kwa kipindi cha Ghaiba Ndogo ya mwaka wa 260 Hijiria. Katika muktadha huu, Ayatullah Khamenei amekielezea kipindi hicho kwa njia ya sitiari iliyojengwa katika sura ya maisha ya mwanadamu mmoja aliyeishi umri wa miaka 250. [6] Maudhui na Mwelekeo wa Kitabu Kwa mujibu wa utangulizi wa kitabu cha "Mwanadamu wa Miaka 250”, kazi hii inaonekana kujikita katika kuelezea misingi mikuu kadhaa ya kifikra kuhusiana na Maimamu wa Kishia: • Kwanza kabisa, kitabu hichi kinabainisha kuwa Maimamu wa Kishia hawakujifunga tu katika mapambano ya kielimu, kiitikadi, na kiimani; badala yake, mnyororo wa maisha yao yote endelevu ulikuwa na mwelekeo thabiti wa kisiasa. [7] • Pili, Maimamu watukufu (Maasumina) wanatazamwa kuwa na shakhsia, mwelekeo, shabaha, na nia moja iliyoungana na iso na utengano kati yao. Hivyo basi, kuanzia wakati wa kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w) hadi mwaka wa 260 Hijiria, lengo lao kuu lilikuwa ni kuasisi serikali ya Kiislamu. [8] • Tatu, kitabu hichi kinafafanua kuwa Maimamu hawa hawakukumbatia mapambano ya kutumia silaha; ingawaje pia hawakuonekana kuwashutumu moja kwa moja wale waliotumia nguvu za kijeshi, ila katu wao wenyewe hawakushiriki katika harakati hizo. [9] Muundo wa Kitabu na Mpangilio wa Sura Zake Kitabu Mwanadamu wa Miaka 250 kimeundwa kwa muundo unaojumuisha dibaji fupi, utangulizi, na sura kumi na saba zinazofuatana kwa mtiririko ufuatao. • Sura ya Kwanza: Bwana Mtume (s.a.w.w.) • Sura ya Pili: Uimamu • Sura ya Tatu: Amir al-Muuminina (a.s) • Sura ya Nne: Bibi Fatima az-Zahra (a.s) • Sura ya Tano: Imamu Hassan (a.s) • Sura ya Sita: Imamu Hussan (a.s) • Sura ya Saba: Harakati za Bibi Zainab Kubra na Wajumbe wa Karbala • Sura ya Nane: Mazingira ya Kijamii na Kisiasa Baada ya Tukio la Karbala • Sura ya Tisa: Imamu Sajjad (a.s) • Sura ya Kumi: Imamu Baqir (a.s) — Kipindi cha Ujenzi wa Fikra na Taasisi • Sura ya Kumi na Moja: Mwisho wa Utawala wa Bani Umayyah na Uimamu wa Imamu Sadiq (a.s.) • Sura ya Kumi na Mbili: Imamu Sadiq (a.s) • Sura ya Kumi na Tatu: Mtandao wa Siri • Sura ya Kumi na Nne: Imamu Kazim (a.s) • Sura ya Kumi na Tano: Imamu Ridha (a.s) • Sura ya Kumi na Sita: Imamu Jawad (a.s), Imamu Hadi (a.s.), na Imamu Askari (a.s) • Sura ya Kumi na Saba: Hatima ya Harakati ya “Mwanadamu wa Miaka 250”

Uchapishaji na Uenezaji wa Kitabu Kimataifa Kitabu cha "Mwanadamu wa Miaka 250" kilizinduliwa rasmi mnamo mwaka 2011 (1390 SH) kupitia Kituo cha Uchapishaji cha Sahba, kikiwa na jumla ya kurasa 375. [10] Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, kazi hii ilikuwa imeshafanyiwa uchapishaji upya kwa mara 85. [12]

Kutokana na umuhimu wa maudhui yake, kitabu hichi kimetafsiriwa katika lugha mbalimbali duniani zikiwemo: Kiarabu, Kiingereza, Kiurdu, Kiazeri, Kikurdi, Kituruki cha Istanbul, Kihindi, Kisindi, Kijerumani, Kithailandi, Kihausa, na Kifaransa. [13] Aidha, kitabu hichi kimefasiriwa Kiarabu kwa jina la "Ahl al-Bayt: Ensan bi-Umri 250 Aam" kazi iliyofanywa na Ahmad Sami Wahbi, na kutolewa mnasmo mwaka 1436 Hijiria kupitia taasisi ya Dar al-Wala huko Beirut ikiwa na kurasa 398. [14] Mfululizo wa Matoleo Mablimbali Baada ya kuzinduliwa kwa kitabu cha "Mwanadamu wa Miaka 250", Kituo cha Uchapishaji cha Sahba kilikusanya zaidi ya hotuba 600 za Ayatullah Khamenei ili kuandaa mfululizo wa vitabu vitatu unaojulikana kama "Halaqaat" au Mtirirko na mviringo wa kitabu cha Mwanadamu wa Miaka 250. Lengo kuu la jitihada hii ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila kada ya wasomaji inapata maudhui yanayoendana na mahitaji yake, ambapo toleo la kwanza lilitengwa mahususi kwa ajili ya vijana, huku matoleo mengine mawili yakielekezwa kwa umma unaopenda kufuatilia sira za Maimamu. [15] 1. Mviringo wa Kwanza ulizingatia matini ya awali ya mwaka 2011 na kuratibiwa kwa ajili ya vijana kupitia matumizi ya mifano ya picha pamoja na michoro. [16] 2. Mviringo wa Pili unalenga wasomaji wa kawaida wanaovutiwa na fikra pamoja na mwenendo wa Ahlul-Bayt. [17] 3. Mviringo wa Tatu umesanifiwa katika kurasa 900 kwa ajili ya watafiti na wasomi wanaotaka kupata uchambuzi wa kina wa maisha ya Maimamu. [18] Toleo hili lilijumuisha hotuba 260 na kutoa ufafanuzi wenye uchambuzi mpana zaidi juu ya matukio ya kihistoria. [19] Sura kuu za Mviringo wa Tatu zinajumuisha: • Kipindi cha ukimya na ushirikiano kuanzia kifo cha Mtume hadi kuuawa kwa Uthman. • Kipindi cha mamlaka iliyoambatana na kudhulumiwa; harakati fupi za ujenzi kuanzia amani ya Imam Hasan hadi kuuawa kishahidi kwa Imam Hussain • Kipindi cha ujenzi wa kifikra hadi kufikia ushahidi wa Imam Hasan al-Askari. [19] Mada na Rejea Zinazofungamana na Kazi Hii: • Kiongozi Mkweli (Kitabu) • Muhtasari Mkuu wa Fikra za Kiislamu Katika Qur'ani