Mkopo:Kaburi
Kaburi: Neno kaburi kilugha na kiistilahi hufasiliwa na kutambulika kama mahali pa mazishi ya mwanadamu, likiwa na sifa na hukumu mahususi za kifikiri. Miongoni mwa sifa za kiufundi (adabu) zilizopendekezwa, ni pamoja na kaburi kuwa na muundo wa mstatili (pembe nne), usawa wa juu ulio tambarare, na mfumo wa tuta lenye kimo cha vidole vinne juu ya ardhi. Vigezo hivi vya kisheria vinalenga pia uimara wa kimuundo wa kaburi ili kuzuia mmomonyoko au uharibifu wa haraka wa eneo hilo la makazi ya maiti. Wanazuoni wa Kiislamu, wakitegemea mafundisho ya Qur'ani pamoja na Hadithi mbalimbali, wanasisitiza kuwa ziara ya makaburi ni tendo la kheri linalohimizwa (linalopendekezwa). Pia wanazuoni hao, wamebainisha kuwa ni haramu kufukua kaburi la Muislamu kiasi cha kuubainika na kudhihiri mwili wa marehemu. Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, kitendo hicho kinaruhusiwa tu pindi kunapokuwa na dharura maalumu inayokubalika kisheria.
Ufafanuzi wa Dhana na Umuhimu wa Kaburi Kitaaluma, "kaburi" linatambuliwa kama mahali pa hifadhi ya mwisho ya mwanadamu. [1] Umuhimu wa kimaandiko wa dhana hii unathibitishwa na kuwepo kwa milango mahususi ndani ya makusanyo makuu ya Hadithi. Kwa mfano moja ya rejea muhimu za Hadithi ya Allamah Majlisi, ijulikanayo kwa jina la Bihar al-Anwar imeorodhesha Hadithi 128 zinazofafanua mazingira na kanuni za kaburi. [2] Vilevile, tukirudi kwenye fatwa za wanazuoni mbalimbali, tutakuta adabu (etiquettes) mbalimbali zinazohusiana na utaratibu wa kisheria wa makaburi. [3] Kanuni na Itifaki za Kisheria Kuhusiana na Muundo wa Kaburi Katika vitabu vya fikihi kuna miongozo na mapendekezo mbalimbali kuhusiana na namna ya ujenzi wa kaburi. Miongoni mwa mambo yanayopendekezwa katika ujenzi wa kaburi, ni kwamba kaburi hilo lijengwe kwa umbile la pembe nne, [4] liwe tambarare, [5] na liinuliwe kiasi cha vidole vinne kutoka juu ya mgongo wa ardhi. [6] Urefu wa kutokea ndani ya kaburi hadi juu, unapaswa kulingana na kimo cha mtu wa wastani au kufikia hadi mabegani, hii kwa ajili ya kuhakikisha uhifadhi wa mwili wa marehemu. [7] Aidha, linapswa kujenga kwa ujenzi imara ili liweze kudumu kwa muda mrefu, [8] na jina la marehemu linatakiwa kuwekwa upande wa kichwani mwake kwa ajili ya utambulisho wa maiti huyo. [9] Vilevile, baadhi ya mafaqihi wanashauri waumini kujiandalia makaburi yao mapema kabla dya kufa kwao, kisha waingie ndani yake na wasome Qur’ani huku wakiwa ndani ya kaburi hilo. Aidha miongoni mwa mambo yanayopendekezwa ni kutoa ardhi kwa ajili ya kuzika waumini ndani yake. [10] Uchambuzi wa Kifikhi na Kiitikadi wa Maeneo ya Makaburi Makala asili: Mava Katika utamaduni wa Waislamu, maeneo ya makaburi yanapewa heshima kubwa ndani ya jamii mbalimbali. [11] Pia ni jambo lililozoeleka kwa jamii kuzuru maeneo haya mara kwa mara kwa ajili ya kuwaidhika na kupata ukumbusho juu ya mauti pamoja na kuwakumbuka marehemu waliotangulia. [12] Maandiko ya Kiislamu yameainisha hukumu na adabu maalumu za kuzingatiwa katika maeneo haya. Miongoni mwa mambo yanayozingatiwa katika maeneo hayo ni pamoja na kutoa salamu kwa waliofariki, [13] kudumisha usafi kwa ajili ya heshima ya eneo hilo. [14] Aidha, sheria ya Kiislamu inawataka Waislamu kuhakikisha kwamba wasiokuwa Wailamu hawazikwi katika makaburi ya Waislamu. [15] Mwongozo wa Kisheria kuhusu Ziyara ya Makaburi Makala asili: Kuzuru makaburi Wanazuoni wa Kiislamu huyatambua maandiko ya Qur’ani na Hadithi kuwa ndiyo msingi asili na ulio wazi wenye kuhimiza watu kuzuru makaburi. Wanazuoni hao wametaja fadhila na kheri kadhaa zinazotokana amali hii, na wakisisitiza zaidi kuzuru makaburi ya mitume na waja wema, hii ni ktokana na fadhila walizonzo Mitume pamoja na watu wema. [16] Hata hivyo, Pana hitilafu za kimitazomo kati ya Waislamu wa madhehebu mbalimbali na Mawahabi kuhusu uhalali wa kuzuru makaburi. Kulingana na mawazo ya Kiwahabi, ni haramu kwa Muislamu kwenda kuzuru makaburi. [17] Pia kuna khitilafu miongoni mwa wanazuoni wa Kishia kuhusiana na ushiriki wa wanawake, katika amali ya kuzuru makaburi. Hata hivyo mwelekeo wa mafakihi wengi wa Kishia unasisitiza kuwa ziyara hiyo ni jambo la heri (mustahabb) kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. [18] Ama kwa misingi ya kifikhi ya Kisunni, fatwa iliyo na umashuhuri zaidi ni ile inayokataza na kusema kuwa ni makruhu kwa wanawake kuhudhuria makaburini. [19] Sheria na Hukumu Kuhusiana na Ufukuaji wa Kaburi (Nabshu-al-qubur) Mada asili: Ufukuzi wa Makaburi (Nabshu-al-qubur) Kitaaluma istilahi ya "Nabshu-alqubur" inarejelea uharibifu au uchimbuzi (ufukuaji) wa kaburi unaopelekea kuanikwa kwa mabaki ya mwili wa binadamu. [20] Kuna ijmai (mwafaka) kati ya wanazuoni wa kifikhi wa Kishia [21] na Kisunni [22] juu ya uharamu wa kitendo hichi kabla ya mwili wa marehemu kuharibika na kusagika. Hata hivyo, vikiushi vya kisheria (legal exceptions) vinaruhusiwa chini ya mwavuli wa kuwepo kwa "ulazima wa kisharia" unaoruhusu suala hilo. Ruhusa hii inajumuisha masuala ya "Haqq-al-Nas" (haki za watu), mfano wa hili ni pale ambapo mati fulani atapokuwa amezikwa katika ardhi ya dhuluma (ghasbi), jambo linalotoa uhalali wa kisheria wa kulifukua kaburi hilo ili kurejesha haki ya mmiliki wa ardhi hiyo. [23]