Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Haki ya mgawo wa zamu baina ya wake

Kutoka wikishia

Haki ya mgawo wa zamu baina ya wake: Katika fiqhi ya Kiislamu, haki ya mgawo wa zamu (حقّ قَسْم), ni haki maalumu inayorejelea wajibu wa kisheria uliopo juu ya shingo ya mwanamme mwenye wake zaidi ya mmoja. Kulingana na sheria za Kiislamu, mwnamme wa aina kama hii, huwajibika kugawa nyusiku zake kwa usawa kabisa baina ya wake zake. Wajibu huu unalenga kudumisha uadilifu na haki katika maisha ya ndoa. Hivyo basi, mume mwenye wake wanne hulazimika kutumia kila usiku akiwa pamoja na mmoja wa wake zake, huku akizingatia mpangilio ulio sawa, bila kumfanya yeyote kati yao kujihisi ametengwa au kunyimwa haki yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya wanazuoni wa fiqhi, hakuna khitifafu baina ya wanazuoni mbai mbali juu ya ulazima (wajibu) wa utimizaji wa Haqq Al-Qasm (Haki ya Mgawo wa Zamu za Nyusiku). Uchambuzi wa kifiqhi unaeleza kwamba; haki hii hurejelea hali ya uwepo na muingiliano wa mume katika makazi ya kila mmoja kati ya wake zake katika nyakati za usiku, na si lazima ijumuishe tendo la ndoa ndani yake. Wajibu huu unawakilisha mojawapo ya haki za msingi na za kisheria za mke katika maisha ya ndoa, wajibu huu umeanzishwa kwa madhumuni maalumu kati ya mke na mume, ikiwa ni pamoja na; kuhakikisha uadilifu miongoni mwa wake, kuimarisha mahusiano ya kimahaba, na kujenga utulivu wa kifamilia.

Ufafanuzi wa Haqq al-Qasm na Nafasi Yake katika Fiqhi

Kama ilivyoainishwa katika Fiqhi ya Kishia, kifungu cha Haqq Qasm (Haki ya Mgawo wa Nyusiku) kinahusiana na wajibu wa mume katika kugawa kwa uwiano (usawa) nyakati zake za usiku miongoni mwa wake zake. [1] Kulingana na uchambuzi uliomo katka vyanzo vya Fiqhi ya Imamiyya, haki hii inatambulika kama haki ya kisheria ya mke ndani ya kifungo cha maisha ya ndoa, ikiwa na lengo la kusimamia uadilifu, kusawazisha usawa, na kujenga utulivu katika muundo wa kifamilia. [2] Hivyo basi; iwapo mume ataoa wake zaidi ya mmoja, anatawajibika kisheria kugawa nyusiku zake kwa usawa bila kubagua. [3] Haki hii linachukuliwa kama ni moja ya viunzi muhimu vya haki za kifamilia, hasa haki za kinamama. [4] Suala la haki ya mgawo wa zamu kwa wanawake, ni miongoni mwa masuala yaliofanyiwa uchambuzi wa kina kabisa katika Fiqhi ya Shia, kiasi ya kwamba mada yake inaonekana kuchambuliwa na kuwekewa milango maalumu ndani vyanzo vya Fiqhi mbli mbali. [5] Wanazuoni wote wa Kishia wamekubaliana (wana ijma'a) juu ya ulazima wa haki hiii. [6]

Falsafa ya Kutungwa kwa Sheria ya Haki ya Ugawaji wa Nyusiku

Kama alivyosema Shahid Thani, mtaalamu wa fiqhi wa karne ya kumi Hijria; haki ya mgawo wa usiku (Haqq Qasm) imejengwa na kusimama juu ya msingi wa dhana ya uadilifu, ikitegemea ithibati madhubuti za kisheria zinazopatikana katika vyanzo vya Riwaya mbali mbali pamoja na mafundisho yaliyomo ndani ya Aya ya 19 ya Suratu al-Nisa. [7] Aidha mwnazuoni huyo anaeleza kwamba; dhamira ya kuanzishwa kwa haki hii ni kuimarisha muungano na kuzuia mizozo miongoni mwa wake waliopo chini ya himaya ya mume mmoja. [8] Hali kadhalika, Sahib al-Jawahir, mwanazuoni wa fiqhi wa karne ya kumi na tatu Hijria, anaeleza kwamba; lengo kuu la sheria hii ni kuimarisha husnu al-mu ‘asharah (mahusiano mema) na kusimamia usawa (uadilifu) baina ya wanandoa. [9] Pia uchambuzi wa wanazuoni wa sasa unahitimisha kwa kusema kwamba; lengo la kuasisiwa hukumu hii ni juhudi maalumu za kuinua hisia na mapenzi ya kweli kati ya wanandoa, ili kusisitiza uthabiti wa mfumo wa kifamilia ndani ya jamii ya Kiislamu. [10]

Kuvuliwa kwa Mtume (S.A.W.W) na Hukumu ya Mgawo wa Zamu

Kulingana na taaluma ya sheria za Kiislamu, Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipewa ruhusa ya kipekee ya kuondolewa katika utekelezaji wa haki ya mgawo wa nyusiku (حقّ قسم) zake baina ya wakeze, [11] hukumu ambayo imeifafanua ndani ya Qur’ani kupitia Aya ya 51 ya Suratu al-Ahzab. [12] Ingawa bwana Mtume (s.a.w.w) alipewa haki hii maalumu ya kuwa na hiari katika maamuzi ya haki hii, ila wataalamu wa fani ya tafsiri wanabainisha wakisema kwamba; Mtume (s.a.w.w) alijitahidi kwa kiasi kikubwa katika kudumisha usawa na haki ya ugawaji muda wake kati ya wake zake. Na aliendelea kufanya hivyo isipokuwa katika hali maalum ambazo zilimruhusu kuchukuwa maamuzi tofauti juu ya jambo hilo. [13] Riwaya kadhaa zinaonyesha kwamba; hata katika nyakati za maradhi, bado bwana Mtume (s.a.w.w) alionekana kuzingatia uadilifu huu. [14] Moja ya Hadithi maarufu inamnukuu bwana Mtume (s.a.w.w) akisema: “Ee Mwenye Ezi Mungu, huu ndio mgao wangu ulioko katika uweza wangu, na Wewe ni Mjuzi zaidi juu ya yale yaliyopo nje ya uwezo wangu”. Mwanazuoni ajulikanaye kwa umaarufu wa Sahib al-Jawāhir akitoa ufafanuzi juu ya Hadithi hii anasema kwamba; lile lilikusudia na bwana Mtume (s.a.w.w) ambalo lilikuwa nje ya uwezo wake, ni upendo wa moyoni pamoja na hisia zisizoweza kudhibitiwa kirahisi. [15]

Namna ya Ugawaji wa Zamu za Nyusiku

Kulingana na fatwa za wanazuoni wa fiqhi, mgawanyo wa haki ya nyusiku katika ndoa, ni wajibu maalumu unaomuajibikia mwanamme mwenye zaidi ya mke mmoja. [16] Sharia inaeleza kwamba; endapo mume atakuwa ameoa zaidi ya wake wanne, basi atawajibika kizigawa nyusiku zake kwa mmoja kati ya wake zake, kwa mpangilio ambao kila mmoja akatukuwa akipata haki sawa. Na kila uishapo mzunguko huo, yabidi aanze tena upya mzunguko wake huo bila ya kumdhulu mtu fulani kati yao. Lazkini iwapo mume huyo atakuwa na wake wawili, atatakiwa kutenga nyusiku mbili kwa ajili ya wake zake, na nyusiku mbili kwa ajili ya kazi zake binafsi. Na iwapo atakuwa na wake watatu, basi atatakiwa kutumia nyusiku tatu kwa ajili ya wake zake, huku usiku wa nne ukiwa ni kwa ajili yake mwenyewe. [17]

Ugawaji wa Nyusiku kwa Mume Mwenye Mke Mmoja


Kuna nadharia mbili tofauti miongoni mwa wanazuoni wa fiqhi ya Kishia kuhusiana na hukumu ya mgawanyo na namna ya matumizi ya nyusiku kwa mwanaume mwenye mke mmoja. Baadhi ya wanazuoni wanasema kwamba; hakuna tofauti kuhusiana na hkumu hii, hivyo basi mwanamke awe ni mke pekee au mmoja ya wake walioko chini ya himaya ya mume mmoja, atakuwa na haki kamili ya kuwa na zamu katika mgawanyo wa nysiku za mumewe, kwa hiyo, mume anatakiwa angalau usiku mmoja kati ya nyusiku nne kulala na mmoja wa wake zake, bila ya kutofautisha baina ya yule mwenye mke mmoja au mwenye wake wengi. [18] Hata hivyo, kundi jingine la wanazuoni linaona kwamba haki hiyo haihusiani na ndoa ya mke mmoja, kwani kanuni hiyo imewekwa mahsusi kwa mume mwenye zaidi ya mke mmoja. Miongoni mwa wanaounga mkono mtazamo huu ni pamoja na; Shahid Thani, Sahib al-Jawahir, al-Muhaqqiq al-Sabzawari, na Imamu Khomeinī. [19]

Hukumu za Haki ya Mgawo wa Nyusiku

Kwa mujibu wa maandiko ya fiqhi, haki ya mgawo wa usiku ni utaratibu wa kisheria unaolenga kudhibiti usawa wa ndoa katika jamii ya Kiislamu. Wataalamu wa fiqhi wakifafanua hukumu hii katika vitabu vyao vya fiqhi wanasema kwamba:

1-    endapo mke atakuwa katika hali ya uasi au mume yuko safarini.  [20]

2-    Utekelezaji wa huku hii unahusiana na kipindi cha usiku peke yake. [21]

3-    Haki hii ni mahsusi kwa ndoa ya kudumu na wala haijumuishi ndoa ya muda, bila kujali idadi ya wake walipo ndani ya ndoa hiyo ya muda. [22]

4-    Mwanamke anaweza kuachia na kusamehe haki hiyo kwa ridhaa yake mwenyewe, [23] pia ana haki ya kuirejesha haki hiyo iwapo atataka ataka kufanya katika kipindi kijacho. [24]

5-    Ni muhimu kufahamu kuwa haki hii inahusu kulala pamoja tu, na wala hailazimiani na tendo la ndoa. [25]