Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Hadithi ya "As’habi ka al-Nujum"

Kutoka wikishia

Hadithi ya "As’habi ka al-Nujum" (Mashaba Wangu ni Kama Nyota): ambayo pia inajulikana kama Hadithi ya "Iqtida na Ihtida" (yaani, Ufuasi na Uongofu), ni maja wapo ya Hadithi inayohusishwa na bwana Mtume (s.a.w.w). Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa madhehebu ya Sunni, Hadithi hii ina umuhimu mkubwa na hutumiwa kama msingi wa hoja mbili kuu. Kwanza, ulazima wa kuwafuata Masahaba (wafuasi wa bwana Mtume) (s.a.w.w) bila kuweka shaka au masharti maalumu. Pili, hutumika katika kuthibitisha dhana isemayo kwamba; Masahaba wote ni waadilifu, na walikuwa ni watu wenye kuaminika katika tabia na imani zao Uhalisia wa Hadithi hii ni wenye kutiliwa shaka na wanazuoni wa pande zote mbili. Wanazuoni wa Kishia, pamoja na baadhi ya wataalamu wa Kisunni, wanaichukulia Riwaya hii kuwa ni dhaifu na isiyoaminika, huku wengi wakiamini kuwa ni Riwaya bandia iliyo tungwa na kuenezwa kwa malengo fulani. Kwa mtazamo wa Kishia, hoja kuu ya kuipinga na kuikataa Riwaya hii, inajikita katika misingi ya kimantiki na kiimani. Wanasema kwamba kuikubali Hadithi hii ni sawa na kukiri kuwa Masahaba wote, bila ubaguzi, walikuwa ni watu watoharifu wasio na sifa ya kukosea. Hata hivyo, dhana ambayo inapingana waziwazi na rekodi za kihistoria zinazoonesha kuwepo kwa tofauti kubwa za kimtazamo na hata migogoro mikali iliyopita baina yao. Zaidi ya hayo, Hadithi hii inakinzana moja kwa moja na vyanzo vikuu vya sheria ya Kiislamu. Kuna Aya kadhaa katika Qur'ani pamoja na Hadithi nyingine zilizo sahihi zenye kukosoa waziwazi matendo ya baadhi ya Masahaba. Kwa hivyo, haiwezekani kukubalia na Hadithi hii inayowasifu wote kwa ujumla, huku kukiwa na maandiko mengine yanayowakosoa baadhi yao. Kutokana na changamoto hizi, kumekuwa na kazi nyingi za kitaalamu zilizoandikwa na wanazuoni wa Kishia na Kisunni kwa lengo la kuichambua, kuikosoa na kubainisha udhaifu wake. Wanazuoni wa Kishia wana maoni mbadala kuhusiana na tafsiri ya Hadithi hii. Kwa maoni yao, hata kama Hadithi hii ingekuwa ni sahihi, ila bado maana yake isingeweza kuwahukumu Masahaba wote kwa sifa ya uadilifu. Wao wanasema kwamba, ili Hadithi iendane na mantiki kamili inayokubalika kiakili na kisheria, utabidi kuwahusu Masahaba wachache tu ambao walibaki imara na waaminifu katika kufuata njia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), huku wakiendelea na msimamo huo hata baada ya kifo chake, bila kubadilika au kupotoka. Mtazamo huu unapata nguvu zaidi kutokana na kuwepo kwa nakala mbili tofauti za Hadithi hii katika vyanzo vya Kishia. Katika nakala hizo, Hadithi imekuja na ufafanuzi wa ziada unaowataja watu wa nyumba ya bwana Mtume (s.a.w.w), yaani Ahlul Bayt (a.s), kama ni mfano halisi wa wale "Masahaba" imara ambao ndio chanzo hakika cha mwongozo. Kwa tafsiri hii, Hadithi inakuwa na maana maalum, ikielekeza umma kwa kundi maalum la watu ambao uongofu wao umehakikishwa kisheria. Hati ya Kuthibitisha Uadilifu wa Masahaba Riwaya isemayo “Ashabi ka'l-Nujum” (Masahaba Wangu ni Kama Nyota), inayojulikana pia kwa jina la Hadithi ya Al-Ihtida wa Al-Iqtida (Ufuasi na Uongofu), ni moja wapo ya Hadithi inayohusishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w). Nayo ni ile Hadithi inayowapa Masahaba nafasi maalumu na kuwatambua kama ni vyanzo vya uongofu kwa umma wa KIslamu. [1] Uchunguzi wa mnyororo (mlolongo) wa wapokezi (isnad) wa Hadithi hii uliopo katika vyanzo vya Ahlus-Sunnah, unaonesha kuwa mpokezi wa awali aliyeinkuu Hadithi hii ni Ibnu Humaid [2] (aliyefariki 290 AH). [3] Inaaminika kwamba Hadithi hii hutumika kama msingi mkuu kwa ajili ya kuthibitisha baadhi ya itikadi muhimu katika madhehebu ya Ahl al-Sunnah. Kwa mujibu wa mtazamo huu, Riwaya hii ndio nguzi iliyotumika katika ujenzi wa kujenga kanuni kadhaa ndani ya madhehebu hayo, ikiwemo ulazima wa kuwafuata Masahaba bila kuweka masharti maalumu, [4] pamoja na kuwakubali (wote kwa pamoja kama vyanzo vya mamlaka ya kidini na mifano bora ya kuigwa. [5] Aidha, Hadithi hii inatumika kama ushahidi wa kuthibitisha utakatifu wa Masahaba wote, [6] sifa zao njema, [7] ubora wao dhidi ya watu wengine wote (isipokuwa Mitume), [8] na uadilifu wao wa jumla. [9] Hata hivyo, kuna tafsiri mbadala iliyotolewa na baadhi ya wanazuoni fulani. Wao wanasema kuwa; Lengo la Hadithi hii ni kuthibitisha uaminifu wa Masahaba katika jukumu lao la kupokea na kufikisha habari wanazozinukuu kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w). Hii inamaanisha kwamba; Waislamu wanapaswa kukubali yale waliyoyasimulia na Masahab a hao, lakini haimaanishi kuwepo kwa ulazima wa kufuata maoni yao binafsi katika nyanja za kisheria au fatwa zao, ambazo ni matokeo ya ijitihadi zao wenyewe. [10]

Mtazamo wa Kishia Kuhusiana na Riwaya ya "Ashabi ka Al-Nujum" Wanazuoni wa Kishia wanaihisabu Riwaya hii kuwa ni Hadithi Mawdhuu (ya kughushi au Hadithi bandia). Ili kuthibitisha hilo, wanazuoni hawa wametumia vigezo maalumu vya kitaaluma vya sayansi ya hadithi ('ilmu al-hadith). Mifongoni mwa sababu za kutokubaliana na Hadithi hiyo ni kama ifuatavyo: 1- Udhaifu wa Isnad (Dha'afu Al-Sanad): Mlolongo wa wapokezi wake una kasoro zinazoufanya usiwe wa kuaminika. 2- Mgongano Wake na Vyanzo vya Kihistoria: Maudhui yake (matini) inapingana na data za kihistoria (ta'arikh) zilizothibitishwa ndani ya vitabu mbali mbali, na pia yanakinzana na dalili za kiakili (Al-Adillatu Al-Aqliyya) na dalili nyengine andishi zilinukuliwa (adillah naqliyyah), ambazo ni zenye nguvu zaidi kuliko Hadithi hiyo, kama vile Aya za Qur'ani na Hadithi sahihi. [11] Wanazuoni hawa wanaendelea kusema kwamba; hata kama kinadharia tutajaalia kwamba hadithi hii ni sahihi, pia bado walengwa wake hatoweza kuwa ni Masahaba wote kwa ujumla. Bali ni lazima wakusudiwa wake wawe ni watu (Masahaba) maalum ambao hawakubadilika baada ya Mtume (s.a.w.w). Wao wanabainisha kwamba; watu waliobaki bila ya kubadika, ni Imamu Ali (a.s), Imamu Hassan (a.s), pamoja na Imamu Hussein (a.s.), ambao hadhi yao imethibitishwa katika vyanzo vingine mbali mbali. [12]

Uchambuzi Linganishi wa Matini ya Hadithi Ndani ya Vyanzo vya Kishia na Kisunni Ili kuthibitisha uhalali wa Hadithi ya Ihtida wa Iqtida (Ufuasi na Uongofu), ilibidi kupite uchunguzi maalumu wa kifilolojia kwajili ya kuchunguza mapokezi mbali mbali ya Hadithi hii ndani ya vyanzo vya Kisunni. Mapokezi makuu matatu ya Hatidhi hii yamenukuliwa katika vyanzo mbali mbali vya Kisunni kupitia matini zifuatazo: • Nukuu ya Kwanza: «إنّما اصحابی کالنجوم بأَیهم اقتَدَیتُم اهتَدَیتم» [13] (Tafsiri yake: Hakika Maswahaba wangu ni kama nyota; yeyote yule mtakayemfuata miongoni mwao, mtakuwa mmeongoka). Hapa, kitenzi *اقتَدَیتُم* kinatoa dhana ya kuiga na kufuata mwenendo wao. • Nukuu ya Pili: «إنَّ أصحابی بِمَنزِلَةِ النُجومِ فِی السماء، فَأَیما أَخَذتُم بِه اِهْتَدَیتُم» [14] (Tafsiri yake: Hakika hadhi ya Maswahaba wangu ni sawa na hadhi ya nyota zilizo angani, yeyote yule mtakayeshikamana na mafundisho yake mtakuwa mmeongoka, au mtaongoka). Kitenzi أَخَذتُم hapa kinawasilisha dhana ya kupokea na kukubali mafundisho ya Sahaba yeyote yule kati yao. • Nukuu ya Tatu: «مَثَلُ أَصحابی مَثَلُ النُجوم، مَن اقْتَدی بِشَیءٍ مِنها اِهتَدی» (Tafsiri yake: Mfano wa Maswahaba wangu ni kama nyota, yeyote atakayeiga (atakayefuata) kitu fulani kutoka kwao, ataongoka). Yasemakana kwamba, nukuu ya tatu ndiyo ndiyo inayotajwa kwa nukuu nyingi zaidi miongoni mwa matini mbali mbali za Hadithi hii. [16] Ingawaje Hadithi hii imenukuliwa kwa matini mbali mbali mbali, ila jambo hilo si lenye kudhuru madhumuni na malengo yaliomo ndani yake. [17] Kutambulishwa kwa Ahlul-Bait Kama Kigezo cha Maswahaba Katika Masimulizi ya Kishia Pia Hadithi hii maarufu ni yenye kupatikana ndani ya vyanzo mbali mbali vya Hadithi vya upande wa madhehebu ya Shia, ila mapokezi haya ni yenye kutafautiana na yale yalioko ndani ya vyanzo vya Kisunni, katika kubainisha na kuelezea ni akina nani hasa wanaokusudiwa katika n dani ya kauli hizi mbali mbali zinazohusishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w). Moja ya mapokezi haya muhimu linapatikana katika kitabu kiitwacho Basair al-Darajat, kilichoandikwa na mwanazuoni mashuhuri, Muhammad bin Hassan al-Saffar, aliyeaga dunia mwaka 290 Hijria.

• Muhammad ibn Hasan al-Saffar katika kitabu chake hicho, ananukuu akisema kwamba; baada ya bwana Mtume wa (s.a.w.w), kutilia mkazo na kusisitiza juu ya umuhimu wa kushikamana na Qur'ani pamoja na Sunnah zake (s.a.w.w) kama nguzo na msingi wa Usilamu, pia alijumuisha kauli za Masahaba zake kama ni kigezo chengine cha tatu muhimu katika utendaji wa amali mbali mbali ndani ya Uislamu. Alifafanua akisema kwamba; Masahaba zake wanatumika kama vyanzo vya nuru na uongozi, sawa na nyota zenye nafasi ya kuwaongozi waishiwo aridhini. Pale alipohojiwa kuhusu utambulisho kamili wa Maswahaba hawa, majibu yake yalikuwa ni bayana na yenye uzito muhimu wa kielimu, katika jawabu yake alisema: 'Wao ni Ahlul-Bait zangu.' [18] • Aidha, Sheikh Saduq, ambaye ni mwanazuoni mashuhuri wa Kishia aliyeaga dunia mwaka 381 Hijria, ananukuu simulizi muhimu kuhusu mjadala wa Hadithi ya "Masahaba kama nyota." Simulizi hii ameinukuu ndani ya kitabu chake maarufu kiitwacho Uyun Akhbar al-Ridha. Katika simulizi hii, Imam Ridha (a.s), ambaye ni Imamu wa nane katika mlolongo wa Maimamu wa Kishia, aliulizwa kuhusiana na usahihi na maana halisi ya Hadithi hiyo. Badala ya kuikubali au kuikataa moja kwa moja, Imam Ridha alitoa ufafanuzi wenye masharti juu ya dhana ya Sahaba. Katika maelezo hayo alisema kwamba; neno "Masahaba" katika muktadha wa kuwa viongozi wa kuigwa kama nyota, linawahusu tu wale wafuasi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambao hawakubadilika wala hawakugeuza mwenendo wao baada ya kifo chake. [19] Hoja ya Kuwahusisha Ahlul-Bait Pekee na Hadithi ya Nyota Kutokana na mapokezi yaliyotangulia, hasa yale yanayofafanua maana halisi ya "Masahaba" katika Hadithi ya Nyota, wanazuoni wa madhebu ya Shia wanasimamisha hoja isema kwamba; ni Ahlul-Bait (Watu wa Nyumba ya bwana Mtume) pekee ndio wanaoweza kuwa wahusika halisi wa muktadha wa Hadithi zilizotangulia. Mtazamo huu imetiwa nguvu kupitia Hadithi nyingine kadhaa mashuhuri na zenye kukubalika, ambazo pia zinasisitiza hadhi ya kipekee ya Ahlul-Bait. Miongoni mwa hadithi hizo ni: • Hadithi ya Safina (Jahazi): Ambapo bwana Mtume (s.a.w.w) anawafananisha Ahlul-Bait na jahazi ya Nabii Nuhu; ambayo yeyote atakayeipanda ndani yake ataokoka, na yeyote atakayeacha nayo ataangamia. • Hadithi ya Thaqalain (Vizito Viwili): Ambapo Mtume anausia umma wake kushikamana na Qur'ani na Ahlul-Bait wake, akisema kuwa katu viwili hivyo havitatengana hadi Siku ya Kiyama. • Hadithi ya Kisaa (Shuka): Inayowabainisha hadhi maalum ya Ahlul-Bait (a.s) na kuthibitisha utakaso wao kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu. Halikadhalika, katika baadhi ya vyanzo vya Kisunni, kuna toleo tofauti la Hadithi ya nyota, ambalo badala ya kusema "Masahaba wangu ni kama nyota," riwaya hizo zinasema: "Watu wa nyumba yangu (Ahlul-Bait) ni kama nyota; yeyote mtakayemfuata miongoni mwao, mtaongoka." Toleo kama hili la Hadithi linahisabiwa kama uthibitisho wa ziada kutoka upande mwingine unaounga mkono hoja ya Kishia. [21]

Uhakiki wa Maudhui ya Riwaya ya "Ashabi ka an-Nujum" kwa Mtazamo wa Kishia Wanazuoni wa Kishia wametoa hoja kadhaa za kimantiki pamoja na maandiko mbali mbali mbali katika kukanusha tafsiri inayohalalisha uongofu wa Masahaba wote, kama inavyodokezwa na ufahamu na welewa wa Kisunni kuhusiana na Riwaya ya "Ashabi ka Al-Nujum." Hoja hizi zimechambuliwa na kuwekwa katika kategoria tatu kama ifuatavyo: • Mkinzano wa Kihistoria (Historical Contradiction): Kukubali maudhui ya Riwaya hii kama ilivyoelezwa na wafuasi wa madhehebu ya Ahlu Al-Sunna, kunalazimisha kukubali sifa kadhaa kwa kila Sahaba miongoni mwa Mashaba wa bwana Mtume (a.s.w.w), ikwemo; sifa ya ismah (kutokosea), adala (uadilifu kamilifu), pamoja na uwezo kamili wa kuongoza (hidayah). Hata hivyo, dai hili linaporomoshwa na kupikuliwa na ushahidi wa kihistoria, unaoonesha migogoro kati yao, tofauti za kimitazamo, pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe (fitan). Matukio haya yanafanya dhana ya uadilifu wa pamoja kuwa isiyowezekana. [22] • Mkinzano na Maandiko Matakatifu (Quranic Incompatibility): Maudhui ya Hadithi hii hayawezi kupatanishwa na kuoanishwa na maandiko ya Qur'ani. Kuna Aya kadhaa ziendazo kinyume na welewa wa Kisunni katika kuzifasiri Hadithi zilizotanguli, miongoni mwazi ni kama vile; Aya 15 na16 za Suratu Al-Anfal, Aya ya 16, 23, 25, za Suratu Al-Tawbah, pamoja na Aya ya 11 ya Suratu Al-Jumu'ah. Aya ni zenye kutoa tathmini hasi kwa baadhi ya Masahaba na kuthibitisha uwepo wa kundi la wanafiki (munafiqun) miongoni mwao. Kanuni ya kitaaluma inasema kuwa Yiwaya yoyote (Hadithi) inayopingana na Qur'ani, ambayo ndiyo chanzo kikuu cha sheria, haiwezi kukubalika ndani ya uwanja wa sheria. [23] • Mkinzano na Riwaya kwa Riwaya (Inter-Hadith Contradiction): Hadithi hii inapingana na kundi jengine la Riwaya zitokazo kwa bwana Mtume (s.a.w.w). Kundi hilo la Riwaya kinzani linajumuisha: onyo dhidi ya kuwafuata Masahaba wote bila kubagua, [Maelezo 1: (تَكُونُ بَيْنَ أَصْحَابِي فِتْنَةٌ يَغْفِرُ اللَّهُ لَهُمْ لسابِقَتِهُم، إِنِ اقْتَدَى بِهِمْ قَوْمٌ مِنْ بَعْدِهِمْ كَبَّهُمُ اللَّهُ تَعَالَى فِي نَارِ جَهَنَّمَ) Tafsiri: "Kutatokea fitina miongoni mwa Masahaba wangu, ambayo Mwenye Ezi Mungu atawasamehe kutokana na kutangulizi kwao [katika imani]. Iwapo kundi la watu baada yao litawaiga wao [katika fitina hiyo], basi Mwenye Ezi Mungu atawatumbukiza katika moto wa Jahanamu." (Kanzu al-Ummal, juz. 11, uk. 87. Chapa ya mwaka 1998 Miladia).] habari kuhusiana na kuritadi (kugeuka) kwa baadhi yao, [Maelezo 2: Riwaya kama vile: Riwaya ya «ذاتُ الشِّمال» "Dhatu Al-Shimal", ambayo ndani yake bwana Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) anatoa habari ya kurudi nyuma (kuritadi) kwa baadhi ya Masahaba baada ya kuondoka kwake (s.a.w.w), pamoja na kuwekwa kwao katika kundi la watu wa kushoto (Ashaabush Shimaal). (Rejea: Sunan Tirmidhi, 1403H, jz. 5, uk. 4. Al-Mustadrak, Hakim An-Naysaburi, 1411H, jz. 34, uk. 8).] matukio ya baadhi ya Masahaba katika kukiri ujinga wao juu ya masuala fulani ya kifiqhi, [24] ushahidi wa kutozingatia kwao baadhi ya maamrisho ya kidini, [25] pamoja na tuhuma dhidi yao kutoka na uanzilishaji wa baadhi ya uzushi (bid'ah) ndi ya dini. [26] Uwepo wa Riwaya hizi kinzani unadhoofisha kwa kiasi kikubwa uhalali wa tafsiri za Kisunni kuhusiana na maudhui ya hadithi ya "nyota", pamoja na Hadithi zinazotumika katika kuwakosha Masahaba. [27]

Maoni ya Ahlu Al-Sunna Juu ya Udhaifu wa Hadithi ya “As’habi ka Al-Nujum” Katika taaluma ya Ulum al-Hadith (Sayansi ya Hadithi), tathmini ya isnadi (mnyororo wa wapokezi) na matni (maudhui) ya Riwaya ndiyo kigezo msingi cha kuikubali au kuikataa Hadithi fulani. Riwaya inayofahamika kama "As'habī kal-nujūm" imepitia uchambuzi mkali wa kitaalamu kutoka upande wanazuoni mbali mbali wa madhehebu ya Ahlu Al-Sunna, na hatimaye kuhukumiwa kuwa ni dhaifu au ya ni kutungwa. Miongoni mwa wanazuoni hao ni pamoja na; Ibnu Hazmi al-Andalusi (aliyefariki 456H), ambaye aliitaja kuwa ni "batili na ya uongo", [28] apmoja na Ibnu Abdul Barr al-Qurtubi (aliyefariki 463 H) aliyesema kuwa mnyororo wa wapokezi wake "hauwezi kuwa hoja. [29] Wanazuoni wengine kama vile Ibnu Qudamah, [30] Abu Hayyan al-Andalusi, [31] Ibn al-Qayyim al-Jawziyyah, [32] na Ibn Abi al-Izz al-Hanafi [33] paia nao waliunga mkono mtazamo huu. Katika zama za karibuni, mmuhaddith Muhammad Nasir al-Din al-Albani (aliyefariki 1420 H), baada ya kukusanya na kuchunguza njia za mpokezi yake yote, aliihukumu Hadithi ya “As’habi ka Al-Nujum” kuwa ni Hadithi bandia (ya kuzuliwa). [34]

Ukosoaji wa Hadithi ya "As'habi kal-nujum" haikuishia kwa wanazuoni hao waliotajwa awali. Bali kuna kundi jengine la wataalamu mahiri wa Ahl al-Sunnah walioingia uwanjani katika kuidadisi Hadithi mashuhuri. Miongoni mwa wanazuoni hawa ni pamoja na; Al-Baihaqi (aliyefariki 458 H), [35] Ibn Taymiyyah (aliyefariki 728 H), [36] Ibn al-Mulaqqin (aliyefariki 804 H), [37] Al-Sakhawi (aliyefariki 902 H), [38] na Al-Mubarakfuri (aliyefariki 1353 H). [39] Wanazuoni hawa wameihukumu Riwaya hii na kuitaja kuwa ni Hadithi yenye udhaifu wa hali ya juu kabisa. Pia walisisitiza kuwa chanzo chake kinatokana na vitabu visivyo na tahamani na visivyo na hadhi katika uwanja wa hadithi. 

Aidha, kwa mtazamo wa ilm al-rijal (taaluma ya tawasifu za wapokezi), Hadithi hii inakumbana na changamoto kubwa zaidi. Wanazuoni wa jarh wa ta'dil (sayansi ya kukosoa na kusifu wapokezi wa Hadithi) wa Ahl al-Sunnah wameweka bayana kuwa baadhi ya wapokezi (ruwat) waliohusika katika isnad (mnyororo wa upokezi) wa Riwaya hii, walikuwa ni dhu'afa (dhaifu) na wengine walituhumiwa kuwa ni ja'il (wazushi wa Hadithi). Hukumu hii ya kitaalamu inapelekea riwaya hii kukosa mashiko ya kutumika kama hoja (hujjah) ya kisheria au kiitikadi. [40]