Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Bayanie Game Dovvom Inqilab (Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi)

Kutoka wikishia

Bayanie Game Dovvom Inqilab (Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi): ni waraka maalumu uliondaliwa na Sayyid Ali Khamenei, aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Waraka huu ulitolewa rasmi mnamo tarehe 11 Februari mwaka 2019, katika maadhimisho ya kuadhimisha mwaka mwaka 40 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Waraka huu, ulitolewa ukiwalenga vijana, ulikuja ukifafanua chimbuko la kihistoria na changamoto zilizojitokeza wakati wa mchakato wa Mapinduzi hayo, huku ukibainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miongo minne iliyopita. Aidha, Azimio hili linaweka bayana dira na dhamira za siku zijazo za Mapinduzi haya ya Kiislamu katika nyanja mbalimbali, ikiwemo; sayansi utafiti, kuimarisha mambo ya kiroho na kimaadili, pamoja na usimamiaji wa haki na mapambano dhidi ya ufisadi. Hivyo basi, hadhira kuu ya Azimio hili ni vijana, ambao wanatazamwa kama mhimili mkuu mfumo wa Kiislamu uliopiga hatua katika nyaja mbalimbali, ambao wanachukuliwa kama ni fursa adhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Wanazuoni mashuhuri kama akiwemo Nasir Makarim Shirazi, mmoja wa warejelewa katika masuala ya kisheria (Marja'a), na Mahdi Shab-Zinde-Dar, mwalimu mbobezi wa fikihi katika chuo cha Qom, wote kwa pamoja wameunga mkono Azimio hili na kulitambua kama mwongozo madhubuti na wa kieleimu. Kwa upande wake, Sayyid Ahmad Khatami ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Maalumu la Sheria la Irani (Majlis Khubregani), amesema kwamba, mizizi ya imani ya Kiongozi Mkuu kwa vijana imetokana na nyenendo, Sira pamoja na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w), ambaye aliwateua vijana watatu kwa ajili ya kushika nyadhifa nyeti katika uongozi wake. Ili kueneza waraka huu, kulifanyika makongamano kadhaa katika maeneo mbamimbali ya mji wa Qom na Tehran yaliobeba anuani ya "Hatua ya Pili ya Mapinduzi".  Aidha kilizinduliwa kitabu maalumu chenye lengo la kufafanua Azimio hili kwa ajili ya makundi mbalimbali, hususan vijana, akitabu ambacho kulikuja kuchapishwa katika msimu wa kipupwe (Spring) cha mwaka 2020.

Mazingira, Maudhui, na Walengwa wa Azimio Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi lilitolewa rasmi mnamo tarehe 22 Bahman 1397 Hijiria Shamsi katika maadhimisho ya miaka arobaini ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [1] Waraka huu umekuja kuelezeaq mwelekeo wa Mapinduzi uliongia katika hatua ya pili ambayo imejikita katika mchakato wa "kujijenga, kuunda jamii, na kuleta ustaarabu". Hadhira na walengwa wa azimio hili ni vijana, ambao wanatazamwa kama mhimili mkuu wa kutimiza mfumo wa Kiislamu uliopiga hatua na kuleta fursa adhimu kwa ajili ya mustakabali wa nchi. [2] Walengwa wakuu wa Tamko la Hatua ya Pili ni vijana; ambao kwa mujibu wa matini ya tamko hilo, wanatarajiwa kuanza “awamu nyingine ya jihadi kuu ya kuijenga Iran adhimu yenye haiba ya Kiislamu.” [3] Katika muktadha huo, vijana wanabainishwa kama mhimili msingi katika utekelezaji wa mfumo wa Kiislamu wenye maendeleo; hali inayodhihirisha kuwa mwendelezo wa mkondo wa Mapinduzi ya Kiislamu unapaswa kuendelezwa kwa juhudi, umakini na utambuzi kamili wa vijana hao. [4] Zaidi ya hayo, tamko hilo linatathmini kuwa rasilimali yenye matumaini makubwa zaidi ya taifa ni nguvu kazi ya kibinadamu yenye vipaji na ufanisi, iliyoasisiwa juu ya msingi imara wa kiimani na kidini. Sambamba na hilo, kundi la vijana wenye umri chini ya miaka arobaini linachukuliwa kuwa ni fursa ya kimkakati na yenye thamani kubwa kwa maendeleo ya taifa. [5] Maudhui ya Azimio

Maudhui ya Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi kwanza inajikita katika kuelezea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyojiri mwaka wa 1979 Miladia, pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa kuasisiwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha, waraka unaweka wazi kwamba, lengo kuu na azma ya Mapinduzi hayo ni kuanzisha ustaarabu mpya wa kisasa wa Kiislamu na kuweka "utayari kwa ajili ya kuchomoza kwa jua la uongozi mkuu wa Imamu Mahdi (roho zetu ziwe fidia kwake)". [6]

Katika sehemu mahususi ya Azimio la Hatua ya Pili, kumetolewa kufafanua maalumu kuhusiana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Mapinduzi. Mafanikio hayo yanajumuisha uthabiti na usalama wa kudumu katika ulinzi wa ardhi ya Iran dhidi ya chokochoko za nje. Aidha, waraka huo unabainisha kuwepo kwa ujenzi wa miundombinu muhimu ya kiuchumi na kimaendeleo, kuimarishwa kwa ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya nchi, na kupanda kwa upeo wa kisiasa miongoni mwa raia. Hali kadhalika, mafanikio mengine ni pamoja na kuzingatia uadilifu katika ugawaji wa rasilimali za umma, ustawi wa kiroho na kimaadili ndani ya jamii, na msimamo thabiti wa kusimama dhidi ya mabeberu na wababe wa ulimwengu. [7] Sehemu ya mwisho ya Azimio la Hatua ya Pili inajikita katika kufafanua dira ya mustakabali na kutoa miongozo kuhusu hatima ya Mapinduzi ya Kiislamu kupitia mada saba mahususi. Ndani ya waraka huu, sayansi na utafiti ndivyo vitu vilivyopewa kipaumbele cha kwanza kabisa, ambapo kufuatia kubainishwa kwa mafanikio ya Iran ya kushika nafasi ya kumi na sita kati ya mataifa mia mbili ulimwenguni katika nyanja mbili hizo, vijana wanahimizwa kuendeleza mkondo huo kwa hisia kali zaidi za uwajibikaji. [8] Ukuaji wa Hali ya Kiroho na Maadili Katika Hatua ya Pili ya Mapinduzi Ndani ya Azimio la Hatua ya Pili, mchakato wa kukuza hali ya kiroho na maadili unabainishwa kuwa ni suala lenye kuhitaji ushirikiano wa dhati kutoka katika mamlaka za kiserikali. Hata hivyo, imewekwa bayana kuwa tunu hizi mbili haziwezi kupatikana kupitia amri au maelekezo ya kulazimisha. Azimio hili linasisitiza kuwa asasi husika za kiserikali, pamoja na watu binafsi na taasisi zisizo za kiserikali, zote kwa pamoja zina wajibu wa kuandaa na kutekeleza mipango kabambe ya muda mfupi na wa kati na kati, ili kudhibiti na kuzuia shughuli zote zinazopingana na misingi ya kiroho na kimaadili. [9] Sera za Kiuchumi Kwa mujibu wa Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi, suluhu ya kudumu ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili nchi imejikita katika utekelezaji wa sera za Uchumi Himimilivu (Resistance Economy), ambazo mipango yake ya kiutendaji inapaswa kuandaliwa na kutekelezwa katika sekta zote. [10] Sifa kuu za sera hizo zimeainishwa kuwa ni pamoja na ukuzaji wa uchumi wa ndani, kuelekea katika uzalishaji unaozingatia elimu na teknolojia, na kuufanya uchumi kuwa ni wa wananchi wenyewe, na sio serikali kushikilia hatamu za umiliki wa uchumi wa nchi. Aidha, azimio hili linasisitiza umuhimu wa kuepuka utegemezi wa nchi za nje, likihimiza mfumo wa kiuchumi unaojitegemea na usioyumbishwa na masharti ya kimataifa. [11] Uadilifu na Mapambano dhidi ya Ufisadi Katika Bayani ya Hatua ya Pili ya Mapinduzi, ingawa imesisitizwa kwamba kiwango cha ufisadi miongoni mwa watendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ni kidogo zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine, hasa ikilinganishwa na utawala wa Pahlavi (utawala wa kabla ya Serikali ya Kiislamu), hata hivyo viongozi wote wanakumbushwa wajiepushe na kila aina ya riziki isiyo halali. Aidha, taasisi za usimamizi na mashirika ya serikali yametajwa kuwa na jukumu la msingi katika kuzuia na kupambana na kuongezeka kwa ufisadi. [12] Uhuru na Kujitegemea

Kitaifa Katika Azimio la Hatua ya Pili, msisitizo mkubwa umewekwa katika kubainisha suala la uhuru na kujitegemea, huku ukiyataja mawili hayo kuwa ni miongoni mwa thamani kuu za Kiislamu na ni zawadi za Mwenye Ezi Mungu kwa wanadamu. Hivyo basi, kila mmoja na hususan serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ana wajibu wa kisheria na kimaadili wa kulinda na kuhifadhi tunu mbili hizi. [13] Hata hivyo, imebainishwa kuwa kujitegemea hakupaswi kutafsiriwa kama kufuinga siasa na uchumi wa nchi ndani ya mipaka yake pekee. Vilevile, uhuru haupaswi kufafanuliwa kwa namna inayopingana na maadili, sheria, thamani za kimungu, pamoja na haki za umma. [14]

Heshima ya Kitaifa, Mahusiano ya Nje, na Misingi ya Kidiplomasia Azimio la Hatua ya Pili, limemetaja misingi miku mitatu muhimu kwa ajili ya kutunza heshima yake ya kitaifa ndani ya mahusiano yake na nchi za nje. Misingi mitatu hiyo ni; kuweka mipaka mbele ya adui, kujenga mahusiano mema na nchi rafiki, na kulinda heshima ya taifa ndani ya mahusiano yake na nchi mbalimbali. [15] Mtindo wa Maisha Katika Azimio la Hatua ya Pili, imebainishwa kwa uwazi kuwa jitihada za nchi za Magharibi katika kupigia debe na kueneza mtindo wa maisha wa Kimagharibi nchini Iran, zimesababisha madhara makubwa katika nyanja mbalimbali za kimaadili, kiuchumi, kidini, na kisiasa nchini mwake. Waraka huu unasisitiza kuwa kukabiliana na athari hizo hasi kunahitaji jihadi jumuishi na yenye akili na tafakuri hali ya juu kabisa, ili kulinda utambulisho wa kitaifa na kidini wa nchi hiyo. [16] Uwakilishi wa Kielelezo na Taswira ya Umoja wa Kitaifa

Sanjari na kuchapishwa kwa Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi katika tovuti ya Ofisi ya Uhifadhi na Uenezi wa Kazi za Ayatullah Khamenei, imetoa picha mahususi ilioambatanishwa na matini ya waraka huo. Picha hiyo inawaonyesha watu wa matabaka na kada mbalimbali za kijamii wakiwa kando ya Sayyid Ali Khamenei, ambao ni miongoni mwa wanazuoni wa kidini, wanachama wa Basiji (Valantia), wafanyakazi, madaktari na wauguzi, wahandisi, wanamichezo, waalimu, wasanii, pamoja na wanafunzi. [17] Jambo la kipekee katika taswira hiyo ni kwamba bendera ya msafara huo imeshikiliwa mikononi mwa mwanamke, jambo linaloashiria nafasi yake ya kimsingi katika harakati za kistaarabu. [18]

Miitikio Kuhusu Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi Baada ya kuzinduliwa kwa Azimio la Hatua ya Pili na Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kulitokea wimbi kubwa la mapokezi chanya kutoka kwa wasomi, viongozi wa kidini, na wanaharakati mblimbali wa kijamii. [19] Miongoni mwao ni Nasir Makarim Shirazi, ambaye ni mmoja wa warejelewa wakuu katika masuala ya kisheria (Marja’a al-Taqlid) mjini Qom, ambapo katika masomo yake ya juu ya fikihi (Dars-e Kharij), aliuelezea waraka huo kuwa ni waraka jumuishi na makini mno. Aidha mwanazuoni huyu alisisitiza akisema kuwa; azimio hili limebeba mkakati madhubuti na wa kivitendo kwa ajili ya mustakabali wa miaka arobaini ijayo ya Mapinduzi ya Kiislamu. [20] Mahdi Shab-Zinde-Dar, ambaye ni mmoja wa mafaqihi wa Baraza la Walinzi wa Sheria za Nchi na mwalimu wa masomo ya juu ya fikihi (Dars-e Kharij), amelifafanua azimio hili akisema kuwa ni lenye maudhui yaliyokomaa na la kieleimu kabisa. Kutokana na umuhimu wa wake, mwanazuoni huyu aliamua kutenga darsa maalumu kwa ajili ya kulichambua na kulifafanua azimio hili. [21] Kwa upande mwingine, Sayyid Ahmad Khatami, mwanachama wa Baraza la Wataalamu wa Sheria (Majlis Khubregan), amebainisha akisema kuwa msingi wa imani ya Kiongozi Mkuu kwa vijana unatokana na Sira na Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w), ambaye katika historia yake aliwateua vijana watatu kushika nyadhifa nyeti na muhimu ndani ya uongozi wake. [22] Taqi Misbah Yazdi, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Sheria (Majlis Khubregan), anaamini kwamba, lengo kuu la kutoa Azimio hili ni kuhamisha urithi wa kale kwenda kwenye kizazi kipya. Katika uchambuzi wake, anasisitiza kuwa nadharia inayodai "kila mapinduzi hufa" si sahihi, kwani mapinduzi pekee yanayokabiliwa na hatari ya mauti ni yale mapinduzi ya kimaada. Badala yake, Mapinduzi ya Kiislamu yana sifa ya kudumu na kutoporomoka, hii n i kwa sababu thamani zake zimefungamanishwa kikamilifu na fitra (asili na maumbile) ya mwanadamu. [23] Kwa mujibu wa uchambuzi wa Mehdi Golshani, mjumbe wa kudumu wa Akademia ya Sayansi nchini Iran, sababu hasa ya Azimio la Hatua ya Pili kuwalenga vijana ni kutokana na kwamba kizazi hicho ndicho nukta ya matumaini kwa ajili ya ujenzi wa mustakabali wa nchi. Aidha, anabainisha akisema kuwa; kwa mtazamo wa Sayyid Ali Khamenei, kizazi hichi hakijaathiriwa sana na maslahi mpito ya kimaada. [24] Aidha, Mohsin Ismaili, mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Sheria, amelitambua azimio hili kama moja ya nyaraka muhimu za fikihi ya kisiasa (political jurisprudence), akililinganisha na kitabu maarufu cha Tanbih al-Ummah wa Tanziih al-Millah cha Muhammad-Hussein Na'ini. Kwa mujibu wake, waraka huu una umuhimu katika nyanja tatu: ubainishaji wa malengo makuu ya Mapinduzi, tathmini ya utendaji wa miaka arobaini, na uchoraji wa njia ya kuelekea mustakbali wa kesho. [25] Sayyid Ibrahim Raisi, mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Sheria, alilifafanua Azimio la Hatua ya Pili kama nukta ya mgeuko (turning point) katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu, inayobainisha mafanikio ya miaka arobaini na kutoa mwongozo wa kistratejia kwa mustakabali wa mfumo na harakati za mapinduzi hayo. Akitoaufafanuzi wa juu ya waraka huu anasema kwamba; waraka huu umetupa picha ya wazi kabisa inayoonesha kwamba ustaarabu wa Kiislamu ni lengo linaloweza kufikiwa. [26] Kwa upande wake Sayyid Mohammad-Mahdi Mirbaqiri ameliweka azimio hili katika daraja la juu zaidi kuliko kitabu cha Tanbih al-Ummah cha Na'ini, kwani yeye amelifananisha na kitabu kiitwacho Wasiyyatname Siasi Ilahi (Wasia wa Kisiasa na Kiungu) cha Imam Khomeini. Yeye anasema kuwa, lengo la azimio hili ni kuweka misingi ya kinadharia (theorizing) ya mienendo ya jamii ya Kiislamu kuelekea ujenzi wa ustaarabu wa Kiislamu. [27] Mipango ya Uenezaji na Machapisho Kuhusiana na Azimio Kufuatia kutolewa kwa Azimio la Hatua ya Pili, makongamano kadhaa yalifanyika nchini Iran na kazi nyingi za kieleimu zikachapishwa, ili kuimarisha uelewa wa waraka huo. Miongoni mwa mipango na mazao ya uenezaji wa waraka huu ni: • Kongamano la Kimataifa la Hatua ya Pili ya Mapinduzi, lenye kichwa kidogo kisemacho Ulgue Nidhame Inqilabi Tamaddunsaaz "Mfumo wa Mapinduzi Unaosisi Ustaarabu," lililofanyika mjini Tehran mnamo Februari 5, mwaka 2020 Miladia. [28] • Kitabu cha "Asre Jadid" (Zama Mpya) kilichoandikwa na Seyed Mohammad-Mahdi Mirbaqeri kilichozinduliwa mnamo mwaka wa 2019 Miladia, kikichambua dhana na mikakati ya azimio hilo ambacho kilichapishwa na Taasisi ya Tamaddune Newini Islami. [29] • Kongamano la Kitaifa la "Azimio la Hatua ya Pili na Ustaarabu Mpya wa Kiislamu" lilifanyika mjini Qom mnamo Februari 13, 2020, [30] na hatimaye kulizinduliwa mkusanyiko wa kazi za kieleimu wenye juzuu sita. [31] • Mfululizo wa masomo wenye anuani ya"Ranje Shirin" (Maumivu Matamu) kazi ya Ruhullah Abbasi iliochapishwa mwezi wa Machi mwaka 2020 Miladia. Kazi hii ilitoa ufafanuzi muhimu juu ya nafasi ya misikiti. [32] • Kitabu chenye anuani ya “Bayaniyye Game Dovvome Islami” (Azimio la Hatua ya Pili ya Mapinduzi ya Kiislamu). Kitabu hichi chenye kurasa 181kilizinduliwa na Kituo cha Uchapishaji cha Baqir al-Olum katika msimu wa kipupwe wa mwaka 2020 Miladia ili kuwafikia vijana. [33]