Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Barua za Mtume kwa Wafalme

Kutoka wikishia

Barua za Mtume kwa Wafalme: Barua hizi ni zile ambazo Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliwatumia watawala wa maeneo mbalimbali, akiwaalika kuikubali dini ya Uislamu na kuingia katika wigo wa ujumbe wake. Barua hizi, kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria vya Kiislamu, zilikuwa ni sehemu ya hatua ya kimkakati ya kueneza daʿwah nje ya Uarabuni baada ya kuimarika kwa dola ya Kiislamu huko Madina. Katika baadhi ya barua hizo, pamoja na mwaliko wa kuingia katika Uislamu, pia kulikuwepo na maonyo ndani yake. Kwa mfano, kwa Heraclius, Kaizari wa Dola ya Roma ya Mashariki, na kwa Khosrow II, mfalme wa Uajemi, ilisisitizwa kwamba watawala wanakabiliwa na dhima ya dhambi zitendwazo na raia wao. Aidha, kwa watawala wa Damascus na Oman, ilielezwa kuwa kuukubali Uislamu kungedhamini kuendelea kwa mamlaka yao chini ya mfumo mpya wa kisiasa, ilhali kuikataa wito huo kungeweza kusababisha kuporomoka kwa utawala wao. Kwa upande mwingine, mtawala wa Bahrain alionywa kwamba; iwapo atakataa wito huo, atawajibika kulipa jizya. Majibu ya wafalme hawa yalitofautiana, Najashi mfalme wa Uhabeshi aliingia katika Uislamu bila ya pingamizi, na Khosrow Parviz mfalme wa Uajemi aliamua kurarua barua ya bwna Mtume (s.a.w.w.w). Baadhi ya viongozi kama vile mfalme wa Bahrain walikataa moja kwa moja mwaliko huu. Vyanzo vya historia vinataja nyakati tofauti za kutuma kwa barua hizi, waandishi wengi wanataja mwaka wa sita baada ya Hijra na kipindi cha baada ya mkataba wa Hudaybiyyah.