Mkopo:Balehe kwa wasichana
Balehe kwa wasichana: Suala la ubalehe wa watototo wa kike linarejelea kipindi cha uondokaji wa kipindi cha utoto na uingiaji wa kipindi cha utuuzima, kinachowafanya wahusika wake kuwajibikiwa na sheria za kidini. Kulingana na fatwa za wanazuoni, kuna sababu tano zinazoweza kutumika katika kuthibitisha ubalehe ni wa msichana fulani: kufikia umri wa ruhusa ya kuadhibiwa kisheria, kuona damu ya hedhi, kuota njozi zinazohusiana na masuala ya kijinsia, kuota nywele ngumu kwenye sehemu ya chini ya tumbo (kinenani), na kushika mimba. Msichana yeyote yule anayepatwa na mojawapo ya mambo hayo, huhesabiwa kuwa tayari anastahili kupewa sifa ya balehe.
Kuna khitilafu za maoni miongoni mwa wanasheria wa dini kuhusiana na umri wa kubalehe. Wengi wa wanazuoni wa Kishia wa wanaamini kuwa, wasichana hufikia balehe yeke mwishoni mwa mwaka wa tisa wa umri wake, hisabu inayozingatia mwezi mwandamo. Kinyume cha maoni hayo, wengine wanasema kuwa, umri hasa wa ubalehe ni miaka kumi na tatu. Kuna pia kuna waliotofautisha wajibu wa kidini, ambao wanaweka umri wa miaka kumi kwa baadhi ya hukumu, na miaka kumi na tatu kwa baadhi ya hukumu nyingine. Uchambuzi wa Dhana ya Kubalehe na Nafasi Yake Makala Kuu: Kubalehe "Ubalehe/Balehe" ni istilahi ya kifiqhi inayorejelea hali ya kufikia umri na kipindi maalum cha maisha, ambapo mtu huanaanza kukabiliwa na majukumu ya kidini, na hupaswa (huwajibika) kufuata sheria za kiislamu kikamilifu. [1] Wanazuoni wengi wa fiqhi wameutambua umri wa miaka tisa kuwa ndiyo kiwango sahihi cha kubaleghe kwa wasichana. Kwa msingi huo, katika zama za leo—yaani karne ya ishirini na moja— utambuzi wa umri huo unaombebesha msichana majukumu mbalimbali, umezua aina kadhaa za mijadala na ukjosoaji kuhusiana na masuala ya ndoa, kubeba dhamana za kisheria, na kutekeleza wajibu wa kidini kwa wasichana waliofikia umri huo. [2] Hali hii imewapelekea wanazuoni wa fiqhi wa kizazi cha sasa kuyachunguza upya masuala haya kwa kurejea vyanzo vya riwaya za kidini pamoja na mitazamo ya wanazuoni wa kale, ili kuyapima kwa mizani ya uelewa wa kina na uhalisia wa wakati uliopo. [3] Viashiria vya Kimaumbile vya Baleghe kwa Wasichana Maana ya viashiria vya kimaumbile vin ayokusudia hapa, ni dalili za kifizikia zinazojitokeza katika mwili wa wasichana, ambazo zimenukuliwa moja kwamoja kutoka katika Riwaya za Maimamu watoharifu, na kutambuliwa kuwa ndiyo alama halisi zinazoashiria balehe kwa watoto wa kike. [4] Viashiria hivyo ni kama ifuatavyo: Mzunguko wa Hedhi Kwa mujibu wa wanazuoni wa fiqhi ya Kishia, na kwa kuegemea mapokezi yaliomo katika vyanzo vya Hadithi, kuanza kwa hedhi huhesabiwa kuwa ni mojawapo ya dalili muhimu za kufikia baleghe kwa wasichana. [5] Baadhi ya wanazuoni hawa wanaamini kwamba, kipindi cha mzunguko wa hedhi huanza pale msichana anapofikisha umri wa miaka tisa. [6] Kulingana na mtazamo hou, damu yoyote ile inayoonekana kabla ya kufikia umri huo—hata kama ina sifa zote za damu ya hedhi—haihewezi kuhisabiwa kuwa ni damu ya hedhi. Kwa mtazamo wao, damu ya hedhi ni ile tu inayojitokeza baada ya msichana kufikisha umri wa miaka tisa, na damu hiyo pekee ndiyo inayozalisha athari na hukumu za kisheria zinazohusiana na hedhi. Kwa msingi huu, kundi hili la wanazuoni huchukulia hedhi kuwa ni dalili ya baleghe katika hali mahsusi tu, nayo ni pale ambapo umri halisi wa msichana fulani utakapokuwa haujulikani. [7] Ujauzito Kwa mujibu wa mtazamo wa baadhi ya wanazuoni wa fiqhi, ujauzito huhesabiwa kuwa ni mojawapo ya viashiria vya kufikia baleghe kwa wasichana. Hii ni kwa sababu ya kwamb, suala hilo ndilo linalothibitisha kuwepo kwa hali ya kutoka kwa manii pamoja na uwepo wa damu ya hedhi kwa msichana fulani. [8] Kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh Tusi, mwanamke katika hali ya kawaida ya kimaumbile hawezi kupata ujauzito kabla ya kuanza kwa hedhi. Aidha, ujauzito hutokana na kuchanganyika kwa manii ya mwanamke na ya mwanamume. Kwa msingi huo, ujauzito—kwa kuwa ni matokeo yanayolazimiana na hedhi pamoja na kutoka kwa manii—hutambuliwa kuwa ni moja ya dalili za kufikia baleghe. [9] Ihtilamu (Njozi za Kijinsia) na Kuota kwa Nywele Ngumu Ihtilamu, yaani kutoka kwa manii kupitia njozi za kijinsia, huhisabiwa kuwa ni miongoni mwa dalili na alama za pamoja za kufikia baleghe kwa wasichana pamoja na wavulana. [10] Hata hivyo, wapo wanaoona kwamba wanawake hawana sifa ya kutokwa na manii kama wanaume, na kwa msingi huo hudai kuwa ihtilamu na kutokwa kwa manii ni mambo yanayowahusu wanaume peke yao. [11] Kinyume na mtazamo huo, kuna wanazuoni wengine wa fiqhi kama vile Sahib al-Urwa, wanaoamini kuwa wanawake pia ni nao hutokwa na manii kama ilivyo kwa wanaume, hivyo basi wanazuoni hawa huidhoofisha ile kauli inayokanusha sifa hiyo kwa wanawake. [12] Aidha, kuota kwa nywele ngumu katika eneo la chini ya tumbo ni miongoni mwa dalili za pamoja za baleghe kwa watoto wa kike na wa kiume, suala ambalo halina khitilafu mbele ya wanazouni mbalimbali. [13] Umri wa Baleghe kwa Wasichana
Baadhi ya wanazuoni wa fiqhi wanauhisabu umri kuwa ni miongoni mwa viashiria vya msingi vya kufikia baleghe. [14] Hata hivyo, kuna mitazamo tofauti kutoka kwa wanazuoni mbalimbali kuhusu umri halisi wa kufikia baleghe kwa wasichana. Mitazamo tofauti ya kifiqhi kuhusiana na suala hili ni kama ifuatavyo: Miaka Tisa Kwa mujibu wa maoni yanayokubalika zaidi miongoni mwa wanazuoni wa fiqhi ya Kishia, wasichana hufikia kiwango cha kubalehe mwishoni mwa miaka tisa ya umri wao (kutimia miaka tisa kamili). Hii ni kwa hesabu ya kalenda ya mwezi mwandamo (Hijiria). Kwa hisabu ya kalenda ya Miladia, uri huo huwa ni takribani miaka minane, miezi minane na siku ishirini. [15] Msingi wa maoni haya umeelezwa kuwa ni riwaya zilizopokelewa na kusambaa kwa wingi mno (al-mustafidhu), [16] zikinasibishwa na Maimamu watoharifu (a.s). [17] Yusuf ibn Ahmad Bahrani, anayejulikana kama Sahib al-Hada’iq, anasema kwamba kuna Riwaya nyingi mno zinazotaja umri wa miaka tisa kuwa ndiyo umri hasa wa kufikia baleghe kwa wasichana. [18] Vilevile, Sayyid Ahmad Khunsari ameliona suala hili kuwa halina dosari wala shaka ndani yake, hii ni kwa kuzingatia wingi wa Riwaya zilizopokewa kuhusu jambo hilo. [19] Pamoja na hayo, baadhi ya watafiti wanaamini kuwa Riwaya hizo zinahusiana na hali na mazingira maalumu ambayo yalifanya wasichana wake (katika zama fulani) wafikie balehe zao wakiwa katika umri wa miaka tisa. [20] Kwa mfano, Mohammad Ebrahim Jannati anasema kuwa hakuna Riwaya zilizojataja umri fulani kama kanuni (kwa nia ya kujenga kanuni) ya jumla na ya lazima kuhusiana na suala hili, bali umri mbalimbali uliotajwa kupitia Riwaya tofauti, unatokana na tofauti za kimazingira, sababu za kijenetiki na kifizikia, pamoja na mitindo ya lishe za jamii na watu mbalimbali. [21] Yusuf Sanei akitoa ufafanuzi wake kuhusiana na suala hili anasema kwamba, Riwaya hizo zinapingana na kanuni ya urahisi katika dini (kanuni inayodai kuwepo kwa urahisi katika dini), kwa sababu Riwaya hizi zinaonekana kuwatwika wasichana wa miaka tisa mzigo mzito wa majukumu na hukumu za kisheria, pamoja na kuwakabili kwa adhabu kamili za kisheria, hali ambayo haiendani na udhaifu wao wa kimwili, ukosefu wa ukomavu wa mwili, pamoja na kutokuwepo kwa uwezo wa kuolewa katika umri huo. [22] Miaka Kumi Miongoni mwa wanazuoni wa fiqhi waliotaja umri wa miaka kumi kuwa ndio umri hasa wa kufikia baleghe kwa wasichana, ni Sheikh Tusi katika kitabu chake al-Mabsut, [23] pamoja na Ibnu Hamza, mwanazuoni wa karne ya sita Hijria, katika kitabu chake al-Wasila. [24] Hoja inayotolewa kwa ajili ya kuunga mkono mtazamo huu, imejengwa juu ya msingi wa Riwaya chache zisizo mashuhuri [25] zinazoutaja umri wa miaka kumi kuwa ndiyo kiwango cha wanawake cha kufikia balehe zao. [26] Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Sahib al-Jawahir, ni kwamba, Sheikh Tusi na Ibn Hamza katika baadhi ya kazi zao nyingine, walionekana kujiondoa katika mtazamo wao mwanzo, na wakatoa fatwa nyengine mpya kabisa inayolingana na maoni ya wanazuoni mashuhuri. [27] Aidha, baadhi ya wanazuoni wakizifasiri Riwaya hizo wanasema kwamba, umri wa miaka kumi unaokusudiwa humo ni mwishoni mwa miaka tisa, na kwa msingi huo, mtazamo huo haupingani na kauli mashuhuri inaoutaja umri wa miaka tisa kuwa ndiyo kigezo cha balehe za wanawake. [28] Miongoni mwa wanazuoni wa fiqhi ya Kishia wa karne ya kumi na nne ya Shamsi, kuna wanazuoni maalumu walioutambua umri wa miaka kumi na tatu kuwa ndiyo kiwango cha wasichana kufikia balehe zao. Miongoni mwa wanazuoni walioshikamana na mtazamo huu, ni Mohammad Ishaq Fayyaadh [29] na Yusuf Sanei. [30] Msingi wa msimamo huu umejengwa na kusimama juu ya Riwaya ya Ammar al-Sabaati, iliyopokewa kutoka kwa Imamu Ja'far al-Sadiq (a.s). [31] Kwa mujibu wa maelezo ya Riwaya hiyo, miaka kumi na tatu ndiyo umri wa mtu kuingia katika hatua ya kubalehe, bila ya kutofautisha kati ya wavulana na wasichana. [32] Utenganishaji wa Taklifa (Majukumu) kwa Mujibu wa Aina Zake Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Mujtaba Normufidi, mtafiti na mhadhiri wa Hawza ya Qum, baadhi ya wanazuoni wa fiqhi wamechagua mwelekeo wa kutofautisha kati ya aina mbalimbali za taklifa (majukumu ya kisheria). [33] Hii ni kwa lengo la kuoanisha Riwaya zinazoonekana kutofautiana kimitazamo. Kwa mfano, Faidhu Kashani (aliyefariki mwaka 1091 Hijria) alieleza akisema kwamba, umri wa taklifa za wasichana katika masuala ya mtu binafsi, ikiwemo; Sala na funga, ni miaka kumi na tatu. Na miaka tisa ni umri unaozingatiwa katika utekelezaji wa adhabu za kisheria. Na miaka kumi ni kwa ajili ya masuala ni maalumu kwa ajili ya masuala yanayohusiana na kuachia huru mtumwa na kuandika wasia. [34] Aidha, Sadeqi Tehrani anafafanua akisema kwamba: “Kwa wasichana na wavulana, miaka kumi ni umri uohusiana na masuala ya amali, kama vile swala pamoja na taklifa nyingine zinazotegemea akili. Ila katika suala la funga—ambalo kipimo chake ni uwezo wa kimwili—ni umri wa miaka kumi na tatu. [35]