Mkopo:Balehe au baleghe
Balehe au baleghe (بلوغ): ni nomino ya kidhahania katika istilahi ya fiqhi inayorejelea kitendo cha kufika katika hatua maalumu ya kiumri ambapo sheria za amri na makatazo ya Kiislamu humwelekea mhusika aliyefikia umri huo. Mafaqihi, kwa kutegemea mfululizo nukuu za Hadithi kutoka kwa Maimamu (a.s), wameweza kuainisha vigezo maalumu vinavyoashiria kuingia katika hatua ya kubalehe. Kwa mujibu wa kauli mashuhuri, wavulana huingia kwenye balehe baada ya kutimiza umri wa miaka kumi na tano ya Kihijria, huku wasichana wakiingia kwenye hatua hiyo baada ya kutimiza miaka tisa kulingana na tarehe ya Hijria. Pia kuna mafaqihi wengine wanaoona kuwa, mtoto wa kike hifikia umri wa kubalehe baada ya kutimiza miaka kumi na tatu ya Kihijiria. Kibiolojia, kuna aina mbili za alama na viashiria vya kubalehe: alama za pamoja na alama mahususi. Ihtilam (kuota njozia zinazohusiana na masuala ya kijinsia) na kuota kwa nywele ngumu kwenye kinena, ni alama za pamoja zinazoashiri kuingia katika hatua ya kubalehe, ila kupata hedhi ni alama mahususi kwa jinsia ya kike peke yake. Ili damu ihisabiwe ni hedhi na iwe na shinikizo la kuandamwa na hukumu za kisheria, ni lazima mhusika wa damu hiyo awe tayari ameshafikisha miaka tisa. Kudhihirika kwa kiashiria chochote kile miongoni mwake kutapelekea mhusika kutambulika kisheria kuwa ni mbalehe. Kufuatia hatua hiyo ya ukuaji, binadamu huingia katika mzingo wa uwajibikaji wa kisheria (taklifu) na huhisabiwa kuwa ni mzungumziwa na mkusudiwa wa moja kwa moja wa kanuni na taratibu za kidini, zikiwemo zile za kiibada, kisheria, kijinai, kiuchumi, na nyinginezo. Uchambuzi wa Dhana na Hadhi Yake Kisheria Kisheria na katika epistemolojia ya kifikihi, balehe hutambuliwa kama istilahi maalumu inayorejelea kuingia kwa mhusika wake katika kilele cha umri kinachozalisha majukumu na kumwajibisha kuzingatia kanuni za Sharia. [1] Maadamu balehe ndiyo kigezo cha msingi cha kuanza kwa mzigo wa uwajibikaji, hali hii inachukua nafasi ya kipekee ndani ya sayansi ya fikihi; hali iliyowapelekea mafaqihi kufanya uchambuzi wa kina juu ya dhati yake, ishara zake, na kanuni zake za kisheria. [2] Wasomi wa fikihi wanabainisha kwamba, balehe balehe si sifa tosha inayomfanya mja kuwajibikiwa na makumu ya kisheria. Bali sambamba na mhusika kuwa na sifa hii ila pia anapaswa kufikia utimilifu wa akili pamoja na kuwa na uwezo wa utendaji katika mchakato wa kutekeleza majukumu mbalimbali ya kisheria. [3] Kutokana na msingi huo, mjadala huu umepenya na kushamiri katika takriban milango yote ya fikihi. [4] Dalili na Alama za Kubalehe Kuna alama na dalili kadhaa za kubalehe zilizoanishwa katika fiqhi, uanishaji ambao umetegemea zaidi kwenye hadithi za Maimamu Maasumu (a.s). Ukomavu wa kisheria (balehe ya kimwili na akili) wa mtu fulani huthibitishwa kupitia vigezo vya umri au kwa kudhihiri kwa alama za kimaumbile za balehe; ambapo kutimia kwa moja ya vigezo hivi kunatosheleza kuwa ni kigezo cha kufikia umri wa balehe. Rai mashuhuri miongoni mwa mafaqihi wa madhehebu ya Shia inaeleza kuwa wavulana hufikia balehe baada ya kukamilisha umri wa miaka kumi na tano ya Hijria (inayokadiriwa kuwa miaka 14, miezi sita, na siku 12 ya kalenda ya Miladia), ilhali kwa wasichana ni baada ya kukamilisha miaka tisa ya Hijria (takriban miaka minane, miezi minane, na siku 20 za kalenda ya Miladia). [5] Licha ya hayo, wanazuoni wengine wa sheria, wakiwemo Muhammad Ishaq Fayyadh [6] na Yusufu Saani’i [7] wakiegemea baadhi ya nukuu, [8] wameamua kutoa hukumui tofauti kuhusiana na wanawake. Wao wamesema kwamba; watoto wake huanza hukuabiliwa na majukumu ya kisheria wakiwa na miaka kumi na tatu.
Katika muktadha wa alama za kimaumbile za balehe, kuna alama za pamoja zinazoshirikisha jinsia zote mbili, nazo ni ihtilamu (kutokwa na manii) [9] na uotaji wa nywele ngumu katika kinena. [10] Ama kuanza kuona hedhi ni ishara mahususi inayowahusu watoto wa kike peke yao. [11] Pamoja na hayo, baadhi ya mafaqihi wakibainisha suala la hedhi wanasema kwamba, damu inayotoka kabla ya binti kutimiza miaka tisa haihesabiki kisheria kuwa ni hedhi, hata kama itabeba sifa zote za damu hiyo; bali damu ya hedhi ni ile tu inayotoka baada ya mtoto wa kike kutimiza umri uliotajwa. Hivyo basi damu inayoonekana baada ya kutimiza umri huo ndiyo moja ya vigezo vinavyotumika katika ulazima na uwajibu wa kutekeleza hukumu za kisheria. Kulingana na rai hii, kigezo pekee cha kuthibitisha balehe kwa wasichana ni umri wa miaka tisa. [12]
Ithibati ya Ukomavu wa Kisheria (Balehe)
Iwapo mtu fulani anadai kufikia upeo wa balehe kwa nia ya kudai au kuthibitisha jambo fulani makamani, ithibati ya dai lake inakubalika kisheria chini ya mojawapo ya mazingira matatu yafuatayo:
1. Ikiwa misingi ya balehe yake itakuwa imaithibitika kwa kupata ihtilamu (hii ni kwa jinsia zote mbili) au kwa kuingia kwenye mzunguko wa hedhi (hii ni kwa wasichana). Sharti la kukubalika kwa hoja zake zitategemea kuwepo kwa uwezekano wa kutosha wa kibaiolojia kwa mhusika huyo. [13] 2. Ikiwa hoja yake itakuwa ni uotaji wa nywele vigumu kinenani mwake, dai hilo linathibitishwa kupitia uchunguzi wa kimwili, jambo ambalo litabidi kuchunguzwa na anayerhusiwa kisheria kufanya hivyo (kama vile dokta au anayefanana naye). [14] 3. Ikiwa mhusika atategemea kigezo cha kiumri kama ithibati ya balehe yake, dai hilo halitakubalika isipokuwa kwa kuwasilisha "Bayyinah" (hoja), itakayosimama kupitia ushuhuda wa mashahidi waadilifu wanaokubalika katika taratibu za kisheria. [15] Athari za Kifiqhi na Kisheria za Balehe Mara tu baada ya mtu kuhitimu maisha ya utototni na kuingia katika hatua ya ukomavu wa kisheria (balehe), anajumuishwa na kuingia ndani ya jamii inayokabiliwa na majukumu sheria za Kiungu. Hapo hugeuka na kuwa ni miongoni mwa waelekezewao kanuni na taratibu za kisharia; kuanzia zile za kiibada, kifiqhi, kijinai pamoja na zile zinazohusiana na nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii. [16] Hata hivyo, kwa mujibu wa maandiko yaliyonukuliwa na Mir Abd al-Fattah Maraghi katika kitabu chake Al-Anawin, ambaye ni mwanazuoni wa karne ya kumi na tatu ni kwamba; katika hukumu nyingi za kiutaratibu (al-ahkam al-wadh’iyyah)—mathalani kanuni zinazohusu mirathi, fidia ya damu, dhima ya mali pamoja na hukumu za umilki—balehe haijaonekana kutajwa kama ni moja ya sharti la msingi ndani mchakato wa utekelezaji wake. Bali hukumu hizo huwagusa na kuwajumuisha hata wale ambao bado hawajafikia umri wa balehe. [17] Balehe ya Mapema na Balehe ya Chelewa Balehe ya mapema ni tukio la kimaumbile linalojitokeza kwa baadhi ya watoto wa zote mbili ya kike na ya kiume. Kikawaida tukio hili hujiri chini ya vichocheo vya urithi, hali ya hewa, afya, na lishe. Kutokana kuwepo kwa vichocheo hivyo, alama za balehe huonekana mapema kwa mhusika kuliko watoto wengine wa rika lake. [18] Balehe ya chelewa nayo tukio linaloweza kuwakumba watoto wa jinsia zote mbili, ingawa hali hii imeenea zaidi kwa wavulana kuliko wasichana. Inadhaniwa kuwa kukosekana kwa alama za balehe hadi kufikia umri wa miaka kumi na saba ni kithibitisho cha balehe ya kuchelewa. [19]