Mkopo:Badaa
Badaa: ni itikadi maalumu inayohusiana na dhana ya kudhihirika kwa kazi ya Mola iliyo kinyume na matarajio ya waja Wake. Badaa ni miongoni mwa imani makhususi za mashehebu ya Shia. Kwa mtazamo wa wanazuoni wa Shia Imamiyya, badaa katika ulimwengu wa kimaada ni sawa mageuzi katika nyanja za kisheria. Nadharia ya badaa ina nafasi maalumu ndani ya mfumo wa itikadi za Kishia, kiasi ya kwamba Hadithi zinaipa kipaumbele na kuithamini zaidi ikilin ganishwa na itikadi nyengine za Kishia. Baadhi ya wanazuoni wa madhehebu ya Ahlu al-sunna, waituhumu itikadi ya badaa wakisema kwamba, imani hii ni sawa na kumsifu Mungu kwa sifa za ujinga, na ni kama vile Yeye alijutia hali ya mwanzo na kuamua kuleta marekebisho na mabadiliko ndani yake. Kwa maoni yao imani hii ni sawa na Mungu alikuwa na elimu juu ya jambo fulani, kisha jambo hilo hudhihiri katika mfumo mwengine na kuifanya elemu Yake ya mwanzo kuwa nje ya tokeo linalojiri baadaye. Kwa upande wa pili, wanazuoni wa Shia Imamiyya wanasimama kinyume na maelezo hayo. Wakitegemea Riwaya mbalimbali za upande wa Shia, wanasema kwamba, si sawa kabisa na nikufuru iliyowazi kumnasibisha Mwenye Ezi Mungu na sifa ya ujinga. Wao wanasema kwamba, dhana ya badaa inahusiana na Mungu kwa maana ya kwamba, Yeye kupitia uwezo alionao huamua kuyageza mambo fulani na kuyaleta katika sura ambayo haikutarajiwa na waja Wake, huku akiwa na elimu kamili ya hali zote mbili (iliyofuata na ile ya mwanzo). Kuna chambuzi mbalimbali zilizonukuliwa kutoka katika Riwaya kuhusiana na dhana hii, miongoni mwazo ni pamoja na; kujenga matumaini ya Mungu ndani ya nyoyo za waumini, kujenga hamasa ya kushikamana na dua na shufaa kutokana na makosa yao mbalimbali. Uchambuzi wa Kiisimu (Dhana) na Nafasi Yake Dhana ya badaa «بِداء» ni istilahi maalumu inayohusiana na nyanja za kiitikadi (teheolojia). Katika nyanja za kiitikadi, dhana ya badaa humaanisha hali ya kudhihiri kwa jambo fulani na kuchukuwa sura mpya kinyume na ile iliyotangulia. Kiuhalisia katika tukio la badaa, Mwenye Ezi Mungu huchukuwa hatua ya kuliondoa jambo la awali na kuthibitisha jambo jengine katika nafasi ya jambo hilo, huku akiwa na elimu kamili ya mawili hayo. [1] Kulingana na ufafanuzi wa Sheikh Mufid, badaa ni udhihirikaji wa jambo fulani kutoka kwa Mwenye Ezid Mungu, kinyume na matarajio yaliopo katika hali ya kawaida. [2] Badaa ni itikadi mahususi ya madhehebu ya Shia peke yake. [3] Uhusianao Kati ya Badaa na Ufutwaji wa Sheria Mirdamad katika kitabu chake “Nibrasu al-Dhiyaa”, anasema: Badaa katika ulimwengu wa kimaada ni sawa na ufutwaji wa sheria uliopo katika nyanja za kisheria. [4] Muhammad Hussein Kashifu al-Ghitaa naye katika kitabu chake “Aslu al-Shia wa Usuliha”, anasema: kama ilivyo katika uwanja wa kisheria, kwamba kulingana na maslahi fulani Mwenye Ezi Mungu huondoa (hufuta) hukumo fulani na kuweka mahala pake hukumu nyengine mpya, vivyo hivyo katika ulimwengu wa kimaada, Mwenye Ezi Mungu huamua kudhihirisha tukio fulani litakalokuja baadaye, ambapo wakati mwengine huamua kuwapasha habari Malaika Wake wa karibu au Mitume wake kuhusiana na tukio hilo, kisha Mitume hao na wakawapasha habari watu wa umma wao juu ya tukio hilo, ila Mwenye Ezi Mungu akatenda vyengine kabisa, kinyemu na matarajio ya tukio hilo la mwanzo lililokuwa likisubiriwa kulingana na babari hizo za mwanzo. [5] Kwa mujibu wa ufafanuzi uliokuwepo ndani ya vyanzo vya Riwaya kuhusiana na dhana ya badaa, yaonekana kuwa dhana hii ni yenye kufungamana na nyilimwengu zote mbili; ulimwengu wa kimaada ikiwemo suala la kuakhirishwa kwa nyakati za mauti kutokana na kuwajali jamaa zake au kuharakiwa na mauti kwa yule atendaye dhambi, pamoja na ulimwengu wa kisheria ikiwemo suala la kubadilishwa kwa kibla cha Waislamu kutoka Baitu al-Maqdis kwenda kwenye Al-kaaba iliyoko mjini Makka. [6] Umuhimu wa Dhana ya Badaa Mbele ya Mashia Dhana ya Badaa ni yenye umuhimu mkubwa ndani ya itikadi za Shia. [7] Kulingana na maelezo ya Jaafar Subhani, ni vitavu vichache mno miongoni vilitungwa na Mashia kwa ajili ya masula ya kiitikadi na kifalsafa, ambavyo havikutaja dhana ya badaa ndani yake. Bali kuna makala na vitabu kadhaa miongoni mwa wanazuoni wa Shia vilivyoandikwa kuhusiana na dhana hii. [8] Kuna idadi ya kazi 25 andishi zilizoorodheshwa na Agha Bozorge Tehrani katika “al-Dhari’a” kuhusiana na dhana ya badaa. [9] Dhana ya badaa imetengewa milango maalumu ndani vyanzo mbalimbali vya Riwaya za Kishia. Kwa mfano sheikh ametenga mlango maalumu uitwao “Babu al-Badaa”, kwa ajili ya mada ya badaaa katika kitabu chake kijulikanacho kwa jina la al-Kafi. [10] Sheikh Saduq naye pia ametenga mlango maalumu kwa ajili ya dhana ya badaa katika kitabu chake kiitwacho “al-Tauhid”. Mlango ambao umekuja na Riwaya 11 kwa ajili ya uchambuzi wa mada hiyo. [11] Pia tukirudi wa Majlisi, tutamkuta amekusanya Riwaya 70 katika kitabu chake cha Biharu al-Anwar, zilizokuja kuzungumzia dhana ya badaa huku zikibeba mzizi halisi wa neno badaa ndani yake. Aidha mwanazuoni hayo amekusanya Riwaya zote zenye kuhusiana na upendekezwaji wa kuomba dua na umuhimu wa kutoa sadaka kwenye mlango wenye orodha ya Riwaya zinazotumika katika kuthibitisha dhana ya badaa. [12] Iamani juu ya dhana ya badaa ni miongoni mwa masuala yaliopewa sisitizo na umuhimu maalumu ndani ya baadhi ya Riwaya. Katika moja ya Riwaya za bwana Zurara aliyoinukuu kutoka Imamu Baqir na Imamu Sadiq (a.s) kuna maelezo yasemayo kwamba: “مَا عُبِدَاللَّهُ بِشَيْءٍ مِثْلِ الْبَدَاءِ؛” (Hakuna nyezo iliyotumika kumwabudia Mwenye Ezi Mungu kama ilivyo nyenzo ya badaa). [13] Pia Imamu Sadiq (a.s) katika moja ya Riwaya iliyonukuliwa na Hisham bin Salim anasema: “مَا عُظِّمَ اللَّهُ بِمِثْلِ الْبدَاءِ؛.” Hakana sehemu (nyanja) ayotukuzwa Mwenye Ezi Mungu kama alivyotukuzwa kwenye badaa. [14] Ukosoaji Dhidi ya Badaa Baadhi ya wanazuoni akiwemo Ahmad Ka’abi Balhi [15] (aliyefariki: 319 Hijiria), ambaye ni mfasiri na mwanatheolojia wa upande Mu’utazili pamoja na Fakhru al-Razi, [16] wanakosoa dhana ya badaa wakisema kwamba, imani juu ya badaa ni sawa na kumnasibishia Mungu sifa ya ujinga, kwani badaa hupelekea mabadiliko ndani ya elimu ya Mungu. Hili ni moja miongoni mwa mambo yaliopelekea wanazuoni wa Kiwahabi kuwakwaruza wafwasi wa madhehebu ya Shia Imamiyya. [17] Kwa dhana zao, dhana ya badaa ishikiliwayo na Mashia inamaanisha kwamba, hapo awali Mungu alipanga mpango wa kufanya jambo fulani kulingana na maslahi yaliyoyaona ndani ya mipango Yake, kisha akaghairi kutokana na utambuzi mpya juu ya maslahi hayo, jambo linalomaanisha kuwepo kwa ujinga wa Mungu katika utambuzi wake wa awali, jambo ambalo limemfanya kubadili mawazo yake baada ya kupata utambuzi kamili juu ya uhalisia na matokeo ya jambo hilo. [18] Mashia wakijijaribu kujibu okosoaji huu wanasema: “Aina kama hiyo ya badaa ni sifa ya kibinadamu na ni kufuru ya kabisa kuichukuwa sifa kama hiyo na kupachika nayo Mwenye Ezi Mungu”. [19] Kuna Riwaya kadhaa katika vyanzo vya Shia zinazosimama dhidi kumsifu Mwenye Ezi kwa sifa kama hiyo. [20] Miongoni mwa Riwaya hizo ni zile zitokazo kwa Imamu Sadiq (a.s), zisemazo: • “Amemkufuru Mola Mtukufu yule anayedhani kwamba, Mwenye Ezi mungu ametenda jambo fulani kutokana kujutia wazo lake la mwanzo”. • “Hakuna chochote kile kinachojiri kwa Mwenye Ezi Mungu, isipokuwa elimu yake ilikuwa wazi kabisa mbele Yake”. [21] • “Hakuna chochote kile kinachojiri mbele ya Mungu, ambacho hujiri kutoka na ujinga wa Mungu uliokitangulia kitu hicho”. [22] Khitilafu Zilizopo Kati ya Medhehebu ya Kiislamu Kuhusiana na Badaa ni Khitilafu za Kilugha Kulingana na imani ya Sheikh Saduq, khitilafu zilizopo kati ya mdhehebu mbalimbali za Kiislamu kuhusiana na dhana ya badaa, ni khitilafu za kilugha (katika utumiaji wa maneno). Kwani hakuna hata mmoja kati yao anayekataa kuwepo kwa hali ya kufutwa na kuondolewa kwa baadhi ya sheria au dini fulani ndani ya zama mbalimbali, na wala hakuna anayekataa kuwepo maskini aliyefanywa tajiri au mfu aliyefufuliwa n.k. [23] Yeye anaamini kwamba, mambo kama hayo yaliyosheheni kweye Hadithi na Aya za Qur’ani, ambayo hakuna hata mmoja kati ya Waislamu anayekinzana nayo, ni yenye uhusianao wa moja kwa moja na dhana ya badaa. [24] Aidha Sayyid Muhammad Husseina Tabatabai, naye pia anaamini kwamba, khitilafu zilizopo kati ya Waislamu kuhusiana na dhana hiyo, ni khitilafu za kilugha tu, akifafanua suala hili anasema: “Kama kutapita tafakuri ya kina kuhusiana na dhana hii, katu hakutakuwa na mzozo utakaoendelea juu ya jambo hilo”. [25] Pia tukirudi kwenye vyanzo vya Hadithi vya upande wamadhehebu ya Ahlu al-Sunna, tutakuna nukuu kadhaa kuhusiana na dhana ya badaa. [26] Aidha vyanzo hivyo vinahimiza na kutoa bishara njema kwa wale wajengao mahusiano mema na jamaa zao, jambo lenye uhusiano wa moja kwa moja na dhana badaa. [27] Jee Badaa ni Hupelekea Mabadiliko Kwenye Elimu ya Mungu? Imamu Sadiq (a.s) anasema: إِنَّ لِلَّهِ عِلْمَیْنِ: عِلْمٌ مَکْنُونٌ مَخْزُونٌ لَا یَعْلَمُهُ إِلَّا هُوَ، مِنْ ذَلِکَ یَکُونُ الْبَدَاءُ و عِلْمٌ عَلَّمَهُ مَلَائِکَتَهُ وَ رُسُلَهُ وَ أَنْبِیَاءَهُ فَنَحْنُ نَعْلَمُهُ؛ Kwa hakika Mwenye Ezi Mungu ana aina mbili za elimu; elimu iliofichika na iliyohifadhiwa Kwake, ambayo hakuna aijuwaye ila Yeye peke Yake, hii ndiyo elimu itendayo badaa. Na elimu ya pili ni ile elimu anayowajuza nayo Malaika Wake, Mitume Yake pamoja na Manabii Wake, nasi twaijua elimu. Koleini: Kitabu cha Al-Kafi, juz. 1, uk. 147. Kulingana na itikadi za Mashia, kuamini dhana ya badaa hakupelekea wala hakulazimiani na ujinga wala kupatikana kwa mabaediliko katika elimu au matakwa ya Mungu. [28] Baadhi ya wanazuoni wakitegemea Aya ya 39 ya Suratu al-Raad {Malezo 1: یَمْحُو اللَّهُ مَا یَشَاءُ وَیُثْبِتُ وَعِنْدَهُ أُمُّ الْکِتَابِ؛ / Mwenye Ezi hufuta alitakalo na hulithibitisha alitakalo, na katika kuu iko mkononi mwake (Aya ya 39 ya Suratu al-Raad)} pamoja na baadhi ya Riwaya, [29] akiwemo Allama Majlisi na Muhammad Hussein Tabatabai wanaamini kwamba, Mwenye Ezi Mungu ametayarisha mbao mbili, na kila litokealo huwa tayari katika orodha zilizomo mbaoni humo. Moja ya mbao mbili hizo ni Lauhu al-Mahfudh; mbao hii huorodhesha matukio yote thabiti yasiyopatwa na mabadiliko au mageuzi fulani ndani yake. Mbao ya pili ni ile iitwayo Lauhu Mahwi wa al-Ithbaat; mbao hii huorodhesha mambo ya Mwenye Ezi Mungu yenye uwezo wa kupata mabadiliko kulingana na hali pamoja na matakwa ya Mungu, huku Mungu akiwa na elimu kamili juu ya mambo yote bila ya kuponyokwa kati fulani ndani yake. Miongoni mwa mifano inayoweza kuingia katika mbao hii, ni yule mtu aliyeandikiwa kuishi miaka hamsini, ila baada ya kutoa sadaka au kujenga mahusiano mazuri na jamaa zake, Mwenye Ezi Mungu huiondoa hitima ya mwanzo na kumpa hatima mpya kabisa inayopindukia umri wa hatima ya mwanzo. Au pia yawezekana mtu kutenda jambo fulani ambalo hatima yake ni kupungukiwa na umri wake ulikwisha wekwa kwenye mbao ya Mahwi wa al-Ithbaat. Mashi wameyapa mabadiliko haya jina la badaa. [30] Mwanazuoni maarufu ambaye ni mfasiri wa Qur’ani na mwanafalsafa maarufu wa Kishia ansema: “Hakunabadiliko linalopatikana kwenye dhati ya Mungu katika upatikanaji wa tukio la badaa, mabadiliko haya hutokea kwenye uwanja wa elimu ya utendaji wake. [31] Kulingana na ufafanuzi wa mwanazuoni huyu, elimu ya dhati ya Mungu ni elimu ya kiazali (isiyo na mwanzo katika uwepo wake) na kiabadi (isiyo na mwisho katika uwepo wake), nayo ni elimu isikubali aina yoyote ile ya mabadiliko ndani yake, ila elimu ya mendo Yake ni sawa na utokeaji matendo Yake, ambayo huwezekana kupupitiwa na mabadiliko ndani yake. [32]
Dhana ya Badaa Hailazimiani Wala Haimpelekei Mungu Kusifika kwa Sifa ya Ujinga Mulla Saleh Mazandarani akifafanua dhana ya badaa anesema: “Elimu ya Mwenye Ezi Mungu ni ya kiazali (ya tangu na tangu isiyo na mwanzo), na tokea hapo mwanzo alikuwa na elimu kamili juu ya mabadiliko yatakayokuja kutokana na kuondoka au kuja kwa maslahi ya jambo fulani. Hivyo basi yeyote yule anayeamini kinyume na hivyo, kwa mfano adai kwamba leo Mwenye Ezi Mungu ameweza kujua jambo fulani ambalo hapo mwanzo hakuwa na elimu nalo, bila shaka kwa usemi wake huo atakuwa amemkufuru Mwenye Ezi Mungu. [33] Kulingana na maelezo ya Abudullahi Jawad Amuli, Mwenye Ezi Mungu ni mwenye elimu angazi (shuhudi), yenye kuangaza kila kita tokea azili (zama tangu zisizo na mwanzo) hadi abadi (zama endelevu zisizo na mwisho), hivyo Yeye ni Mjuzi wa mabadiliko na matokeo ya kila kitu, na Yuwajua wazi mabadiliko yote yanayojiri ya yatakayojiri kuhusiana na vitu hivyo kutoka zama moja hadi nyengine. Hivyo basi, mbele ya Mwenye Ezi Mungu hakuna suala mipaka ya zama katika utokeaji matukio mbalimbali, bali akili na jicho la mwanadamu ndilo linaloangaza kulingana na dhana ya zama na nyakati mbalimbali. [34] Mifano ya Mtukio ya Kihistoria ya Kutokea kwa Badaa Ifuatayo ni miongoni mwa mifano ya kihistoria fkuhudiana na badaa, iliyoripotiwa kutoka katika Qur’ani na vyanzo vya Hadithi: • Tukirudi katika Qur’ani tunakutana na ile kesi ya watu wa Nabii Yunus iliyoripotiwa ndani ya Suratu Al-Yunus, Aya ya 98). Kwa mujibu wa Aya hii, baada ya watu Nabii Yunus kupinga mara kwa mara maagizo ya mola wao, Mwenye Ezi Mungu alianza kudaa adhabu maalumu dhidi yao. Baada ya Nabii Yunus kukata tamaa juu uongofu wa watu hao, aliamua kuachana nao na kutafuta usalama wa roho yake. Hata hivyo, mmoja ya wenye hekima kati yao kutambua na kuona alama za adhabu zinavyokaribia, aliwakusanya wenzake na kuwaamrisha kufanya toba mbele ya Mola wao. Mwenyezi Mungu, kwa rehema yake, alipokea toba hiyo na kuwaondolea adhabu iliyokuwa taya imeshakaribia kupia alama mbalimbali. [35] • Aidha kati ya matukio ya badaa yaliripotiwa na Qu’ani, ni ughairishwaji wa amri ya Nabii Ibrahim. Aya ya 102 hadi 107 za Suratu Saaffaat, zinafafanua zikisema kwamba, Nabii Ibrahim aliamriwa kumchinja mwnawe (Ismail), naye akaamua kumchukua mwanawe machinjioni kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mola wake. Ila baada ya yeye kuonesha utayari wake katika kutekeleza amri hiyo, Mwenye Ezi Mungu alidhihirisha badaa ilipo nyuma ya pazia la ghaibu. Hivyo basi akatangaza wazi kwamba hiyo ilikuwa ni mtihani maalumu kwa ajili ya kupima kiwango cha utiifu wa Nabii Ibrahim pamoja na mwanawe. [36] • Aya ya 142 ya Suratu al-Aaraaf ni nyengine inayoashiria kuwepo kwa mbaadhi ya matukio ya badaaa. Kwa mujibu wa Aya hii, Nabii musa alipaswa kutengana na umma kwa muda wa siku 30, kwa ajili ya kuelekea kwenye miadi ya Mola wake yenye lengo kumkabidhi sheria za Mungu. Ila baada ya hapo aliongezewa siku 10 nyengine za ziada, jambo ambalo lilikuwa ni mtihani maalumu kwa Wana wa Israili. [37] • Miongoni mwa matukio yanayohusiana na badaa yaliyoripotiwa ndani ya vyanzo vya kihistoria vya Shia, ni vifo vya baadhi ya watoto wa Mimamu wao, waliamini kwamba walikuwa ndio warithi halisi wa nafasi za baba zao. Watoto hao ni Ismail mwana mkuu wa Imamu Sadiq (a.s), [38] pamoja na Muhammad mwana wa Imamu Hadi (a.s). [39] Kwa mujibu wa imani za baadhi ya Mashia, Isamail ndiye aliyekuwa na haki ya kushika nafasi ya Uimamu baada ya Sadiq (a.s), na Muhammad ndiye aliyekuwa na haki ya kushika nafasi ya Imamu Hadi (a.s). Ila vifo vyao vilivyotokea katika zama za uhai wa baba zao, vinafasiriwa kama ni badaa iliyowaondoa watoto hao katika nafasi hizo. [40] Matokeo ya Imani Juu ya Badaa Miongoni mwa matokeo au natija zinazojiri kwa waumini wa imani ya badaa ni kama ifuatavyo: • Kukiri Juu ya Uwezo wa Mungu: Kukiri na kusalimu amri mbele ya uwezo wa Mungu usio na mipaka, ni miopngoni mwa mihili muhimu ya itikadi. Hii ni kwa maana ya kwamba, kama kutotokea mabadiliko fulani ndani undedaji wa Mungu ambao kikawaida hutendeka kwa njia fulani inayotarajiwa na waja wake, hiyo haitapelekea kuteterekwa imani ya mja. Kwani yeye anakuwa na welewa tosha ya kwamba, Mola wake aweza kubadilisha matokeo mbalimbali kulingana na maslahi yalivyo. [41] • Kuimarika kwa Matumaini: Itikadi ya badaa hujenga matumaini maalumu ndani ya nyoyo za waumini, jambo ambalo hawanya wasikate tamaa kutokana na matokea fulani. Na hii huwapa tamaa ya kuendelea na kuomba Mola wao kupitia dua zao zenye matumaini ya kupata mabadiliko kutoka kwa Mungu. [42] • Kukanusha Badaa Kunapelekea Uzorotaji: Ukanushaji wa badaa hupelekea kuamini imani kuwepo kwa hatima iliyotanguliwa na muhuri wa kalamu ya Mungu na isyoweza kubadilika. Hii huwapelekea waja kukata tamaa na kuwa wavivu wa kuomba dua na kushikana na jitihada zinazoweza kubadilisha hatima yao, [43] hali kwamba, hakuna hata Muislamu mmoja mwenye kutengana au kukanusha faida za dua. [44] • Matumaini Juu ya Toba: Imani juu ya badaa humpa muumini matumaini ya kukubaliwa toba yake na kupata msamaha wa Mola wake. Pia humfanya aepukane na makosa makuwa kwa tamaa ya kupata msamaha wa makosa yake madogo madogo yaliyotangulia. [45] Makala Zinazofungamana Kadhaa na Qadar