Mkopo:Aya ya 34 ya Suratu an-Nisaa
Aya ya 34 ya Suratu an-Nisaa اَلرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَی النِّسَاءِ: inayoanza kwa kauli isemayo “Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake” (An-Nisaa: 34) ni Aya inaelekezea dhana ya uwajibikaji na usimamizi wa mwanamme juu ya mwanamke ndani ya taasisi ya familia. Aya hii pia inabainisha wajibu wa kila upande katika uhusiano wa ndoa; mwanamme kubeba jukumu la kugharamia mahitaji ya maisha, na mwanamke kulinda mali, heshima na amana za mwnamme (mume) katika mipaka ya maadili ya Kiislamu. Katika vyanzo vya tafsiri vya Ahl al-Sunna, kumetajwa sababu mbalimbali za kushuka (asbab al-nuzul) kwa Aya hii. Hata hivyo, baadhi ya wafasiri wa Kishia wamezichambua na kuzikosoa Riwaya hizo.
Kwa mujibu wa maoni ya wafasiri wa Kishia, Aya hii inabeba maana kuu tatu. Kwanza, inaeleza nafasi ya mwanamme katika kusimamia familia, ikisisitiza dhana ya uti wa mgongo kwa maana ya uongozi wenye mipango madhubuti, uwajibikaji wa kiuchumi, na uangalizi wa ustawi wa familia. Pili, Aya inataja majukumu ya pande zote mbili za mume na mke, ikiwemo jukumu la mume kutoa matumizi na jukumu la mke kulinda heshima na hadhi ya familia. Tatu, Aya inaelekeza mbinu za kukabiliana na hali ya kutotii kwa mke, kwa mpangilio unaoanzia nasaha, kisha kujitenga kitandani, na hatimaye adhabu nyepesi isiyokuwa ya kuumiza, kwa sharti la kutanguliza uadilifu na kuepuka aina yoyote ile ya ukatili unaoweza kusababisha madhara. Miongoni mwa wafasiri wa Kishia, Muhammad Sadiqi Tehrani na Sayyid Hasan Mustafawī wanaamini kwamba; Aya hii haibebi maana ya uongozi wa kimamlaka au uwakala wa wanaume juu ya wanawake, bali inaeleza wajibu wa wanaume kusimamia na kutekeleza mahitaji ya wanawake katika masuala ya maisha ya kifamilia. Kitabu huru kiitwacho Risala Badia, kilichoandikwa na Sayyid Muhammad‑Hussein Husseiniy Tehraniy, ni kitabu maalumu kilichochunguza Aya hii kwa mtazamo wa kifalsafa na kifiqhi, kikifafanua nafasi ya mwanamume na mwanamke katika mfumo wa haki na majukumu ya kifamilia. Matini ya Aya na Maana Yake ﴿الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ وَبِمَا أَنْفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّهُ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا ٣٤﴾ Wanaume ni wasimamizi wa wanawake (ndio wenye mamlaka juu ya wanawake) kwa sababu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baina yao kwa wengine (wanawake), na kwa sababu ya matumizi wanayoyatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni watiifu, na ni walinzi wa siri (na heshima za waume zao) kwa yale ambayo Mwenye Ezi Mungu ametaka yalindwe. Na wale ambao mnakhofu uasi wao, basi washawishini kwa mawaidha; kisha jitengeni nao katika malazi; na ikiwa bado haitoshi, chukueni hatua ya kuadhibu kwa upole. Ila wakikutiini, basi msitafute njia yoyote ya kuwadhuru. Hakika Mwenye Ezi Mungu ni Mwenye utuku Juu na Adhimu mno.
Suratu al-Nisaa Aya ya 34.
Aya ya thelathini na nne ya Suratu An-Nisa ni andiko maalumu la kisheria, liinalotumika kama rejea kuu ya kifiqhi na kijamii inayohalalisha dhana ya Usimamizi (Guardianship) na mamlaka ya kiutawala ya wanaume dhidi ya wanawake, [1] na katika muktadha wa kifamilia. [2] Wasomi na wafasiri wa Qur’anai wanaeleza kuwa, kupitia aya hii, Mwenyezi Mungu amefanya upembuzi yakinifu kuhusu hadhi (status) na majukumu ya mwanaume, huku akibainisha mipaka ya kiutendaji. Aidha, andiko hili limeainisha wajibu mbadala (reciprocal duties) wa mke kwa mumewe. Muundo huu wa kimajukumu unawasilishwa kama nyenzo ya kistratejia ya kuzuia mmomonyoko wa maadili na kuvunjika kwa taasisi ya ndoa, jambo ambalo ni muhimu kwa maisha ya kijamii. [3] Sababu ya Kushuka kwa Aya Hii Wafasiri wa Ahl al-Sunna wataja sababu mbili kuu za kushuka kwa Aya ya “Al-rijal qawwaamuuna ala al-nisaa”: 1. Sa‘ad bin Rabii na mkewe Habiba: Baadhi ya vitabu vya tafsiri vinaripoti kuwa Sa‘ad bin Rabii, mmoja wa wakubwa wa Ansari, alimpiga mkewe ambaye ni Habība kwa madai ya kutotii. Habiba, akiwa pamoja na baba yake, walikwenda kumlalamikia Mtume (s.a.w.w) juu ya tukio hilo. Mwanzoni Mtume (s.a.w.w) alisema: “Mwanamke ana haki ya kulipiza kisasi.” Lakini kabla hatua haijachukuliwa, ikateremshwa Aya “ar-rijaalu qawwamuuna ala an-nisaa’…”. Baada ya kushuka kwa Aya, Mtume (s.a.w.w) akasema: “Rudini; tulikusudia jambo, lakini Allah amekusudia jambo jingine, na lile Alilotaka Yeye ndilo bora zaidi.” [4] 2. Swali la wanawake juu ya urithi: Kwa mujibu wa maelezo ya Fakhr Razi, sababu ya kushuka kwa aya hii ni maswali na mazungumzo ya baadhi ya wanawake waliodadisi wakisema ni kwa nini wanaume hupata sehemu kubwa zaidi ya urithi. Hivyo basi mujibu wa Razi, Aya hii ilishuka kama jibu la dadisi hizo, ikibainisha kuwa wanaume wamepewa majukumu kadhaa ya kifedha, kama vile kulipa mahari na kugharamia matumizi ya familia. Kwa hivyo, sehemu yao kubwa ya urithi inalingana na majukumu yao ya kifedha. [5] Sayyid Muhammad‑Hussein Tabatabai anaamini kuwa, Riwaya zinazodai kuwa Habiba alipigwa na mumewe (Saad bin Rabi) inayohusishwa na kushuka kwa aya ya hii, zinakabiliwa na matatizo makubwa ya kihoja na kiitikadi. Akifafanua suala hili anasema; hata kama tukikubaliana na usahihi wa Riwaya hizi, bado haziwezi kuthibitisha kuwa bwana Mtume (s.a.w.w) alitoa hukumu. Yeye anaamini kuwa bwana Mtume (s.a.w.w) hakutoa uamuzi wa kisheria, bali alijibu swali tu. Kwani ili hukumu ya kisheria itolewe, pande zote mbili za mgogoro zinapaswa kuwepo mbele ya bwana Mtume (s.a.w.w) kama hakimu. Pili
Kukubaliana na Riwaya hizi kunamaanisha dai la kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alikosea na alitoa hukumu isiyo sahihi, na hapo ndipo Qur’ani ikashuka kwa ajili ya kumrekebisha. Hili linapingana moja kwa moja na itikadi ya kutokukosea kwa bwana Mtume (s.a.w.w). Haiwezekani Mtume atoe hukumu ya kisheria yenye makosa, kisha Qur’ani imrekebishe. Kwa sababu hizi mbili, Tabatabai anahitimisha kuwa sababu hii ya kushuka kwa Aya husika haiwezi kukubalika kama sababu sahihi ya kushuka Aya hiyo. [6] Maudhui ya Aya Imeelezwa kwamba Aya hii inabeba maudhui kadhaa ya kimsingi yanayohusiana na muundo na uthabiti wa familia katika mtazamo wa Kiislamu. Kwanza kabisa, inazungumzia uwajibikaji na uongozi wa mwanaume ndani ya familia (kama uti wa mgongo), yaani jukumu la kusimamia na kulinda maslahi ya familia kwa misingi ya haki na wajibu. Pili, inabainisha wajibu wa mwanaume kugharamia mahitaji ya maisha, jambo linalohusishwa na dhima yake ya kiuchumi katika ndoa. Tatu, Aya inaashiria uwiano wa haki na wajibu baina ya wanandoa, kwa lengo la kudumisha utulivu, mshikamano na uendelevu wa familia. Nne, inatoa miongozo ya kushughulikia hali ya usugu wa kutotii amri kwa upande wa mke, kwa madhumuni ya kuzuia migogoro isisababishe kusambaratika kwa taasisi ya ndoa. [7] Usimamizi na Uongozi katika Familia Makala kuu: Mamlaka ya wanaume juu ya wanawake Kwa ujumla wafasiri wametoa mitazamo mitatu mikuu ya kitafsiri katika kutafsiri ibara isemayo: “الرجال قوامون على النساء” iliyoko katika Aya ya 34 ya Sura al-Nisaa: • Mtazamo wa Kwanza: Wanazuoni wengi wa Kishia wameielewa dhana ya mamlaka ya wanaume kama ni uongozi na usimamizi wa familia, wakaitaja kwa istilahi kama vile uangalizi, [8] ulinzi (usimamizi) wa kisheria (uwalii), [9] mamlaka au uongozi wa familia. [10] • Mtazamo wa Pili: Baadhi ya wafasiri wameifasiri dhana hii kwa maana ya kusimamia, kuhudumia na kutekeleza majukumu yanayohusu wanawake, si kwa maana ya kuwatawala bali kuwasimamia kutekeleza wajibu wao. [11] Sayyid Hassan Mostafawi pia anaamini kwamba Aya ya hii inaashiria kusimamia na kushughulikia mambo yanayohusiana na wanawake peke yake, na wala haimaanishi kuwatawala au kuwaweka chini ya mamlaka. [12] • Mtazamo wa Tatu: Kundi jingine miongoni mwa wanazuoni, limeunganisha mitazamo miwili hiyo, likieleza kwamba malaka yaliyotajwa katika Aya hii, haimaanishi kuwasimamia kwa namana ya kutoa amri na kuwakataza tu, bali pia ni imaanisha kujali hadhi ya wanawake na kushughulikia maslahi yao, kwa namna inayodumisha utulivu wa familia. [13] Majukumu ya Kiafiki Kati ya Wanandoa
Kulingana na mitazamo ya wanazuoni wa tafsiri wa mrengo wa Kishia, sehemu nyingine ya Aya ya 34 ya Suratu an-Nisa isemayo: (وَبِمَا أَنْفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ) imekuja kuelezea majukumu ya kisheria na kimaadili ya wanandoa kila mmoja kwa mwenzake. Wasomi hawa wanafafanua kuwa maudhui ya kipengele hichi yanalenga jukumu la mume la kugharamia mahitaji ya kimsingi ya maisha kwa hadhi inayostahiki. Hii inajumuisha utoaji wa mahitaji yote ya mke pamoja na watoto wake, kulipa mahari, pamoja na jukumu la kuhifadhi mfumo na fungamano la taasisi ya familia. [14]
Kulingana na tafsiri zilizopo mikononi mwetu, mkabala wa majukumu aliyopewa mume kwa kila mmoja kati ya watu wa familia yake, pia Mwenye Ezi Mungu amempa mke jukumu la kuwa mnyenyekevu, mwenye ushirikiano, na mshikamanifu katika mfumo wa kifamilia. Mke anapaswa kutekeleza kikamilifu wajibu wake wa ndoa kwa kumtii mume wake na kulinda heshima pamoja na mali za mumewe, hii haihusiani tu na kipindi cha kuwepo mume huyo, bali hata katika kipindi cha kutokuwepo kwake. Hivyo, anawajibika kuhifadhi hadhi na heshima ya mume na kuepuka kabisa usaliti dhidi ya mumewe. [15] Njia na Mchakato wa Kuhifashi Familia Katika Sehemu ya mwisho ya Aya hii, Mwenye Ezi Mungu amekuja kufafanua mbinu za kisheria za kuamiliana na wanawake wakaidi (Naashizah). Wanazuoni wa tafsiri wanasisitiza kuwa mume anawajibika kutekeleza mikakati iliyoainishwa na sheria (nasaha, kujitenga kimalazi, na ashabu ya kipigo ya kiwango cha chini) kwa mfumo wa kimantiki wa hatua kwa hatua pasina kuvuka mipaka ya usawa (uadilifu). [16] Makarim Shirazi, katika kazi yake ya Tafsir Nemooneh, amechambua mlolongo wa hatua hizo kama ifuatavyo: • Mchakato wa Kunasahi (فَعِظُوهُنَّ): Hatua ya kwanza inayohusisha utoaji wa miongozo ya kimaadili kwa namna ya kirafiki na ufafanuzi wa athari haribifu za mienendo ya mke. • Kukihama kitanda (Hijr): Ikiwa athari ya nasaha haitaleta faida, hatua inayofuata ni kujitenga na mke ndani ya mazingira ya malazi (وَاهْجُرُوهُنَّ فِی الْمَضاجِعِ). Sayyid Muhammad Hussein Tabataba'i anabainisha akisema kuwa, dhana hii haimaanishi kutelekeza kitanda, bali ni kutoa ishara kuonesha kutokuridhika kwako kupitia lugha ya mwili, kama vile kugeuza mgongo na kusitisha mahusiano ya kimahaba huku mkiwa katika kitanda kimoja. [17] • Adhabu ya Kinidhamu (وَاضْرِبُوهُنَّ): Katika hali ya ukaidi uliokithiri unaotishia utengamano wa familia, hatua ya mwisho inayofuatia, ni adhabu nyepesi kama ilivyoelezwa katika Riwaya [18] na vyanzo vya fiqhi. [19] Sharti la msingi la kisheria kuhusiana na hatua hii, ni kwamba adhabu hiyo isisababishe jeraha, kuvunjika kwa kiungo, wala mchubuko au alama ya weusi mwilini. [20]3
Katazo la Kushiriki Wanawake Bungeni Sayyid Muhammad Hussein Husseiniy Tehraniy, akitegemea Aya hii na kuaimbatanisha na baadhi ya Hadithi, anaona kuwa; kisheria hairuhusiwi wanawake kuingia katika Bungeni (yaani hawaruhusiwi ni wajumbe wala wawakilishi), hata kama wanawake hao wamefikia daraja ijitahidi. Yeye anaamini kuwa Mabunge ya zama hizi hayana tu jukumu la kutoa ushauri, bali yana mamlaka mkuu katika uongozi wa taifa. Aidha, kila bunge lina dhima ya kupanga sera katika nyanja zote za kiserikali, zikiwemo siasa, masuala ya kijamii, uchumi, utamaduni, na usalama (kama vile masuala ya vita na amani), pamoja na kusimamia muhimili wa utekelezaji. Kwa mujibu wa mtazamo wake, kiwango hiki cha mamlaka na uongozi mkuu wa umma hakiendani na ushiriki wa wanawake bungeni. [21] Mada Zinazohusiana: • Aya za nushuz • Nushuz • Mamlaka ya Wanaume juu ya Wanawake • Adhabu ya kimwili kwa wanawake