Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Aftab dar Masaf (Jua Katika Mapambano)

Kutoka wikishia

Aftab dar Masaf (Jua Katika Mapambano): ni jina la kitabu chenye anuani ndogo Sababu na Mwelekeo wa Tukio la Ashura, nacho ni kitabu kilichoandaliwa kupitia na matini ya hotuba za Sayyid Ali Khamenei, aliyekuwa ni Kiongozi wa pili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Matini hii imejikita katika kujadili nafasi ya Imamu Hussein (a.s) pamoja na kuchambua kwa kina muktadha na matukio yaliyoambatana na tukio la mapambano ya Karbala ya mwaka 61 Hijria. Matini ya kitabu hichi yanahusiana na hotuba zilitolewa katika kipindi cha kuanzia mwaka 1978 hadi 2011. Hichi kitabu chenye jina la Aftab dar Masaf (Jua Katika Mapambano) kimepangwa katka sura sita; ambapo ndani yake anajadiliwa Imam Hussein sambamba na kubainishwa kwa sababu, mazingira na malengo ya harakati zake. Kadhalika kitabu hichi kinazungumzia hali za wafuasi wake na wapinzani wake katika tukio la mapambano ya Karbala. Pia kinajumuisha baadhi ya dua zilizonukuliwa kutoka kwake pamoja na ziara zinazohisana naye. Uchapishaji wa awali wa kitabu hichi ulikamilika mnamo mwaka wa 2013 Miladia. Kutokana na mahitaji au umuhimu wake, matini hii iliduriwa na kuchapishwa mara kwa mara. Na hadi kufikia mwaka 2022 kitabu hichi kileweza kuchapishwa mara mara kumi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji mbalimbali. Pia matini ya kitabu hichi ilizaa akitabu chengine kipya kabisa kilichofahamika kwa jina la “Darsehaye Ashura” (Mafunzo Kutoka katika Tukio la Ashura). Mwandishi Makala Kuu: Sayyid Ali Khamenei Mwandishi wa kitabu hichi, ni Sayyid Ali Husseini Khamenei, aliyekuwa akishikilia nafasi ya uongozi mkuu nchini Iran. Kiongozi alipambanua na kudhihiri kama mwanazuoni na mchambuzi mahiri wa historia ya Kiislamu. Kupitia hotuba na kumbukumbu zake mbalimbali, alifanya upembuzi yakinifu wa historia, jambo lililopelekea baadhi ya uchambuzi huo kugeuzwa kuwa vitabu vya rejeo muhimu kabisa. Miongoni mwa kazi zake madhubuti, ni kama vile: Ensane 250 Saleh (Mtu wa Miaka 250), Pishvaye Sadeq (Kiongozi Mkweli), na Doo Imame Mojahed (Maimamu Wawili Wapiganaji). [1] Katika muktadha wa tukio la Karbala, mbali na kitabu cha msingi cha Aftab dar Masaf, pia kuna kazi nyengine tatu ziliandikwa kutoka katika za hotuba zake mbalimbali. Kazi hizo tatu maridani ni: Chahar Goftar (Kauli Nnne), Darshaye Ashura (Mafunzo Kutoka katika Tukio la Ashura), na 72 Sokhane Ashurai (Kauli za Kiashura). [2] Muundo na Maudhui za Kitabu Husika Maudhui ziliyomo katika kitabu cha Aftab dar Mesaf (Jua Katika Mapambano) chenye anuani fafanuzi isemayo: Ilal wa Ab’aade Haaditheye Ashura (Sababu na Vipengele vya Tukio la Ashura), zimepangwa kwa kuzingatia mfuatano wa wakati wa hotuba za Ayatullah Khamenei kuanzia mwaka 1978 Sh hadi 2011 Miladia. [3] Kitabu hichi kimegawanywa katika sura sita kuu, na muhtasari wa maudhui zake ni kama ifuatavyo: 1. Mambo ya Jumla: Sehemu hii inajumuisha mijadala ya utangulizi kama vile mafundisho ya Uislamu, maarifa ya Kiislamu, jamii ya Kiislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), Maimamu wa Kishia, pamoja na masuala ya kijamii na kisosholojia. [4] 2. Imamu Hussein (a.s): Sura hii inahusisha mada kadhaa ndani yake, kama vile: maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imau Hussein (a.s), haiba na shakhsia ya Imamu yake, pamoja na mafunzo yanayopatikana kutoka katika maisha na msimamo wake (a.s). [5] 3. Ashura: Sehemu hii inajadili vipengele mbalimbali, kama vile: utambuzi wa harakati za Imamu Hussein (a.s), mazingira yaliyopelekea mapinduzi yake, malengo ya harakati za mapinduzi yake, mbinu za mapambano, sifa za mapambano yake, siri ya kudumu kwa harakati za Imamu Hussein (a.s), wajibu na mambo yanayopaswa kuzingatiwa kuhusiana na Ashura, pamoja na upotoshaji uliofanywa kuhusu tukio hilo. [6] 4. Wasaidizi wa Ashura: Sehemu hii inawatambulisha baadhi ya watu mashuhuri walioshiriki katika tukio la Ashura, akiwemo: Zainab al-Kubra (a.s), Hadhrat Abbas (a.s), Ali al-Akbar (a.s), Muslim bin Aqil, Qasim bin Hassan, na Abdullah bin Hasan. [7] 5. Maadui wa Ashura: Sehemu hii inafafanua sifa za wale walioandaa mazingira na kusababisha kutokea kwa tukio la Ashura, akiwemo: Muawiyah bin Abi Sufian na Yazid bin Muawiyah, pamoja na kuelezea sifa zilizokuwa zikitawala katika zama zao. [8] 6. Ziara na dua: Sehemu hii imekuja kutoa utangulizi na ufafanuzi wa baadhi ya dua zilizopokewa kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) pamoja na ziara zilizopokewa kuhusiana naye, kama vile Dua ya Arafa, Ziara ya Ashura, na Ziara ya Arubaini. [9] Miongoni mwa sifa muhimu za kitabu hichi, ni kuepuka uandishi wenye utata katika matini yake, kugawa maudhui zake kwa mpangilio unaorahisisha uelewa kwa wasomaji wake, [10] pamoja na kuweka muhtasari wa mambo muhimu pembezoni mwa kurasa za kitabu zake, ili kuwawezesha wasomaji kuyafikia kwa urahisi zaidi yale malengo muhimu yaliokusidiwa kuwafikia. [11] Historia ya Uchapishaji Kitabu cha Aftab dar Masaf (Jua Katika Mapambano), kilikusanywa kwa juhudi za "Taasisi ya Kiutamaduni ya Hadith Lauh wa al-Qalam" na kuchapishwa na taasisi ya “Intishaarat Inqlabe Islami” (Islamic Revolution Publications). [12] Mara ya kwanza kilichapishwa mwaka 2013. [13] Kitabu hiki kilisanifiwa katika jumla ya kurasa 1040, ambapo katika matoleo mapya, kurasa 362 zinazojumuisha faharasa na orodha za majina ziliondolewa na kuwekwa katika tovuti ya taasisi ilichapisha kitabu hicho. [14] Hadi kufikia mwaka 2023, kitabu hichi kimechapishwa upya kwa mara kumi tofauti. [15] Aidha, kuna kitabu chengine kilichotolewa kutoka katika kitabu hichi mama, amabacho kimepewa jina la Dars-haye Ashura (Masomo ya Ashura), kitabu ambacho kimeandikwa kikiwa na kurasa 264 na kuchapishwa na taasisi hiyo hiyo iliyotajwa hapo mwanzo. [16]