Mkopo:Adhabu ya Zinaa
Adhabu ya Zinaa (Haddu al-Zinaa): ni adhabu maalumu ya Kiislamu inayotolewa dhidi ya mwanamme na mwanamke waliotenda tendo la kujamiiana bila ya kuwepo uhalali wa ndoa baina yao. Kulingana na hali na masharti tofauti ya watendaji wa tendo hili, adhabu hii hutekelezwa kupitia moja ya njia tatu zifuatazo: Ima huuawa, hupigwa mawe, au huchapwa bakora. Adhabu hii hutekelezwa pale tu mtenda wa kosa hili atakapokuwa ametimiza masharti fulani yanayoruhusu kuadhibiwa kwake. Mashariti haya ni kufikia umri wa kubalehe, kuwa na akili timamu, kutenda tendo hilo kwa hiari, na kuwa amelitenda tendo hilo huku akiwa naufahamu fika uharamu wa tendo la zinaa. Ili adhabu itekelezwe, ni lazima kosa la zinaa liwe lithibitishwa na mhusika huyo au kupitia ithibati maalumu inayoweza kudhaminiwa na kupata ushahidi wa mashahidi halali. Miongoni mwa mambo yanayopelekea kupata adhabu ya kuuawa, ni kuzini na jamaa wa karibu (maharimu) au kumbaka mwanamke fulani bila ya ridhaa yake. Adhabu ya kupigwa mawe humkabili yeyote yule afanyaye zinaa hali ya kuwa yumo katika maisha ya ndoa (muhsan), ilhali adhabu ya viboko hutolewa kwa wale wote wasiokuwa na uwezo wa kuwa na uhusiano wa halali (waliobaki bila ya ndoa kutokana na hali ngumu walizonazo). Kwa wanaume walikuwa tayari wameshaoa lakini bado hawajafanya tendo la ndoa na wake zao, pamoja na adhabu ya viboko, pia huongezewa adhabu ya kuhamishwa mijini mwao kwa muda wa mwaka mmoja huku wakiwa vipara (wamenyolewa nywele). Kwa mujibu wa maelezo ya Allama Tabatabai, mwanafalsafa wa Kishia, madhumuni makuu ya adhabu hizi ni kuzuia maovu na uharibifu wa maadili katika jamii. Kwa mtazamo wa wanazuoni wa fiqhi ya Kishia, utekelezaji wa adhabu ya zinaa ni jukumu la Imamu Maasumu au mwakilishi wake. Aidha kuna mitazamo tofauti, huhusiana na namna ya utekelezaji wa adhabu hizi katika kipindi cha ghaiba (kutowepo kwa Imamu Mahdi). Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa, faqihi mwenye sifa kamili, ndiye mwenye jukumu la utekelezaji wa sheria hizi, ilhali wengine wanaamini ulazima wa kusitishwa kwa sheria hizi katika kipindi cha ghaiba ya Imamu Maasumu. Utambulisho wa Dhana na Nafasi yake ya Kisheria
Adhabu au haddi ya zinaa ni hukumu maalumu ya kisheria ndani ya fiqhi ya Kiislamu inayolenga kuadhibu na kukomesha muingiliano wa kimwili usio wa halali kati ya jinsia mbili (ya kike na ya kiume). [1] Hukumu hii hubadilika na kutofautiana kulingana na sifa pamoja na mazingira maalum ya mtendaji wa kosa hilo. [2] Kupitia Aya ya 2 ya Suratu An-Nur, Quran imetoa mwongozo maalumu wa namna ya kuwapa adhabu wazinifu. Allamah Tabatabai akifafanua mtazamo wake anasema: “Kwa kuzingatia maelezo ya Aya hii, mchakato wa utekelezaji wa haddi ya zinaa (adhabu za zinaa) unapaswa kufanyika bila ya kuyzingatia msingi wa huruma katika adhabu hiyo, kwani lengo la adhabu hii ni kuleta kemeo kali dhidi ya dhambi hii hatari, jambo linalofikiwa kupitia msisitizo na ukali katika utekelezaji wa adhabu zake. [3] Kuna ripoti mbalimbali katika vyanzo vya Hadithi [4] zinazoeleza umuhimu na mbinu za utekelezaji wa adhabu hizi. [5] Katika kazi yake ya Al-Kafi, Kulaini amewasilisha mapokezi maalumu yanayohusu haddi ya zinaa ndani ya milango kumi na tisa mahususi aliyoitayarisha ndani ya kazi hiyo. [6] Wanazuoni wa Kishia wameichambua haddi (adhabu) hii katika sehemu maalumu zinazohusiana na hukumu za jinai. [7] Aidha, Sheria ya Adhabu ya Kiislamu nchini Iran imebainisha kanuni zote zinazohusiana na adhabu ya zinaa, sheria ambazo zinapatikana kuanzia ibara ya 221 hadi ibara ya 232. [8]
Vigezo vya Kisheria vya Kuthibiti kwa Adhabu ya Zinaa
Kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni wa fiqhi ya Kishia, utekelezaji wa adhibu ya zinaa hauwezi kutekelezwa isipokuwa baada mhusika kutimiza masharti yaliowekwa na sheria ya Kiislamu. Masharti hayo n i kama ifuatavyo:
• Kwanza kabisa, ni lazima mtenda kosa hilo awe amefikia umri wa kisheria wa kubalehe. [9] • Pili, lazima awe na akili timamu, yaani asiwe mwendawazimu. [10] • Tatu, ni lazima tendo hilo la zina liwe limefanywa kwa hiari yake mwenyewe, na si kwa kulazimishwa. [11] • Nne, ni lazima mtenda kosa hilo awe na ufahamu kamili juu ya uharamu wa tendo la zina. [12] • Tano, ni lazima muingiliano wa kimwili (dukhul) uwe umetimia ipaswavyo, yaani kiungo cha uzazi cha mwanamme kiingie ndani ya tupu ya mwanamke au sehemu kubwa ya kiungo hicho iingie ndani ya utupu wa mbele au nyuma ya mtendwa huyo. [13] • Sita, usiwe huouwe umepita kinyume na sheria, kwa maana mwanamme na mwanamke huyo wasiwe katika uhusiano wa ndoa wala wa umiliki mwengine wa halali unaozingatiwa na sheria ya Kiislamu (ujakazi kwa maana ya Kiislamu). [14] • Saba, lazima kuwepo ufahamu wa kumtambua mhusika wa upande wa pili, kwani endapo mtu atafanya tendo la ndoa kwa kudhani kuwa anayeshirikiana naye ni mwenza wake halali (kitendo kinachoitwa waty bil shubha), basi tendo hilo halitahisabiwi kuwa ni tendo la zinaa.[15] Taratibu za Kisheria za Uthibitishaji wa Kosa la Zinaa
Katika nyanja za kifiqhi, kuna mchakato maalumu wa kuthibitisha makosa ya zinaa. Mchakato huu hutegemea misingi miwili mikuu: iqrar (ukiri wa mkosaji) na bayyinah (ushahidi thabiti). Ufafanuzi wa masharti ya misingi miwili hi ni kama ifuatavyo:
• Iqrar: Uhalali wa kisheria wa ukiri hunategemea matamshi ya mhusika ya kutamka na kukiri kosa lake mara nne. [16] • Bayyinah: Uthibitishaji kupitia bayyinah (ithibati bobevu), unahitaji ushuhuda wa wanaume wanne waadilifu. Kulingana na kauli ya wanazuoni walio wengi, kama kutakosekana uwezekano wa kupata idadi ya wanaume wanne, itabidi kutosheka na wanaume watatu na wanawake wawili. [17] Ila kama ushahidi huo utatolewa na wanaume wawili na wanawake wanne, basi hakutawezekana kumpa adhabu nyengine zaidi ya kumtia pakora, na hivyo adhabu kupopolewa mawe huondolewa moja kwa moja. [18] Ushahidi wa mashahidi fulani hauwezi kusimama kama msingi wa haddi (ashabu), isipokuwa pale tu maelezo yao yanapobainisha utimilifu wa masharti ya jinai. Mfano muhimu wa mashatri hayo ni dukhul (penitresheni) pamoja na hiari ya pande zote katika utendaji wao; kinyume chake, mashahidi hao watakabiliwa na haddi ya qadhf (adhabu tuhuma) kwa kuwatumu wahanga wao kwa tuhuma zisizothibitika. [19] Aidha, kulingana na fatwa za kifiqhi, ni vyema (mustahabu) kwa mashahidi hao kujiepusha na harakati za utoaji wa ushahidi wa zinaa. Pia ni vyema (mustahabu) kwa kadhi kutumia lugha ya ishara na mafumbo ili kuwakengeusha waachane na mchakato wao wa kutoa ushahidi huo. [20] Kategoria za Haddi (Adhabu) za Zinaa Katika mfumo wa kifiqhi wa Kishia, kuna aina tatu za adhabu zimependekezwa kwa ajili ya kosa la zinaa. Adhabu hizo ni kulingana na sifa za watendaji wake pamoja na mazingira husika. Katika mazingira fulani, haddi ya zinaa inajumuisha kumuua mhusika aliyetenda kosa hilo. Mifano ya mazingira hayo ni: • Kuzini na maharimu wa kinasaba (mathalani mama au binti); [21] huku baadhi ya wasomi wengine wakiingiza ndani ya hukumu hii maharimu wa kiapo cha ndoa pamoja na wale kunyonya ziwa moja. [22] • Uhusiano wa kimwili (uzinifu) kati ya kafiri dhimmi na mwanamke Mwislamu. [23] • Ubakaji wa kutumia nguvu na mamlaka. [24] • Mwanamume kuingiliana kimwili na mke wa mzazi wake (baba). [25] • Mhusika huru (mwanamme au mwanamke) asiyekuwa katika mfungo wa ndoa (ghairi-muhsan) anayerudia kosa la zinaa kwa mara ya tatu au ya nne, baada ya utekelezaji wa adhabu ulifanyika dhidi yake katika makosa yaliyotangulia. [26] Adhabu ya Kupigwa Mawe (Rajm)
Iwapo mwanamme na mwanamke wataingia kwenye tendo la zinaa huku wkiwa na sifa ya ihasan (walio katika ndoa na wenye uwezo wa kukutana na wenzi wao wa halali), basi kisheria adhabu yao itakuwa ni kupigwa mawe. [27] Hata hivyo, adhabu ya zinaa hutofautiana kwa mhusika asiyekuwa na sifa ya ihsan. [28]
Adhabu ya Mijeledi, Uhamisho, na Kunyolewa Nywele Hukumu ya mwanamme au mwanamke aliyezini akiwa ni balehe na mwenye akili timamu, huku akiwa hana fursa ya uhusiano wa halali wa kimwili, ni kuchapwa mijeledi mia moja. [29] Kwa upande wa watumwa, adhabu yao ni mijeledi hamsini bila kujali kama wana sifa ya ihsan au la. [30] Aidha, kuna hukumu kali zaidi inayotolea kwa wanaume waliooa lakini bado hawajakamilisha mwingiliano wa kimwili na wake zao. Huku ya wanaume hao ni kuchapwa pakora, kisha kunyolewa nywele na kuhamisho na kupelekwa mji mwengine kwa muda wa mwaka mmoja. [31] Kwa mujibu wa mtazamo wa wanazuoni wengi, wanawake hawatakiwi kuhusishwa na adhabu ya uhamisho na kunyolewa nywele zao, bali adhabu mbili hizi ni kwa ajili ya wanaume peke yao. [32] Ni Nani Hasa Mwenye Mamlaka ya Kutekeleza Adhabu ya Zinaa? Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa Kishia, wakati wa kuwepo kwa Imamu Ma’asumu (a.s.), jukumu la kutekeleza adhabu za kisheria za Kiislamu—ikiwemo adhabu ya uzinifu—linamhusu Imamu mwenyewe au mtu anayeteuliwa naye kwa ajili ya utekeleza wa kazi hiyo. [33] Ila kuna tofauti za maoni kuhusu kipindi cha ghaiba (kutowepo kwa Imamu): baadhi ya wanazuoni wanaamini kuwa faqihi mwenye sifa kamili ndiye anayekuwa na mamlaka ya kutekeleza adhabu hizo; [34] wengine wanasisitiza kuwa utekelezaji wa adhabu za kisheria ni haki ya pekee ya Imamu Ma’asumu, na hivyo faqihi hana hana haki ya kushika mamlaka hayo wakati wa ghaiba. [35] Aidha, kuna waliosimama katikati baina ya nadharia mbili hizi bila ya kutoa msimamo ulio wazi kuhusiana na suala hili. [36] Miongozo ya Kisheria Katika Utekelezaji wa Adhabu za Zinaa Taratibu za utekelezaji wa adhabu ya zinaa zilizotajwa ndani ya muktadha wa kifiqhi ni kama ifuatavyo: • Hali ya Mavazi: Mwanamme huachwa bila mavazi (isipokuwa sehemu ya siri). [37] • Hali ya Mavazi ya Mwanamke: Nguo za mwanamke zinatakiwa kuwa ni zenye kusitiri kufungwa vizuri ili kuzuia ufichukaji wa maungo yake wakati wa mchakato wa adhabu ya mijeledi au rajm (kupigwa mawe). [38] • Miundombinu ya Adhabu: Utekelezaji wa rajm unahitaji uchimbaji wa handaki (shimo) kwa ajili ya kumuingiza mhusika ndani yake. [39] • Hatua ya Utekelezaji wa Adhabu ya Bakora: Upigaji bakora unabidi uanzwe na mashahidi walitoa ushahidi. [40] • Mkao wa Mtendwa: Imeelezwa kuwa mwanamme hukabili mijeledi hali akiwa amesimama wima, huku mwanamke akiwa katika hali ya kukaa kitako. [41] • Maeneo ya Adhabu: Mapigo ya mijeledi yanapaswa kutawanywa mwilini kwa nguvu inayostahiki, bila ya kupiga kichwani na uso mwa mtuhumiwa huyo. [42] • Ushiriki wa Kijamii na Kishahidi: Ni sharti kwa kundi la Waislamu kuhudhuria katika eneo la utekelezwaji wa adhabu ya zinaa. [43] • Hatua ya Utekelezaji wa Adhabu ya Kupiga Mawe: Endapo kosa lilikubalika kupitia ushahidi wa mashahidi fulani, mashahidi ndiwo wanochukua jukumu la kuanza kurusha mawe. [44]
Je, Yawezekana Kutekeleza Adhabu ya Zinaa kwa Kutegemea Vipimo vya Udaktari? Mamlaka za kisheria za kidini (Viongozi wakuu wa kidini, yaani mafaqihi) wamekataa kutambua vipimo vya udaktari kama njia ya kuthibitisha kosa la zinaa. [45] Aidha, wanaamini kuwa maarifa anayopata jaji kupitia vipimo hivyo hayawezi kuwa na hadhi fulani ndani ya mahakama za Kiislamu, hivyo maarifa hao hayawezi kuwa ni hoja ya kisheria (hujjat) mbele ya mahakama hizo. Na wala haiwezekani kutoa adhabu yoyote ile kwa mtuhumiwa fulani anayetuhumiwa kupitia maarifa yanayotegemea vipimo hivyo. [46] Kwa mfano, Sayyid Ali Khamenei anakataa kabisa vipimo hivyo. Pia Mohammad Fadhel Lankarani anazihisabu ithibatiba za kidaktari kuwa si ithibati tosha kwa ajili ya kumpa mtuhumiwa fulani adhabu ya kosa la zinaa. [47]