Mi’raj al-Sa’dah (kitabu)
Mi’raj al-Sa’dah (Kiarabu: مِعْراجُ السَّعادة) ni kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kifarsi na Mulla Ahmad Naraqi (aliyeaga dunia 1245 Hijiria) na kinazungumzi maudhui ya akhlaq na maadili ya Kiislamu. Imeelezwa kuwa kitabu hiki ni mukhtasari wa kitabu cha Jami’ al-Sa’dat kilichoandikwa na Mulla Mahdi Naraqi; licha ya kuwa kuna tofauti katika mbinu na mtindo wa uandishi.
Katika kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah kumependekezwa kanuni jumla za kutibu tabia mbaya; kila moja kati ya tabia hizi mbaya hutibika kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume chake. Kwa mujibu wa kitabu hiki, kila fadhila ina mpaka maalumu ambaoo unaitwa uwiano (hali ya kati na kati); na ifrat na tafrit (kuchupa mipaka na kuzembea kupita kiasi) katika hilo kunahesabiwa kuwa ni jambo baya na tabia isiyofaa.
Kuhusiana na kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah kuna nakala na machapisho ya kitabu hiki ambayo yanatofautiana; miongoni mwayo ni chapisho la Taasisi ya Uchapishaji ya Hijrat Qom ambayo imesambaza nakala ya kitabu hiki ikiwa na kurasa 797. Sheikh Abbas Qomi amekifanyia muktasari kitabu hiki na kukipa anuani ya “al-Maqamat al-Aliyya fi mujibat al-Sa’dah al-Abadiyah”.
Umuhimu na Nafasi Yake
Sheikh Abbas Qomi, anasema kuwa, Mi’raj al-Sa’dah ni kitabu bora kabisa cha kimaadili (akhlaq) cha lugha ya Kifarsi na ni lazima kwa watu wote kuwa na kitabu hiki. [1] Kadhalika maktaba ya kiakhlaq ya Naraqeyn ambayo inatajwa na baadhi ya waandishi imechukuliwa kutoka katika nadharia za Mulla Ahmad Naraq katika Mi’raj al-Sa’dah na Mulla Mahdi Naraqi katika kitabu cha Jami’ al-Sa’adat. [2] Katika maktaba ya akina Naraqi, kila fadhila ina mpaka maalumu ambao unaitwa uwiano (hali ya kati na kati) na ifrat na tafrit (kuchupa mipaka na kuzembea kupita kiasi) katika hilo kunahesabiwa kuwa ni jambo baya na tabia isiyofaa. [3]
Inaelezwa kuwa, kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah kiliathirika na kitabu cha Kīmīyā-yi Sa'āda cha Muhammad al-Ghazali. [4] Kadhalika kitabu cha “al-Maqamat al-Aliyya fi mujibat al-Sa’dah al-Abadiyah” kilichoandikwa na Sheikh Abbas Qomi ni muktasari kitabu hiki. [5]
Hata hivyo kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah kimekosolewa na baadhi na miongoni mwa ukosoaji huo ni: Kutotumia hadithi kama hoja, ushahidi wa kitajiriba na kiuzoefu na vielelezo vya kiakhlaqi (kimaadili) kwa vyanzo vyenye itibari na vilevile kupuuza maneno ya shakhsia wakubwa. [6]
Mwandishi
- Makala Kuu: Mulla Ahmad Naraqi
Ahmad bin Muhammad-Mahdi bin Abidhar Naraqi, ambaye ni mashuhuri kwa jina la Mulla Ahmad Naraqi na Fadhil Naraqi (aliyefariki 1245 Hijiria) ni mtoto wa Mulla Mahdi Naraqi, mmoja wa wanazuoni na Maulamaa wa Kishia katika karne ya 13 Hijiria. [7] Alisoma kwa kwa walimu na wanazuoni mbalimbali kama Sayyid Muhammad-Mahdi Bahr al-Ulum, Mirza Mahdi Shahristani, Sheikh Ja’far Kashif al-Ghitaa, Sahib Riyadh na kadhalika. [8] Baada ya kifo cha baba yake, alichukua jukumu la Umarjaa katika eneo alilozaliwa. [9] Mulla Ahmad amealifu na kuandika vitabu vingi katika elimu mbalimbali za Kiislamu ambapo idadi yake imetambuliwa kuwa inafikia 35; na miongoni mwa vitabu hivyo ni: Mustanad al-Shi’ah, Awaid al-Ayyam na Mi’raj al-Sa’dah. [10]
Maudhui na muundo
Kitabu cha Mir’raj al-Sa’dah kina milango mitano ambapo kila faslu ina ina faslu tofauti tofauti:
- Mlango wa kwanza: Utanguzi wenye faida.
- Mlango wa pili: Tabia mbaya na jinsi mtu anavyojiweka.
- Mlango wa tatu: Kulinda tabia njema kunako kupotoka na kukengeuka na kadhalika.
- Mlango wa nne: Fadhila za kimaadili na jinsi ya kujipamba na tabia njema.
- Mlango wa tano: Siri na adabu za ibada. [11]
Mlango wa kwanza wa kitabu unaanza na faslu ambayo lengo lake ni kubainisha nukta hii kwamba, kuitambua nafsi ni utangulizi wa kumtambua Mwenyezi Mungu na mwandishi ananukuu ubeti wa mashairi kutoka kwa mshairi Sanai. [12] Sehemu ya mwisho ya kitabu nayo ni falsu kuhusiana na thawabu na fadhila za kumzuru Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s) na sehemu kuhusiana na adabu za kufanya ziara. [13]
Mbinu za kutibu tabia mbaya
Katika kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah kumependekezwa kanuni jumla za kutibu tabia mbaya; kila moja kati ya tabia hizi mbaya hutibika kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume chake. [14] Hata hivyo, Naraqi anaamini kuwa, kuondolewa sababu na mazingira ya kuundika tabia mbaya [15] na vilevile kuwa na ufahamu kuhusiana na athari za kidunia na kiakhera za tabia hizo [16] ni jambo lenye taathira katika kutibu tabia mbaya. Kwa muktadha huo, baada ya kubainisha kila tabia mbaya anajishughulisha na kueleza sababu, mazingira na taathira zake kidunia na kiakhera na kisha anabainisha mbinu na mikakati ya kutibua tabia hizo mbaya. [17]
Naraqi anaamini kuhusiana na suala la kuchuma tabia ambapo anasema, mwanadamu kwanza anapaswa kuilea nguvu ya matamanio, kisha nguvu ya ghadhabu na baada ya hapo nguvu ya akili. [18] Kadhalika anaamini katika mlango wa fadhila za kimaadili ya kwamba, mwanadamu kwanza anapaswa kutenda fadhila na tabia njema mpaka hilo liwe ni jambo analolimiki na lililojikita katika nafsi yake. [19]
Tofauti ya Mi’raj al-Sa’dah na Jami’ al-Sa’adat
Agha Bozorg Tehrani katika kitabu chake cha al-Dhari’ah amekitambua kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah kwamba, kimechukuliwa kutoka katika kitabu cha Jam’i al-Sa’adat, kilichoandikwa na Mulla Mahdi Naraqi (aliyeaga dunia 1209 Hijria) bali ni tarjuma yake ya kifarsi. [20] Pamoja na hayo, vitabu hivi viwili vinatofautiana katika mbinu ya ufafanunzi na mpangilio wa maudhui. [21] Miongoni mwa tofauti hizo ni:
- Utendaji: Katika kitabu cha Jami’i al-Sa’dat utendaji wa kiakili unahisika zaidi. (umekolea zaidi) Lakini katika kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah maudhui zinabainishwa kwa kutolewa ushahidi wa hadithi au funzo kutoka katika nakili na akili na kutaja mashairi. [22]
- Mpangilio wa Milango: Utaratibu na mpangilio pamoja na anuani za milango na faslu za vitabu hivi viwili unatofautiana; kwa mfano mlango wa kwanza wa kitabu cha Jami’ al-Sa’dat una faslu 16, lakini mlango wa kwanza wa kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah una faslu 10. Kadhalika baadhi ya faslu za Jami’ al-Sa’adat hazipo katika Mi’raj al-Sa’dah na kinyume chake pia. [23]
Pamoja na hayo katika kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah katika baadhi ya sehemu kumebainishwa kwa mapana na marefu maudhui zilizoko katika kitabu cha Jami’ al-Sa’adat. [24]
Nakala na usambazaji
Kitabu cha Mi’raj al-Sa’dah kina chapa na nakala tofauti tofauti. Agha Bozorg Tehran anasema kuwa, nakala ya mwaka 1238 Hijiria nchini Iraq na nakala ya mwaka 1265 Hijria nchini Iran ndizo zilizokuwa nakala za kale zaidi za kitabu hiki. [25]
Masuala yanayo fungamana
Vyanzo
- Āgā Buzurg al-Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-shīʿa. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1403 AH.
- Al-Nazarīyya fī al-Qurʾān. Edited by ʿAbd al-Ṣabūr Shāhīn. Kuwait: 1973.
- Bustānī, Biṭrus. Muḥīṭ almuḥīṭ: qāmūs muṭawwal lughat al-ʿarabīyya. Beirut: 1987.
- Darrāz, Muḥammad ʿAbdullāh. Dastūr al-akhlāq fi l-Qurʾān, dirāsat muqārina lil-akhlāq. [n.p]. [n.d].
- Jalālī, Muḥammad Riḍā. Miʿrāj al-saʿāda dar āyīna-yi tārīkh wa falsafa-yi taʿlīm wa tarbīyat. Winter 1380 and Spring 1381.
- Narāqī, Mahdī b. Abī Dhar. ʿIlm-i akhlāq-i Islāmī: tarjuma-yi jāmiʿ al-saʿādāt. Translated by Jalāl al-Dīn Mujtabawī. Tehran: 1381 Sh.
- Narāqī, Aḥmad b. Muḥammad Mahdī. Kitāb Miʿrāj al-saʿāda. Tehran: Jāwīdān, [n.d].
- Narāqī, Mahdī b. Abī Dhar. Jāmiʿ al-saʿādāt. Edited by Muḥammad Kalāntar. Najaf: 1967.
- Narāqī, Aḥmad. Miʿrāj al-saʿāda. Qom: Hijrat, 1377 SH.