Lauhu Al-Mahfudhi

Kutoka wikishia

Lauhu Al-Mahfudhi ( لوح المحفوظ): Ni mahali halisia pa Qurani, ambapo ndani yake kumeandikwa matukio yote ya ulimwengu, ambayo hayawezi kubadilika na kwenda kinyume na yaliomo ndani ya “Luhu al-Mahfudhi” hiyo. Kuielewa “Luhu al-Mahfudhi” ni muhimu katika kuelewa uhalisia wa Qurani. Hii ni kwa sababu ya kwamba; Kulingana na baadhi ya wafasiri, “Luhu al-Mahfudhi” ni kituo cha msingi kwa vitabu vyote vya mbinguni, ikiwa ni pamoja na Qurani. “Luhu al-Mahfudhi” huchukuliwa kuwa ni kituo cha elimu iyendao sawa na elimu ya Mwenye Ezi Mungu, elimu ambayo haiwezi kubadilika na kwenda kinyume na yaliomo ndani ya kituo hicho, na kwamba matukio yote ya ulimwenguni huwa yameandikwa ndani yake. “Luhu al-Mahfudhi” tofauti na kituo au ubao wa “Lauhu almahwi wa al-ithbati”, ambao kikawada ndani huwa kumeandikwa yale matukio ya ulimwengu ambayo hayapigwa muhuri wa kuhitimisha juu ya utokeaji wake, matukio ambayo huweza kubadilika kulingana upatikanaji wa masharti fulani. “Luhu al-Mahfudhi” huchukuliwa kuwa ni miongoni mwa mambo ya ghaibu ambayo hayawezi kuhisiwa au kudirikiwa kwa viungo vya hisia. Sifa muhimu zaidi ya lauhu almahfudh ni ujumlishaji wake wa matukio yote ya duniani. Baadhi ya wafasiri wameihisabu ibara au neno “Luhu al-Mahfudhi” kuwa ni lugha ya kitamthilia (figurative language) inayo ashiria ya elimu ya Mwenye Ezi Mungu. Wanazuoni wengine wakitegemea Aya nyingine za Qurani, wameamua kupingana mtazamo huu. Baadhi ya wanafalsafa nao wameilinganisha “Luhu al-Mahfudhi” na “akili tendaji عقل فعال ” au Jibril, lakini mtazamo huu umepingana na dhahiri ya sheria na haujathibitishwa kihalali na hoja za Qurani wala riwaya. [Maelezo: “akili tendaji عقل فعال ” au kwa lugha ya Kilatini ni “demiurgus” nayo ni akili au kiumbe namba 10 aliyeumbwa miongoni mwa akili kumi za mwanzo. Akili hii imepewa jina la akili tendaji kutokana na utendani wake, ikiwa ni kiungo halisi baina ya Mungu na viumbwa vyake, kazi yake halisia ni; kukamilisha maumbile ya viumbe wa Mwenye Ezi Mungu, moja wapo ikiwa ni kuzijenga nafsi za wanadamu, kisha kuziboresha hadi kufikia kiwango cha akili…] Rejea kitabu Hikmatu al-Muta’alia fi al-Asfari al-Arba’a, cha Sadr al-Din Muhammad Mulla Sadra Shirazi, J. 3, uk. 431, chapa ya Qom ya Mustafawi, toleo la tatu la mwaka 136 Hijiria. Baadhi ya watafiti wa dini ya Kiislamu, wakirejea kwenye Aya za Qurani, wanaamini kwamba; Maimamu kumi na nne wanajua yaliyomo ndani ya Lawhul Mahfuz. Kwa upande mwingine, baadhi ya wafasiri, wanachukulia kuwa; Suala la kuwa na ufahamu wa Lawhul Mahfuz ni milki maalum ya Mwenyezi Mungu peke yake, wala hakuna kiumbe mwengine yeyote yule mwe uwezo wa kujua yaliomo ndani yake. Kulingana na maelezo yaliotolewa na watafiti wa Kiislamu, ni kwamba; Suala la kuandikwa kwa matukio yote ya ulimwenguni katika “Lawhul Mahfudhi” haimaanishi kwamba binadamu huingia katika sindikizo la lazima katika utendaji wa amali na kazi zake mbali mbali; kwani utokeaji wa matendo ya binadamu, hutokea na kufanyika kupitia hiari na uhuru wa binadamu mwenyewe. Na hilo ndilo lililoandikwa katika “Lawhul Mahfudhi” kuhusiana na matendo ya mwanadamu, na ujuzi wa Mwenye Ezi Mungu hauibadilishi ukweli hou katika utendekaji wake. Nafasi ya “Lawhul Mahfudhi” Ndani ya Tafiti za Kiislamu Lawhu al-Mahfudhi: ni neno la Kiqur’ani linaloashiria mahali au kituo halisi cha Qur’ani ambamo Qur’ani ilikumo ndani yake kabla ya kuteremshwa hatua kwa hatua kwa Mtume (s.a.w.w). [1] Allama Tabataba’i, mwandishi wa tafsiri ya Al-Mizan, anaamini kuwa; Qur’ani iliyopo katika Lawh al-Mahfudhi haiwezi kueleweka na binadamu wa kawaida; hivyo basi Mwenye Ezi Mungu aliiteremsha kwa kiwango cha chini ili iweze kueleweka na wanadamu wa kawaida. [2] Kulingana na maelezo yaTabataba’i, vitabu vyote vya mbinguni vilivyoteremshwa kwa Mitume wengine, vimechukuliwa kutoka kwenye kituo cha Lawh al-Mahfudhi, na hiyo ndio sababu ya Qur’ani kuitambua “Lauhu al-Mahfudhi” kwa jina la Umm al-Kitab (Kitabu Kikuu au Kitabu Asili). [3] Kwa hiyo, kuifahamu na kuielewa “Lawhu al-Mahfudhi” ni jambo lenye umuhimu mkubwa katika kuzielewa Aya zinazohusiana na uteremshaji wa Qur’ani, uhifadhiwaji wake kutokana na upotoshaji, pamoja masuala yanayohusiana na ufunuo wa Qur’ani. [4] Allama Majlisi mwandishi wa kitabu “Biharu al-Anwar” akielezea kuhusiana na “Lawhu al-Mahfudhi”, akiiita kituo hicho kuwa ni kibao kinacholingana au kiendacho sawa na elimu ya Mwenye Ezi Mungu, ambapo matukio yote ya ulimwengu huwa yameandikwa ndani yake na wala hayawezekani kubadilika. [5] Kulingana na maelezo yaliyo toela na Ja’far Subhani, ambaye ni mfasiri wa Qur’ani wa upande wa Madhehebu ya Shia, ni kwamba; ndai ya kibao hicho kumerekodiwa matukio yote yanayohusiana na binadamu ambayo bila shaka yatatendeka tu na hayawezi kurudi nyuma. [6] Kutokana na kurekodiwa kwa matukio ya uhakika yatakayo tokea ulimwenguni humu ndani ya kitabu hicho, “Lawhu al-Mahfudhi” inahisabiwa kuwa ni mahali pa uamuzi wa Kiungu. [7] Kinyume chake, kuna kibao kingine kinachoitwa “Lawhu al-Mahwu wa al-Ithbat” ambamo ndani yake huwa mmerikodiwa yale matukio ya ulimwengu ambayo hayana uhakika katika utokeaji wake, ambayo huweza kubadilika kulingana matukio au kukamilika kwa masharti fulani. [8] Neno “Lawhu al-Mahfudhi” limetajwa mara moja tu ndani ya Qurani, neno ambalo linapatikana katika Aya isemayo: “Fi Lawhin Mahfuudhin فِي لَوْحٍ مَحْفُوظٍ”. [9] Baadhi ya wafasiri wanaamini kuwa; Pia katika Aya nyingine za Qurani, kuna marejeo tofauti yanayo husiana na “Lawhu al-Mahfudhi”; miongoni mwa marejeo hayo ni “Kitabun Mubin كِتَابٍ مُبِينٍ”, [10] yenye maana ya “Kitabu Kilicho Wazi”, “Kitabun Maknun كِتَابٍ مَكْنُونٍ”, [11] kwa maana ya “Kitabu Kilichofichwa” na “Ummu al-Kitabi أُمِّ الكِتَابِ”, [12] kwa maana ya “Mama wa Vitabu”. [13] Uhakika na Utambulisho Wake “Lauhu al-Mahfudhi” au kwa Kiswahili tunaweza kuuita Ubao wa Hifadhi; kiuhalisiana na mambo ya ghaibu na haiwezi kueleweka kupitia hisia au kupitia majaribio fulani ya kibinadamu. [14] Kulingana na Mwanazuoni aitwaye Muhammad Hadi Ma’rifat na Nasir Makarim Shirazi, ambao ni miongoni mwa wafasiri wa Kishia; “Lauhu al-Mahfudhi” ni kugha ya kitamthilia inayo maanisha ya elimu ya Mwenye Ezi Mungu, hiyvo basi haiwezi kufikiriwa kuwa kitu kinachoweza kuhisiwa wala si kitu cha kiroho au chombo fulani, ukurasa fulani, au mahali maalum. [15] Walakini, Muhammad Taqi Misbah Yazdi, mwandishi wa kitabu kiitwacho “Qur’ani Shenasi”, aneukataa mtazamo huu na kuuhisabu kuwa si mtazamo sahihi. Muhammad Taqi Misbah Yazdi anaamini kwamba; kutokana na tafsiri zinazo tolewa na Qur’ani kuhusiana na ubao huo, kama vile Aya isemayo: “Na kwake ndiko kunako kitabu cha asili وَعِندَهُ أمُّ الْكتَابِ”, yaonekana wazi kwamba, ubao huu siyo kiini wala dhati ya Mwenye Ezi Mungu, bali ni kiumbe cha Mwenye Ezi Mungu. [16] Baadhi ya watafiti wamekuja na nadharia sita tofauti kuhusiana na maana ya “Lauhu al-Mahfudhi”. Inasemekana kwamba; matumizi ya neno Ubao na Kalamu yaliokuja katika Qur’ani, ni kwa ajili ya kuzikaribisha akili kwa lugha ya mfano, na haipaswi kulinganishwa na kalamu na karatasi za vitabu vya kawaida. [18] Mtazamo wa Kifalsafa na Kiirfani Baadhi ya wanafalsafa wamefananisha Lawhu al-Mahfudh na ‘Aqlu Fa'al (Akili Tendaji) au Jibrilu, [19] au ni nasi kuu ya kifalak, ambayo Mwenye Ezi Mungu huchapisha viumbe vyake ndani yake, kisha viumbe hivyo hukamilika kupitia ulimwengu wa nafsi hiyo. [20] Katika welewa wa kitasawwufu na kiirfani katika kuutambua ulimwengu, imeelelezwa ya kwamba; kalamu ndio chanzo cha “Lawhu al-Mahfudhi”. [21] Muhyiddin Ibnu ‘Arabi, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa fani ya tasawwufu, anaamini kuwa; elimu ya Mwenye Ezi Mungu kuhusiana na viumbe vyake, ni eliimu ya jumla jamala au elimu kwa ufupi na si elimu bambanifu, na kalamu ni pambanuzi yenye kutoa maelezo ya kina juu ya elimu hiyo ndani ya “Lawhu al-Mahfudhi”. [22] Hata hivyo, baadhi ya watafiti wameona kwamba kulinganisha Lawh al-Mahfuz na dhana za falsafa kama vile kuilinganisha na “jauhar” (kiini asili) au “akili ya kwanza” ni kinyume na maandiko ya sharia, dhana ambazo kiuhalisia hazina dalili kutoka katika Qur’ani wals Riwaya. [23] Sifa za Lawhu al-Mahfudhi Sifa muhimu zilizotajwa kuhusiana na “Lawhu al-Mahfudhi”, ni kwamba; Ubao huu umekesanya kila kitu ndani yake na hakuna kilioko nje ya Ubao huo miongoni mwa matukio ya ulimwengu huu. [24] Kulingana na Hadithi; ndanii yake mmeandikwa taarifa za matukio yote ya ulimwengu huu. [25] Pia kuna baadhi ya sifa zilizotajwa ndani ya Hadithi, kuhusiana na baadhi ya sifa za nje za “Lawhu al-Mahfudhi”, kama vile kuwa na rangi ya zumaridi (emerald). [26] Kulingana na maoni ya mwanachuoni maarufu wa Kishia aitwaye Tabatabai, sifa hizi ni aina fulani ya taswira yenye nia ya kujenga picha ya “Lawhu al-Mahfudhi” kulingana na akili hizi za kimwili (kimaada) za binadamu. [27] Uwezekano wa Kuidiriki na Kuwa na Elimu ya Lawhu al-Mahfudhi Baadhi ya watafiti, wakinukuu baadhi ya Aya za Qur'ani Tukufu, wanaamini kwamba; kuna baadhi ya watu wanaostahiki wanaoweza kupata welewa na ufahamu kutoka kwenye “Lawhu al-Mahfudhi”, wakirejea kwenye Aya za Qur’ani. [28] Watafiti hawa baada ya kukusanya na kuoanisha Aya ya 77 hadi 79 za Suratu Al-Waqi’ah [Maelezo 1: إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ - فِي كِتَابٍ مَكْنُونٍ - لَا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ Bila shaka hii ni Qur’ani Tukufu (ilioko) katika kitabu kilichofichika au kilicho hifadhiwa (ambacho) hakiwezi kuguswa isipokuwa na wale waliotakaswa] na Aya ya 33 ya Suratu Al-Ahzab, [Maelezo 2: إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيراً Bila shaka Mwenye Ezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu na madhambi (nyinyi) Ahlul-Bait na kukuatakaseni kabisa kabisa.] wameibuka na imani ya kuamini kwamba; “Maasumina 14” ni miongoni mwa watu wanaoweza kuwa na elimu ya “Lawhu al-Mahfudhi”. [29] Sayyid Ali Milani, ambaye ni miongoni mwa wanatheolojia wa Kishia, anaamini kwamba; kuna Hadithi zinazo onesha kwamba Maimamu (a.s) wana uhusiano wa moja kwa moja na “Lawhu al-Mahfudhi”. [30] Allama Tabataba’i pia ameitafsiri elimu ya ghaibu ya Mitume na Maimamu kuwa ni ufahamu wao kutoka kwenye “Lawhu al-Mahfudhi”. [31] Hata hivyo, kulingana na baadhi ya Hadithi, ni kwamba; hakuna kiumbe yeyote yule (hata Manabii na Maimamu) anayejua yaliomo ndani ya “Lawhu al-Mahfudhi”, na “Lawhu al-Mahfudhi” iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake. [32] Muhammad Hadi Ma’rifatiy, akitegemea moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s.) pia naye anaamini ya kwamba Mtume na Maimamu (a.s) hawana uwezo wa kuelewa yaliomo ndani ya “Lawhu al-Mahfudhi”. [23]

Kutopingana Kati ya Uhuru wa Mwanadamu na “Lawhu al-Mahfudhi”

Kwa mujibu wa maoni ya watafiti wa Kiislamu; Suala la kuandika yale matukio yote yanayo tarajiwa kutokea ulimwengu ndani ya “Lawhu al-Mahfudhi”, haimaanishi kwamba mwanadamu amelazimishwa kutenda kulingana na yale yaliomo ndani ya “Lawhu al-Mahfudhi”. [35] Misbahu Yazdi, ambaye ni mwanafalsafa wa Kishia, akijibu hoja kuhusiana na utata huu, katika kitabu chake kiitwacho “Khoda Shenaasi” ameandika akisema; Kule kuandikwa kwa matukio ya ulimwengu huu ndani ya “Lawhu al-Mahfudhi”, huwa hakumaanishi kwamba mwanadamu yupo katika sindikizo la lazima katika utndaji wake, kwani miongoni ya yale yalioandikwa ndani ya “Lawhu al-Mahfudhi”, ni kwamba mwandabu atatenda matendo yake kwa uhuru na hiari yake kamili, hivyo basi suala Mwenye Ezi Mungu kuwa na elimu juu ya matendo hayo, hakupelekei kubadilika kwa utendekaji wa matendo hayo. [36] Hii huwa inafanana na yule mwalimu anayejua kabla ya mtihani kwamba mwanafunzi fulani atafaulu au atafeli katika mtihani wake. [37]

Mada zinazo fungamana: Lawhu Mahwu wa al-Ithbati, Kalamu