Kuzungumza kwa Nabii Isa (a.s)
Kuzungumza kwa Nabii Isa akiwa katika maisha ya utotoni: Suala la Nabii Isa kutamka na kuzungumza hali akiwa ni mtoto mchanga, ni moja ya mambo ya ajabu yanayokaribiana na hali ya miujiza. Tukio la Nabii wa Mwenyezi Mungu Isa (a.s) kuzungumza na watu hali akiwa ni mtoto mchanga, lilitendeka kwa ajili ya kumtetea mama yake (Bibi Maryam) (a.s) kutokana na tuhuma za uasherati. Katika tukio hli Nabii Isa (a.s) alionekena kumtetea mama yake, jambo lilifanyika sambamba na kutangaza utume wake mbele ya wanazuoni wa Kiyahudi. [1] Qur’an Tukufu imetaja tukio hili - yaani kuzungumza kwa Isa akiwa mchanga - katika Aya tatu tofauti; Aya ya 46 ya Suratu Al-Imran, Aya ya 110 ya Suratu Al-Ma'ida, na Aya ya 29 ya Surat Maryam. [2] Baadhi ya watafiti wamesema kwamba; wafasiri wengi wamelifasiri neno “المهد al-mahd" kwa maana ya mahali maalumu panapoandaliwa kwa ajili ya kumlaza mtoto, iwe ni mapaja ya mama au kitanda anacholalia mtoto huyo. [3] Lakini kwa upande wa pili, baadhi ya wafasiri wengine kama vile; Sheikh Muhammad Hadi Ma'rifati katika kitabu chake Al-Tamhid wanaeleza kwamba; baada ya kuzaliwa kwa Nabii Isa (a.s) kupita miaka michache, ndipo Bibi Maryam (a.s) alipurudi mjini kwake, kwa hiyo neno " المهد al-mahd" lililopo katika Aya zinazoelezea tukio hili, halimaanishi siku za utoto mwake, bali inamaanisha siku za ukubwani mwake - miaka miwili hadi mitatu - baada ya yeye kuwa na uwezo wa kuzungumza. [4] Vile vile Sayyid Ahmad Khan Hindi, mmoja wa wanazuoni wa Kiislamu - ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa wafasiri wa Quran - anasema kwamba; maana ya neno " المهدal-mahd" halimaanishi siku za kunyonya kwake, wala siku za utotoni mwake, bali neno hili linamaanisha siku za ujanani mwake. [5]
Kulingana na Aya ya 30 hadi 34 ya Surat Maryam, Nabii Isa “Yesu” (a.s) alijitambulisha kama ni mtumishi wa na Nabii wa Mwenye Ezi Mungu aliyepokea kitabu kitakatifu kutoka kwa Mola wake. Pia kulingana na maelezo ya Nabii Isa yaliomo ndani ya Aya hizo, ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu alimbariki na kumfanya awe ni msambazaji wa baraka za Mola wake popote pale aendapo, na wala hakumfanya awe dhalimu au mjeuri, na Mwenye Ezi Mungu alimwamuru kusali, na kutoa zaka, na kumtaka awe mwema kwa mama yake, (Maryam). Nabii Isa anahitimisha maneno yake kwa kujitangazia amani mara tatu; siku ya kuzaliwa kwake, siku ya kifo chake, na siku ambayo Mwenye Ezi Mungu atamfufua kwa ajili ya kuelekea uwanja wa hukumu.
Baadhi ya wanazuoni wa Kishia wanaona hotuba ya Nabii Isa kama ushahidi wa uwezekano wa kuwepo kwa akili na ujuzi unaohitajika kwa Imam katika umri mdogo. [6] Baadhi ya wafasiri wameyahisabu maneno ya Isa kuwa ni miongoni mwa muujiza ya Mwenye Ezi Mungu, huku wengine wakiamini kuwa ilikuwa ni karama maalumu ijulikanayo kwa jina la “Irhas ارهاص”, [Maelezo: Irhas ni jina la miujiza ya mitume inayojitokeza kabla ya wao kufikia daraja ya utume] na wengine wanaamini kuwa ilikuwa ni muujiza maalumu kwa bibi Maryam. [7]
Sheikh Muhammad Hadi Ma'rifah akitoa ufafanuzi wa jambo hili anasema kwamba; Kahuka aina yoyote ile ya miujiza inayopatikana katika asili ya maneno ya Nabii Isa. Hii ni kwa sababu ya kwamba yeye anaamini kuwa; maneno haya ya Nabii Isa (a.s) yalijiri wakati wa utotoni mwake, na wala si jambo la ajabu kwa mtoto mdogo kuzungumza au kutamka maneno fula, ila muujiza hasa ulikuwa pale apokabiliana na watu wa mji wake huku akijibizana nao kwa njia ya utulivu, na kwa kutumia hoja thabiti kama azungumzavyo mtu mwenye uzoefu wa hali ya juu kabisa. Na jambo liliwafanya watu wa mji wake yeye ni mtume wa Mwenye Ezi Mungu na kwamba mama yake hakuwa na hatia ya uasherati. [8]
Fakhr al-Razi, mwandishi wa kitabu cha al-Tafsir al-Kabir, anaamini kwamba; tukio hili la Nabii Isa ni moja wapo ya matukio ya kimiujiza. Yeye anaamini kwamba; kuna tofauti kati ya muujiza uliojitokeza kwake yeye mwenyewe na muujiza unaohusiana na wote wawili kwa pamoja- ikimaanisha kwamba: Kuna muujiza maalumu unahosiana na Nabii Isa peke yake, nao ni kama vile kuzungumza kwake akiwa mchanga, ambao muujiza uliojitokeza kutoka kwake, na pia kuna muujiza unaohusiana nao waote wawili kwa pamoja, nao ni ule kuzaliwa wake, ambao unamhusu Nabii Isa mwenyewe pamoja na Maryam yake. Miujiza hii miwili inatofautiana na miujiza mingine, kwa mfano muujiza wa kufufua wafu ni muujiza maalumu uliyojitokeza mkononi mwake, muujiza ambao haimshirikishi yeye pamoja na mama yake, bali ni muujiza maalumu kwa ajili yake. [9]