Nenda kwa yaliyomo

Kumtetea madhulumu

Kutoka wikishia

Kumtetea madhulumu (mtu aliyedhulumiwa) ni miongoni mwa mambo ambayo yamesisitizwa katika hadithi zilizopokewa katika Uislamu na mafakihi (wanazuoni wa Fiq'hi) wanalitambua jambo hilo kuwa ni wajibu. Imepokewa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwamba, iwapo mtu atasikia mwito (sauti) wa mtu aliyedhulumiwa wa kuomba msaada na asimjibu, huyo si Mwislamu. Wengine wamesema riwaya zilizopokewa kuhusiana na maudhui ya kuwatetea wanaodhulumiwa zimefikia kiwango cha Tawatur (mapokezi yake ni mengi). Mafakihi hawaoni kuwa utetezi kwa wanyonge kuwa ni wa kidini tu au una mpaka makhsusi wa kijiografia, na baadhi yao wametoa fat'wa juu ya wajibu wa kuwatetea watu wa Palestina. Imesisitizwa katika kifungu cha tatu cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran juu ya "kuwaunga mkono bila kusita wanyonge (wastadhaafu) wa dunia". Murtadha Mutahhari na Sayyid Muhammad Beheshti, miongoni mwa wanazuoni wa Kishia, wamesema kwamba, katika Uislamu, kukubali na kuridhia dhulma ni jambo baya kama ilivyo kufanya dhulma. Imam Ali (a.s) amenukuliwa katika Nahj al-Balaghah akisema kwamba, watu ambao ni madhaifu na wasio na uwezo, katu hawawezi kujitetea na kukabiliana na dhulma, na haki haipatikana isipokuwa kwa hima na kujitahidi.

Nafasi

Wanazuoni wa Kiislamu wametilia mkazo sana suala la kumtetea nmadhulumu na wanaamini kwamba, kufanya hivyo ni wajibu wa kiakili na kimaumbile [1] ambao umekokotezwa na kusisitizwa mno katika hadithi na Qur'ani na hata hilo limetambuliwa kuwa ni wajibu. Musawi Sabzevari anaamini kwamba, hadithi zinazozungumzia kumtetea aliyedhulumiwa zimefikia kiwango cha tawatut (zimepokewa kwa wingi). [2] Makarem Shirazi mfasiri wa Qur'ani Tukufu akitegenmea Aya ya 75 katika Surat al-Nisaa anasema kuwa, kumtetea aliyedhulumiwa ni moja ya vielezo vya jihadi ya kujihami. [3] Katika hadithi kumetajwa ujira wa kumtetea madhulumu ni kuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w) [4] na ni kafara ya madhambi makubwa. [5] Imamu Swadiq (a.s) amenukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ya kwamba amesema: Iwapo mtu atasikia mwito (sauti) wa mtu aliyedhulumiwa wa kuomba msaada na asimjibu, huyo si Mwislamu. [6] Kabla ya Uislamu, Mtume alishiriki katika mkataba wa Hilf al-Fudhul ambao ulikuwa ni kumtetea madhulumu mbele ya dhalimu akiwa mjumbe na mwakilishi wa Bani Hashim. [7] Sayyid Ali Khamenei: Kumtetea madhulumu daima ni nukta inayong'ara. Kutokuwa pamoja na dhalimu, kukataa rushwa ya mwenye nguvu na utumiaji mabavu na kusisitiza haki kutendeka ni thamani ambazo katu hazichakai katika dunia. Sifa hizi daima huwa ni zenye thamani katika mazingira na hali yoyote ile. [8] Murtadha Mutahhari anaamini kuwa, Mwenyezi Mungu amekataza kuwasema vibaya na kuwaita kwa majina mabaya watu wengine isipokuwa kwa aliyedhulumiwa. Anaamini kwamba, kwa mujibu wa Aya za Qur'an, [9] Mwenyezi Munguu amemruhusu aliyedhulumiwa apaze sauti na kusema maneno mabaya… asome mashairi na sababu ya hilo ni kwa ajili ya kuhakikisha haki inapatikana. [10]

Kumtetea madhulumu ni katika mipango ya utawala wa Imamu Ali (a.s)

Baada ya Imamu Ali (a.s) kupewa baia na kiapo cha utiifu na hivyo kushika hatamu za uongozi akiwa Khalifa na kiongozi wa Waislamuu alibainisha kuwa, kutetea madhulumu na kuchukua haki yake iliyoporwa ni katika mipango ya utawala wake. [11] Amesema katika khutba ya Shaqshaqiya kwamba: Moja ya sababu za kukubali kushika hatamu za uongozi (baada ya kuuawa Othman) ni mkataba na ahadi ambayo Mwenyezi Mungu aliichukua kutoka kwa wanazuoni kwa ajili ya kumtetea aliyedhulumiwa. [12] Kadhalika Imamu Ali baada ya kupigwa upanga na Ibn Muljam aliwausia Maimamu Hassan na Hussein (as) kwamba, kuweni adui wa dhalimu na waokozi na wasaidizi wa madhulumu. [13]

Wajibu wa kisheria wa kumtetea madhulumu

Sahib al-Jawahir na Kashif al-Ghitaa ambao miongoni mwa mafakihi wa Kishia wanasema kuwa, endapo kutakuwa na dhana ya kubakia salama na kuwa na uwezo wa kumsaidia madhulumu, basi jambo hilo huwa Wajib Kifai (wakifanya wajibu huo baadhi ya watu, kwa wengine wajibu huo unawaondokea). [14] Jawad Tabrizi (aliaga dunia 1385 Hijria Shamsia), mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia amelihesabu suala la kumtetea aliyedhulumiwa kuwa ni jambo la wajibu. [15

Kutetea mataifa yaliyodhulumiwa

Kwa mujibu wa fat'wa ya Mafakihi ni kwamba, kuwatetea wanyonge na waliodhulumiwa hakuna mipaka ya kijiografia. [16] Mafakihi kama Muhammad Hussein Kashif al-Ghitaa, [17] Ayatullah Borujerdii [18] na Imamu Khomeini [19] waliitoa fat'wa ya kuwa wajibu kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina. Katika kifungu cha tatu cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, inasisitizwa juu ya "kuwaunga mkono bila kusita wanyonge (wastadhaafu) wa dunia". [20]

Kulaumiwa madhulumu asiyejitetea

Murtadha Mutahhari, mwanazuonii na mwanafalsafa wa Kishia anaaminii kwamba, katika Uislamu suala la kuonyesha udhaifu limekemewa. Kwa mtazamo wake ni kuwa, kama ambavyo Uislamu unamtambua dhalimu kuwa ni adui, vivyo hivyo unamtambua kuwa ni adui mtu ambaye anasalimu amri mbele ya adui licha ya kuwa ana nguvu za kukabiliana naye. [21] Imamu Ali amenukuliwa akisema kuwa, watu ambao ni madhaifu na wasio na uwezo, katu hawawezi kujitetea na kukabiliana na dhulma, na haki haipatikana isipokuwa kwa hima na kujitahidi. [22] Muhammad Beheshti, mujtahidi na mwanasiasa wa Kishia naye amesema, katika Uislamu kukubali dhulma ni dhambi kama ilivyo kufanya dhulma, na kama mtu atakubali na kuridhia dhulma, kabla ya yote anapaswa kujilaumu yeye mwenyewe. Anatumia Aya ya 38 ya Surat al-A'raf ambayo baadhi ya watu wa motoni watamtaka Mwenyezi Mungu awape adhabu maradufu watu wengine; wakisema kuwa, hao ndio waliowapoteza wao. Qur’an katika kujibu inasema kuwa, dhambi ya makundi yote mawili iko sawa na makundi yote mawili yatapewa adhabu maradufu. [23]