Nenda kwa yaliyomo

Kalimullah (Lakabu)

Kutoka wikishia

Kalimullah (Kiarabu: كليم الله (لقب)) Neno kalimullah linatokana na lugha ya Kiarabu, nalo ni neno lililojengeka kwa maneno mawili “Kalimu na Allah”, amabapo “Kalimu” humaanishawa msemezwa huku neno “Alla” likiwa na maana ya Mungu. Kwa hiyo jina Kalimullah lina maana ya “Msemezwa na Mungu”. Jina hili ni lakabu maalum ya Nabii Musa (a.s), [1] na asili ya kupatikana kwa jina hili imetokana na kule Mwenye Ezi  Mungu kuzungumza Nabii Musa (a.s) moja kwa moja bila ya kumtuma Jibrilu na kama ni mfikishaji wa ujumbe utokao kwa Mwenye Ezi Mungu. Hilo ndilo lililopelekea yeye kuitwa Kalimullah, [2] jambo ambalo lilikuwa ni heshima maalum kwa Nabii Musa (a.s). [3]

Kwa mujibu wa Aya ya 164 ya Suratu An-Nisa, Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Musa (a.s), kama asemavyo: "WAKALLAMALLAHU MUSA TAKLIMA وکَلَّمَ الله مُوسی تَکْلیماً؛; Na Mungu alizungumza na Musa kwa maneno". [4] Pia Mwenye Ezi Mungu amezungumzia sula hili katika Aya ya 143 na 144 za Suratu Al-A'raf [5]. Si Aya hizo zenye kuelezea kisa cha Nabii Musa cha kuzungumza na Mola wake, bali pia ukirudi kwenye Aya ya 11 ya Surah Ta-Ha utakuta neno "NUDIYA" (aliitwa) ambalo pia nali linashiria tukio hii. Watafiti mbali mbali wa Kiislamu [6] na wa Kiyahudi [7] wameyataja mazungumzo haya kuwa ni maalum na makhususi kwa Nabii Musa (a.s) peke yake. [8] Wayahudi wamepewa jina la "Kalimiy" kwa sababu ya sifa ya Kalimullah alionayo Nabii Musa (a.s). [9]

Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu pia alizungumza na Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika tukio la Mi'raj, pia kuna Hadithi kadhaa zinazoshiria mazungumzo haya. [10] Wao wanaamini kwamba; Kuwepo mazungumzo ya moja kwa moja baina ya Mungu mtume wake, ni tukio maalum lililotoke kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Nabii Musa (a.s). [11] Watafiti wa kidini ameyaelezea maneno Mungu kwenye mazungumzo hayo, kuwa ni maneno yaliotamkwa bila ya kutumia nyenzo za kimwili, kwa kuwa kuzungumza yafanyikayo kupitia ulimi, ni ishara ya kuwape kwa mwili, hali ya kuwa Mwenye Ezi Mungu hana mwili. [12]

Borusawi, ambaye ni mfasiri wa Qur’ani wa karne ya kumi na mbili, akielezea sababu ya Musa (a.s) kupewa sifa hii, inatokana na kuungua ulimi wake katika zama za utotoni mwake. Na Mwenye Ezi alizungumza na Nabii Musa ili kumfidia kutokana na kuungua, na kumpa jna jina hilo la Kalimullah. [13] Mfasiri huyu aliendelea katika kufafanua tukio hili kwa shairi unaorejelea tukio hili akisema:

"Kila shida ni utangulizi wa faraja, aligeuka akawa msemezwa na Mungu baada ya ulimi wa Kalim kuungua". [14]

Wafasiri wengine wametoa maelezo tofauti juu ya sababu ya lakabu hii ya Kalimullah, wakisema kwamba; Pale Mungu alipojitokeza kwa mara ya kwamnza kabisa mbele ya Musa (a.s), alijitambulisha alijitambulisha kwa kusema: "INNI ANA RABBUKAإِنِّی أَنَا رَبُّک؛ ; Mimi ni Mola wako", kwa hiyo unabii wa Musa (a.s) ulianza kwa neno la Mungu, na hili ndilo lililomfanya aitwe "Kalimullah". [15]

Rejea

Vyanzo