Kabila la Nakha'
Kabila la Nakha (Kiarabu: قبيلة نخع) ni kizazi mashuhuri zaidi cha kabila la al-Madh'hij [1] na linahusishwa na Jasr bin Amr [2] ambaye kutokana na kuwa mbali na kabila lake waliitwa Nakhai'. [3] Makazi ya kabila hili yalikuwa ardhi ya Yemen na baada ya kusilimu na kuingia katika Uislamu walihama na kuelekea katika maeneo ya Kufa na Misri. [4]
Takribani watu 200 wa kabila la Nakhai' ambao walitoa kiapo cha utii huko Yemen kwa Muadh bin Jabal swahaba wa Mtume (s.a.w.w), katika nusu ya mwaka wa 11 Hijiria walikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) na kusilimu. [5] Mtume aliliombea dua kabila la Nakhai' na akawaombea baraka kwa Mwenyezi Mungu. [6] Kabila la Nakhai' lilishiriki katika vita vya Qadisiyyah na watu miongoni mwa kabila hilo waliuawa kishahidi. [7] Kadhalika watu miongoni mwa kabila hilo walishiriki pia katika vita vya Yarmuk. [8]
Watu miongoni mwa kabila la Nakhai' walishiriki bega kwa bega na jeshi la Imam Ali (a.s) katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan. [9] Kabila la Nakhai' lilikuwa na watu mashuhuri sana. Baadhi yao ni:
- Malik al-Ashtar, [10] kamanda mashuhuri wa Imam Ali (a.s) katika vita vya Jamal na Siffin na mmoja wa wafanyakazi na gavana wake wa Misri. [11]
- Kumayl bin Ziyad al-Nakha'i mmoja wa maswahaba wa Imam Ali (a.s) ambaye aliuawa shahidi na Hajjaj bin Yusuf. [12]
- Artat bin Ka'b, alikuwa mmoja wa shakhsia wakubwa wa kabila hili ambaye alikwenda na watu wake kwa Mtume na aliuawa shahidi katika vita vya Qadisiyyah. [13]
- Ibrahim, mtoto wa Malik al-Ashtar, yeye alitoa kiapo cha utii kwa Mukhtar al-Thaqafi na alishiriki katika harakati na mapinduzi yake, [14] na aliuawa na Ubaidullah bin Ziyad. [15]
- Sanan bin Anas al-Nakha'I [16]. Huyu alikuwa katika jeshi la Omar bin Sa'd katika tukio la Karbala na kwa mujibu wa baadhi ya nukuu ndiye aliyemuua shahidi Imam Hussein (a.s). [17]
- Mussa bin Umran al-Nakha'i, mpokezi wa Ziyara ya al-Jami'a al-Kabira kutoka kwa Imam Hadi (a.s). [18]
Kuna kundi la Waarabu linaloishi katika baadhi ya maeneo ya Iran kama Birjand ambalo inasemekana asili yao ni Waarabu wa kabila la Nakha' ambalo likiwa pamoja na jeshi la Hazim bin Khuzaymah katika utawala wa Mansur Abbas (utawala: 136-158 Hijiria) lilifunga safari kwenda Khorasan kwa ajili ya kwenda kukabiliana na harakati na mapinduzi ya wananchi wa Khorasan na Sistan na likakaa katika eneo la Khosf. [19]
Kuna kitabu kilichoandikwa na Muntadhir al-Qaim na Maryam Saidiyan kinachoitwa Qabileh Nakha'i Dar Tarikh Eslam va Tashayyu ta payan qarn sevom Hijri" ambacho kinaelezea mchango na nafasi ya kabila la Nakha' katika matukio ya historia ya Uislamu na Uishia na maingiliano yao na Ahlul-Bayt (a.s) katika karne tatu za awali. [20]
Rejea
Vyanzo
- Amuzgar, Yusuf. Tārikhce-e Mukhtasar-e A'rab-e Janūb-e Khurasan (Manteqe-e Arab Khane). Jurnal Farhang Wa Adab. juz. 6, uk. 32 & 35, 1387 HS/2009.
- Bamtharaf, Muhammad Abdul Qadir, Al-Jāmi' (Jāmi' Shamula A'lām Al-Muhājirin Al-Muntasibīn Ilā Al-Yaman Wa Qabā'ilihim). Baghdad: Dar Ar-Rasyid, tanpa tahun.
- Firuzabadi, Muhammad bin Ya'qub, Al-Qāmus Al-Muhīth, Beirut: Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah, 1415 H.
- Ibn Athir, Ali bin Muhammad, Asad Al-Ghābah Fi Ma'rifah As-Shahābah, Beirut: Dar Al-Fikr, 1409 H.
- Ibn Hajar, Ahmad bin Ali. Al-Ishābah Fī Tamyīz Ash-Shahābah. Riset Adil Ahmad Abdul Maujud, Ali Muhammad Mua'awwadh. Beirut: Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah, 1415 H.
- Ibn Hazm Andalusi, Ali bin Ahmad. Jamharah Ansāb Al- 'Arab. Beirut: Dar Al-Kutub AL-Ilmiyyah, 1418 H.
- Ibn Jauzi, Abdurrahman bin Ali. Al-Muntadzam, Riset Atha, Muhammad Abdul Qadir, Atha, Muhstafa Abdul Qadir, Beirut: Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah, 1412 H.
- Ibn Kathir Damisyqi, Ismail bin Umar, Al-Bidāyah Wa An-Nihāyah, Beirut: Dar Al-Fikr, 1986.
- Ibn Sa'd, Muhammad bin Sa'd. Ath-Thabaqāt Al-Kubrā. Riset Muhammad Abdul Qadir Atha. Beirut: Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah, 1990.
- Ketabi Darbare-e "Qabīle-e Nakha' Dar Tarīkh-e Eslām" Muntasyir Syud. Site Mehr News Agency, diakses tanggal 30 September 2021.
- Qabīle-e Nakha' Dar Tārikh-e Eslām Wa Tasyayyu' Tā Pāyān-e Qarn-e Sawwum-e Hejri. Site Gisoom, diakses tanggal 30 September 2021.
- Saidiyan, Maryam, Jaigāh-e Buzurgān-e Nakha' Dar Ulūm Wa Farhang-e Eslāmi Dar Du Qarn-e Nukhust-e Hijri. Jurnal Adabiyat Wa Ulum-e Ensan. juz. 12-13, uk. 70, 1388 HS/2010.
- Shaduq, Muhammad bin Ali, Man Lā Yahdhuruhu Al-Faqīh, Qom: Nasyr-e Eslami, 1413 H.
- Shahari, Salmah bin Muslim, Al-Ansāb, Revisi Muhammad Ishan, Umman, Wizarah At-Turats Al-Qaumi Wa Ats-Tsaqafah, 1427 H.