Nenda kwa yaliyomo

Adhuhuri ya kisheria

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Jua kupinduka)
Kuainisha wakati wa kupinduka jua

Adhuhuri ya Kisheria au Zawali (Kiarabu: الظهر الشرعي أو الزوال) ni wakati wa jua kupinduka na kuacha usawa wa kati. Wakati wa zawali au adhuhuri ya kisheria ni pale kiashiria (alama) cha kivuli (fimbo, mkuki au kitu kingine kinapochomekwa ardhini ili kuamua mchana) kinapofikia kiwango kifupi zaidi wakati wa mchana.[1] Adhuhuri ya kisheria ni mwanzo wa wakati wa Sala ya adhuhuri.

Kwa mujibu wa mafaqihi, ikiwa kiashiria kitawekwa wima ardhini, wakati ambapo kivuli chake kinafikia kiwango chake cha chini kabisa huitwa Zawali au adhuhuri ya kisheria.[2]

Hukumu Zinazohusiana na Sharia Mchana

Maudhuri ya adhuhuri kisheria au adhuhuri kwa mujibu wa sheria ya fikihi, hujadiliwa katika mlango wa nyakati za Sala[3] na Saumu ya msafiri katika vitabu vya fikihi. Baadhi ya hukumu zinazohusiana na maudhui hii ni:

  • Adhuhuri ya kisheria hubadilika kulingana na maeneo kwa mujibu wa jiografia na kadhalika masiku na misimu ya mwaka.[4]
  • Kwa mujibu wa fat’wa za mafakihi ni kwamba, adhuhuri ya kisheria ni mwanzo wa wakati wa Sala ya adhuhuri.[5]
  • Kwa mujibu wa nadharia ya mafakihi, kama aliyefunga Saumu atasafiri kabla ya adhuhuri ya kisheria, Saumu yake itabatilika.[6]
  • Kama msafiri atarejea katika mji wake kabla ya adhuhuri au akafika sehemu ambayo amekusudia kukaa siku kumi, ikiwa hajafanya jambo linalobatilisha Saumu, anapaswa kufunga Saumu ya siku hiyo, na ikiwa ameleta jambo linalobatilisha Saumu, basi sio wajibu kwake kufunga siku hiyo.[7]

Rejea

  1. Husseini Sistani, Taqf al-Masal Jami, Juzuu 1, Toleo la 953
  2. Tabatabai Yazdi, Al-urwat al-uthqa, 1421 H. juzu 2, uk. 252; Imam Khomeini, Tawdhihu al-masail, 1391 S, Mas'ala 729, uk. 116; Makarim Shirazi, Tawdhihu al- masail, 1429 H, Bakhashe namazi, Mas'ale 672
  3. Tabatabai Yazdi, Al-urwat al-uthqa, 1421 H. juzu 2, uk. 673.
  4. Tabatabai Yazdi, Al-urwat al-uthqa, 1421 H. juzu 2, uk. 252.
  5. Tabatabai Yazdi, Al-urwat al-uthqa, 1421 H. juzuu 2, uk. 252; Imam Khomeini, Tawdhihu al-masail, 1391 S, Mas'ala 729, uk 116; Makarim Shirazi, Tawdhihu al- masail, 1429 H, Bakhashe namazi, Mas'ale 672.
  6. Bani Hashim Khomeini, Tadhihu al-masail marjii, 1381 S,juz. 1, uk. 953
  7. Bani Hashim Khomeini, Tadhihu al-masail marjii, 1381 S,juz. 1, uk. 994

Vyanzo