Israeli (Lakabu)
- Usichanganywe na utawala wa Israel.
Israeli (Kiarabu: إسرائيل) ni lakabu ya Nabii Yaqub au Yakobo. Kulingana na kitabu cha tafsiri ya Majma‘u al-Bayan, neno Israeli katika lugha ya Kiebrania humaanisha Mteule wa Mungu au Mtumishi wa Mungu.[1] Sheikh Tusi maana ya jina hili, anasema kwamba; «Israeli' limeundwa kunatokana na maneno mawili; la kwanza ni Isra, ambalo linamaanisha mtumishi, na la pili ni «Il», linalomaanisha Mwenye Ezi Mungu, na hivyo «Israeli» likawa na maana ya Mtumishi wa Mungu.[2] Kulingana na wafasiri wa Kishia, neno 'Israeli' lililopo katika Aya ya 93 ya Surat Al-Imran, na Aya ya 58 ya Surat Maryam, linamhusiana moja kwa moja na Yakobo au Yaqub.[3] Hii ndiyo sababu hasa ya wana wa nabii Yakobo au Yaqub na vizazi vyake kumepewa jina la Bani Israeli katika Qur’ani.[4]
KatikaTaurati kuna kisa kinachoeleza kwamba; Moja kati ya nyusiku (wingi neno usiku), Mwenye Ezi Mungu alishindana na Yakobo kwa kupigana naye mieleka, na baada ya Mwenyezi Mungu kushindwa na kudhibitiwa na nabi 'Yakobo/Yaaquub', alimwambia nabi huyo kwa kusema: 'Niachilie, kwa kuwa tayayari usiku umeshaanza kupambazuka,' Hapo Yakobo au Yaqub akajibu: 'Sitakuachilia hadi unibariki.' Mwenye Ezi Mungu akamwuliza: Jina lako ni nani? Naye akajibu: Yakobo au Yaqub, Mwenye Ezi Mungu akamwambia: Kuanzia sasa hvi jina lako si Yakobo au Yaqub, bali utajulikana kwa jina la Israeli, kwa sababu umeonyesha nguvu zako dhidi ya Mungu pamoja na binadamu na hatimae ukawashinda.[5]
Rejea
- ↑ Tabarsi, Majma' al-Bayan, juz. 1, uk. 182.
- ↑ Sheikh Tusi, Al-Tabiyan fi Tafsir al-Quran, Dar Ihya al-Turath al-Arabi, juz. 1, uk. 180.
- ↑ Tabarsi, Majma'u al-Bayan, 1415 AH, juz. 2, uk. 344; Subhani, Manshor Jawid, Muasase Imam Sadiq (a.s), Qom, juz. 11, uk. 325.
- ↑ Rouhi, «Kuonekana kwa Wana wa Israeli katika Quran na Maagano», 1384 S, uk. 58.
- ↑ Agano la Kale, 1393 S, juz. 1, uk. 234-236.
Vyanzo
- Rouhi, Abulfadhl, «Simayi Bani Israil Dar Qur'an wa Ahdein», katika Jarida la Marafat, Na. 95, Aban 1384 S.
- Subhani, Jafar, Manshor Jawid, Qom, Muasase Imam Sadiq (a.s), 1390 S.
- Sheikh Tusi, Muhammad ibn Hassan, Al-Tabiyan fi Tafsir al-Qur'an, Beirut, Dar Ihya al-Turath al-Arab, Beta.
- Tabarsi, Fadhl ibn Hassan, Majma’ al-Bayan fi Qur’an, Beirut, Muasasat al-Aala Lil-Matbuat, 1415 AH.
- Agano la Kale (juz. 1: Books of the Law or Torah), iliyotafsiriwa na Pirouz Sayar, Tehran, Nashr Hermes, 1393 S.