Hotuba ya Gharaa

Kutoka wikishia

Hotuba ya Gharaa (Kiarabu: الخطبة الغرَّاء) ni moja ya hotuba maarufu ndani ya kitabu cha Nahj al-Balagha. [1] Hotuba hii inajulikana kwa jina la Hotuba ya Gharaa (yaani hotuba yenye nuru na kung'aa) kutokana na ufasaha na wa hali ya juu uliotumika ndani yake. [2] Ibn Abi Al-Hadid anaiona hotuba hii kuwa ni moja ya karama za Imamu Ali (a.s). [3] Katika hotuba hii yenye maneno mepesi ndani yake, kumetumika mbinu kadhaa za kifasaha na kiubunifu zilizostawisha ibara zake. Miongoni mwa nyezo za lugha ailizomo ndani yake ni pamoja na; tashbihi, saj’u (vibwagizo), istiara (sitiari) na mafumbo. [4] Kulingana na Riwaya ya Sayyid Radhiy, ambaye ni mkusanyaji wa Nahj al-Balagha, ni kwamba; Pale walipoisikia hotuba hii, walitetemeka kwa hofu na kulia kutokana na uzito wa yaliyomo ndani yake. [5]

Yaliyomo katika hotuba hii yanahusisha mada nne kuu: 1. Mwanadamu na historia yake 2. Kulaani mapenzi ya dunia 3. Ushauri wa kuwa na takwa pamoja na sifa za wacha Mungu 4. Maelezo ya matukio baada ya kifo. Katika sehemu inayohusiana na mwanadamu na historia yake, ambayo inachukuliwa kuwa ndio mada muhimu zaidi ya hotuba hii, imejadili masuala muhimu ndani ya maisha ya mwanadamu. Masuala muhimu hayo ni pamoja na; kifo cha mwanadamu, neema alizopewa, kughafilika kwake, maisha ya kidunia, kuwaidhika kwa mwanadamu, na kutoweka kwa dunia. [6] Kwa mujibu wa maelezo ya Abū Nuʿaim al-Iṣfahānī katika Ḥilyatu al-Awliyaa’i wa Ṭabaqati al-Aṣfiyaa, ni kwamba; Imamu Ali (a.s) alitoa hotuba hii wakati ambapo mwili wa mmoja marehemu ulipokuwa tayari umeshawekwa kaburini, huku familia yake iligubikwa na kilio na maombolezo. [7]

Sayyid Abdul-Zahra Hussainiy Khatib, mwandishi wa kitabu Masadir Nahji al-Balaghati wa Asaniduhu, anaamini kuwa; si wa lazima wala hakuna haja katika kutathmini uhalali wa hotuba hii, kufanya utafiti wa sanad (mlolongo wa wapokezi) ya hotuba hii. Kutofanya hivyo ni kwa sababu ya kwamba; kiwango cha juu cha ufasaha na ubunifu katika hotuba hii ni cha kipekee kabisa, kiasi kwamba hakuna yeyote mwenye uwezo wa kuiwasilisha mada fulani kwa kiwango kama hicho isipokuwa Maasumu tu (aliyetakaswa na Mola wake). [8] Mbali na Nahj al-Balagha, sehemu za hotuba hii pia zinaweza kupatikana katika kazi nyengine andishi, kama vile Tuhafu al-Uqul [9] na Hilyatu al-Awliya wa Tabaqatu al-Asfiyaa. [10] [11]

Kulingana na maelezo ya Abdul-Zahra Hussaini Khatib,ni kwamba;  Katika kitabu Al- Iqdu al-Farid, [12] kuna hotuba nyingine ya Imamu Ali  (a.s), ambayo imeitwa Hotubatu Al-Gharaa kimakosa. [13] Vivyo hivyo, katika Taysir al-Matalib, hotuba nambari 185 ya Nahj al-Balagha imepewa jina la Hotuba Al-Gharaa. [14] Sayyid Sadiq Musawi, katika kitabu Tamamu Nahj al-Balagha, anachukulia Hotuba nambari 237 ya Nahju al-Balagha kuwa sehemu ya Hotubatu Al-Gharaa. [15]

Nambari ya mpangilio wa hotuba hii hutofautiana kulingana na matoleo na machapisho mbalimbali ya Nahj al-Balagha. [16]

Jina la Chapisho Nambari ya Hotuba
Al-Muujamu Al-Mufahrasa, Subhi Al-Saleh 83
Faidhu Al-Islam, Sherehe ya Khui, Mullasaleh, Ibnu Abi Al-hadid 82
Ibnu Maitham 80
Abdu 79
Mola Fathullahi 84
Fi Dhilali 81

Matini na Tafsiri ya Khutbatu Al-Gharraa

اَلْحَمْدُ لِلهِ الَّذی عَلا بِحَوْلِهِ، وَ دَنا بِطَوْلِهِ، مانِحِ كُلِّ غَنیمَة وَ فَضْل، وَ كاشِفِ كُلِّ عَظیمَة وَ اَزْل {17}

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametukuka kwa nguvu Zake na amekaribia kwa ukarimu Wake, Mtoaji wa kila neema na fadhila, na mwepeshaji wa kila shida na dhiki.

اَحْمَدُهُ عَلی عَواطِفِ كَرَمِهِ، وَ سَوابِغِ نِعَمِهِ، وَ اُومِنُ بِهِ اَوَّلاً بادِیاً، وَ اَسْتَهْدیهِ قَریباً هادِیاً، وَ اَسْتَعینُهُ قاهِراً قادِراً وَ اَتَوَكَّلُ عَلَیهِ كافیاً ناصِراً

Namshukuru Yeye kwa ukarimu Wake wa kina na neema Zake zisizokoma, na namuamini Yeye kama wa kwanza Mwanzilishi ya viumbe. Na namwomba mwongozo Wake akiwa Yeye ndiye wa karibu na mwongozaji, na ninamwomba msaada Wake akiwa Yeye ndiye Mshindi na Mwenye uwezo, na namtegemea Yeye akiwa Yeye ndiye mtoshelezaji na msaidizi.

وَ اَشْهَدُ اَنَّ مُحَمَّداً صَلَّی اللهُ عَلَیهِ وَ آلِهِ عَبْدُهُ وَ رَسُولُهُ، اَرْسَلَهُ لاِنْفاذِ اَمْرِهِ، وَ اِنْهاءِ عُذْرِهِ، وَ تَقْدیمِ نُذُرِهِ

Na ninashuhudia kwamba Muhammad (s.a.w.w) ni mja Wake na Mtume Wake, ambaye alimtuma kutekeleza amri zake, kukamilisha hoja Yake, na kufikisha maonyo Yake.

اُوصیكُمْ عِبادَ اللهِ بِتَقْوَی اللهِ الَّذی ضَرَبَ لَكُمُ الْاَمْثالَ، وَ وَقَّتَ لَكُمُ الْاجالَ، وَاَلْبَسَكُمُ الرِّیاشَ، وَ اَرْفَعَ لَكُمُ الْمَعاشَ، وَ اَحاطَ بِكُمُ الْاحْصاءَ،

Enyi waja wa Mungu, ninakuusieni kumcha Mwenye Ezi Mungu, ambaye amekupigieni mifano (ya kila aina), akakupangilieni muda (ahadi) wa maisha yenu, na akakuvisheni mavazi (akakusitirini tupu zenu), akaziinua riziki zenu (akaboresha maisha yenu), na akakuzungukeni kwa ujuzi wake wa kina (kupitia hisabu makini mno).

وَ اَرْصَدَ لَكُمُ الْجَزاءَ، وَ آثَرَكُمْ بِالنِّعَمِ السَّوابِغِ وَالرِّفَدِ الرَّوافِغِ، وَ اَنْذَرَكُمْ بِالْحُجَجِ الْبَوالِغِ، وَ اَحْصاكُمْ عَدَداً، وَ وَظَّفَ لَكُمْ مُدَداً فی قَرارِ خِبْرَةٍ وَ‌ دارِ عِبْرَةٍ،

Na amekuandalieni malipo, akakuinueni kwa baraka zisizokoma na neema zisizohisabika, na akakuonyeni kwa hoja na dalili kamili. Na Amekuhisabuni kwa idadi, na akakuweeni muda muaalu wa kuishi duniani, ambayo ni nyumba ya mitihani na sehemu ya mazingatio (mafunzo).

اَنْتُمْ مُخْتَبَرُونَ فیها وَ مُحاسَبُونَ عَلَیها، فَاِنَّ الدُّنْیا رَنِقٌ مَشْرَبُها، رَدِغٌ مَشْرَعُها، یونِقُ مَنْظَرُها، وَ یوبِقُ مَخْبَرُها. غُرُورٌ حائِلٌ، وَ ضَوْءً آفِلٌ، وَ ظِلٌّ زائِلٌ، وَ سِنادٌ مائِلٌ.

Ninyi mumo katika majaribio (mitihani) ndani yake, na mnatathminiwa (mtahisabiwa) kulingana na mitihani hiyo. Hakika vinyaji vyake si visafi, na chanzo cha michirizi yake ni kichafu, mwonekano wake ni mzuri, ila mwisho wake ni kuangamia. Ni pazia danganyifu la mpito, mwanga unaotoweka, kivuli kinachopotea, na nguzo inayopindika (isiyotegemeka).

حَتّی اِذا اَنِسَ نافِرُها، وَ اطْمَاَنَّ ناكِرُها، قَمَصَتْ بِاَرْجُلِها، وَ قَنَصَتْ بِاَحْبُلِها، وَ اَقْصَدَتْ بِاَسْهُمِها، وَ اَعْلَقَتِ الْمَرْءَ اَوْهاقَ الْمَنِیةِ،

Hata atakapo anasika mtegemezi wake (aliyeitegemea), na kupata utulivu mkimbizi wake (aliyeikimbilia), itamshika miguu yake, na itamdhibiti kwa kamba zake, na itatuma mishale yake, na itamfunga mtu huyo na kumwongoza mautini.

قائِدَةً لَهُ اِلی ضَنْكِ الْمَضْجَعِ، وَ وَحْشَةِ الْمَرْجِعِ، وَ مُعاینَةِ الْمَحَلِّ، وَ ثَوابِ الْعَمَلِ.

Itamwongoza na kumuelekeza kwake, hadi kwenye malazi ya dhiki (kaburi), na marejeo ya upweke (yatishayo), na kumkutanisha na mahali (pa milele), na malipo ya amali.

وَ كَذلِكَ الْخَلَفُ یعْقُبُ السَّلَفَ، لاتُقْلِعُ الْمَنِیةُ اخْتِراماً، وَلایرْعَوِی الْباقُونَ اجْتِراماً، یحْتَذُونَ مِثالاً، وَ یمْضُونَ اَرْسالاً اِلی غایةِ الانْتِهاءِ، وَ صَیورِ الْفَناءِ.

Na vivyo hivyo (hali ya dunia), wajao hushika nafasi za walio tangulia. Kifo hakisimami kwa kuwaondoa waliotangulia, na wala wale wanaobaki hawaachi maouvu (hawajifunzi kutokana na vifo vya waliotangulia). Wanafuata mifano ya waliowatangulia (katika uasi wao), na wanaendelea bila kukoma hadi mwisho wa safari yao, na hatimae kuangamia na kutokomea.

حَتّی اِذا تَصَرَّمَتِ الْاُمُورُ، وَ تَقَضَّتِ الدُّهُورُ، وَ اَزِقَ النُّشُورُ، اَخْرَجَهُمْ مِنْ ضَرائِحِ الْقُبُورِ، وَ اَوْكارِ الطُّیورِ، وَ اَوْجِرَةِ السِّباعِ، وَ مَطارِحِ الْمَهالِكِ، سِراعاً اِلی اَمْرِهِ، مُهْطِعینَ اِلی مَعادِهِ،

Hadi pale mambo yatakapomalizika, nyakati kupita, na ufufuo ukawadi, Atawatoa kutoka kwenye makaburi (yao). Makazi ya ndege, mapango ya wanyama pori, na maeneo ya hatari, kwa haraka mno (vyote vitaelekea) kwenye amri Yake, (vyote) vitakimbilia kwenye marejeo yake (uwanja wa hukumu).

رَعیلاً صُمُوتاً، قِیاماً صُفُوفاً، ینْفِذُهُمُ الْبَصَرُ، وَ یسْمِعُهُمُ الدَّاعی، عَلَیهِمْ لَبُوسُ الاِسْتِكانَةِ، وَ ضَرَعُ الاِسْتِسْلامِ وَ الذِّلَّةِ،

Wamehudhuria kwa makundi wakiwa kimya kabisa, hali wakiwa wamesimama safu kwa safu, huku wote wakiwa kwenye mashiko ya jicho la Mwenye Ezi Mungu, na sauti ya mwito ikiwafikia. Wamegubikwa na nguo ya unyenyekevu, na kuwaingiza kwenye magubiko kwenye hali unyonge wa kujisalimisha na kudhalilika.


قَدْ ضَلَّتِ الْحِیلُ، وَ انْقَطَعَ الاَمَلُ، وَ هَوَتِ الاَفْئِدَةُ كاظِمَةً، وَخَشَعَتِ الْاصْواتُ مُهَینِمَةً، وَاَلْجَمَ الْعَرَقُ، وَ عَظُمَ الشَّفَقُ، وَ اُرْعِدَتِ الْاسْماعُ لِزَبْرَةِ الدّاعی اِلی فَصْلِ الْخِطابِ، وَ مُقایضَةِ الْجَزاءِ، وَ نَكالِ الْعِقابِ، وَ نَوالِ الثَّوابِ.

Siku ambayo hakutakuwa na suluhisho litakalofaa (ujanja wote utapotea), matarajio yamekatika, mioyo itakuwa imejaa hofu na kugubikwa na ukimya, sauti zitarudi chini na kufifia, jasho hadi kinywani, na hofu ya dhambi imekolea mno, masikio yanatetemeka kutokana mngurumo wa sauti wa mwito wa Mungu unao tangaza hukumu ya wazi kati ya haki na batili, na kila mmoja kufikia malipo ya matendo mema na mabaya, na kupewa adhabu na thawabu.

عِبادٌ مَخْلُوقُونَ اقْتِداراً، وَ مَرْبُوبُونَ اقْتِساراً، وَ مَقْبُوضُونَ احْتِضاراً، وَ مُضَمَّنُونَ اَجْداثاً، وَ كائِنُونَ رُفاتاً، وَ مَبْعُوثُونَ اَفْراداً، وَ مَدینُونَ جَزاءً، وَ مُمَیزُونَ حِساباً.

Huu ni umati wa waja walioumbwa kwa uwezo wa Muumba, na wameongoza na kuwekwa mikonono mwa Mola wao (wamelelewa) bila hiari zao. Wamekufa kwa hudhurio la malaika, na miili yao imekumbatiwa na makaburi, na wamegeuka na kuingia katika hali ya kuoza, na watafufuliwa kutoka makaburi mwao hali wakiwa peke yao, na watalipwa  jaza zao kulingana na matendo yao, na hali zao zitatofautiana kupitia hesabu ya Mungu.


قَدْ اُمْهِلُوا فی طَلَبِ الْمَخْرَجِ، وَ هُدُوا سَبیلَ الْمَنْهَجِ، وَ عُمِّرُوا مَهَلَ الْمُسْتَعْتِبِ، وَ كُشِفَتْ عَنْهُمْ سُدَفُ الرِّیبِ، وَ خُلُّوا لِمِضْمارِ الْجِیادِ، وَ رَوِیةِ الْارْتِیادِ، وَ اَناةِ الْمُقْتَبِسِ الْمُرْتادِ فی مُدَّةِ الْاجَلِ وَ مُضْطَرَبِ الْمَهَلِ.

Hao walipatiwa muda duniani ili kutoka katika upotofu, na walielekezwa kwenye njia iliyo wazi, na wakapatiwa nafasi ya kujirkebisha, pazia tatanishi liliondolewa mbele ya macho yao, waliachiliwa katika uwanja wa mashindano ya kuelekea katika mambo mema, na walipatiwa nafasi ya kutafakari ili kufikia viwango bora na kufikia nuru ya kufuzu katika kipindi cha maisha na nafasi ya muda waliopewa.

فَیا لَها اَمْثالاً صائِبَةً، وَ مَواعِظَ شافِیةً، لَوْ صادَفَتْ قُلُوباً زاكِیةً، وَ اَسْماعاً واعِیةً، وَ آراءً عازِمَةً، وَاَلْباباً حازِمَةً.

Ni mifano ya ajabu ilioje, ambayo sahihi na ya kweli, na ni mawaidha yenye ponya, yatakukutana na mioyo safi, masikio sikivu, fikra thabiti, na akili zenye busara.

فَاتَّقُوا اللهَ تَقِیةَ مَنْ سَمِعَ فَخَشَعَ، وَ اقْتَرَفَ فَاعْتَرَفَ، وَ وَجِلَ فَعَمِلَ، وَ حاذَرَ فَبادَرَ، وَ اَیقَنَ فَاَحْسَنَ، وَ عُبِّرَ فَاعْتَبَرَ، وَ حُذِّرَ فَحَذِرَ، وَ زُجِرَ فَازْدَجَرَ، وَ اَجابَ فَاَنابَ، وَ رَجَعَ فَتابَ، وَ اقْتَدی فَاحْتَذی، وَ اُرِی فَرَأی.

Kwa hivyo, mcheni Mungu kwa kiwango cha yule aliyesikia (wito) na akainama (akarukuu) kwa unyenyekevu, aliye fanya dhambi kisha akakiri kosa lake, akaogopa na akaanza kutenda matendo mema, akajihadhari na akakimbilia kwenye utiifu, aliye ifikia yakini na akatenda wema, aliye funzwa (aliyepewa mazingatio) akajifunza (akazingatia). Aliyepewa onyo, akakhofu, aliyezuiliwa na dhambi na akajizuia, aliyejibu wito wa haki na kujisogeza (kwa Allah), aliyejiondoa kwenye dhambi na katubu, akafuata viongozi wa njia ya haki na akashikamana na njia yao, aliye ongozwa akaongoka.

فَاَسْرَعَ طالِباً، وَ نَجا هارِباً، فَاَفَادَ ذَخیرَةً، وَ اَطابَ سَریرَةً، وَ عَمَّرَ مَعاداً، وَ اسْتَظْهَرَ زاداً لِیوْمِ رَحیلِهِ، وَ وَجْهِ سَبیلِهِ، وَ حالِ حاجَتِهِ، وَ مَوْطِنِ فاقَتِهِ، وَ قَدَّمَ اَمامَهُ لِدارِ مُقامِهِ.

Basi aliharakisha kutafuta ukweli (haki) na akupata wokovu kwa kuepuka ubaya. Akajiwekea akiba kwa ajili ya Akhera yake, akajisafisha nafsi yake, akajijenga kwa ajili ya Siku ya Kiyama (akajiandaa kwa ajili ya Akhera), na akapakiza mizigo wa mahitaji yake juu ya mnyama wake, kwa ajili ya siku ya kuondoka kwake (siku ya kifo chake), ambayo ni safari iliyojaa hatari (ndani yake), (mzigo ambao utamfaa) wakati wa uhitaji wake, na katika hali au mahali pa umaskini wake. Aliitanguliza mbeleni akiba (yake) kwa ajili ya makazi yake ya milele.

فَاتَّقُوا اللهَ عِبادَ اللهِ جِهَةَ ما خَلَقُكُمْ لَهُ، وَ احْذَرُوا مِنْهُ كُنْهَ ما حَذَّرَكُمْ مِنْ نَفْسِهِ، وَ اسْتَحِقُّوا مِنْهُ ما اَعَدَّ لَكُمْ بِالتَّنَجُّزِ لِصِدْقِ میعادِهِ، وَالْحَذَرِ مِنْ هَوْلِ مَعادِهِ.

Kwa hivyo, mcheni Mwenye Ezi Mungu, enyi waja wa Mungu, kwani hilo ndiyo lengo la kukuumbeni. Na mkhofuni kwa kina kama vile alivyo kutahadharini kuhusiana na nafsi yak. Tendeni na jitayarisheni (kwa matayarisho meme) ili muweze kustahiki kutoka Kwake yale aliyokuandalieni, na ili  muweze kupata yale aliyokuahidini, na tahadhari kutokana na msiba wa hofu wa siku ya marejeo Yake.


Sayyid Razi ananukuu sehemu nyingine ya khutba hii kama ifuatavyo:

جَعَلَ لَكُمْ اَسْماعاً لِتَعِی ما عَناها، وَ اَبْصاراً لِتَجْلُوَ عَنْ عَشاها، وَ اَشْلاءً جامِعَةً لِاَعْضائِها، مُلائِمَةً لِاَحْنائِها، فی تَرْكیبِ صُوَرِها، وَ مُدَدِ عُمُرِها، بِاَبْدان قائِمَة بِاَرْفاقِها، وَ قُلُوب رائِدَة لِاَرْزاقِها، فی مُجَلِّلاتِ نِعَمِهِ، وَ مُوجِباتِ مِنَنِهِ، وَ حَواجِزِ عافِیتِهِ.

Amekupeni masikio ili mukisikie kile alichokikusudia, na (akakueni) macho ili yapembua giza na yaone (haki), na viungo vilivyokamilika seheme zake, viendazo sawa na vilivyopo (ndani ya mwili), katika kujenga muundo wa sura zake na muhula wa maisha ya kila kimoja kati yavyo, (vimehimiliwa) kwa miili inayosimama kwa msaada wa viungo vyake, na mioyo inayotafuta riziki zake, (huku viumbe) vyote vikiwa katika wingi wa neema Zake, matakwa ya fadhila Zake, na ngao za afya Yake.

وَ قَدَّرَ لَكُمْ اَعْماراً سَتَرَها عَنْكُمْ، وَ خَلَّفَ لَكُمْ عِبَراً مِنْ آثارِ الْماضینَ قَبْلَكُمْ: مِنْ مُسْتَمْتَعِ خَلاقِهِمْ، وَ مُسْتَفْسَحِ خِناقِهِمْ،

Na akakukadirieni muda wa maisha yanu, huku akiwa amekuficheni kiwango cha makadirio ya maisha hayo, akakuekeeni mifano (ili mjifunze), kutoka katika athari zilizoachwa na waliotangulia kabla yenu: kutokana na manufaa waliyojivunia kutoka katika dunia hii, na kutokana na urefu wa maisha waliokuwa nayo kabla ya mauti kuwafikia.

اَرْهَقَتْهُمُ الْمَنایا دُونَ الْامالِ، وَ شَذَّبَهُمْ عَنْها تَخَرُّمُ الْاجالِ. لَمْ یمْهَدُوا فی سَلامَةِ الْابْدانِ، وَ لَمْ یعْتَبِرُوا فی اُنُفِ الْاوانِ.

Lakini mauti yaliwafikia kabla ya wao kuyafikia matamanio (matarajio) yao, na kukatika kwa kamba ya maisha kukawatenganisha yale matamanio yao. Wakati walipokuwa na afya, hawakujiandaa kwa ajili ya Akhera yao, na hawakujifunza pale ambapo wakati bado ulikuwa ungalipo.

فَهَلْ ینْتَظِرُ اَهْلُ بَضاضَةِ الشَّبابِ اِلاّ حَوانِی الْهَرَمِ؟ وَ اَهْلُ غَضارَةِ الصِّحَّةِ اِلاَّ نَوازِلَ السَّقَمِ؟ وَ اَهْلُ مُدَّةِ الْبَقاءِ اِلاّ آوِنَةَ الْفَناءِ؟

Je, kijana aliyefikia kilele cha ujana wake anaweza kutarajia chochote chengine isipokuwa kuufikia uzee na ukongwe? Na je yule mtu mwenye afya njema, anaweza kusubiri chochote zaidi ya uwezekano wa kukabiliwa na magonjwa mbalimbali? Na kwa yule aliye hai sasa, je, kuna anachokisubiri isipokuwa kufikiawa (kuwadia) na wakati wa kifo chake?

مَعَ قُرْبِ الزِّیالِ، وَ اُزُوفِ الْانْتِقالِ، وَ عَلَزِ الْقَلَقِ، وَ اَلَمِ الْمَضَضِ، وَ غُصَصِ الْجَرَضِ، وَ تَلَفُّتِ الْاسْتِغاثَةِ بِنُصْرَةِ الْحَفَدَةِ وَالْاقْرِباءِ وَ الْاعِزَّةِ وَ الْقُرَناءِ.

Kadiri wakati wa kuondoka na kuachana na maisha unavyokaribia, kunazuka hofu na wasiwasi, maumivu ya uchungu ya moyoni, na kumeza mate (kwa uchungu wa maumivu). Mtu hutazama pande zote kwa matumaini, akitafuta faraja kutoka kwa watoto, jamaa, marafiki, na mwenzi wake wa ndoa, akihitaji msaada na upendo katika safari hiyo ya mwisho ya kuachana na maisha yake.

فَهَلْ دَفَعَتِ الْاقارِبُ؟ اَوْ نَفَعَتِ النَّواحِبُ؟ وَ قَدْ غُودِرَ فی مَحَلَّةِ الْامْواتِ رَهیناً، وَ فی ضیقِ الْمَضْجَعِ وَحیداً،

Je, hawa wote waliokaribu (jamaa na familia) wana uwezo wa kumzuia mtu asikutane na mauti? Je, wale wanaomlilia wana msaada wowote kwake? Hali ya kwamba maiti wao tayari amewekwa kaburini, na ameachwa peke yake katika malazi yenye nafasi iliyo finyu mno,

قَدْ هَتَكَتِ الْهَوامُّ جِلْدَتَهُ، وَ اَبْلَتِ النَّواهِكُ جِدَّتَهُ، وَ عَفَتِ الْعَواصِفُ آثارَهُ، وَ مَحَا الْحَدَثانُ مَعالِمَهُ، وَ صارَتِ الْاجْسادُ شَحِبَةً بَعْدَ بَضَّتِها، وَ الْعِظامُ نَخِرَةً بَعْدَ قُوَّتِها، وَ الْارْواحُ مُرْتَهَنَةً بِثِقَلِ اَعْبائِها، مُوقِنَةً بِغَیبِ اَنْبائِها، لاتُسْتَزادُ مِنْ صالِحِ عَمَلِها، وَ لاتُسْتَعْتَبُ مِنْ سَییءِ زَلَلِها.

Tayari wadudu wameshaila ngozi yake na kuikata vipande vipande, na tayari vichakazaji vimeshauchakaza mwili wake, uliokuwa safi na mwororo, kuwa wa zamani. Upepo mkali umefuta athari zake, na matukio (mapito) ya zama yameshafuta alama zake (alama za uwepo wake); miili ambayo ilikuwa mibichi, tayari imeshachakaa (imeshakonga), na mifupa iliyokuwa imara imeshakaa. Roho zimebaki na mizigo ya madhambi zao, sasa wamekuwa na uhakika kuhusu habari za ghaibu baada ya kifo kwao. Huko, hawatakuwa na uwezo wa kuongeza mema yao, wala hawatapata ruhusa ya kumwomba Mungu msamaha kutokana na makosa yao.

اَوَلَسْتُمْ اَبْناءَ الْقَوْمِ وَ الْاباءَ؟ وَ اِخْوانَهُمْ وَ الْاقْرِباءَ؟ تَحْتَذُونَ اَمْثِلَتَهُمْ، وَ تَرْكَبُونَ قِدَّتَهُمْ، وَ تَطَؤُونَ جادَّتَهُمْ؟

Je, ninyi mlio hai si watoto wa watu hawa—wazazi wenu, ndugu zao, na jamaa zao—ambao mnawafuata kwa nyenendo zao, mnapita njia walizopita, na kufuata nyayo zao?

فَالْقُلُوبُ قاسِیةٌ عَنْ حَظِّها، لاهِیةٌ عَنْ رُشْدِها، سالِكَةٌ فی غَیرِ مِضْمارِها، كَاَنَّ الْمَعْنِی سِواها، و كَاَنَّ الرُّشْدَ فی اِحْرازِ دُنْیاها.

Basi, mioyo imekuwa migumu na katika kujitafutia fungu la la kiroho (kutenda amali njema), imesahau kutafuta mwongozo na mafanikio yake, na kuelekea katika njia isiyo sahihi, kana kwamba wao sio wakusudiwa wa makusudio ya Haki (Amri na makatazo ya Mungu), na kana kwamba uongofu na wokovu vipo katika kujikusanyia mali za dunia.

وَ اعْلَمُوا اَنَّ مَجازَكُمْ عَلَی الصِّراطِ، وَ مَزالِقِ دَحْضِهِ، وَ اَهاویلِ زَلَلِهِ، وَ تاراتِ اَهْوالِهِ.

Na jueni kwamba mapito yenu yenu ni juu ya Sirati, mahali ambapo miguu huteleza, na ni eneo lenye hofu, woga, na hatari za kila aina.

فَاتَّقُوا اللهَ عِبادَاللهِ تَقِیةَ ذِی لُبٍّ شَغَلَ التَّفَكُّرُ قَلْبَهُ، وَ اَنْصَبَ الْخَوْفُ بَدَنَهُ، وَ اَسْهَرَ التَّهَجُّدُ غِرارَ نَوْمِهِ، وَ اَظْمَاَ الرَّجاءُ هَواجِرَ یوْمِهِ، وَ ظَلَفَ الزُّهْدُ شَهَواتِهِ، وَ اَرْجَفَ الذِّكْرُ بِلِسانِهِ، وَ قَدَّمَ الْخَوْفَ لِاَمانِهِ،

Basi, mcheni (mkhofuni) Allah enyi waja wa Mungu, kueni na taqwa ya kiwango cha mtu mwenye busara ambaye moyo wake umeshughulishwa na tafakuri, na hofu ya adhabu imeudhoofisha (imeuumiza) mwilini mwake. Ibada ya usiku imepunguza usingizi kutoka machoni mwake, na matumaini ya rehema za Mungu yamemfanya avumilie kiu ya joto la mchana. Kujizuia na mapenzi ya dunia kumemfanya aepukane na matamanio yake, na kumdhukuru Allah kumeufanya ulimi wake uwe mwepesi. Amechagua hofu ili apate amani katika Siku ya Kiyama.

وَ تَنَكَّبَ الْمَخالِجَ عَنْ وَضَحِ السَّبیلِ، وَ سَلَكَ اَقْصَدَ الْمَسالِكِ اِلَی النَّهْجِ الْمَطْلُوبِ، وَ لَمْ تَفْتِلْهُ فاتِلاتُ الْغُرُورِ، وَ لَمْ تَعْمَ عَلَیهِ مُشْتَبِهاتُ الْامُورِ، ظافِراً بِفَرْحَةِ الْبُشْری، وَ راحَةِ النُّعْمی، فی اَنْعَمِ نَوْمِهِ، وَ آمَنِ یوْمِهِ،

Na ameepuka fikra zinazoweza kumzuia kuifikia njia ya wazi ya Haki, na akufuata njia ifaayo zaidi ili kufikia mfumo lengwa (uliokusudiwa ambayo ni njia ya Mungu). Mitelezo ya kiburi na majivuno haijamrudisha nyuma na kumweka nje ya njia ya Haki, na wala mikanganyiko haikuweza kufichika mbele yake. Amefanikiwa kupata bishara njema  (ya Mungu wake ya kuingia Peponi), na starehe ya maisha ya Akhera katika makazi ya malazi yake yenye utulivu zaidi, na mchana wake ulio salama zaidi.

قَدْ عَبَرَ مَعْبَرَ الْعاجِلَةِ حَمیداً، وَ قَدَّمَ زادَ الْاجِلَةِ سَعیداً، وَ بادَرَ مِنْ وَجَل، وَ اَكْمَشَ فی مَهَل، وَ رَغِبَ فی طَلَب، وَ ذَهَبَ عَنْ هَرَب، وَ راقَبَ فی یوْمِهِ غَدَهُ، وَ نَظَرَ قَدَماً اَمامَهُ.

Amevuka kivuko cha safari ya dunia (kwenda Akhera) kwa namna iliyokubalika (inayostahiki sifa), , na ametuma mbele yake akiba kwa ajili ya Akhera kwa furaha kabisa. Akafanya haraka katika kuyakimbilia mema kwa sababu ya khofu, na ametumia muda wake kwa bidii. Akaonesha hamu katika kutafuta radhi za Mola wake, na akaepuka dhambi kutokana na kumkhofu Mwenye Ezi Mungu. Aliitazama kesho yake kupitia leo yake, na daima aliangalia mbeleni kwake kwa azma thabiti.

فَكَفی بِالْجَنَّةِ ثَواباً وَ نَوالاً، وَ كَفی بِالنّارِ عِقاباً وَ وَبالاً، وَ كَفی بِاللهِ مُنْتَقِماً وَ نَصیراً، وَ كَفی بِالْكِتابِ حَجیجاً وَ خَصیماً.

Basi, Pepo inatosha kuwa ni thawabu na malipo, na Moto unatosha kuwa ni adhabu na mateso. Na yatosha Mwenyezi Mungu kuwa ndiye mlipaji wa kisasi na msaidizi, na Qur'ani inatosha kuwa  ni hoja na mpinzani Siku ya Kiyama.

اُوصیكُمْ بِتَقْوَی اللهِ الَّذی اَعْذَرَ بِما اَنْذَرَ، وَ احْتَجَّ بِما نَهَجَ، وَ حَذَّرَكُمْ عَدُواًّ نَفَذَ فِی الصُّدُورِ خَفِیاً، وَ نَفَثَ فِی الْاذانِ نَجِیاً، فَاَضَلَّ وَ اَرْدی، وَ وَعَدَ فَمَنّی، وَ زَینَ سَیئاتِ الْجَرائِمِ، وَ هَوَّنَ مُوبِقاتِ الْعَظائِمِ،

Ninakuusieni kumcha Mwenye Ezi Mungu, ambaye amekupeni onyo (la wazi lisilo kubali udhuru wa aina yoyote), na akajenga hoja kamilifu mbele yenu kwa njia ya uwazi. Amekuonyeni dhidi ya adui anayeingia kwa siri vifuani (mwenu), akinong'ona kwa uficho masikioni (mwenu), hatimae humtenga mja kutoka kwenye njia sahihi na kumpeleka kwenye machafu. Adui huyo huwahidi (waja kwa hadaa) mambo ya kupoteza na kumuingiza mtu kwenye tamaa zisizofaa, huku akizipamba dhambi na kuzipa sura ya kuvutia, na akadogosha madhambi kubwa kuangamizazo (ili yaonekane nyepesi).

حَتّی اِذَا اسْتَدْرَجَ قَرینَتَهُ، وَ اسْتَغْلَقَ رَهینَتَهُ، اَنْكَرَ ما زَینَ، وَ اسْتَعْظَمَ ماهَوَّنَ، وَ حَذَّرَ ما اَمَّنَ.

Humdangaya pole pole yule aliye karibu yake (rafiki yake), hadi amfanye kuwa ni atamteka na mtumwa (mfwasi) wake, kisha huyakanya yale aliyopambia, na kuyakuza yale aliyoyadogosha, na atawatishia kwa kile alichodai kuwa ni chenye amani kwao.

اَمْ هذَا الَّذی اَنْشَأَهُ فی ظُلُماتِ الْارْحامِ، وَ شُغُفِ الْاسْتارِ: نُطْفَةً دِهاقاً، وَ عَلَقَةً مُحاقاً، وَ جَنیناً وَ راضِعاً، وَ وَلیداً وَ یافِعاً.

Katika sehemu nyingine ya khutba, Imam anasema kuhusu uumbaji wa binadamu:

Huyu ndiye mwanadamu ambaye Mungu alimuumba katika viza vya tumbo la mamaye, akiwa ndani ya gamba la hifadhi: akiwa tone la mbegu lenye kutoja, na damu iliyojikusanya bila kuwa na umbo maalumu, kiumbe kilichozaliwa kutoka tumboni, akiwa katika umbila la mtoto anyonyaye, kisha akawa mtoto mdogo mwenye nguvu kamili, kisha akawa kijana.

ثُمَّ مَنَحَهُ قَلْباً حافِظاً، وَ لِساناً لافِظاً، وَ بَصَراً لاحِظاً، لِیفْهَمَ مُعْتَبِراً، وَ یقْصِرَ مُزْدَجِراً.

Kisha akampa moyo wenye kuhifadhi, na ulimi wa kusema, na macho yenye kuangaza (kuona), ili aelewe kwa kutafakari, na ajizue (ajilinde na dhambi) hali akiwa ni mwenye kuwaidhika (kukatazika).

حَتّی اِذا قامَ اعْتِدالُهُ، وَ اسْتَوی مِثالُهُ، نَفَرَ مُسْتَكْبِراً، وَخَبَطَ سادِراً، ماتِحاً فی غَرْبِ هَواهُ، كادِحاً سَعْیاً لِدُنْیاهُ، فی لَذّاتِ طَرَبِهِ، وَ بَدَواتِ اَرَبِهِ، لایحْتَسِبُ رَزِیةً، وَلایخْشَعُ تَقِیةً،

Ila baada ya kupata ukamilifu wa kimaumbila na kusimama imara, mwanadamu hutoka kwenye njia ya haki kwa majivuno na kiburi. Kawa mshupavu wa kupotoka, na hatimae akapotea, akachota ayachotayo kupitia ndoo ya matamanio yake. Alijitahidi kwa bidi kubwa kufikia malengo ya kidunia, akaingia katika kila aina ya starehe na furaha, akafanya chochote kile kilichomvutia bila ya kujali athari zake. Hakuwahi kufikiria kuwa anaweza kukumbwa na janga au kupinduliwa, na wala hakujizuia na dhambi yoyote.         

فَماتَ فی فِتْنَتِهِ غَریراً، وَ عاشَ فی هَفْوَتِهِ یسیراً، لَمْ یفِدْ عِوَضاً، وَلَمْ یقْضِ مُفْتَرَضاً.

Hivyo aliumaliza umri wake katika hali ya kughafilika na kufitiniuka (na fitina za dunia), na akaishi maisha yake mafupi akiwa katika dimbi la dhambi. Hakujinufaisha na neema za Mungu alizobarikiwa nazo, wala hakuekeleza wajibu aliyopewa.

دَهِمَتْهُ فَجَعاتُ الْمَنِیةِ فی غُبَّرِ جِماحِهِ، وَ سَنَنِ مِراحِهِ، فَظَلَّ سادِراً، وَ باتَ ساهِراً، فی غَمَراتِ الْالامِ، وَ طَوارِقِ الْاوْجاعِ وَالْاسْقامِ، بَینَ اَخ شَقیق، وَ والِد شَفیق، وَ داعِیة بِالْوَیلِ جَزَعاً، وَلادِمَة لِلصَّدْرِ قَلَقاً،

Ghafla akahujumiwa na machungu ya mauti huku akiwa mwishoni mwa safari ya uasi wake na matamanio na raha za dunia. Akabaki katika hali ya mshangao na kuchanganyikiwa, akisubiri usiku kucha hadi asubuhi bila kulala, akiwa na maumivu makali na magonjwa tofauti yaliokithiri zaidi wakati wa usiku. Wakati huo, alikuwa amezungukwa na ndugu mwenye msiba na baba mwenye upendo, mkewe alia kwa machungu, na binti akipigaye kifua chake kwa huzuni.

وَالْمَرْءُ فی سَكْرَة مُلْهِیة، وَ غَمْرَة كارِثَة، وَ اَنَّة مُوجِعَة، وَ جَذْبَة مُكْرِبَة، وَ سَوْقَة مُتْعِبَة.

Hayo hutokea huku mtu huyo akiwa katika hali ya ulevi wa mauti (sakaratu al-maut) unaomvuruga, akielea katika wimbi la janga linalomkumba. Analia kwa uchungu, akivutwa kwa mvuto (mauti) wenye maumivu makali na msukumo uchoshao.

ثُمَّ اُدْرِجَ فی اَكْفانِهِ مُبْلِساً، وَ جُذِبَ مُنْقاداً سَلِساً،

Kisha huwekwa kwenye sanda yake, akiwa katika hali ngumu ya kukata tamaa, anasafirishwa kuelekea kaburi kwake bila ya kuwa na hali yoyote ile kujitetea.

ثُمَّ اُلْقِی عَلَی الْاعْوادِ، رَجیعَ وَصَب وَ نِضْوَ سَقَم، تَحْمِلُهُ حَفَدَةُ الْوِلْدانِ وَ حَشَدَةُ الْاخْوانِ، اِلی‌دار غُرْبَتِهِ، وَ مُنْقَطَعِ زَوْرَتِهِ.

Kisha, huwekwa kwenye jeneza, akiwa amepweteka kama ngamia aliye konda na aliye jaa uchovu kutokana na shida za safari, huku akibebwa na watoto wa wanawe (wajukuu zake) na gurupu na ndugu mbali mbali, kuelekea nyumba ya ugenini kwake, na mahali ambapo familia yake haitamtembelea tena (haitakuwa pamoja naye tena).

حَتّی اِذَا انْصَرَفَ الْمُشَیعُ، وَ رَجَعَ الْمُتَفَجِّعُ، اُقْعِدَ فی حُفْرَتِهِ نَجِیاً لِبَهْتَةِ السُّؤالِ وَ عَثْرَةِ الْامْتِحانِ.

Hadi pale watakapo tawanyika washinikiza, na wanaoomboleza kurudi majumbani mwao, huinuliwa na kuwekwa kitako kaburini humo, akiwa peke yake, akipigwa maswali yenye yashangazayo na kukabiliwa na changamoto za majaribio.

وَ اَعْظَمُ ما هُنالِكَ بَلِیةً نُزُولُ الْحَمیمِ، وَ تَصْلِیةُ الْجَحیمِ، وَ فَوْراتُ السَّعیرِ، وَ سَوْراتُ الزَّفیرِ.

Na kadhia kubwa zaidi itakayo mkabili katika sehemu hiyo, ni balaa ya kutumbukia katika maji ya moto, na kuingizwa katika moto wa Jahannam, na kuonjwa na miale ya moto wa Jahannam, na mgurumo mkali wa moto huo.

لا فَتْرَةٌ مُریحَةٌ، وَ لادَعَةٌ مُزیحَةٌ، وَ لاقُوَّةٌ حاجِزَةٌ، وَ لامَوْتَةٌ ناجِزَةٌ، وَ لاسِنَةٌ مُسْلِیةٌ، بَینَ اَطْوارِ الْمَوْتاتِ، وَ عَذابِ السّاعاتِ.

Katika adhabu hiyo, hatapata utulivu wala mapumziko ya kumpumzisha, wala hakuna faraja ya kuondokewa na shida, hakuna kizuizi cha kuepusha maumivu, wala hakuna kifo kinachoweza kumkomboa (ili aepukana na adhabu), na hakuna lepe la usingizi la kumpunguzia huzuni yake. Atabaki katikati ya aina mbalimbali za mauti na adhabu zinazoendelea.

اِنّا بِاللهِ عائِذُونَ. عِبادَ اللهِ! اَینَ الَّذینَ عُمِّرُوا فَنَعِمُوا، وَ عُلِّمُوا فَفَهِمُوا، وَ اُنْظِرُوا فَلَهَوْا، وَ سُلِّمُوا فَنَسُوا؟ اُمْهِلُوا طَویلاً، وَ مُنِحُوا جَمیلاً، وَ حُذِّرُوا اَلیماً، وَ وُعِدُوا جَسیماً؟!

Hakika sisi tunamwomba Mwenye Ezi Mungu atulinde kutokana na maafa haya. Enyi waja wa Mungu! Wako wapi wale ambao Mwenye Ezi Mungu aliwapa uhai na kuwaneemesha kwa neema zake, waliopata elimu na wakawa na welewa wa kuujua ukweli, waliopewa muda wa kutosha, lakini wakabaki katika hali ya kughafilika? Waliojaliwa afya na ustawi, lakini wakaipuuza neema hiyo. Walikuwa na wakati wa kutosha, wakapewa kheri, wakaonywa juu ya adhabu, na wakaahidiwa malipo makubwa ya thawabu!

اِحْذَرُوا الذُّنُوبَ الْمُوَرِّطَةَ، وَالْعُیوبَ الْمُسْخِطَةَ. اُولِی الْابْصارِ وَ الْاسْماعِ، وَالْعافِیةِ وَالْمَتاعِ! هَلْ مِنْ مَناصٍ اَوْخَلاصٍ؟ اَوْ مَعاذٍ اَوْ مَلاذٍ؟ اَوْ فِرار اَوْ مَحار اَمْ لا؟

Jihadharini na dhambi ziingizazo kwenye matatizo, na aibu zinazomchukiza Mwenye Ezi Mungu. Enyi mlio na uwezo wa kuona (haki) na kusikia (ukweli), mliojaaliwa afya na mali! Je, kuna mahali pa kutorokea au njia yoyote ya kukimbia (mahakama ya Mungu)? Je, kuna pa kujikinga au mahali pa kujificha dhidi ya hasira ya Mwenye Ezi Mungu? Je, kweli mnaweza kuepuka athari za matendo mabaya au kukwepa wajibu wenu, au hamuwezi?

فَاَنّی تُؤْفَكُونَ؟ اَمْ اَینَ تُصْرَفُونَ؟ اَمْ بِماذا تَغْتَرُّونَ، وَ اِنَّما حَظُّ اَحَدِكُمْ مِنَ الْارْضِ ذاتِ الطُّولِ وَ الْعَرْضِ قیدُ قَدِّهِ، مُتَعَفِّراً عَلی خَدِّهِ.

Basi, mnadanganyika na kitu gani? Mnapelekwa wapi? Ni nini hasa kinachokupumbazeni, haki yenu katika rdhi hii ni sehemu ndogo mno, haizidi zaidi ya urefu na upana wa miili yenu, atalala humo huku uso wake ukiwa umelala mavumbini.

اَلْانَ عِبادَ اللهِ، وَ الْخِناقُ مُهْمَلٌ، وَالرُّوحُ مُرْسَلٌ فی فَینَةِ الْارْشادِ، وَ راحَةِ الْاجْسادِ، وَ باحَةِ الْاحْتِشادِ، وَ مَهَلِ الْبَقِیةِ، وَ اُنُفِ الْمَشِیةِ، وَ اِنْظارِ التَّوْبَةِ، وَ انْفِساحِ الْحَوْبَةِ، قَبْلَ الضَّنْكِ وَالْمَضیقِ، وَ الرَّوْعِ وَ الزُّهُوقِ، وَ قَبْلَ قُدُومِ الْغائِبِ الْمُنْتَظَرِ، وَ اَخْذَةِ الْعَزیزِ الْمُقْتَدِرِ.

Enyi waja wa Mungu, hu ndiyo wakati wa kuchukua hatua kabla kamba ya mauti haijakufikieni, wakati ambao roho zenu zipo huru katika kuufikia uongofu, na miili yenu upo salama, na nafasi ya kutenda matendo mema ni pana. Muda wa uhai, hiari, na uwezo wa kufanya maamuzi bado viko mikononi mwenu, na milango ya toba na kurejea kwa Mwenye Ezi Mungu iko wazi. Hii ni fursa kwenu, itumieni kabla ya wakati kuwa finyu, na kungia kwenye kaburi lenye dhiki, na kukabiliwa na hofu ya kuangamia, na kifo kuondoa roho zenu kutoka katika miili yenu. Chukueni hatua kabla ya kuja kwa mjumbe wa mauti, ambaye huja bila kuchelewa, basi itumieni fursa yenu kabla ya kufikwa na adhabu ya Mwenye Ezi Mungu Muweza.

Imesimuliwa kuwa, wakati Amir al-Mu’minin Ali (a.s) alipotoa khutba hii, miili ilitetemeka, machozi yakatiririka, na mioyo ikajawa na hofu na mshtuko kutokana na uzito wa maneno yake.

Rejea

Vyanzo