Nenda kwa yaliyomo

Haw'ab

Kutoka wikishia
Njia ya harakati ya jeshi la Imam Ali (a.s) na njia ya harakati ya As-hab al-Jamal.

Haw'ab (Kiarabu: الحَوْأب) lilikuwa ni dimbwi na shimo la maji karibu na Basra kwenye njia ya kuelekea Makka [1], ambalo wanajeshi wa Vita vya Jamal walipitia hapo. Dimbwi hili lilikuwa la binti ya Kalb bin Wabara, mkuu wa kabila la Banu Kalb bin Wabara. [2] Kwa mujibu wa Ibn Qutaiba Dinawari, mmoja wa wanahistoria wa karne ya 3 Hijria, Mtume (s.a.w.w) alimshauri mke wake Aisha kukaa mbali na Haw'ab na tukio lake (Vita vya Jamal). Mtume (s.a.w.w) amesema:

«Siku itafika ambapo mbwa wa Haw'ab watakuja kumbwekea mmoja wenu, na hiyo itakuwa siku ambapo atakuwa kwenye upotovu wa wazi.’ Kisha akamgeukia Aisha na kusema: Humayra (Aisha) angalia usije ukawa wewe ndiye mke yule». [3]

Kwa mujibu wa Ahmad bin Hanbal, kiongozi wa madhehebu ya Hanbali ni kuwa, katika tukio la Vita vya Jamal na kuondoka kwa kundi la Nakithina kutoka Basra kwenda kupigana na Imam Ali (a.s), Aisha kila alipokuwa akifika sehemu njiani, alikuwa akiuliza jina la mahali hapo, mpaka wakayafikia maji ya Haw'ab na mbwa huko wakabweka. Alipojua jina la mahali hapo, aliamua kujitenga na jeshi ili arejee[4]; hata hivyo Abdallah bin Zubeir alikusanya watu 50 ambao walitoa ushahidi kwa kuapa kwamba, eneo hilo sio Haw'ab. [5] Kwa mbinu hiyo wakafanikiwa kubadilisha uamuzi wa Bibi Aisha. [6]

Rejea

Vyanzo