Mpaka wa ruhusa ya sala ya safari

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Hadd al-Tarakhkhus)

Hadd al-Tarakhkhus / mpaka wa ruhusa ya kisheria (Kiarabu: حَدِّ تَرَخُّص) ni masafa ambayo msafiri akiyakata anapaswa kuanzia hapo na kuendelea asali Sala zake za rakaa nne kwa kuzipunguza na kuzisali kwa sura ya rakaa mbili kama ambavyo anaweza kufungua kama yuko katika Swaumu. Kwa mujibu wa hadithi, eneo hili ni mahali ambapo sauti ya adhana ya mji haisikiki na wala kuta zake hazionekani.


Tofauti ya masafa na Hadd al-Tarakhkhus

Moja ya masharti ya kusali Sala kwa kupunguza safarini ni msafiri kuwa na nia ya kutoka katika makazi yake na kwenda na kurejea kwa uchache kuwe na umbali wa farsakh za kisheria nane (baina ya kilomita 40-45). Umbali huu wa farsakh nane unatambulika kwa jina la masafa ya kisheria. [1]

Msafiri anapaswa kusali Sala yake wa kupunguza (kusali rakaa mbili Sala ambayo asili yake ni rakaa nne) na kufungua Saumu yake pale atakapokuwa amekata masafa maalumu ya safari yake. Kiwango hiki cha masafa maalumu kinatambulisha kwa jina la Hadd al-Tarakhkhus (mpaka wa ruhusa ya kisheria). Hukumu hii ina kigezo kilele cha mtu anapowasili katika mji wake au anapowasili katika mahali ambapo amekusudia kubakia hapo kwa muda wa siku kumi. [2]


Kiwango cha Hadd al-Tarakhkhus

Kwa mujibu wa hadithi za Maimamu wa Waislamu wa Kishia, hadd tarakhkhuss (mpaka wa ruhusa ya kisheria) ni mahali ambapo adhana ya mji au kijiji haisikiki na kuta zake hazionekani. [3] Mafakihi wa Kishia wametofautiana kuhusiana na kwamba, je masharti yote mawili yanapaswa kutimia au kutimia sharti moja kunatosheleza. [4] Katika baadhi ya barabara kuu za Iran kuna mabango yaliyowekwa ambayo yanaonyesha mpaka wa ruhusa ya kisheria ya miji (hadd tarakhkhus). [5]

Kigezo cha mafakihi cha kuonekana au kutoonekana kuta na majengo ya kawaida ni katika ardhi tambarare. Kuanzia zama ambazo kumeanzishwa miji mikubwa na adhana inarushwa hewani kupitia vipaza sauti, suala la kuainisha mpaka wa ruhusa ya kisheria limekuwa mushkili na tatizo. Baadhi ya mafakihi wanaamini kuwa, katika miji mikubwa kigezo cha hadd al-tarakhkhus ni kuta za mwisho za eneo (kitongoji) na sio kuta za mji. [6]


Hukumu

  • Kwa mujibu wa fat’wa ya wanazuoni na mafakihi wengi wa Kishia, kama mwenye kufunga Saumu atafungua Saumu yake mwanzo wa safari na kabla ya kufika katika mpaka wa ruhusa ya kisheria (had tarakhkhus), anapaswa kulipa Swaumu ya siku hiyo na vilevile kutoa Kafara. [7]
  • Kwa mujibu wa fat’wa ya baadhi ya Marajii Taqlid, kutoka msafiri katika had tarakhkhus ya mahali ambapo amekusudia kukaa siku kumi, kunapelekea kuswali kwa kupunguza kwa Sala ambazo ni za rakaa nne. Hata hivyo baadhi yao wanasema kuwa, kutoka katika eneo hilo kwa muda wa saa moja au masaa mawili kwa siku au saa kadhaa katika kipindi cha siku kumi inaruhusiwa, huku wengine wakiachia suala la kuainisha kiwango hicho kwa ada na mazoea. [8]

Vyanzo

  • Hāshimī Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd. Farhang-i Fiqh muṭābiq-i madhhab-i Ahl al-Bayt. Qom: Muʾassisa-yi Dāʾirat al-Maʿārif-i Fiqh-i Islāmī, 1390 Sh.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Wasāʾil al-Shīʿa. Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1416 AH.
  • Ṭabāṭabāʾī Yazdī, Muḥammad Kāẓim. Al-ʿUrwa al-wuthqā. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1420 AH.