Dua ya thelathini ya Sahifa Sajjadiya
Dua ya thelathini ya Sahifa Sajjadiya: ni moja wapo ya dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (Amani iwe juu yake). Kaitka dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anaomba msaada kutoka kwa Mungu ili, apate uwezo wa kulipa deni na kuhifadhi heshima yake. Kupitia dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anajadili athari za umaskini na utajiri katika maisha ya binadamu, huku akiomba hifadhi ya kuepukana na kutokana na ubadhirifu kutoka kwa Mola. Kuwa na roho ya ukarimu na kusikamana na njia ya wastani, kupenda kukaa na maskini na kuepukana na kiburi na majivuna, ni miongoni mwa maombi mengine ya Imamu (a.s) aliyoyaomba kutoka kwa Mola wake, katika dua hii ya thelathini ya Sahifa Sajjadiyya. Dua ya thelathini ni miongoni mwa dua zilizofafanuliwa kupitia tafsiri chambuzi mbali mba za Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa vitabu vya tafsiri viilivyochambua dua hii pamoja na dua nyengi za Sahifa Sajjadiyya, ni pamoja na kitabu; Diyare Ashiqan kiilichoandikwa na Hussein Ansarian, pamoja na Shuhud wa Shenakht kiilichoandikwa na Hassan Mamduhi Kermanshahi. Pia kuna tafsiri chambuzi kadhaa za lugha ya Kiarabu zenye uchambuzi wa dua hii ndani yake, miongoni mwazo ni kitabu kiitwacho Riadhu al-Salikina kazi ya Sayyid Ali Khan Madani. Mafunzo Yaliomo Ndani ya Dua ya Thalathini Mada za msingi ya dua ya thelathini ya Sahifa Sajjadiya, ni kuomba msaada kutoka kwa Mungu ili kulipa na kuepukana na matatizo ya deni. Imamu Sajjad (a.s) katika dua hii, anajadili athari za umaskini na utajiri katika maisha ya binadamu, na anamuomba Mola wake amruzuku riziki za kutosha ili kufikia hadhi ya kuwa karibu na Moala wake, pamoja kupata uweza wa kutoa sadaka kupitia riziki hizo. [1] Mafundisho ya dua hii yamekuja katika miktadha: • Kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu, kwa ajili ya kuhifadha hema na kutafuta utulivu wa kiakili na kimawazo kutokana madeni. • Athari hasi za madeni katika akili na mawazo ya binadamu. • Kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu, ili kupata hfadhi dhidi ya udhalilishaji wa madeni katika maisha ya kidunia na matatizo yake baada ya kifo. • Maombi ya kuomba uwokozi wa kuokolewa na shida za madeni na kupata wasaa mali na rizki toshelezi. • Kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu, ili kupata ulinzi dhidi ya israfu na upindukiani wa mipaka. • Maombi ya kuomba moyo mkunjufu wenye sifa ya ukarimu na kushika njia ya wastani katika masuala mabi mbali. • Maombi ya kumuomba Mungu uwezo wa kupataji kipato halali. • Kutafuta hifadhi ya Mwenye Ezi Mungu dhidi ya ghururi, jeuri, na majisifu yanayochochewa na umiliki wa rasilimali nyingi. • Dua ya kuomba majaaliwa ya kuwa na utashi wa kuandamana na mafukara na kuwa na ustahimilivu katika mwingiliano wa kijamii nao. • Kuomba thawabu za maisha ya baadaye kama ni fidia ya dhiki za ulimwengu wa hivi sasa. • Kukiri fadhila, ukarimu mkuu, na utukufu usio na kifani alionao Mwenye Ezi Mungu. • Utumiaji wa rasilimali kama nyenzo ya kupata ukaribu wa kiroho mbele ya Mwenye Ezi Mungu. Tafsiri Chambuzi za Dua ya Thalathini Kuna vitabu kadhaa vyenye tafsiri chambuzi ya Dua ya thelathini, vilivyoambatanisha tafsiri ya dua hiyo pamoja na dua nyengine mbalimbali zilizomo ndani ya kitabu Sahifa Sajjadiyya. Mingoni mwa vikitabu hivyo ni kitabu kiitwacho Diare Ashiqan, kazi ya Hussein Ansarian, [3] Shuhud wa Shenakht, kazi ya Mohammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi, [4] pamoja na Sharh wa Tarjome Sahifa Sajjadiyya kazi iliyofanya na Syed Ahmad Fahri. [5] Vitabu hivi vimechambua na kufafanua dua za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya kwa lugha ya Kiajemi ili kutoa ufahamu wa kina kwa wazungumzaji wa lugha hiyo. Aidha, kuna waandishi kadhaa walioshughulikia kazi ya uchambuzi wa dua ya thelathini pamoja na dua nyengine za Sahifa Sajjadiya kwa lugha ya Kiarabu. Miongoni mwa kazi chambzi zilizoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, ni pamoja na; Riadhu al-Salikin, kazi ya Sayyid Ali Khan Madani, [6] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya kazi ya Mohammad Jawad Mughniyya, [7] Riadhu al-Arifina kazi ya Mohammad bin Mohammad Darabi [8], na Afaqi al-Ruh kazi ya Sayyid Mohammad Hussein Fadhlullah. [9] Kazi zote zimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu ili kuimarisha uelewa wa safi wa kimantiki na kiisimu wa dua hizo. Pia maneno maalum ya dua hii yamechambuliwa na kufafanuliwa kisarufi na kiisimu, ili kurahisisha welewa wa dua za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vinavyohusika na kazi hiyo ni pamoja na; Ta'liqati ala al-Sahifa al-Sajjadiyya kilichoandikwa na Faidhu Kashani [10] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya kazi ya Izzu al-Din Jazayiri. [11]
Matini ya Kiarabu Pamoja na Maelezo Yake kwa Kiswahili وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الْمَعُونَةِ عَلَي قَضَاءِ الدَّيْنِ
Na moja kati ya dua zake, amani iwe juu yake, ni ile dua yake katika kutafuta msaada wa kulipa deni yake kutoka kwa Mola wake. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ هَبْ لِيَ الْعَافِيَةَ مِنْ دَيْنٍ تُخْلِقُ بِهِ وَجْهِي، وَ يَحَارُ فِيهِ ذِهْنِي، وَ يَتَشَعَّبُ لَهُ فِكْرِي، وَ يَطُولُ بِمُمَارَسَتِهِ شُغْلِي Ewe Mwenye Ezi Mungo! Mteremshie rehema Zako Muhammad na Aali zake, na unijaalie nafuu dhidi ya deni linaloporomosha hadhi ya sura yangu, na (uniepushe na deni) linalosababisha mchafuko katika fikra zangu, na (uniepushe na deni) linalozalisha mtiririko wa mawazo yangu kwa ajili yake, na ambalo kushughulisha kunapelekea kurefuka kwa mchakato wa majukumu yangu. وَ أَعُوذُ بِكَ، يَا رَبِّ، مِنْ هَمِّ الدَّيْنِ وَ فِكْرِهِ، وَ شُغْلِ الدَّيْنِ وَ سَهَرِهِ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَعِذْنِي مِنْهُ، وَ أَسْتَجِيرُ بِكَ، يَا رَبِّ، مِنْ ذِلَّتِهِ فِي الْحَيَاةِ، وَ مِنْ تَبِعَتِهِ بَعْدَ الْوَفَاةِ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَجِرْني مِنْهُ بِوُسْعٍ فَاضِلٍ أَوْ كَفَافٍ وَاصِلٍ. Na ninatafuta hifadhi Kwako, Ee Mola Mlezi, dhidi ya adhabu (matatizo) ya deni athari za kisaikolojia na kiakili zinazosababisha na fikra deni hilo, na (ninatafuta hifadhi Kwako kutokana na) uzito wa majukumu ya deni na usumbufu wake unaonyima usingizi. Hivyo basi, Mteremshie rehema Zako Muhammad pamoja na Aali zake, na unikinge dhidi ya deni hilo. Na ninakuomba unilinde, Ee Mola Mlezi, dhidi ya athari yake yenye kudunisha hadhi katika maisha ya hapa duniani, na dhidi ya mwendelezo wa madhila yake baada ya kufariki. Hivyo basi, Mteremshie rehema Zako Muhammad na Aazi zake, na uniepushe nalo kupitia wasaa wa fadhila au kipato toshelezi (kinachokidhi mahitaji yangu). اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ احْجُبْنِي عَنِ السَّرَفِ وَ الِازْدِيَادِ، وَ قَوِّمْنِي بِالْبَذْلِ وَ الِاقْتِصَادِ، وَ عَلِّمْنِي حُسْنَ التَّقْدِيرِ، وَ اقْبِضْنِي بِلُطْفِكَ عَنِ التَّبْذِيرِ، وَ أَجْرِ مِنْ أَسْبَابِ الْحَلَالِ أَرْزَاقِي، وَ وَجِّهْ فِي أَبْوَابِ الْبِرِّ إِنْفَاقِي، وَ ازْوِ عَنِّي مِنَ الْمَالِ مَا يُحْدِثُ لِي مَخِيلَةً أَوْ تَاَدِّياً اِلَي بَغْيٍ أَوْ مَا أتَعَقَّبُ مِنْهُ طُغْيَاناً. Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu Muhammad na Aali zake, na unikinge na ubadhirifu na upidukiaji mipaka katika utashi wa kidunia. Uninyooshe kupitia nyenzo ya ukarimu na utoaji wa wastani (matumizi ya wastani), na unifundishe namna ya kukadiria. Unizuie kwa upole wako kutokana na ufujaji, na uzipitishe riziki zangu katika njia za halali. Uelekeze matumizi yangu katika milango ya kheri na ukarimu wa kutoa sadaka, na uniepushe na mali itakayoniletea majivuno, au kunipeleka kwenye ujeuri, au ambayo itanifanya nikiuke mipaka na kuingia kweye dhulma, au itakayonifanya kubaki nyuma kiuadui. اللَّهُمَّ حَبِّبْ إِلَيَّ صُحْبَةَ الْفُقَرَاءِ، وَ أَعِنِّي عَلَى صُحْبَتِهِمْ بِحُسْنِ الصَّبْرِ Ewe Mola wangu! Ujaalie moyo wangu uwe na mapenzi ya kusuhubiana na mafukara, na unisaidie kuwa na subira katika usuhuba wangu huo. وَ مَا زَوَيْتَ عَنِّي مِنْ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْفَانِيَةِ فَاذْخَرْهُ لِي فِي خَزَائِنِكَ الْبَاقِيَةِ Na chchote kile ulichoniondolea miongoni mwa mapambo ya dunia hii ipitayo, kifanyie kuwa ni akiba kwangu katika hazina Zako za Akhera zisizo na kikomo. وَ اجْعَلْ مَا خَوَّلْتَنِي مِنْ حُطَامِهَا، وَ عَجَّلْتَ لِي مِنْ مَتَاعِهَا بُلْغَةً إِلَى جِوَارِكَ وَ وُصْلَةً إِلَى قُرْبِكَ وَ ذَرِيعَةً إِلَى جَنَّتِكَ، إِنَّكَ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ، وَ أَنْتَ الْجَوَادُ الْكَرِيمُ. Na yajaalie (Ewe Mola), yale uliyoniruzuku miongoni mwa mapambo yake yapitayo, na neema zake ulizoniharakishia, yawe ni njia ya kunifikisha karibu Nawe, na ni nyenzi ya kujikurubisha Kwako, na sababu ya kuingia Peponi Mwako. Hakika Wewe ni Mwenye fadhila adhimu, nawe ndiye Mwingi wa kutoa na Mkarimu.