Dua ya ishirini na tisa ya Sahifa Sajjadiyya
![]() Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH. | |
Mtoaji / Mwandishi | Imamu Sajjad (a.s) |
---|---|
Lugha | Kiarabu |
Msimulizi / Mpokezi | Mutawakkil ibn Harun |
Mada | Maombi wakati wa shida na mahitaji ya riziki |
Chanzo | Sahifa Sajjadiyah |
Tafsiri kwa Lugha ya | Kifarsi |
Dua ya Ishirini na Tisa ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء التاسع والعشرون من الصحيفة السجادية), ni miongoni mwa dua iliyopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Kikawaida dua hii husomwa wakati wa ugumu wa maisha, ambapo mja humuelekea Mola wake wasaa wa riziki. -+Imamu Zain al-Abidin (a.s) katika dua hii, anatuelezea jinsi ya Mwenye Mungu anavyowatahini waja wake kwa mtihani shida ya kipato, jambo linalosababisha baadhi ya waja hao kuwa na dhana potofu kuhusiana ugawaji wa riziki. Aidha, dua hii inalaumu juhudi zisizo na kiasi katika utafutaji wa riziki, hukuku ikisisitiza kwamba; Njia pekee ya kukomesha mfadhaiko na wasiwasi wa nafsi, ni kujenga imani kamili juu ya ahadi ya Mwenye Ezi Mungu alioitoa kwa wanadamu kuhusiana na udhamini wa rizki maishani mwao.
Dua ya ishirini na tisa imechambuliwa kwa kina katika vitabu vya tafsiri chambuzi za maandiko ya Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa tafsiri zilizoandikwa kwa lugha ya Kifarsi, ni Shuhud wa Shinakht, kilichoandikwa na Hassan Mamduhi Kermanshahi, pamoja na Riyadhu as-Salikin, kazi iliyofanya na Sayyid Ali Khan Madani kwa lugha ya Kiarabu.
Mafunzo ya Kielimu ya Dua ya Ishirini na Tisa
Mhimili mkuu wa dua ya ishirini na tisa ya Sahifa Sajjadiyya, unahusiana na aina ya ombi linaloombwa wakati wa dhiki ya kiuchumi. Kwa mujibu wa maelezo ya Mamduhi Kermanshahi, katika dua hii Imamu Sajjad (a.s) anatufunza kwa kutufafanulia dhana ya upweke na umoja kamili wa Mwenye Ezi Mungu (Tauhidi) katika muktadha wa utoaji uruzuku.[1] Misingi ya kielimu ya dua hii imegawanywa katika vipengele vikuu vitano[2] kama inavyofafanuliwa hapa chini:
- Uchunguzi wa majaribio wanayojaribiwa nayo mwanadamu kupitia matarajio yasiyo na ukomo pamoja na dhiki ya kipato.
- Chanzo cha mtazamo hasi dhidi ya mitihani na mashaka, matarajio yasiyo na kikomo, na athari zake.
- Kutamani kudokolea macho viumbe wenye uhai mrefu, ni kielelezo cha kutokuwa na dhana njema juu ya uruzuku wa Mwenye Ezi Mungu.
- Ugumu wa upataji wa riziki kama kigezo kinachoashiria kuwepo kwa ukosefu wa uhakika wa kiimani (yakini).
- Dhana ya uombaji, uyakinifu, na itikadi kamili juu ya Mwenye Ezi Mungu kama mbinu ya kujikomboa kutoka kwenye dhiki ya upataji riziki.
- Juhudi zisizo na tija katika harakati za kiuchumi.
- Kipato cha maishani mwenu pamoja na ahadi mlizopewa, vyote vipo mbinguni (kwa Mola wenu).
- Utokomeshaji wa mfadhaiko wa kiakili kuhusiana na riziki, hukamilika kupitia imani thabiti juu ya Mruzuku (Mwenye Ezi Mungu).
- Ahadi ya Mungu ya kuhakikisha uwasilishaji wa riziki zake kwa waja wake.[3]
Maelezo
Dua ya ishirini na tisa imeshereheshwa (imefafanuliwa) kwa lugha ya Kiajemi kupitia vitabu kadhaa vilivyoshughulikia uchambuzi wa dua za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa kazi zilizochambua na kufasiri dua hii, na pamoja na; Shahud wa Shenakht, kazi ya Mohammad-Hasan Mamduhi Kermanshahi,[4] na Sharhe wa Tarjomeh Sahife Sajjadiyye, kazi ya Sayyid Ahmad Fahri.[5] Aidha, kuna wanazuoni kadhaa walikuja kuifasiri na kufafanua dua hii kwa lugha ya Kiarabu.
Miongoni mwa kazi chambuzi zilizoandikwa kuhusiana na dua hii kwa lugha ya Kiarabu, ni pamoja na; Riyadhu al-Salikina, kitabu kilichandikwa na Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fi Dhiilali al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi ya Muhammad Jawad Mughniyya,[7] Riyadhu al-Arifina, utunzi wa Muhammad ibnu Muhammad Darabi[8] na Afaqi al-Ruh, kazi ya Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Vilevile, istilahi za dua hii zimekusanya na kuchambuliwa kupitia wanazuoni maalumu walioamua kujitolea katika utoaji wa huduma ya kielimu kwa jamii. Miongoni mwa kazi zilizofanya kuhusiana na jambo hili ni kama vile; Ta'aliqati Ala al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi andishi ya Faidhu Kashani,[10] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi ya Izzu al-Din Jaza'iri.[11]
Matn Kamili kwa Kiarabu Pamoja na Tafsiri ya Kiswahili
وَ کانَ مِنْ دُعَائِهِ علیهالسلام إِذَا قُتِّرَ عَلَیهِ الرِّزْقُ
اللَّهُمَّ إِنَّک ابْتَلَیتَنَا فِی أَرْزَاقِنَا بِسُوءِ الظَّنِّ، وَ فِی آجَالِنَا بِطُولِ الْأَمَلِ حَتَّی الْتَمَسْنَا أَرْزَاقَک مِنْ عِنْدِ الْمَرْزُوقِینَ، وَ طَمِعْنَا بِآمَالِنَا فِی أَعْمَارِ الْمُعَمَّرِینَ.
فَصَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ هَبْ لَنَا یقِیناً صَادِقاً تَکفِینَا بِهِ مِنْ مَئُونَةِ الطَّلَبِ، وَ أَلْهِمْنَا ثِقَةً خَالِصَةً تُعْفِینَا بِهَا مِنْ شِدَّةِ النَّصَبِ
وَ اجْعَلْ مَا صَرَّحْتَ بِهِ مِنْ عِدَتِک فِی وَحْیک، وَ أَتْبَعْتَهُ مِنْ قَسَمِک فِی کتَابِک، قَاطِعاً لِاهْتِمَامِنَا بِالرِّزْقِ الَّذِی تَکفَّلْتَ بِهِ، وَ حَسْماً لِلِاشْتِغَالِ بِمَا ضَمِنْتَ الْکفَایةَ لَهُ
فَقُلْتَ وَ قَوْلُک الْحَقُّ الْأَصْدَقُ، وَ أَقْسَمْتَ وَ قَسَمُک الْأَبَرُّ الْأَوْفَی: «وَ فِی السَّماءِ رِزْقُکمْ وَ ما تُوعَدُونَ».
ثُمَّ قُلْتَ «فَوَ رَبِّ السَّماءِ وَ الْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِثْلَ ما أَنَّکمْ تَنْطِقُونَ».
Na miongoni mwa maombi ya mtukufu Imamu (a.s) ilikuwa ni ile dua, aliyokuwa akiiomba pale alipokumbwa na upungufu au taabu ya kupata riziki kutoka kwa Mola wake. Dua hii imekuja katika mfumo wa ibara zisemazo:
Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika Wewe umetutahini kwa jaribio la kutokuwa na yakini juu ya rizki zetu, na hivyo tukawa na shaka na wahaka katika jambo hilo, na pia umetutahini matarajio yasiyo na kikomo katika (na kusahau ajali) maishali mwetu, jambo ambalo limetufanya tukatafuta rizki Yako kutoka kwa viumbe ambao wao wenyewe wanaruzukiwa (kama sisis), na kwa matarajio yetu hayo, tukatamani kufikia umri wa wale waliopewa maisha marefu (miongoni mwa waja Wako).
Hivyo basi, mteremshie Rehema (Zako) Muhammad na Aali zake, na utunukishe yakini ya kweli itakayotuepusha na mzigo wa jitihada (tabu) za kutafuta (rizki), na utumiminia (nafsini mwetu) itikadi kamilifu itakayotukinga na ukali wa (maumivu ya) mchoko.
Na uifanye ahadi Yako uliyoidhihirisha katika wahyi Wako, kisha ukaisisistiza kwa kuifuatanisha na kiapo Chako katika maandiko Yako, iwe ndio chanzo cha kututenganisha na mihangaiko yetu juu ya kutafuta riziki ambayo Unayowadhaminia waja Wako, na iwe ndiyo suluhu ya mwisho dhidi ya kujishughulisha na kile ambacho uliloliwekea dhamana ya kulitimiza.
Na umenena na kauli Yako ndiyo ya haki timamu na yenye kiwangu kamili cha ukweli, na umetulia kiapo, na kiapo chako ndicho chenye utekelezaji mwema na kamilifu zaidi. (Na yote yapo mbinguni; rizki zenu pamoja na yale mnayoahidiwa).
Kisha ukanena: "Hivyo, naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, kwamba uwepo wa riziki na yale mliyoahidiwa ni jambo la hakika, sawa na uhakika wa uwezo wenu wa kutamka.
Rejea
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 2, uk. 529.
- ↑ Tafsiri na maelezo ya dua ya ishirini na tisa ya Sahifa al-Sajjadiyah, Tovuti ya Erfan.
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 2, uk. 529-542.
- ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 4, uk. 529-542.
- ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1388 S, juz. 2, uk. 487-494.
- ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 4, uk. 311-337.
- ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 373-376.
- ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 381-387.
- ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 89-98.
- ↑ Faydh Kashani, Taqaqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 65-66.
- ↑ Jazairi, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 158-159.
Vyanzo
- Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
- Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
- Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
- Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
- Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
- Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
- Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
- Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
- Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.