Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Tano ya Sahifatu Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Tano ya Sahifatu Sajjadiyyah
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH.

Mtoaji / MwandishiImamu Sajjad (a.s)
LughaKiarabu
Msimulizi / MpokeziMutawakkil ibn Harun
MadaKujiombea nafsi yako, jamaa na marafiki na kuomba baraka na mwongozo
ChanzoSahifa Sajjadiyah
Tafsiri kwa Lugha yaKifarsi

Dua ya Tano ya Sahifatu Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الخامس من الصحيفة السجادية) ni dua maarufu iliyoripotiwa kutoka kwa Imamu Sajjadi (a.s), ambayo ndani yake Imamu Sajjad (a.s) anajiombea dua kwa ajili ya nafsi yake, familia yake, na marafiki zake ili wapate na uimara wa kusimama katika njia ya haki, na pia ameitumia dua hii katika kuomba neema, uongofu, ukuruba na Allah pamoja na amani. Miongoni mwa yale aliyoyaakisi Imamu Sajjadi (a.s) katika dua hii, ni mapoja na maajabu yasiyokuwa na mwisho katika uumbaji (Wake Allah Subhanahu Wata’ala), athari ya kuziegemea (na kutaraji) rehema za Allah, kutambua au kukiri neema za Allah, pamoja na utawala wa Mungu usio na kikomo wala kifani.

Dua hii ya tano inapatikana katika vitabu mbali mbali vya tafsiri ya Sahifatu Sajjadiyya kama vile; Diyaar Ashiqiin cha Hussein Ansarian kilicho andikwa kwa lugha ya Kifarsi na Riyaadhu as-Saalikin cha Sayyid Ali Khan Madani kilicho andikwa kwa lugha ya Kiarabu.

Maudhui

Muktadha mkuu wa dua ya tano ya Sahifatu Sajadiya, unaakisi maombi ya Imamu Sajjad katika kujiombea nafsi yake, familia, pamoja na marafiki zake, ili wapate uthabiti au uimara wa kusimama kidete katika njia sahihi ya kumtumikia Mwenye Ezi Mungu. Dua ambayo haikutumika katika kuomba mambo yanayohusiana masuala ya kiroho peke yake, pia ndani yake mna maombi ya kuomba neema, uongofu, na amani. Muktadha wa dua hii umekuja na vipengele vifuatavyo:

  • Maajabu ya uumbaji (wa Mungu) yasiyo na mwisho yanayo akisi ukuu au uadhimu wa Mwenye Ezi Mungu.
  • Utawala na ufalme wa Mwenye Ezi Mungu ni usio na mwisho.
  • Kuomba nusura na kuwa huru kutokana na udhalili wa dunia na adhabu ya Akhera.
  • Maombi ya kuomba rehema kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu, ambaye rehema Zake hazina mwisho wala kikomo.
  • Dua ya kuomba ukuruba wa Mwenye Ezi Mungu.
  • Kuomba heshima ya kibinadamu kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu Mtukufu.
  • Kuomba kupata hifadhi ya kutofedheheka mbele ya Mungu Mjuzi wa siri zilizofichika ndani ya nyoyo za kila mwanadamu.
  • Matokeo na hatima ya kuegemea kwenye rehema za Mungu: (kujitosheleza Naye, na kutokuwa na hofu ya kuachana na wengine).
  • Kutafuta hifadhi chini ya kivuli cha mipango ya Mungu dhidi ya hila za maadui na matukio ya zama mbali mbali.
  • Kuomba kinga dhidi ya shari na hila za Shetani.
  • Kuomba neema ya kupata ulinzi na uongofu kutoka kwa Mungu.
  • Kuomba amani na afya ya moyo, faraja ya mwili, na uwezo wa kuhimidi shukurani na kumdhikiri Mwenye Ezi Mungu.
  • Kutafuta msaada na uongofu kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu dhidi ya shari ya udhalilishaji na upotofu.
  • Kuomba hadhi na baraka kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu.
  • Kuutambua na kuukiri uadhimu wa Mungu na neema Zake.
  • Heshima na hadhi ya wale wanaoinua mikono yao na kumuomba Mwenye Ezi Mungu (ambao hakuna wanachokiona zaidi ya Mola wao).[1]

Tafsiri za Dua ya Tano

Tafsiri ya Dua ya Tano ya Sahifatu Sajadiya, inapatikana katika vitabu mbali mbali vya tafsiri ya kitabu Sahifatu Sijadiyya vilizoandikwa kwa lugha ya Kifarsi, ambapo vipengele vya dua hii vimefasiri na kupewa ufafazi wa kutosha kabisa vitabu humo. Miongoni mwa vitabu hivi ni; Diyaaru Ashiqaan cha Hussein Ansarian,[2] Shuhud wa Shina'akht cha Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi,[3] na Asraare Khamuushan cha Muhammad Taghi Khaleji.[4]

Aidha, kuna vitabu kadhaa vya tafsiri ya Kiarabu ya kitabu Sahifatu Sajjadiyya vilivyofasiri Dua hii ya Tano ya Sahifat Sijadiyya. Miongoni mwa tafsiri ya Kiarabu ya dua hii inapakana katika kitabu; Fi Dhilaal al-Sahifati al-Sijadiyya cha Muhammad Jawad Mughniyya,[5] Riyadh al-Aarifiin cha Muhammad bin Muhammad Darabi,[6] Afaq al-Ruh cha Sayyid Muhammad Hussein Fadlallah[7] na Riyadhu al-Salikin fi Sharhi Sahifati Sayyid al-Sajidiin cha Sayyid Ali Khan Madani.[8] Pia wake umechambuliwa na kufafanuliwa katika kitabu kiitwacho Ta'liiqat Ala al-Sahifa al-Sijadiyya cha Faidh Kashani.[9]

Matini Pamoja na Tafsiri Yake

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ لِنَفْسِهِ وَ لِأَهْلِ وَلَايَتِهِ

يَا مَنْ لَا تَنْقَضِي عَجَائِبُ عَظَمَتِهِ، صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ احْجُبْنَا عَنِ الْإِلْحَادِ فِي عَظَمَتِكَ

وَ يَا مَنْ لَا تَنْتَهِي مُدَّةُ مُلْكِهِ، صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَعْتِقْ رِقَابَنَا مِنْ نَقِمَتِكَ

وَ يَا مَنْ تَنْقَطِعُ دُونَ رُؤْيَتِهِ الْأَبْصَارُ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَدْنِنَا إِلَي قُرْبِكَ

وَ يَا مَنْ تَصْغُرُ عِنْدَ خَطَرِهِ الْأَخْطَارُ، صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ كَرِّمْنَا عَلَيْكَ.

وَ يَا مَنْ تَظْهَرُ عِنْدَهُ بَوَاطِنُ الْأَخْبَارِ، صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ لَا تَفْضَحْنَا لَدَيْكَ.

للَّهُمَّ أَغْنِنَا عَنْ هِبَةِ الْوَهَّابِينَ بِهِبَتِكَ، وَ اكْفِنَا وَحْشَةَ الْقَاطِعِينَ بِصِلَتِكَ حَتَّى لَا نَرْغَبَ إِلَى أَحَدٍ مَعَ بَذْلِكَ، وَ لَا نَسْتَوْحِشَ مِنْ أَحَدٍ مَعَ فَضْلِكَ.

اللَّهُمَّ فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ كِدْ لَنَا وَ لَا تَكِدْ عَلَيْنَا، وَ امْكُرْ لَنَا وَ لَا تَمْكُرْ بِنَا، وَ أَدِلْ لَنَا وَ لَا تُدِلْ مِنَّا.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ قِنَا مِنْكَ، وَ احْفَظْنَا بِكَ، وَ اهْدِنَا إِلَيْكَ، وَ لَا تُبَاعِدْنَا عَنْكَ إِنَّ مَنْ تَقِهِ يَسْلَمْ وَ مَنْ تَهْدِهِ يَعْلَمْ، وَ مَنْ تُقَرِّبْهُ اِلَيْكَ يَغْنَمْ.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اكْفِنَا حَدَّ نَوَائِبِ الزَّمَانِ، وَ شَرَّ مَصَايِدِ الشَّيْطَانِ، وَ مَرَارَةَ صَوْلَةِ السُّلْطَانِ.

اللَّهُمَّ إِنَّمَا يَكْتَفِي الْمُكْتَفُونَ بِفَضْلِ قُوَّتِكَ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اكْفِنَا، وَ إِنَّمَا يُعْطِي الْمُعْطُونَ مِنْ فَضْلِ جِدَتِكَ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَعْطِنَا، وَ إِنَّمَا يَهْتَدِي الْمُهْتَدُونَ بِنُورِ وَجْهِكَ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اهْدِنَا.

اللَّهُمَّ إِنَّكَ مَنْ وَالَيْتَ لَمْ يَضْرُرْهُ خِذْلَانُ الْخَاذِلِينَ، وَ مَنْ أَعْطَيْتَ لَمْ يَنْقُصْهُ مَنْعُ الْمَانِعِينَ، وَ مَنْ هَدَيْتَ لَمْ يُغْوِهِ إِضْلَالُ الْمُضِلِّينَ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ امْنَعْنَا بِعِزِّكَ مِنْ عِبَادِكَ، وَ أَغْنِنَا عَنْ غَيْرِكَ بِإِرْفَادِكَ، وَ اسْلُكْ بِنَا سَبِيلَ الْحَقِّ بِاِرْشَادِكَ.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْ سَلَامَةَ قُلُوبِنَا فِي ذِكْرِ عَظَمَتِكَ، وَ فَرَاغَ أَبْدَانِنَا فِي شُكْرِ نِعْمَتِكَ، وَ انْطِلَاقَ أَلْسِنَتِنَا فِي وَصْفِ مِنَّتِكَ.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْنَا مِنْ دُعَاتِكَ الدَّاعِينَ إِلَيْكَ، وَ هُدَاتِكَ الدَّالِّينَ عَلَيْكَ، وَ مِنْ خَاصَّتِكَ الْخَاصِّينَ لَدَيْكَ، يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ.

Na miongoni mwa dua zake (a.s), ilikuwa ni ile dua aliyokuwa akijiombea amani kwa ajili ya nafsi yake na waliokuwa chini ya taa yake.

(Katika dua hii alikuwa akiomba kwa kusema:) Ewe Yule (Mola) ambaye maajabu ya ukuu wake hayana mwisho! Mshushie rehema na amani Mtume Muhammad na Aali zake, na utulinde na hatari ya uasi mbele ya utukufu wako.

Na Ewe Yule ambaye utawala wake (hauna mwisho) hautakwisha, Mshushie rehema na baraka Zako Muhammad na Aali zake, na utuepushe (tutoe huru) kutokana maangamizi yako (hasira zako).

Na Ewe ambaye macho hukoma bila ya kukuona, mshushie rehema Zako Muhammad na aali zake, na utukurubishe katika ukaribu wako.

Na Ewe ambaye mambo yote mazito hudogoka mbele ya utukufu wake, mrehemu Muhammad na Aali zake, na utukirimu kwa ukarimu wako.

Na Ewe ambaye siri (na habari za ndani) hudhihirika mbele yako, msalie (mshushie rehema Zako) Muhammad na Aali zake, na usitufedheheshe mbele yako.

Ewe Mola! Kwa ukarimu na hisani yako, tutosheleze (ili tusihitaji ukarimu wala hisani kutoka kwa viumbe Wako). Na kwa hisani na jazaa yako, utukinge na dhiki na simanzi ya kunyimwa hisani za wengine. Hivyo, (kwa ukarimu na utoaji wako mkuu), tusielekeze raghba zetu kwa ukarimu na utoaji wa yeyote yule (mwengine isipokuwa wewe), na kwa fadhila na hisani zako, tusimhofu kiumbe chochote kile (zaidi Yako).

Ee Mungu! Mshushie rehema Muhammad pamoja na Aali zake. Na utufungulie njia yenye manufaa kwetu, wala usitufungulie njia ya hasara kwetu. Na Utupangie yenye manufaa kwetu, wala usitupangie yenye hasara yetu. Na Utupe ushindi dhidi ya wengine, wala usiwafanye wengine kuwa ni washindi dhidi yetu.

Ee Mola! Msalie Muhammad na Aali zake. Na utulinde na ghadhabu zako, na utuhifadhi kwa hifadhi Yako, na utuongoze (ili tuelekee) Kwako, wala usituweke mbali na uwepo Wako. Hakika husalimika yule Unayemhifadhi, na huelimika yule Unayemwongoza, na hunufaika yule Unayemweka karibu Yako.

Ewe Mola! Mrehema Muhammad na Aali zake. Na utuepushe na ukali wa misukosuko mibaya ya nyakati, na utulinde na shari za mawindo ya Shetani, na ukali wa ghadhabu za mtawala.

Ewe Mola! Hakika, waridhikao huridhika kwa hisani ya nguvu zako; basi Mrehemu Muhammad na Aali zake, na ututosheleze (kupitia nguvu za hisani zako). Bila shaka, wale watoao hutoa kwa hisani ya ukarimu wako; basi Mrehema Muhammad na Aali zake, na uturuzuku kwa hisani ya ukarimu wako. Na bila shaka, wale waongokao huongoka kwa nuru ya uso Wako; basi Mrehema Muhammad na Aali zake, na utuongoze (kwa nuru yauso yako mtukufu).

Ewe Mola! Bilas haka yeyote yule utakayemuunga mkono, hawezi kudhuriwa (wala kudhalilishwa) na udhalilishaji wa wadhalilishaji, na yeyote yule utakayemtunuku, hawezi kupungukiwa (kunyimika) kutokana na unyimaji wa wanyimaji; na yeyote yule utakayemuongoa, hawezi kupotoshwa na upotoshaji wa wapotoshaji. Basi (Ewe Mola wetu), Mrehema Muhammad na Aali zake, na utuepushe na uovu wa waja wako kwa utukufu wako, na tutosheleze kwa utoaji (ufadhili) Wako na isiyekuwa Wewe , na tuongoze kwenye njia ya haki kwa uongofu wako.

Ee Molo wetu! Mbariki Muhammad na kizazi chake (Aali zake). Na jaalia amani na utulivu wa mioyo yetu uwe katika kuutaja utukufu wako (katika kushikamana na utajo wa Utukufu Wako), na jaalia mapumziko ya miili yetu, iwe ni kupitia shukrani za neema zako, na (jaalia) wepesi (ufasaha) kwenye ndimi zetu katika kuuelezea ukarimu wako.

Ewe Mola wetu! Mbariki Nabii Muhammad pamoja na familia yake (Aali zake), na utujaalie tuwe miongoni mwa walinganiaji Wako wanaowaita (watu) na kuwataka waje kwako, na (tujaalie tuwe miongoni mwa) waongozaji wanaoelekeza (watu) upande wako, na (tujaalie tuwe miongoni mwa) miongoni mwa wateule Wako wa pekee; Ewe Mwenye huruma (Mrehemevu) zaidi kuliko (au kati ya) warehemevu wote.

🌞
🔄

Rejea

  1. Ansarian, Diyar Asheqan, 1372, juz. 3, uk. 347-565; Khalji, Asrar Khamooshan, 1385, uk. 299-536
  2. Ansarian, Diyar Asheqan, 1372, juz. 3, uk. 347-565
  3. Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 337-356.
  4. Khalji, Asrar Khamooshan, 1383 S, juz. 2, uk. 299-536.
  5. Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 107-118.
  6. Darabi, Riadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 97-103.
  7. Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 115-131.
  8. Madani Shirazi, Riadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 2, uk. 135-173.
  9. Faidh Kashani, Taaliqat Ala al-Sahaifa al-Sajadiyeh, 1407 AH, uk. 29-30.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.