Nenda kwa yaliyomo

Dhana ya “Labbaika ya Hussein”

Kutoka wikishia

Dhana ya “Labbaika ya Hussein”: Ni kauli-tamko ya kitamaduni katika madhehebu ya Kishia inayofanya kazi kama ni jibu la kiibada kwa ajili ya kuitikia mwito wa Imamu Hussein (a.s) aliyoutoa kwa ajili mapambano ya Karbala. Vyanzo vya kihistoria vinabainisha kwamba; Imamu Hussein (a.s) aliomba msaada mara kadhaa katika mapambano yake dhidi ya wafwasi wa Yazid bin Muawia. Maarufu zaidi ya wito wa kutaka msaada ulitolewa siku ya Ashura kupitia kauli isemayo: “Hal min nasirin yansuruni?” (Je, yupo msaidizi atakayenisaidia?) Ambayo imekuwa ni miongoni mwa mihimili ya utambulisho wa kumbukumbu za Ashura. Kwa mtazamo wa kijamii na kitamaduni, “Labbaika ya Hussein” ni tamko la uaminifu, mshikamano wa kijamii na utayari wa kutoa msaada kwa Imamu Hussein (a.s). Kauli hii hulifanya tukio la Karbala litazamwe kama mwendelezo wa kihistoria (historical continuum) na imekuwa ni chombo cha kudumisha “dira ya Ashura” katika ulimwengu wa kiroho na kimatendo kwa waumini. Aidha, kauli hii inafasiriwa kama alama ya kupinga utawala na uendeshaji wa kibeberu, mapambano dhidi ya ukandamizaji, na msimamo wa kukataa aina zote zile za udhalili. Labbaika ya Hussein, ni semi na kauli mbiu ya Kishia inayojitokeza katika ibada za maombolezi ya Muharram kama tamko la utii na mapenzi kwa Imamu Hussein (a.s). Ushawishi wa kauli hii umechochea kuibuka kwa kazi kadhaa kisanaa, kama vile; mashairi, michoro pamoja na filamu). Kaulii hii pia huonekana kutumika katika nyanja za kivita pamoja na mazishi ya mashahidi mbali mbali. Kwa urudufu wa kimuundo na kimaana, kauli imezalisha semi nyengine kadhaa tanzu zinazotumika katika harakatia za kihimaya, maandamano na pa moja naibada za umma, miongoni mwazo ni pamoja na; “Labbaika ya Haidar,” “Labbaika ya Mahdi,” na “Labbaika ya Khamenei.

Utambulisho Labbaika ya Hussein kama semi na kauli maarufu ya siku ya Ashura, [1] hueleweka kama mwitikio wa waumini wa kuitikia wito wa Imamu Hussein (a.s). [2] Kimaandishi, simulizi zinaonesha kwamba; kuanzia Makka hadi Iraq, Imamu Hussein (a.s) alitoa kauli kahdda za miito ya kuomba usaidizi. [3] Miongoni mwa miito hiyo, ni ule mwito aliyoutoa akiwa mjini Makka. Mwito huu ulibeba ujumbe usemao; (Mimi ninaelekea mahali ambapo mbwamwitu wa jangwani wataniraruararua… (Hivyo basi) yeyote yule aliye tayari kutoa damu yake kwa ajili yangu, basi aje Karbala). [4] Pia mwito wake mwengine, ni ule ulioko kwenye barua aliyowatuma wakuu wa mji wa Basra, akiwataka wakuu hao kumpa himaya na kumuunga mkono katika harakati zake za mapambano. [5] Kilele cha mwito huu ni kilipatikana katika hotuba yake ya Ashura, [6] iliyoambatana na kauli mbiu isemayo; “Hal min nasirin yansuruni?” (Je, kuna msaidizi yeyote yule atakayenisaidia?) [7] Kauli hii imekuwa ni moja ya mihimili mikuu na maarufu zaidi inayotumika katika kuadhimisha tukio la Karbala, hasa hasa tukio la siku ya Ashura. [7] Nafasi na Umuhimu wa Kauli ya Labbaika ya Hussein Tokea zama za tukio la Ashura hadi leo, Mashia mara kwa mara wamekuwa na kawaida ya hutangaza mshikamano wao na Imamu Hussein (a.s), kupitia kauli isemayo: “Labbaika ya Hussein”. [8] Kikawaida, Mashia hutumia kauli hii kama ni tangazo la kutangaza utayari wao wa kushikamana na Imamu Hussein (a.s), kama ni wafuasi wa Imamu Hussein (a.s), ambao wako tayari kujitolea kwa maisha yao, mali zao na hata watoto wao kwa ajili ya kushikamana na njia ya Imamu Hussein (a.s). [9] Imeelezwa kuwa kauli mbiu hii, ni moja ya kauli mbiu za kimataifa, [10] wala haikufungamani tu na kipindi fulani cha kihistoria; [11] bali nembo maalumu inalolitambulisha tukio la Ashura kama mkondo endelevu wa kihistoria unaoendelea katika zama tofauti. [12] Hivyo, pamoja na kudhamini uhai wa tukio la Ashura, [13] pia kauli mbiu hii, imedumisha muktadha na urithi wa fikra ya Ashura. [14] Imeelezwa kwamba; Miongoni mwa athari za kauli mbiu ya: “Labbaika ya Hussein”, ni kuleta matunda ya heshima na hadhi, kujiepusha na udhalili na fedheha, [15] kupambana na dhuluma na kujitoa muhanga katika njia ya haki, [16] kujikomboa kutokana na nguvu za utawala haramu, [17] kuvuruga njama za maadui [18] na kuvunja utawala wa ubeberu. [19] Hiyo ndiyo sababuiliyopelekea, kauli mbiu hii kutazamwa kama ni alama ya kupinga ubeberu na ya kukataa udhalilishaji. [20] Baadhi ya wataalamu pia wameihisisha kauli mbiu hii na ushindi, uimara na uenezaji wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, wakisema kwamba; ushikamanaji na utekelezaji wa kauli mbiu hii ndiyo sabau hasa kufanikiwa katika sekta hizo mbali mbali. [21] Labbaik katika Matini za Kidini Tangu enzi za kale, Istilahi ya neo “Labbaik” imekuwa ikitumika kama ni fomula maalumu ya mwitikio wa kukubali mwito wa mwingine. [22] Masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), pia nao walionekana kuitumia istilahi hii katika mazingira na miktadha tofauti. [23] Miongoni mwa matukio yaliyoitikiwa kwa mwitikio wa kauli ya Labbaik, ni tukio la vita vya Hunain (Ghazwatu Hunain). [24] Kutokana na ushahidi huu wa kihistoria na kimaandishi, yale madai wa Mawahabi yasemayo kwamba; matumizi ya istilahi hiyo kwa wasiyekuwa Mungu ni shirk hayawezi kuwa na nafasi yeyote ile ndani tafakuri za jamii ya Kiislamu. [25] Zaidi ya hapo, katika mojawapo ya matini za Ziara za Imamu Hussein (a.s) zinazohusishwa na Imamu Ja‘far al-Sadiq, imeelezwa kwamb; miongoni mwa adabu za ziara katika kumzuru Imamu Hussein (a.s), ni kurudia (kukariri) mara saba ibara isemayo “Labbaika da‘i Allah.” [26] Pia katika Ziara Rajabiyya ya Imamu Hussein, tunakuta Imamu (a.s) anahutubiwa kwa kauli isemayo “Labbaika ya da‘i Allah.” [27] Kadhalika, katika Du‘ā al-‘Ahd, kuna kauli isemayo “Labbaik”, ambayo inahusiana na suala la kuitikia mwito wa Imam Mahdi (a.s). [28] Wataalamu na watafiti wa lugha wanasema kwamba; neno “labbaika” kiasili lina ya “utiifu” [29] na “ijaba” (kuitikia mwito). [30] Wataalamu hawa wanaamini kwamba; neno “labbaik”—ambalo asili yake ni “labban laka”, [31] linamaanisha kubaki katika hali ya utayari wa kutii na kuitikia mwito wa mtu fulani. [32] Neno hili hutumika pia kama ni “talbiya” (Labbayka Allahumma Labbayk, Labbayka la sharika laka Labbayk), ibara ambayo hutamkwa wakati wa kuingia katika ihramu ya Hija ya Tamattu‘u (Hija ya Wajibu) au ‘Umra. [33]

Matumizi ya Kauli Mbiu Kauli-mbiu “Labbaik ya Husayn” hutumiwa katika ibada za maombolezo na katika kuonyesha mahaba na utiifu kwa Imam Husayn (a.s.), na pia kauli hii katika nyanja za kitamaduni na sanaa pamoja na halfa mbali mbali zinazohusiana na masuala ya kimapinduzi. Katika amali za maombolezo mbali mbali ya kidini, hasa katika maadhimisho ya tukio la Karbala, semi ya “Labbaika ya Hussein” huibuka kama kauli mbiu inayotamkwa ndani ya nchi mbali mbali katika muktadha wa kuadhimisha tukio hilo kimataifa. Miongoni mwa nchi zinazotumia ibara hiyo ni nembo maalumu katika maadhimisho hayo ni pamoja na; Nigeria, [35] Uturuki, [36] Lebanoni, [37] Iran, [38] Iraq, pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya ikiwemo Uholanzi. [39] Katika siku ya Ashura, jamii za wa watu wa Iraq—hasa wakaazi wa mji wa Tuwairij [40] na watu wa kabila la Bani Asad, [41] huitamka kauli mbiu hii pale wanapoingia katika haram ya Imamu Hussein (a.s.). Kuna mikusanyiko kadhaa mikubwa nchini Iran, iliyopewa jila “Ijtima‘i Labbaik ya Hussein”. Pia pale Mashia wanapotekeleza desturi yao ya kubadilisha bendera zilizoko kwenye maeneo matukufu (Atabāt ‘Āliyāt) kabla ya kuingia msimu wa maombolezo, mara nyingi amali hiyo huambatana na kauli isemayo “Labbaik ya Hussein”. [43] Aidha, mnamo mwaka 1397 (kwa kalenda ya Shamsia), kuna bendera kubwa yenye maandishi yasemayo “Labbaik ya Hussein”, ambayo ilitanda eneo lote lililoko katika Baina al-Haramain, Karbala, ambayo iliwasilishwa hadharani wakati wa matembezi ya Arbaʿīn yaliyofanyika mwaka huo. [45] Sayyid Hassan Nasrallah akiwahutubia waandamanaji wa kutetea Maeneo Matakatifu mwaka 2004: Kauli mbiu ya “Labbaika ya Hussein”, inamaanisha uwepo thabiti katika uwanja wa mapambano, hata kama utakuwa ni wewe tu ndiye uliepo uwanjani humo, na hata pale jamii inapojiondoa na kukuacha peke yako, au ikakushutumu na kukutelekeza bila nusura. Aidha, “Labbaika ya Hussein”, yaani ni ule uwepo wako binanfsi katika uwanja huo, unaoandamana na rasilimali yako, mke pamoja na watoto wako. [45] Katika Nyanja za Sanaa na Utamaduni Katika nyanja za utamaduni na sanaa, kauli mbui ya “Labbaika ya Hussein”, imeonekana kuakisiwa vya kutosha ndani ya sanaa mbali mbali, zikwemo sanaa za mashairi pamoja na kazi mbalimbali za kitamaduni na kisanii. [46] Kuna kazi kadhaa za kisanii zililzotungwa na kuwasilishwa kwa anwani ya “Labbaika ya Hussein”. Miongoni mwa kazi hizo ni video ya muziki iitwayo “Labbaika ya Hussein”, iliyoimbwa na Sadegh Ahangaran, iliyotolewa kwa mnasaba wa adhimisho la siku ya Arubaini (Arbaeen). [47] Katika fani ya kaligrafia, pamoja na kuandikwa kwa kazi nyingi zenye ibara ya “Labbaika ya Hussein”, bado kumekuwa na miito maalumu ya mashindano ya uandishi wa kaligrafia kuhusiana na sentensi hii. [48] Matumizi ya Labbaika ya Hussein Katika Matukio Mbali Mbali ya Kisiasa Ndani ya matukio mbalimbali ya kijamii na kisiasa, nchi mbali mbali zimeonekana kutumia semi wa “Labbaika ya Hussein” kama ni nembo maalu ya mwamko katika jamii zao. Baada ya kutolewa kwa fatwa ya jihadi na Ayatullah Sayyid Ali Sistani dhidi ya Daesh, makundi ya wananchi wa Iraq yaliipokea fatwa hiyo kwa ukelele wa “Labbaika ya Hussein” [49] huku wakiiweka mbele kauli hiyo, katika harakati na operesheni zao mbali mbali za kupambana dhidi ya vikozi vya Daesh. [50] Kauli mbiu hiyo imeendelea kuonekana kutumika katika mbali mbali za umma, hususan katika maziko ya kuwazika mashahidi wa muqawama nchini Iran, [51] Iraq [52] na Lebanon. [53] Vilevile, kwa urudufu wa kimuundo na kimaana, kuna tanzu kadhaa zilizoibuka zikiwa na muundo kama huo, ambazo zimeonekana kutumika katika makongamano, maandamano na ibada za umma. Miongoni mwa tanzu hizo ni pamoja na; “Labbaika ya Rasula Allah,” [54] “Labbaika ya Haidar,” [55] “Labbaika ya Zainab,” [56] “Labbaika ya Qur’an,” “Labbaika ya Mahdi,” [57] “Labbaik ya Abalffadhl,” [58] “Labbaika ya Khomeini,” na “Labbaik ya Khamenei.” [59]