Dansi

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Dansi (cheza ngoma))

Dansi (Kiarabu: الرقص ) ni mchezo unaofuata mdundo wa muziki unaopigwa kwa kutumia ala za kisasa kwa mfano gitaa, kinanda, tarumbeta n.k. Kwa maneno mengine ni kuwa, dansi ni hali ya kucheza na ni harakati ya mpigo wa wimbo ambayo kikawaida huambatana na kuimba na muziki. Mafakihi wengi wanatambua aina zote za kudansi na kucheza muziki kuwa ni haramu; hata hivyo baadhi yao wanaamini kwamba, kudansi ambako ni haramu ni kule kunakoambatana na jambo la haramu; kwa mfano kucheza na kudansi ambapo kunapelekea kuibua matamanio ya kijinsia. Baadhi ya wanazuoni wa fikihi ambao wanaamini kwamba, kitendo chenyewe tu cha kudansi na kucheza ni haramu, wameondoa baadhi ya hali za kudansi na kuzitaja kuwa sio haramu; kama vile mwanamke kudansi mbele ya mwanamke mwenzake, na mwanamke kumdansia mumewe endapo kudansi huko hakutaambatana na haramu nyingine.

Utambuzi wa Maana

Kudansi au kucheza ni harakati ya mpigo wa wimbo ambayo kikawaida huambatana na kuimba na muziki [1] Mafakihi hujadili maudhui ya kudansi na kucheza muziki katika sehemu ya Makasib muharramah (biashara za haramu) na Masail Mustahdathah (mas'ala mapya). [2]

Hukumu ya Kudansi

Kuhusiana na hukumu ya kifiq'h ya kudansi kuna mitazamo miwili jumla: Mtazamo wa kwanza ambao mafakihi wengi wameshikana nao ni kwamba, kucheza au kudansi ni haramu. [3] Hata hivyo kwa mujibu wa mtazamo wa pili, kudansi au kucheza, huwa haramu pale kitendo hicho kinapoambatana na jambo la haramu [4] au kucheza huku kutakapopelekea kuchochea matamanio ya kijinsia. [5] Kadhalika kwa mujibu wa mafakihi, kuangalia dansi au watu wanaocheza dansi na muziki hukumu yake ni sawa na kucheza dansi yenyewe. [6] Na haijuzu kama hilo litapelekea kuchochea matamanio ya kijinsia, kuunga mkono ujasiri wa kutenda dhambi na hivyo kupelekea ufisadi. [7]

Sababu ya Kuharamishwa Dansi

Katika maandiko ya kifiq'h kuna hoja kadhaa zilizotajwa za kuwa haramu dansi ambazo ni kama ifuatavyo:

  • Dansi ni kielelezo na mfano wa wazi wa upuuzi (lahw) na pumbao au kufanya jambo la kipuuzi ni haramu. [8]
  • Katika hadithi zilizonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) kudansi kumekatazwa kwa sura jumla(mutlaq). [9]
  • Kudansi ni chimbuko la ufisadi na jambo hilo linaondoa haya na soni. [10]

Kuruhusiwa Dansi Katika Baadhi ya Sehemu

Akthari ya mafakihi ambao wanatambua dansi kuwa ni haramu, wamezungumzia kutokuwa haramu katika baadhi ya sehemu:

  • Mume au mke kumdansia mwenziwe: Baadhi ya mafakihi wanaamini kuwa, inajuzu mke kumdansia mumewe. [11] katika kundi hili, kuna ambao wamejuzisha pia mume kumdansia mkewe, [12] na kuna kundi jingine ambalo lenyewe linaona kuwa haijuzu mume kumdansia mkewe. [13] Hata hivyo kuruhusiwa mke au mume kumdansia mwenzake kunaruhusiwa kwa sharti kama hakutaambatana na jambo la haramu. [14] Muhammad-Taqi Bahjat Foumani, mmoja wa Marajii Taqlidi anasema kuwa, ni haramu mume au mke kumdansia mwezake. [15]
  • Mwanamke kumdansia mwanamke mwenzake: Kwa mujibu wa fat'wa za baadhi ya mafakihi ni kwamba, kudansi na kucheza pekee pia ni haramu, lakini inajuzu mwanamke kumdansia mwanamke mwenzake. [16] Hata hivyo hukumu hii ni pale inapokuwa kwamba, kudansi huku hakujaambatana na haramu nyingine kama ghina (kuimba nyimbo) na pale kusiwepo na mwanaume mwingine yeyote yule hata ambaye ni maharimu wa mwanamke. [17]

Rejea

Vyanzo

  • Ardebili, Mirza Yusuf, (cet. 1, 1418 H). Risalah fi al-Ghina'. Riset dan revisi: Ali Akbar Zamaninejad. Qom: Mersad.
  • Khui, Sayyied Abul Qasim, Shirath al-Najah. Qom: Maktab Nasyr al-Muntakhab, cet. 1, 1416 H.
  • Sistani, Sayyied Ali, Al-Fatawa al-Muyassarah. atas upaya Sayid Abdulhadi al-Hakim. Qom: Kantor Ayatullah Sistani.
  • Al-Kasyani, Izzuddin Mahmud. Mishbah al-Hidayah wa Miftah al-Kifayah. Revisi: Jalaluddin Homai. Teheran: Nasyr-e Homa, 1376 S.
  • Behjat, Muhammad Taqi, Estefta'at, Qom: Kantor Ayatullah Behjat, cet. 1, 1428 H.
  • Fadhil Lankarani, Muhammad, Ajwibat al-Sa'ilin, Qom: Kantor Ayatullah Fadhil Lankarani, cet. 1, 1416 H.
  • Fadhil Lankarani, Muhammad, Jami' al-Masa'il, Qom: Amir-e Qalam, cet. 1, 1425 H.
  • Gulpaigani, Sayyied Muhammad Ridha, Irsyad al-Sa'il, Beirut: Dar al-Shafwah, cet. 2, 1414 H.
  • Khamenei, Sayieyd Ali. Ajwibat al-Istifta'at, Qom: Kantor Ayatullah Khamenei, cet. 1, 1424 H.
  • Makarim Shirazi, Nashir. Estefta'at-e Jadid, Qom: Entesyarat-e Madrasah Imam Ali bin Abi Thalib as, cet. 2, 1427 H.
  • Muntazeri, Hussein Ali, Resaleh-ye Estefta'at, Qom: n.p, cet. 1, n.d.
  • Mehrabani, Amin, Raqsh dalam Ensiklopedia Dunia Islam, Teheran: Yayasan Kebudayaan dan Kesenian Buku Panduan, 1394 S.
  • Shirazi, Sayyied Shadiq. Istifta'at al-Ghina'. (n.d.).
  • Tabrizi, Jawad, Estefta'at-e Jadid. (cet. 1, n.d.)
  • Tabrizi, Jawad, Shirat al-Najah. (n.d.).
  • Yayasan Ensiklopedia Islam, Farhang-ge Feqh Mothabeq-e Mazhab-e Ahl-e Beit. Qom: Nasyr-e Da'erah al-Ma'aref-e Eslami, cet. 1, 1389 S.
  • Nouruzi-thalab, Ali Reza, Motale'eh-ye Tathbiqi-ye Raqs-e Syiva wa Raqs-e Sama dalam majalah Bag-e Nazar. Teheran: Pusat Riset Kesenian, Arsitektur, dan Pemangunan Kota Nazar, 1393 S.