Nenda kwa yaliyomo

Batuli

Kutoka wikishia

Batuli (Kiarabu: البتول) Ni jina maalum alilopewa Bibi Fatima (a.s) ambalo kwa mujibu wa maelezo ya wanazuoni ni kwamba yeye alipewa jina hilo kutokana na sifa pekee alizo nazo ukilinganisha na wanawake wengine. Yaani Bibi Fatima kilugha, kimatendo na kifikra ni mwanamke mwenye sifa pekee katika jamii ya wanaadamu, jambo ambalo limepelea yeye kuitwa Batuli. Imamu Ali (a.s) naye ameitwa mume wa Batuli kwa kuwa yeye ameoana na Bibi Fatima (a.s). Hata Bibi Mariamu pia naye yasemekana kwamba alikuwa akiitwa Batuli.

Batuli kilugha

Neno Batuli (بَتْل): Ni neno la Kiarabu ambalo ni maana ya kutenganisha kitu kutoka katika kitu chengine au kwa maana kukata. Kwa hiyo Batuli (بَتُول) hutumika kumrejelea mwanamke bikira anaye kaa mbali na kujitenga na wanaume, ambaye amejitenga na ndoa na wala hana hamu au hisia yoyote kuhusiana na wanaume. [1] Kwa mfano, bibi Mariamu, mama wa nabii Issa (a.s), yeye alijulikana kama ni (بَتُول), kwa sababu kule yeye kujitenga na wanaume. [2] Pia jina Batuli linaweza kutumika kumrejelea mwanamke ambaye amemshiba Mungu wake na kumweke yeye peke yaka ndani ya my wake, kisha akajitenga na kukata mguu wake juu ya mambo ya kidunia. [3]

Sababu ya Bibi Fatima (a.s) kuitwa Batul

Sababu ya bibi Fatima (a.s) kuitwa al-Batul inaelezwa kama ifuatavyo:

  • Kulingana na Hadithi mbalimbali, bibi Fatimah (a.s) alipewa jina la al-Batul kwa sababu yeye hakuwa na hedhi.[Maelezo 1]
  • Alikuwa ni tofauti na wanawake wengine wa wakati wake; Yeye alitofautiana nao kimatendo, kitabia, na elimu. Yeye alikuwa amefikia hali ya kukata mguu katika kuiendea duni na hakuwa na jingine lililomo moyoni mwake zaidi ya Allah.
  • Alikuwa ni mbora kuliko wanawake wengine katika kuwa na haya, dini, hadhi, na nasaba.

Zawju al-Batul (mume wa al-Batul)

Zawju al-Batul “mume wa al-Batul”: Ni jina alilopewa Imamu Ali (a.s) baada ya ndoa yake na Bibi Fatima (a.s). Katika hotuba aliyoitoa baada ya kurudi kutoka Vita vya Nahrawan, Imam Ali (a.s) alijielezea na kujitambulisha kwa jina hilo.

Maelezo

  1. Baadhi ya wakati sifa pee isiyo ya kawaida huwa na thamani kubwa. Kama vile sifa ya Nabii Isa kutamka na kujielezea hali akiwa mtoto mchang, sifa ambayo ilikuwa kitendo kisicho cha kawaida, kilicho tendeka kwa idhini ya Mwenye Ezi Mungu, kitendo hicho kilimsafisha mama yake kutokana na tuhuma za watu walikuwa na nia mbovu. Kwa hiyo, ingawa sifa ya kuto kuwa na hedhi kwa wanawake ambao wako katika umri wa kuona hedh,i kunaweza kuwa ni ugonjwa hatari sana na hata kuwaletea madhara, lakini kwa nguvu na hekima za Mwenye Ezi Mungu, yeye amewajaali wanawake maalumu kutokuwa na hedhi, pia akawaepushi madhara yanayo sababishwa na kuto ona hedhi. Jambo ambalo limwewafanya wanawake hao kuwa na fursa kubwa; kwa sababu wanawake katika siku maalum (siku zao za hedhi) hawawezi kusali, kufunga, kuingia kwenye Msikiti Mtakatifu (wa Makka), Msikiti wa Mtume (wa Madina), kusimama ndani ya misikiti, na kugusa maneno na Aya za Qur’ani. Lakini Bibi Fatima (a.s) kutokana na neema na umakini maalum wa Mwenye Ezi Mungu ameepukana na vizuizi kama hivyo. Kuna Hadithi zisemazo kwamba; Kwa msingi huo huo ulioelezwa hapo juu, Mwenye Ezi Mungu amewafanya mabinti wote wa Mitume walio pita kuwa na sifa kama hiyo. Bwana Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hedhi ni jambo lisilopendeza kwa mabinti wa Mitume.” Imenukuliwa Hadithi kutoka kwa Sheikh Saduqu, isemayo: ((أَنَّ النَّبِيَّ (ص) سُئِلَ مَا الْبَتُولُ فَإِنَّا سَمِعْنَاكَ يَا رَسُولَ اللهِ تَقُولُ إِنَّ مَرْيَمَ بَتُولٌ وَ فَاطِمَةَ بَتُولٌ فَقَالَ (ص) الْبَتُولُ الَّتِي لَمْ تَرَ حُمْرَةً قَطُّ أَيْ لَمْ تَحِضْ فَإِنَّ الْحَيْضَ مَكْرُوهٌ فِي بَنَاتِ الْأَنْبِيَاءِ ; Mtume (s.a.w.w) aliulizwa, "Ni nini maana ya Batul? Hakika sisi tumekusikia, ewe Mtume wa Mwenye Ezi Mungu, ukisema kwamba Mariamu ni Batul na Fatima ni Batul."Bwana Mtume (s.a.w.w) akasema, "Batul ni yule ambaye kamwe hajawahi kuona wekundu, yaani hakuwahi kupata hedhi. Kwa maana kwamba hedhi ni jambo lisilopendeza (makruhu) kwa binti za manabii. kitabu ‘Ilalu al-Shara’i, chapa ya Al-Maktabatu Al-Haydariyya, Juzuu ya 1, ukurasa 181.

Rejea

Vyanzo

  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Tabriz: Maktabat Banī Hāshimī, 1381 AH.
  • Jawharī, Ismāʿīl b. Ḥammād. Al-Ṣiḥāḥ. Beirut: Dār al-ʿIlm li-l-Malāyyīn, 1410 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1365 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Edited by Muḥammad Bāqir Bihbūdī. Beirut: Muʾassisat al-Wafāʾ, 1403 AH.
  • Māzandarānī, Muḥammad Sāliḥ b. Ahmad. Sharḥ uṣūl kāfī. Edited by Abu l-Ḥassan Shaʿrānī and Sayyid ʿAlī Āshūr. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī li-ṭibaʿat wa al-Nashr wa al-Tawzīʿ, 1421 AH.
  • Maḥallātī, Ḍhabīḥ Allāh. Rayāḥīn al-sharīʿa dar tarjuma-yi bānwān-i dānishmand-i shīʿa. Tehran: Dār al-Kitāb al-Islāmī, [n.d].
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1374 Sh.
  • Nūrī, Ḥusayn b. Muḥammad Taqī. Khātima al-mustadrak al-wasāʾil. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1408 AH.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Bayt al-Aḥzān. Translated to Farsi by Ishtihārdī. Qom: [n.d].
  • Qundūzī, Sulaymān b. Ibrāhīm. Yanābīʿ al-mawadat li-dhawi l-qurbā. Edited by Sayyid Alī Jamāl Ashraf Ḥusaynī. [n.p]: Dār al-Uswa li-ṭibaʿat wa al-Nashr, 1416 AH.
  • Rāghib al-Iṣfahānī, Ḥusayn b. Muḥammad al-. Mufradāt alfāẓ al-Qurʾān. Translated to Farsi by Sayyid Ghulām Riḍā Khusrawī Ḥusaynī. Tehran: Intishārāt-i Murtaḍawī, 1375 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿIlal al-sharāʾiʿ. Edited by Sayyid Muḥammad Ṣādiq Baḥr al-ʿUlūm. Najaf: Manshurāt al-Maktaba al-Ḥaydariyya, 1385 AH/1966.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Maʿānī al-akhbār. Qom: Jāmiʿa-yi Mudarrisīn, 1403 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Edited by al-Bi'tha Institute. Qom: Dār al-Thiqāfa li-ṭibaʿat wa al-Nashr wa al-Tawzīʿ, 1414 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Dalāʾil al-imāma. Qom: Dār al-Dhakhāʾir, [n.d].
  • Ṭurayḥī, Fakhr al-Dīn b. Muḥammad al-. Majmaʿ al-baḥrayn. Edited by Sayyid Aḥmad Ḥusaynī. 3rd edition. Tehran: Kitabfrūshī Murtaḍawī, 1375 Sh.