Barua ya Imamu Ali (as) kwa Othman bin Hunaif
Barua ya Imamu Ali (a.s) kwa Othman bin Hunaif (Kiarabu: رسالة الإمام علي إلى عثمان بن حنيف) ni barua ambayo Imamu Ali (a.s) aliiandika akimhutubu Othman bin Hunaif mtumishi wake huko Basra. Barua hii ni mojawapo ya barua za Nahj al-Balagha, na lengo lake kuu ni kumlaumu Othman bin Hanaif kwa kushiriki katika mwaliko wa hafla ya kifalme, bila ya kuwepo kwa maskini.[1] Baadhi ya watafiti wameichukulia barua hii kuwa ni mfano wenye nguvu zaidi kwa nadharia ya upeo wa juu wa dini.[2] Pia imesemwa, kupitia barua hii, mtu anaweza kujua shakhsia ya Imam Ali (a.s) katika uwanja wa siasa na uongozi.[3] Kwa msingi huo, barua hii imetajwa katika vitabu vya kueleza nadharia ya kisiasa ya Uislamu.[4] Kutokana na kuwa barua hii inaelezea aina ya utawala wa Imam Ali (a.s), imetambulishwa kuwa mojawapo barua muhimu za Imam Ali (a.s) kwa watumishi.[5]
Katika nakala nyingi za Nahaj al-Balagha, barua hii imewekwa katika orodha nambari 45.[6]
Jina la nakala: Al-Mu’jam al-Mufahras, Sobhi Salih, Faydh al-Islam, Mullah Saleh, Ibn Abil Hadid, Abduh. Nambari ya barua 45.[7] Khui, Ibn Maytham, Fi Dhilal, Namba ya barua 44. Mullah Fat’hullah. Nambari ya barua 48.
Baadhi ya nukta ambazo Imamu Ali (a.s) aliusia watu wazifuate katika barua hii ni hizi zifuatazo: Utakasifu, uchamungu, kuwajali masikini, udhibiti wa matamanio ya kinafsi, kutosheka (kukinai), kuepuka israfu, kuwa pamoja na watu katika matatizo yao (kuwaliwaza), kuishi maisha ya kawaida (yasiyo ya kifahari), kumfuata Imamu katika njia ya maisha na kuwa mwangalifu kwa mialiko na vikao vya kuhudumiwa na kukirimiwa kwa chakula.[8]
Katika barua hii, pamoja na kutambua ubaya wa umatabaka kumebainishwa mikakati ya kukabiliana nayo.[9] Wahakiki wanasema kuwa, barua hii ni mfano na kigezo mwafaka cha kimaadili na kijamii katika kukabiliana na ubaguzi na umatabaka katika jamii.[10]
Sehemu za barua ya Imam Ali kwa Othman bin Hunaif zimenukuliwa katika kitabu cha Amali kilichoandikwa na Sheikh Swaduq[11] na katika vitabu vingine.[12] Kwa mujibu wa baadhi ya watafiti, barua hii aliandikiwa Othman bin Hunaif mwanzoni mwa utawala wa Imam Ali (a.s) mwaka wa 36 Hijiria.[13] Mbali na maelezo na tarjumi ya barua ya 45 ya Nahaj al-Balagha kumeandikwa vitabu vinavyoeleza na kubainisha barua hii kwa lugha za Kifarsi na Kiarabu. Baadhi ya vitabu hivyo ni:
- Barua ya wazi ya Imamu Ali kwa Othman bin Hunaif, gavana wa Basra; Mwandishi Muhammad Muhammadi Ishtihardi.[14]
- Uongozi na Uchaji Mungu, mwandishi: Mustafa Delshad Tehrani.[15]
- Sharh Kitab Amirul-Muumina (as) Ilaa Othman bin Hunaif al-Ansari, mwandishi: Hashim Milani.[16]
- Ali va Kargozaran hokomat. Mwandishi: Ali Akbar Hamidzadeh.[17]
Andiko la Barua
أَمَّا بَعْدُ، یا ابْنَ حُنَیفٍ فَقَدْ بَلَغَنِی أَنَّ رَجُلًا مِنْ فِتْیةِ أَهْلِ الْبَصْرَةِ دَعَاكَ إِلَی مَأْدُبَةٍ فَأَسْرَعْتَ إِلَیهَا تُسْتَطَابُ لَكَ الْأَلْوَانُ وَ تُنْقَلُ إِلَیكَ الْجِفَانُ وَ مَا ظَنَنْتُ أَنَّكَ تُجِیبُ إِلَی طَعَامِ قَوْمٍ عَائِلُهُمْ مَجْفُوٌّ وَ غَنِیهُمْ مَدْعُوٌّ فَانْظُرْ إِلَی مَا تَقْضَمُهُ مِنْ هَذَا الْمَقْضَمِ فَمَا اشْتَبَهَ عَلَیكَ عِلْمُهُ فَالْفِظْهُ وَ مَا أَیقَنْتَ بِطِیبِ وُجُوهِهِ فَنَلْ مِنْهُ أَلَا وَ إِنَّ لِكُلِّ مَأْمُومٍ إِمَاماً یقْتَدِی بِهِ وَ یسْتَضِیءُ بِنُورِ عِلْمِهِ أَلَا وَ إِنَّ إِمَامَكُمْ قَدِ اكْتَفَی مِنْ دُنْیاهُ بِطِمْرَیهِ وَ مِنْ طُعْمِهِ بِقُرْصَیهِ أَلَا وَ إِنَّكُمْ لاتَقْدِرُونَ عَلَی ذَلِكَ وَ لَكِنْ أَعِینُونِی بِوَرَعٍ وَ اجْتِهَادٍ وَ عِفَّةٍ وَ سَدَادٍ فَوَاللهِ مَا كَنَزْتُ مِنْ دُنْیاكُمْ تِبْراً وَ لاادَّخَرْتُ مِنْ غَنَائِمِهَا وَفْراً وَ لاأَعْدَدْتُ لِبَالِی ثَوْبِی طِمْراً وَ لاحُزْتُ مِنْ أَرْضِهَا شِبْراً وَ لاأَخَذْتُ مِنْهُ إِلَّا كَقُوتِ أَتَانٍ دَبِرَةٍ وَ لَهِی فِی عَینِی أَوْهَی وَ أَوْهَنُ مِنْ عَفْصَةٍ مَقِرَةٍ بَلَی كَانَتْ فِی أَیدِینَا فَدَكٌ مِنْ كُلِّ مَا أَظَلَّتْهُ السَّمَاءُ فَشَحَّتْ عَلَیهَا نُفُوسُ قَوْمٍ وَ سَخَتْ عَنْهَا نُفُوسُ قَوْمٍ آخَرِینَ وَ نِعْمَ الْحَكَمُ اللهُ وَ مَا أَصْنَعُ بِفَدَكٍ وَ غَیرِ فَدَكٍ وَ النَّفْسُ مَظَانُّهَا فِی غَدٍ جَدَثٌ تَنْقَطِعُ فِی ظُلْمَتِهِ آثَارُهَا وَ تَغِیبُ أَخْبَارُهَا وَ حُفْرَةٌ لَوْ زِیدَ فِی فُسْحَتِهَا وَ أَوْسَعَتْ یدَا حَافِرِهَا لَأَضْغَطَهَا الْحَجَرُ وَ الْمَدَرُ وَ سَدَّ فُرَجَهَا التُّرَابُ الْمُتَرَاكِمُ وَ إِنَّمَا هِی نَفْسِی أَرُوضُهَا بِالتَّقْوَی لِتَأْتِی آمِنَةً یوْمَ الْخَوْفِ الْأَكْبَرِ وَ تَثْبُتَ عَلَی جَوَانِبِ الْمَزْلَقِ وَ لَوْ شِئْتُ لَاهْتَدَیتُ الطَّرِیقَ إِلَی مُصَفَّی هَذَا الْعَسَلِ وَ لُبَابِ هَذَا الْقَمْحِ وَ نَسَائِجِ هَذَا الْقَزِّ وَ لَكِنْ هَیهَاتَ أَنْ یغْلِبَنِی هَوَای وَ یقُودَنِی جَشَعِی إِلَی تَخَیرِ الْأَطْعِمَةِ وَ لَعَلَّ بِالْحِجَازِ أَوْ الْیمَامَةِ مَنْ لاطَمَعَ لَهُ فِی الْقُرْصِ وَ لاعَهْدَ لَهُ بِالشِّبَعِ أَوْ أَبِیتَ مِبْطَاناً وَ حَوْلِی بُطُونٌ غَرْثَی وَ أَكْبَادٌ حَرَّی أَوْ أَكُونَ كَمَا قَالَ الْقَائِلُ: وَ حَسْبُكَ دَاءً أَنْ تَبِیتَ بِبِطْنَةٍ * وَ حَوْلَكَ أَكْبَادٌ تَحِنُّ إِلَی الْقِدِّ أَ أَقْنَعُ مِنْ نَفْسِی بِأَنْ یقَالَ هَذَا أَمِیرُ الْمُؤْمِنِینَ وَ لاأُشَارِكُهُمْ فِی مَكَارِهِ الدَّهْرِ أَوْ أَكُونَ أُسْوَةً لَهُمْ فِی جُشُوبَةِ الْعَیشِ فَمَا خُلِقْتُ لِیشْغَلَنِی أَكْلُ الطَّیبَاتِ كَالْبَهِیمَةِ الْمَرْبُوطَةِ، هَمُّهَا عَلَفُهَا أَوِ الْمُرْسَلَةِ شُغُلُهَا تَقَمُّمُهَا تَكْتَرِشُ مِنْ أَعْلَافِهَا وَ تَلْهُو عَمَّا یرَادُ بِهَا أَوْ أُتْرَكَ سُدًی أَوْ أُهْمَلَ عَابِثاً أَوْ أَجُرَّ حَبْلَ الضَّلَالَةِ أَوْ أَعْتَسِفَ طَرِیقَ الْمَتَاهَةِ وَ كَأَنِّی بِقَائِلِكُمْ یقُولُ إِذَا كَانَ هَذَا قُوتُ ابْنِ أَبِی طَالِبٍ فَقَدْ قَعَدَ بِهِ الضَّعْفُ عَنْ قِتَالِ الْأَقْرَانِ وَ مُنَازَلَةِ الشُّجْعَانِ أَلَا وَ إِنَّ الشَّجَرَةَ الْبَرِّیةَ أَصْلَبُ عُوداً وَ الرَّوَاتِعَ الْخَضِرَةَ أَرَقُّ جُلُوداً وَ النَّابِتَاتِ الْعِذْیةَ أَقْوَی وَقُوداً وَ أَبْطَأُ خُمُوداً. وَ أَنَا مِنْ رَسُولِ اللهِ كَالضَّوْءِ مِنَ الضَّوْءِ وَ الذِّرَاعِ مِنَ الْعَضُدِ وَ اللهِ لَوْ تَظَاهَرَتِ الْعَرَبُ عَلَی قِتَالِی لَمَا وَلَّیتُ عَنْهَا وَ لَوْ أَمْكَنَتِ الْفُرَصُ مِنْ رِقَابِهَا لَسَارَعْتُ إِلَیهَا وَ سَأَجْهَدُ فِی أَنْ أُطَهِّرَ الْأَرْضَ مِنْ هَذَا الشَّخْصِ الْمَعْكُوسِ وَ الْجِسْمِ الْمَرْكُوسِ حَتَّی تَخْرُجَ الْمَدَرَةُ مِنْ بَینِ حَبِّ الْحَصِیدِ. إِلَیكِ عَنِّی یا دُنْیا، فَحَبْلُكِ عَلَی غَارِبِكِ قَدِ انْسَلَلْتُ مِنْ مَخَالِبِكِ وَ أَفْلَتُّ مِنْ حَبَائِلِكِ وَ اجْتَنَبْتُ الذَّهَابَ فِی مَدَاحِضِكِ أَینَ الْقُرُونُ الَّذِینَ غَرَرْتِهِمْ بِمَدَاعِبِكِ؟ أَینَ الْأُمَمُ الَّذِینَ فَتَنْتِهِمْ بِزَخَارِفِكِ؟ فَهَا! هُمْ رَهَائِنُ الْقُبُورِ وَ مَضَامِینُ اللّحُودِ وَ اللهِ لَوْ كُنْتِ شَخْصاً مَرْئِیاً وَ قَالَباً حِسِّیاً لَأَقَمْتُ عَلَیكِ حُدُودَ اللهِ فِی عِبَادٍ غَرَرْتِهِمْ بِالْأَمَانِی وَ أُمَمٍ أَلْقَیتِهِمْ فِی الْمَهَاوِی وَ مُلُوكٍ أَسْلَمْتِهِمْ إِلَی التَّلَفِ وَ أَوْرَدْتِهِمْ مَوَارِدَ الْبَلَاءِ إِذْ لاوِرْدَ وَ لاصَدَرَ هَیهَاتَ مَنْ وَطِئَ دَحْضَكِ زَلِقَ وَ مَنْ رَكِبَ لُجَجَكِ غَرِقَ وَ مَنِ ازْوَرَّ عَنْ حَبَائِلِكِ وُفِّقَ، وَ السَّالِمُ مِنْكِ لایُبَالِی إِنْ ضَاقَ بِهِ مُنَاخُهُ وَ الدُّنْیا عِنْدَهُ كَیوْمٍ حَانَ انْسِلَاخُهُ. اُعْزُبِی عَنِّی، فَوَاللهِ لاأَذِلُّ لَكِ فَتَسْتَذِلِّینِی وَ لاأَسْلَسُ لَكِ فَتَقُودِینِی وَ اَیمُ اللهِ یمِیناً أَسْتَثْنِی فِیهَا بِمَشِیئَةِ اللهِ لَأَرُوضَنَّ نَفْسِی رِیاضَةً تَهِشُّ مَعَهَا إِلَی الْقُرْصِ إِذَا قَدَرْتُ عَلَیهِ مَطْعُوماً وَ تَقْنَعُ بِالْمِلْحِ مَأْدُوماً وَ لَأَدَعَنَّ مُقْلَتِی كَعَینِ مَاءٍ نَضَبَ مَعِینُهَا مُسْتَفْرِغَةً دُمُوعَهَا أَ تَمْتَلِئُ السَّائِمَةُ مِنْ رِعْیهَا فَتَبْرُكَ وَ تَشْبَعُ الرَّبِیضَةُ مِنْ عُشْبِهَا فَتَرْبِضَ وَ یأْكُلُ عَلِی مِنْ زَادِهِ فَیهْجَعَ؟! قَرَّتْ إِذاً عَینُهُ إِذَا اقْتَدَی بَعْدَ السِّنِینَ الْمُتَطَاوِلَةِ بِالْبَهِیمَةِ الْهَامِلَةِ وَ السَّائِمَةِ الْمَرْعِیةِ. طُوبَی لِنَفْسٍ أَدَّتْ إِلَی رَبِّهَا فَرْضَهَا وَ عَرَكَتْ بِجَنْبِهَا بُؤْسَهَا وَ هَجَرَتْ فِی اللّیلِ غُمْضَهَا حَتَّی إِذَا غَلَبَ الْكَرَی عَلَیهَا افْتَرَشَتْ أَرْضَهَا وَ تَوَسَّدَتْ كَفَّهَا فِی مَعْشَرٍ أَسْهَرَ عُیونَهُمْ خَوْفُ مَعَادِهِمْ وَ تَجَافَتْ عَنْ مَضَاجِعِهِمْ جُنُوبُهُمْ وَ هَمْهَمَتْ بِذِكْرِ رَبِّهِمْ شِفَاهُهُمْ وَ تَقَشَّعَتْ بِطُولِ اسْتِغْفَارِهِمْ ذُنُوبُهُمْ أُولئِكَ حِزْبُ اللهِ أَلا إِنَّ حِزْبَ اللهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ فَاتَّقِ اللهَ یا ابْنَ حُنَیفٍ وَ لْتَكْفُفْ أَقْرَاصُكَ لِیكُونَ مِنَ النَّارِ خَلَاصُكَ[18[
Tarjuma ya Barua
Ama baad, ewe mwana wa Hunaif, imenifikia habari ya kwamba kijana mmoja kutoka Basra alikualika kwenye karamu na wewe pia ulikimbilia kwenye karamu hiyo.
Wamekukaribisha kwa vyakula vya rangi kwa rangi na sahani zilizojaa vyakula vilivyoletwa kwako, sikufikiri kwamba ungekubali kuwa mgeni kwenye meza ya watu wanaowatenga (wanaowabagua) wahitaji na kuwaalika matajiri kwenye karamu.
Zingatia tonge ambalo unaling’ata kwa meno yako, tupa nje tonge ambalo halijulikani kwako uhalali na uharamu wake, na kula kile unachojua kuwa kimepatikana kwa njia za halali. Ifahamike kwamba kila Maamuma ni Imamu anayefuatwa na kufaidika na nuru ya elimu yake. Fahamu kwamba Imamu wako ametosheka na nguo mbili kuukuu kutoka kwa ulimwengu wake wote na mikate miwili kwa chakula chake.
Ifahamike kwako kwamba huna uwezo wa kunyenyekea kwa namna hiyo, bali nisaidie kwa kujitolea na juhudi katika ibada, usafi na uadilifu.
Ninaapa kwa Mungu, sikushona dhahabu kutoka kwa ulimwengu wenu, na sikuchukua akiba kutoka kwa ghanima zake nyingi, na badala ya vazi hili kuukuu, sijatayarisha vazi lingine kuukuu.
Ndio, kutokana na kile ambacho mbingu imeweka kivuli juu yake, ni Fadak pekee iliyokuwa mikononi mwetu, ambayo kundi la watu lilikuwa bakhili nayo kwa sababu ilikuwa mikononi mwetu, na tukaiacha kwa ukarimu, na Mungu ndiye mtawala bora.
Je, nifanye nini na Fadak na zisizo za Fadak, ilihali kesho patakuwa pahali pa mtu huyo kaburini, ambapo athari za mtu zitatoweka katika giza lake, na habari zake zitafichwa, shimo ambalo wakiongeza upana wake, na mikono ya kaburi inaweza kuipanua tena, jiwe na donge la ardhi vitaibana, na udongo utarundikwa kuziba nyufa zake.
Hii ndiyo nafsi yangu, ambayo ninaizoesha katika uchamungu, ili iweze kuingia salama Siku ya Hofu Kuu, na kubaki imara kuzunguka mteremko unaoteleza. Lau ningelitaka, kwa hakika ningeweza kutembea kwa asali iliyosafishwa, punje za ngano hii, na mashono ya hariri. Lakini ni jambo lilo mbali kiasi gani kwamba, hawaa na matamanio ya nafsi yanishinde, na uchu na tamaa kubwa inifanye nichague chakula, katika hali ambayo labda kuna mtu huko Hijaz au Yamama ambaye anatamani kipande cha mkate na hakumbuki suala la kushiba.
Au ni jambo lililo mbali kiasi gani kwangu, nilale tumbo likiwa limeshiba na kuweko na matumbo yenye njaa na maini yenye joto (yaliyo na kiu) ambayo yamenizunguka? Au niwe kwa namna ambayo msemaji aseme:
Maumivu haya na aibu hii ni ya kwako wewe ambaye unalala na tumbo limeshiba, na karibu na wewe kuna matumbo ambayo yanatamani hata kula ngozi.
Je nitosheke na lakabu (Amirul-Muuminina na mshika hatamu za uongozi wa Waislamu), katika hali ambayo sikuwa pamoja nao katika masaibu ya zama au katika uchungu wa maisha yao.
Sikuumbwa ili nipate burudani na cha kunishughulisha kwa kula chakula kisafi, kama mnyama aliyefungiwa ambaye mawazo yake ni kula majani tu, au mnyama wa miguu minne aliyeachiwa ambaye kazi yake ni kujaza tumbo kwa majani (malisho). Na hajui nia ya mmiliki wake juu ya kushiba kwake.
Ninaogopa kwamba kwa kuwa nimeachwa huru, au nimeachwa bila kazi au hivi hivi bure bilashi (bila malengo), au niwe katika mshangao na kutangatanga. Ni kana kwamba mzungumzaji anakuambia: Ikiwa hiki ni chakula cha mtoto wa Abi Talib, basi udhaifu na ulegevu wake vitamzuia kupigana kwa ushujaa bega kwa bega na wenzake vitani. Tambueni kwamba, miti ya jangwa ina miti migumu zaidi, na miti ya kijani kibichi ina magome membamba, na mimea ya jangwani ina moto mkali zaidi, na kuzimika kwao ni kwa muda mrefu zaidi.
Mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kama miti miwili inayoota kutoka katika mzizi mmoja, na sisi ni kama mkono. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, ikiwa Waarabu wataungana nami katika vita, sitajiepusha kuwakabili, na ikitokea fursa nitakwenda huko haraka (Sham), na nitajaribu kuipindua ardhi na kuifanya iondokane na mwili (Muawiya) ili kokoto zitoke kwenye mbegu zilizovunwa.
Sayyid Radhii, hajaleta sehemu ya katikati ya barua hii. Ameleta sehemu ya mwisho ya barua hii namna hii:
Ee dunia! Kaa mbali na mimi, kwa maana nimeweka ustadi shingoni mwako, nimetoroka kutoka katika makucha yako, nimetoroka kutoka katika mitego yako, na nimeepuka kutembea kwenye mitego yako.
Wako wapi waliopita mliowadanganya kwa michezo yenu? Yako wapi mataifa uliyojivunia kwa dhahabu na mapambo yako? Sasa hawa ndio mateka wa makaburi, na waliozama makaburini.
Naapa kwa Mwenyezi Mungu, ee dunia, lau ungekuwa ni kiumbe kinacho onekana na chenye kustahili kuguswa, ningekuadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa waja uliowadanganya kwa matarajio yao, na mataifa uliyoyatupa katika korongo la maangamizi, na wafalme ambao umejisalimisha kwa uharibifu na kuwaleta kwenye vyanzo vya maafa, mahali ambapo hakuna usalama katika kuingia na kutoka.
Yeyote anayekanyaga katika miteremko yako huteleza, na yeyote anayepanda maji yako mazito atazama, na yeyote anayejiepusha na mitego yako atafanikiwa.
Na mwenye kusalimika na fitna zako haogopi kushikwa na mashaka ya maisha, na dunia kwake yeye ni kama siku ambayo imefikia mwisho wake.
Kaa mbali na mimi, naapa kwa Mungu kwamba sitanyenyekea kwako ili unifedheheshe, na sitajiweka mikononi mwako hata unipeleke popote utakapo. Ninaapa kwa Mungu, (kiapo ambacho ninaondoa tu mapenzi ya Allah), nitailazimisha (kwa mazoezi) roho yangu kuwa ngumu sana mpaka iridhike kwa kipande cha mkate ipatapo wakati wa kula, na iridhike na chumvi badala ya kitoweo.
Nami nitatia macho yangu katika kilio mchana na usiku ili machozi yasibaki humo kama chemchemi ambayo maji yake yamezama.
Kama vile mnyama anayechunga anavyojaza tumbo lake kwa malisho na kulala, na kundi la kondoo linaloshiba nyasi na kwenda mahali pake pa kulala, je, Ali naye ale kutoka kwenye mizigo yake na kulala?!
Macho yake ni wazi kwamba baada ya miaka mingi aliachwa kama mnyama miguu minne, na kufuata mfano wa kondoo wa malisho.
Hongera kwa yule aliyetekeleza faradhi za Mola wake Mlezi, na akastahimili matatizo, na akajiepusha na usingizi mnono usiku, mpaka usingizi ukampitia, akaichukua ardhi kama zulia lake, na akaweka mkono wake chini ya mto wake miongoni mwa watu ambao hofu yao ya siku ya mwisho imewaweka macho, na ambao mbavu zao zimetenganishwa na kitanda cha kupumzika;
Na midomo yao husema polepole na kwa utulivu wanapomkumbuka Mola wao Mlezi, na dhambi zao zinaondolewa kwa wingi wa msamaha, "Hawa ni kundi la Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba wao ni kundi la kweli la Mwenyezi Mungu.
Rejea
Vyanzo
Mwana wa Hunaif, mche Mungu, na vipande vya mkate wako mwenyewe vinakutosha, ili njia hii ikuokoe na moto wa Jahanamu.[19]