Nenda kwa yaliyomo

Barua ya Imamu Ali (as) Kwa Malik Ashtar

Kutoka wikishia

Barua ya Imam Ali (as) kwa Malik Ashtar ndiyo barua kubwa na yenye maelezo mengi zaidi ya Nahaj al-Balagha kuhusu suala la utawala na siasa au sera za kusimamia na kujongoza jamii. Katika barua hii kumebainishwa, kanuni, misingi, mbinu, sera na maadili ya usimamizi, utawala na uongozi.

Uzingatiaji wa hali ya juu kwa tabaka lisilojiweza kimahitaji, haja ya kuainisha muda kwa ajili ya kukutana na watu, kuchagua washauri imara na wenye busara na kuzuia aina yoyote ya kupeana fursa kwa kujuana ni katika nasaha zilizotajwa katika barua hii. Maagizo haya yameelezwa kuwa ya kipekee.

Imam Ali (a.s.) alimfanya Malik Ashtar kuwa mtawala na Gavana wake wa Misri katika hali ya msukosuko na akamuandikia barua hii atawale kwa kutegemea hilo. Baada ya kuuawa shahidi kwa Malik Ashtar, barua hii iliangukia mikononi mwa Mu'awiyah na akaificha hiyo kwenye hazina yake hadi Omar bin Abdul-Aziz alipokuja na kuifichua na hivyo akaifanya ipatikane na kujulikana.

Kuzingatia nyenzo na nyanja za kiroho za maisha ya watu kulingana na maadili ya kibinadamu na maadili ya Kimungu, kuelezea njia ya utawala inayozingatia kanuni, busara na maadili, na kuelezea kwa ukamilifu vigezo vya sifa na ustahiki kwa sura jumla ni miongoni mwa sifa za barua hii.

Mbali na kutolewa maelezo na tafsiri ya barua hii katika tarjuma na na maelezo yaliyoandikwa kwa ukamilifu juu ya Nahaj al-Balagha, maelezo na tafsiri maalum pia zimeandikwa kwenye barua hii; miongoni mwao: "Al-Rai wa Al-Raiyya" kitabu ambacho kimeandikwa Tawfiq Al-Fakiki, " Hekmat Usul Siyasi Islam” (Hekima ya Misingi ya Kisiasa ya Uislamu) cha Mohammad Taqi Jafari na "Dalalat Dowlat" cha Mustafa Delshad Tehrani.


Utambulisho wa Barua na Umuhimu Wake


Barua ya Imam Ali (as) kwa Malik Ashtar iliandikwa kwa Malik Ashtar na inachukuliwa kuwa barua kubwa na yenye kina zaidi ya Nahaj al-Balagha kuhusu suala la utawala na sera ya usimamizi wa jamii.[1] Katika barua hii, Imam Ali (as) alizungumzia masuala ambayo alisema kwamba wakala wa Kiislamu anapaswa kutumika katika nyanja za kijamii, kisiasa, kisheria, kijeshi na kiutamaduni.[2]

Wengine wamesema kwamba mada mbalimbali maalumu zimewasilishwa katika barua hii na inahusiana na fani nyingi za kitaaluma, ambazo ni lazima mtu awe na ujuzi nazo ili kuielewa kwa undani.[3]


Ingawa barua hii ilitumwa kwa Malik Ashtar Gavana na mtawala wa Misri, lakini kwa mujibu wa Mohammad Taqi Jafari, mmoja wa wafasiri wa Nahaj al-Balagha, mkataba huu sio mahususi kwa Malik Ashtar na jamii ya Misri; bali, ndani yake kumebainishwa kanuni na mbinu za kuwasimamia na kuwaongoza wanadamu wote, katika hali zote na zama zote.[4] Kwa hiyo, barua hii imetafsiriwa na kuelezewa kwa watawala mbalimbali kwa namna ya pendekezo la mtindo wa utawala.[5]

Kwa hiyo, barua hii imetafsiriwa na kufafanuliwa kwa namna ya pendekezo la mtindo wa utawala kwa watawala mbalimbali.[5]

Imesemekana kwamba Mirzai Shirazi, aliyetoa fatwa ya kupiga marufuku tumbaku, alidumu katika kuusoma mkataba huu na akayaweka mapendeklezo yaliyotajwa kuwa katika vipaumbele vyake.[6]

Mirzai Naini, mwandishi wa kitabu Tanbih al-Ummah, ameagiza kusomwa na kutumiwa kwa barua hii kwa watu wote wanaosimamia eneo fulani kwa kiwango chochote kile.[7]

Kwa mujibu wa Ibn Hamdun, mwandishi na mshairi wa Baghdad anasema kuwa, licha ya umbali uliopo kati ya siasa na uchamungu, Imam Ali (a.s) ameviunganisha viwili hivyo katika barua hii.[8] Malenga huyo anaamini kuwa, pindi mtu atakaposoma barua hii basi atakuwa si mhitaji wa maneno mengi ya hekima na busara.[9] Mirza Naini anaona mapendekezo yaliyotajwa katika mkataba huu kuwa adimu sana".[10]

Katika nakala nyingi za Nahaj al-Balagha barua hii imewekwa katika orodha ya 53.[11]


Maudhui


Kulingana na baadhi ya watafiti, katika barua hii, mada za msingi zaidi zinazohusiana na usimamizi na jinsi ya kutawala,[12] katika maeneo matano ya:

1. Misingi 2. Kanuni 3. Mbinu 4. Sera na 5. Maadili yameelezwa.[13]

Mada za barua hii ndefu zimeainishwa katika mihimili kumi ifuatayo:

1.       Umuhimu wa jukumu na masuuliya ya Malik Ashtar.


2.       Ukumbusho wa kimaadili una taathira katika utawala.


3.       Kuwagawa watu katika matabaka mbalimbali.


4.       Kulizingatia na kulipa umuhimu mkubwa tabaka la watu wasiojiiweza.


5.       Ulazima wa kutenga muda kwa ajili ya kukutana na watu.


6.       Kuchagua washauri imara na wenye hekima.


7.       Kuzuiia aina yoyote ya kupeana fursa kwa kujuana.


8.       Kulipa umuhimu suala la amani na kuwa macho na maadui.


9.       Kulipa umuhimuu suala la kufanyika faradhi za kidini kwa ajili ya watu.


10.     Kuomba dua kwa ajili ya kufanikiwa katika kutekeleza majukumu.[14]


Sifa Maalumu


Miongoni mwa sifa maalumu za barua hii tunaweza kuashiria nukta zifuatazo:


. Kueleza mambo muhimu kabisa ya utawala na uongozi ambayo yanajumuisha misingi, kanuuni, mbinu, sera na maadili ya kiutawala na usimamizii kwa kubainisha kwa ufasaha.[15]


. Kuzingatia upande wa kimaada na kiroho wa maisha ya mwanadamu kwa mujibu wa maadili ya kibinadamu na maadili na thamani za Kimungu.[16]


. Kubainisha mchango na nafasi ya serikali na watu kwa njia ya hoja na kwa kuzingatia mafundisho ya ufunuo;[17]


. Kubainisha mbinu ya utawala kulingana na kanuni za busara na maadili kwa njia ya ufanisi;[18]


. Kufafanua vigezo vya ustahiki kwa sura jumla;[19]


. Kufafanua viashiria vya utawala wa sheria kwa uwazi.[20]


Sababu ya Kuandikwa Barua


Kuhusu sababu ya Imamu Ali (as) kuandika barua hii, wamesema kuwa, Imamu aliamua kumfanya Malik Ashtar, ambaye alikuwa mtu mahiri, kuwa mtawala na gavana wake wa Misri, na akaandika barua hii, ambayo ilikuwa ni maelezo kamili na ya kina ya utawala, ili akatawale kwa msingi wake.[21] Mwaka wa kuandikwa barua hii umezingatiwa kuwa ni miezi ya mwisho ya mwaka 37 Hijria au mwanzo wa mwaka 38 Hijria.[22] Katika zama hizo, utawala wa Imam Ali (as) ilikuwa ngumu kutokana na vita vya uporaji[23] na hali ya Misri ilikuwa ya machafuko na Muhammad bin Abi Bakr, aliyekuwa mtawala wa Misri wakati huo, hakuweza kudhibiti hali ya huko [24].


Tukio la Kufahamika Barua Hii Kwa Umma


Barua ya Imamu Ali (as) kwa Malik Ashtar ilitolewa kwa umma katika zama za Omar bin Abdul-Aziz.[25] Kulingana na Ibn Abi al-Hadid, mmoja wa wafasiri wa Kisunni wa Nahaj al-Balagha, [26] na Nassir Makarim Shirazi, mmoja wa Marajii ya Kishia, [27] baada ya kuuawa shahidi Malik Ashtar, barua hii iliangukia mikononi mwa Muawiya na akaificha kwenye hazina yake isionekane na macho ya watu na alikuwa akiisoma mara kwa mara na alishangazwa na yaliyomo ndani yake, mpaka Omar bin Abdul Aziz alipokuja na kuifanya barua hiyo ipatikane kwa umma wakati wa utawala wake.

Hata hiivyo, kwa mujibu wa ilivyoelezwa katika baadhi ya vyanzo, tukio hili lilihusiana na barua ya Imam Ali (a.s.) kwa Muhammad bin Abi Bakr;[28] lakini Ibn Abi al-Hadid na Makarim Shirazi wanaamini kwamba barua ya Imam kwa Muhammad bin Abi Bakr ilikuwa barua ya kimaadili na tukio hili linapaswa kuhusishwa na barua kwa Malik Ashtar. [29].


Itibari na Vyanzo Vingine


Kwa mujibu wa Imam Khomeini, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, barua ya maagizo ya Imamu Ali kwa Malik Ashtar ina maudhui ya kina kiasi kwamba hilo linawezekana kutoka kwa Maasumu tu na kupitia kilichomo ndani yake usahihi wake unaweza kufahamika.[30] Nassir Makarim Shirazi, Mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia naye akitumia kama hoja umashuhuri mkubwa wa barua hii na kunukuliiwa kwake katika vyanzo mbalimbali vya hadithi ameitambua kuwa ina itibari na haina haja ya kufanyiwa utaifiti sanadi na mapokezi yake.[31] Pamoja na hayo, baadhi ya watafiti, baada ya kuichunguza hati ya agano hili, waliitathmini kuwa ni sahihi.[32]

Mbali na Nahj al-Balagha, barua hii imekuja katika vyanzo vya Shia kama katika vitabu vya Da'aim al-Islam[33] na Tuhaf al-Uqul [34] na kutoka vyanzo vya Sunni katika vitabu vya Al-Mujalasa na Jawahir al-. Ilm,[35] Al-Tadhkirah al-Hamduniyah [36] na Nahayah Al-Arab.[37][38]

Najashi na Shaykh Tusi, wanazuoni wawili wa Ilm al-Rijaal wa Kishia katika karne ya 5, bila kutaja maandishi ya khutba hii, walibainisha mlolongo wake wa uwasilishaji na wakamwona msimulizi wake mkuu kuwa ni Asbagh bin Nabatah.[39]

Hata hivyo, hakuna makubaliano kuhusu hati na chanzo cha barua hii; wengine hata wameona kuwa ni bandia; kama walivyosema, mwandishi wa barua hiyo na mpokezi wake walikuwa ni watu wasiokuwa wa Imam Ali na Malik Ashtar.[40]

Pamoja na hayo, imesemwa kwamba baadhi ya watawala wamewaandikia barua baadhi ya magavana kuhusiana na jinsi ya kutawala, bila kutaja chanzo asili.[41]


Kusajiliwa UNESCO


Katika baadhi ya vyanzo, imedaiwa kuwa barua hii, ilichapishwa  na kusambazwa katika Umoja wa Mataifa kama hati rasmi;[42], lakini Seyyed Jamaluddin Dinparvar, Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Nahj al-Balagha alitangaza mwaka 1395 Hijria Shamsi kwamba jambo hilo halikufanyika hadi kufikia mwaka huo.[43] Hata hivyo, sehemu za barua hii zimependekezwa kama mojawapo ya nyaraka za muundo wa serikali katika jamii ya Kiarabu, na sehemu zake pia zimesajiliwa kama hati.[44]

Tarjumi na Maelezo


Mbali na maelezo na tafsiri ya barua ya Imamu Ali kwa Malik Ashtar katika tafsiri na maelezo yaliyoandikwa kwa ukamilifu kwenye Nahaj al-Balagha, kuna makumi ya maelezo na tafsiri maalumu katika Kiajemi na Kiarabu pia yameandikwa kuhusiana na barua hii.[45] Baadhi ya kazi hizi ni pamoja na:


. Adab al-Muluk, tarjumi na ufafanuzi wa barua ya Imamu Ali (as) kwa Malik Ashtar, mwandishi: Muhammad Rafi'i Hassan Husseini Tabatabaii, mashuhuri kkwa lakabu ya Nidham al-Ulamaa Tabrizi (1326-1350 Hijria); pamoja na mukhtasaru wa Sharf (maelezo ya ibn Maytham Bahrani na Sharh ya Muhammad Taqi Jaafarii;[46]

. Al-Rai Wal-Raiyyah, mwandishi: Tawfiq al-Fakiki.[47] Kitabu hiki kimetarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi na Sayyid Muhammad Thaqafi. Kitabu hiki kimesambazwa kikiwa na anuani ya Kishvardori Az Negah Imamu Ali (Kusimamia nchi kwa mtazamo wa Imamu Ali).[48]


. Hukumat Usul Siyasi Eslam: Tarjumi na ufafanuzi wa barua. Mwandishi Muhammad Taqi Jaafari.[49

. Aaineh Kishvardori Az Didgah Imam Ali (as), mwandishi Muhammad Fadhil Lankarani;[50]

. Bist Majlisi Piramun A'hadnameh Maliik Ashtar, mwandishi Reza Ustadi.[51]

. Delalat Dowlat, ufafanuzi wa barua ya 53 ya Nahaj al-Balagha, mwandishi Mustafa Delshad Tehrani;[52]

. Muqtabis al-Siyasah Wa Siyaq al-Riyasahm ufafanyzu wa maneno ya istilahi ngumu za barua, nwandishi:  Nuhammad Abduh;[53]

. Baistihaye Hokmrani, ufafanyuzi wa Kifarsi, Mwandishi: Abbas Kaabi;[54]

. Kandukaveh Dar Modiriyat Alavi, kwa mujibu wa barua namba 53 ya Nahaj al-Balagha, mwandishi: Amir Hoshang Azardashti;[55]

. A'had al-Imam Ali (as) Ila Malik al-Ashtar, sharh ya barua ya 53 ya Nahaj al-Balagha, mwandishi: Ali Ansariyan.[56]

. Maa al-Imam Ali (as) Fi Ahad Malik al-Ashtar, sharh na ufafanuzi wa barua kwa juhudi za Muhammad Baqi Nassiri.[57]

. Manshur Modiriyat, sharh ya utabikishaji (ulinganishaji wa barua hiyo na mapya yaliyopatikana katika elimu ya uongozi), mwandishii: Sayyid Muhammad Muqimi;[58]

. Modiriyat va Modaraa Dar Kalam Imamu Ali (as), sharf na ufafanuzi: Ali Shiravani;[59]

. Nezamnameh Hokomat, ufafanuzui wa barua ya Imamu Ali kwa Malik Ashtar, mwandishi: Muhammad Kazem Mash'hadi;[60]

. Modiriyat va Siyasat, mwandishi: Ali Akbar Zakeri;[61]

. Dowlat Javid, tarjumi na ufafanuzii wa barua, mwandishi: Muhammad Ali Salihi Mazandarani;[62]

. Dastur Hokomat, kitabu hiki kimetarjumiwa kwa lugha tatu. Mtarjumi wa Kifarsi: Muhammad Husseini Foroghii, Kifaransa: Mahmoud Sadiqan na tarjumi ya Kiingereza: Abdallah Bagheri;[63]

. Simai Kargozaran Dar Nahaj al-Balagha, tarjumi ya Kifarsi imefnywa na Sayyid Jamad al-Din Dinparvar;[64]

.Anast Shiveh Hokomat, tarjumi ya Kifarnsi imeafanywa na Sayyid Mahdi Shojai;[65]

. Farman, tarjumi ya Kifarsi, mwandishi: Miirza Muhammad Ibrahim Navad Tehrani.[66]

Nahaj al-Balagha imetarjumiwa pia kwa lugha ya Kiswahili na Sheikh Haroon Pingili.

Kadhalika angalia: Faharasa ya sharh (ufafanuzi) ya Nahaj al-Balagha na Faharasa ya tarjumi za Nahaj al-Balagha.


Andiko la hotuba hii[67] na tarjumi yake kwa mujibu wa Nassir Makarim Shirazi[68] ni kama iifuatavyo.


Andiko la Barua


هَذَا مَا أَمَرَ بِهِ عَبْدُ اللهِ عَلِی أَمِیرُ الْمُؤْمِنِینَ، مَالِک بْنَ الْحَارِثِ الْاَشْتَرَ فِی عَهْدِهِ إِلَیهِ، حِینَ وَلاَّهُ مِصْرَ: جِبَایةَ خَرَاجِهَا، وَجِهَادَ عَدُوِّهَا، وَاسْتِصْلاَحَ أَهْلِهَا، وَعِمَارَةَ بِلاَدِهَا، أَمَرَهُ بِتَقْوَی اللهِ، وَإِیثَارِ طَاعَتِهِ، وَاتِّبَاعِ مَا أَمَرَ بِهِ فِی کتَابِهِ: مِنْ فَرَائِضِهِ وَسُنَنِهِ، الَّتِی لایسْعَدُ أَحَدٌ إِلاَّ بِاتِّبَاعِهَا، وَلاَ یشْقَی إِلاَّ مَعَ جُحُودِهَا وَإِضَاعَتِهَا، وَأَنْ ینْصُرَ اللهَ سُبْحَانَهُ بِقَلْبِهِ وَیدِهِ وَلِسَانِهِ; فَإِنَّهُ، جَلَّ اسْمُهُ، قَدْ تَکفَّلَ بِنَصْرِ مَنْ نَصَرَهُ، وَإِعْزَازِ مَنْ أَعَزَّهُ. وَأَمَرَهُ أَنْ یکْسِرَ نَفْسَهُ مِنَ الشَّهَوَاتِ، وَیزَعَهَا عِنْدَ الْجَمَحَاتِ، فَإِنَّ النَّفْسَ أَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ، إِلاَّ مَا رَحِمَ اللهُ.

Hii ndiyo amri aliyoitoa mja wa Mwenyezi Mungu Ali Amirul-Mu'minin kwa Malik bin Harith Ashtar kwa amri aliyompa, pale alipomteua na kumkabidhi uongozi wa Misri ili akusanye haki za hazina za dola (Baytul Maal) katika ardhi hiyo na kupigana na maadui huko, kutoa juhudi kwa ajili ya matengenezo ya watu wake na kwa maendeleo ya miji na vijiji vyake. Anamuamrisha katika uchamungu wa Mwenyezi Mungu na anamwamrisha kutanguliza na kuchagua kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata aliyoyasema katika kitabu chake (Qur’ani Tukufu), pamoja na faradhi (wajibu) na sunna (mustahabat), amri zilezile ambazo hakuna yeyote  ambaye atapata saada na ufanisi isipokuwa kufuata hayo na kwa kuyakana hayo hatopata mtu isipokuwa taabu na mashaka.

Anamuamuru kusaidia (mafundisho ya) Mwenyezi Mungu kwa moyo wake, mkono wake na ulimi wake, kwa sababu Mwenyezi Mungu aanamsaidia anayemsaidia na humpa izza (heshima) na anayemfanya kuwa mwenye izza na anayempenda na (pia) anaamrisha nafsi yako dhidi ya matamanio na kuizuia wakati wa kuasi, kwa sababu nafsi daima huamuru mtu kufanya mambo mabaya, isipokuwa kwa kile ambacho Mungu amekihurumia.


ثُمَّ اعْلَمْ یا مَالِک أَنِّی قَدْ وَجَّهْتُک إِلَی بِلاَد قَدْ جَرَتْ عَلَیهَا دُوَلٌ قَبْلَک، مِنْ عَدْل وَجَوْر، وَأَنَّ النَّاسَ ینْظُرُونَ مِنْ أُمُورِک فِی مِثْلِ مَا کنْتَ تَنْظُرُ فِیهِ مِنْ أُمُورِ الْوُلاَةِ قَبْلَک، وَیقُولُونَ فِیک مَا کنْتَ تَقُولُ فِیهِمْ، وَإِنَّمَا یسْتَدَلُّ عَلَی الصَّالِحِینَ بِمَا یجْرِی اللهُ لَهُمْ عَلَی أَلْسُنِ عِبَادِهِ، فَلْیکنْ أَحَبَّ الذَّخَائِرِ إِلَیک ذَخِیرَةُ الْعَمَلِ الصَّالِحِ، فَامْلِکْ هَوَاک، وَشُحَّ بِنَفْسِک عَمَّا لایحِلُّ لَک، فَإِنَّ الشُّحَّ بِالنَّفْسِ الْاِنْصَافُ مِنْهَا فِیمَا أَحَبَّتْ أَوْ کرِهَتْ. وَأَشْعِرْ قَلْبَک الرَّحْمَةَ لِلرَّعِیةِ، وَالْمَحَبَّةَ لَهُمْ، وَاللُّطْفَ بِهِمْ، وَلاَ تَکونَنَّ عَلَیهِمْ سَبُعاً ضَارِیاً تَغْتَنِمُ أَکْلَهُمْ، فَإِنَّهُمْ صِنْفَانِ: إِمَّا أَخٌ لَک فِی الدِّینِ، وَإِمَّا نَظِیرٌ لَک فِی الْخَلْقِ، یفْرُطُ مِنْهُمُ الزَّلَلُ، وَتَعْرِضُ لَهُمُ الْعِلَلُ، وَیؤْتَی عَلَی أَیدِیهِمْ فِی الْعَمْدِ وَالْخَطَإِ، فَأَعْطِهِمْ مِنْ عَفْوِک وَصَفْحِک مِثْلِ الَّذِی تُحِبُّ وَتَرْضَی أَنْ یعْطِیک اللهُ مِنْ عَفْوِهِ وَصَفْحِهِ، فَإِنَّک فَوْقَهُمْ، وَوَالِی الْاَمْرِ عَلَیک فَوْقَک، وَاللهُ فَوْقَ مَنْ وَلاَّک! وَقَدِ اسْتَکْفَاک أَمْرَهُمْ، وَابْتَلاَک  بِهِمْ.


Ewe Malik! Tambua kwamba, mimi nimekutuma katika nchi iliyotawaliwa na serikali za uadilifu na dhalimu kabla yako, na watu watayatazama matendo yako kama vile ulivyoyatazama mambo ya watawala waliokuwa kabla yako, nao watasema juu yako kama ulivyokuwa ukisema kuwahusu wao na (tambua) kwamba, watu wema watatambulika kwa yale anayotuma Mwenyezi Mungu kwa ndimi za waja wake. Kwa hiyo,  inapaswa kuhifadhi akiba pendwa zaidi kwako ambayo ni amali njema. Tawala na kudhibiti hawaa na matamanio yako, na uwe bakhili kwa kisicho halali kwako, kwa sababu kujifanyia ubakhili kunakuonyesha njia ya uadilifu katika yale yanayopendwa na kuchukiwa, na fanya moyo wako kuwa kitovu cha rehema, upendo na wema kwa raia. Na usiwe kwao kama mnyama anayewala kama ngawira, kwa sababu wao ni makundi mawili, ama ndugu wa dini au wanadamu wanaofanana nawe katika uumbaji. (Kwa vyovyote vile, unapaswa kuheshimu haki zao na ujue kwamba) kuteleza na makosa hutokea kwa watu na matatizo yanawatokea (ambayo yanawazuia kutekeleza wajibu wao) na wanafanya mambo (ya makosa) kwa makusudi au kwa makosa. Katika hali kama hizi) wape msamaha wako kama unavyopenda na unavyofurahia Mwenyezi Mungu akupe msamaha wake. Kwa sababu wewe uko juu yao na kiongozi wako yuko juu yako, na Mungu yuko juu ya yule aliyekuweka juu yao na kukutaka uwasimamie mambo yao na kukutia majaribuni kupitia wao.


وَلاَ تَنْصِبَنَّ نَفْسَک، لِحَرْبِ اللهِ فَإِنَّهُ لایدَ لَک بِنِقْمَتِهِ، وَلاَ غِنَی بِک عَنْ عَفْوِهِ وَرَحْمَتِهِ. وَلاَ تَنْدَمَنَّ عَلَی عَفْو، وَلاَ تَبْجَحَنَّ بِعُقُوبَة، وَلاَ تُسْرِعَنَّ إِلَی بَادِرَة وَجَدْتَ مِنْهَا مَنْدُوحَةً، وَلاَ تَقُولَنَّ: إِنِّی مُؤَمَّرٌ آمُرُ فَأُطَاعُ، فَإِنَّ ذَلِک إِدْغَالٌ فِی الْقَلْبِ، وَمَنْهَکةٌ لِلدِّینِ، وَتَقَرُّبٌ مِنَ الْغِیرِ. وَإِذَا أَحْدَثَ لَک مَا أَنْتَ فِیهِ مِنْ سُلْطَانِک أُبَّهَةً أَوْ مَخِیلَةً، فَانْظُرْ إِلَی عِظَمِ مُلْک اللهِ فَوْقَک، وَقُدْرَتِهِ مِنْک عَلَی مَا لاتَقْدِرُ عَلَیهِ مِنْ نَفْسِک، فَإِنَّ ذَلِک یطَامِنُ إِلَیک مِنْ طِمَاحِک، وَیکفُّ عَنْک مِنْ غَرْبِک، وَیفِیءُ إِلَیک بِمَا عَزَبَ عَنْک مِنْ عَقْلِک! إِیاک وَمُسَامَاةَ اللهِ فِی عَظَمَتِهِ، وَالتَّشَبُّهَ بِهِ فِی جَبَرُوتِهِ، فَإِنَّ اللهَ یذِلُّ کلَّ جَبَّار، وَیهِینُ کلَّ مُخْتَال.

Kamwe usijiweke katika hali ya kupigana na Mungu, kwa sababu huna subira ya adhabu yake na si kwamba, huhitaji msamaha na rehema zake, na kamwe usijutie msamaha ulioutoa na usijivunie na kufurahia adhabu uliyotoa. Unapokasirika na kutafuta suluhu kwa hilo, usikimbilie kuchukua hatua kali (na usifanye uamuzi wa ghafla). Kamwe usiseme mimi ni Amir; Ninaamrisha, na ninatiiwa, ambapo hii inakuingizia uharibifu moyoni mwako, udhaifu na uharibifu wa dini, na kuja kwa mabadiliko (katika uwezo wako). Na kila inapotokea kiburi na kujiona ndani yako kutokana na athari ya uwezo ulionao ni kutokana na ukubwa wa uweza wa Mungu ulio juu yako na ana uwezo wa kutoa maoni juu ya mambo yako ambayo huna uwezo wa kufanya juu yako mwenyewe, kwa sababu mtazamo huu utakushusha kutoka kwa uasi huo na kupunguza ukali wako na ukali wako na kukurudishia kile kilichopotea kutoka katika nguvu yako ya akili. Jihadhari na kujidai kuwa sawa na Mungu katika ukuu wake na ujiondoe kuwa sawa naye kwa uweza wake, kwa sababu Mungu humdhalilisha kila mwenye nguvu na kila mwenye kiburi na mwenye kujiona.


أَنْصِفِ اللهَ وَأَنْصِفِ النَّاسَ مِنْ نَفْسِک، وَمِنْ خَاصَّةِ أَهْلِک، وَمَنْ لَک فِیهِ هَوًی مِنْ رَعِیتِک، فَإِنَّک إِلاَّ تَفْعَلْ تَظْلِمْ! وَمَنْ ظَلَمَ عِبَادَ اللهِ کانَ اللهُ خَصْمَهُ دُونَ عِبَادِهِ، وَمَنْ خَاصَمَهُ اللهُ أَدْحَضَ حُجَّتَهُ، وَکانَ لِلَّهِ حَرْباً حَتَّی ینْزِعَ أَوْ یتُوبَ. وَلَیسَ شَیءٌ أَدْعَی إِلَی تَغْییرِ نِعْمَةِ اللهِ وَتَعْجِیلِ نِقْمَتِهِ مِنْ إِقَامَة عَلَی ظُلْم، فَإِنَّ اللهَ سَمِیعٌ دَعْوَةَ الْمُضْطَهَدِینَ وَهُوَ لِلظَّالِمِینَ بِالْمِرْصَادِ.

Vitu mahabubu kwako vinapaswa kuwa vitu ambavyo vimekamilika zaidi katika suala la kuzingatia haki, pana zaidi katika suala la haki, na pana zaidi katika suala la kuridhika kwa jumla kwa watu, kwa sababu hasira ya umma wa watu ni huifanya ridhaa ya watu makhsusi (wachache wenye matarajio makubwa) kutokuwa na athari; lakini kutoridhika kwa watu makhsusi kunaweza kusamehewa na kulipwa fidia kwa kuridhika kwa umma kwa ujumla. Na (tambua kwamba) hakuna yeyote miongoni mwa raia anayemlemea zaidi gavana katika suala la gharama za kuishi katika hali ya amani na utulivu, na asiyefaa sana wakati matatizo yanapotokea kuliko mali (ya kujitosheleza na yaliyojaa matarajio). Hao ndio wasioridhika zaidi na uadilifu (na uzingatiaji wa haki sawa miongoni mwa raia) na ndio wenye kusisitiza sana wakati wa kuomba (kitu kutoka kwa serikali) na wenye shukrani kidogo kwa ruzuku na msamaha,  na wakati wa kukabiliana na matatizo subnira na kusimama kwao kidete ni kudogo kuliko watu wote, na tambua kwamba,  watu  tu ndio nguzo ya dini na muundaji wa idadi ya Waislamu na jeshi la ulinzi dhidi ya maadui, basi wasikilize na wazingatie.


وَلْیکنْ أَبْعَدَ رَعِیتِک مِنْک، وَأَشْنَأَهُمْ عِنْدَک، أَطْلَبُهُمْ لِمَعَائِبِ النَّاسِ; فَإِنَّ فِی النَّاسِ عُیوباً، الْوَالِی أَحَقُّ مَنْ سَتَرَهَا، فَلاَ تَکْشِفَنَّ عَمَّا غَابَ عَنْک مِنْهَا، فَإِنَّمَا عَلَیک تَطْهِیرُ مَا ظَهَرَ لَک، وَاللهُ یحْکمُ عَلَی مَا غَابَ عَنْک، فَاسْتُرِ الْعَوْرَةَ مَا اسْتَطَعْتَ یسْتُرِ اللهُ مِنْک مَا تُحِبُّ سَتْرَهُ مِنْ رَعِیتِک. أَطْلِقْ عَنِ النَّاسِ عُقْدَةَ کلِّ حِقْد، وَاقْطَعْ عَنْک سَبَبَ کلِّ وِتْر، وَتَغَابَ عَنْ کلِّ مَا لایضِحُ لَک، وَلاَ تَعْجَلَنَّ إِلَی تَصْدِیقِ سَاع فَإِنَّ السَّاعِی غَاشٌّ، وَإِنْ تَشَبَّهَ بِالنَّاصِحِینَ.


Watu walio mbali na nyinyi na wenye chuki zaidi machoni mwenu wanapaswa kuwa wale ambao wanatafuta zaidi aibu na makosa ya watu, kwa sababu katika watu (wengi) kuna makosa (ambayo yamefichwa machoni na) gavana ndiye anayestahiki zaidi ya yote kuwafunika, kwa hivyo ni muhimu usifunue makosa ambayo yamefichwa kwako. Wajibu wako pekee ni kusahihisha uliyodhihirishiwa, na Mungu atahukumu yaliyofichika kwako.

Funika kasoro na aibu (za wengine) kadiri uwezavyo, ili Mungu afunike kasoro zako unazotaka zifichwe kwa raia wako. Fungua fundo la wale wanaoshikilia kinyongo (kwa wema na upendo) na ukate sababu za uadui na chuki juu yako. Puuza yale ambayo hayakueleweki wala usiwe na haraka ya kuyathibitisha maneno ya waongo, kwa sababu maneno ya waongo ni usaliti, hata kama yanaonekana katika nguo za watoa nasaha na waadhi.


وَلاَ تُدْخِلَنَّ فِی مَشُورَتِک بَخِیلاً یعْدِلُ بِک عَنِ الْفَضْلِ، وَیعِدُک الْفَقْرَ، وَلاَ جَبَاناً یضْعِفُک عَنِ الْاُمُورِ، وَلاَ حَرِیصاً یزَینُ لَک الشَّرَهَ بِالْجَوْرِ، فَإِنَّ الْبُخْلَ وَالْجُبْنَ وَالْحِرْصَ غَرَائِزُ شَتَّی یجْمَعُهَا سُوءُ الظَّنِّ بِاللهِ.


Kamwe usimshirikishe mtu bakhili katika mashauri yako, kwa sababu anakukatisha tamaa ya kufanya mema na kukufanya uogope kuwa mtupu na maskini pia, usishauriane na mtu mwoga ambaye anadhoofisha roho yako katika kufanya mambo, na jihadhari na kushauriana na watu wenye tamaa wanaopamba uchoyo kwa dhulma machoni pako. Kwa sababu "ubakhili" na "hofu" na "tamaa" ni mielekeo tofauti, ambayo jumla yake ni kuwa na dhana mbaya na Mwenyezi Mungu.


إِنَّ شَرَّ وُزَرَائِک مَنْ کانَ لِلْاَشْرَارِ قَبْلَک وَزِیراً، وَمَنْ شَرِکهُمْ فِی الآْثَامِ فَلاَ یکونَنَّ لَک بِطَانَةً، فَإِنَّهُمْ أَعْوَانُ الْاَثَمَةِ، وَإِخْوَانُ الظَّلَمَةِ، وَأَنْتَ وَاجِدٌ مِنْهُمْ خَیرَ الْخَلَفِ مِمَّنْ لَهُ مِثْلُ آرَائِهِمْ وَنَفَاذِهِمْ، وَلَیسَ عَلَیهِ مِثْلُ آصَارِهِمْ وَأَوْزَارِهِمْ وَآثَامِهِمْ، مِمَّنْ لَمْ یعَاوِنْ ظَالِماً عَلَی ظُلْمِهِ، وَلاَ آثِماً عَلَی إِثْمِهِ أُولَئِک أَخَفُّ عَلَیک مَؤُونَةً، وَأَحْسَنُ لَک مَعُونَةً، وَأَحْنَی عَلَیک عَطْفاً، وَأَقَلُّ لِغَیرِک إِلْفاً، فَاتَّخِذْ أُولَئِک خَاصَّةً لِخَلَوَاتِک وَحَفَلاَتِک، ثُمَّ لْیکنْ آثَرُهُمْ عِنْدَک أَقْوَلَهُمْ بِمُرِّ الْحَقِّ لَک وَأَقَلَّهُمْ مُسَاعَدَةً فِیمَا یکونُ مِنْک مِمَّا کرِهَ اللهُ لاَِوْلِیائِهِ، وَاقِعاً ذَلِک مِنْ هَوَاک حَیثُ وَقَعَ. وَالْصَقْ بِأَهْلِ الْوَرَعِ وَالصِّدْقِ; ثُمَّ رُضْهُمْ عَلَی أَلاَّ یطْرُوک وَلاَ یبْجَحُوک بِبَاطِل لَمْ تَفْعَلْهُ، فَإِنَّ کثْرَةَ الْاِطْرَاءِ تُحْدِثُ الزَّهْوَ، وَتُدْنِی مِنَ الْعِزَّةِ.


Wahudumu wako wabaya zaidi ni wale ambao kabla yako walikuwa watumishi wa “watawala waovu” na walishiriki katika dhambi zao. Watu kama hao hawapaswi kamwe kuwa watu wea kuficha siri zako. Hao ni wasaidizi wa watenda dhambi na ndugu wa madhalimu. Hii ni katika hali ambayo, wewe unaweza kuchagua warithi wazuri katika nafasi zao, kutoka kwa wale ambao kwa upande wa suala la mawazo na ushawishi wa kijamii hawako chini ikilinganishwa na wao; lakini hawabebi mzigo mzito wa makosa, dhambi na maasi yao; kutoka kwa wale ambao hawakuwahi kumsaidia dhalimu katika ukandamizaji wake na hawakuwahi kumuunga mkono mtenda dhambi katika dhambi yake. Gharama ya watu hawa ni nyepesi kwenu, na ushirikiano wao na usaidizi wao ni bora zaidi, na mapenzi yao kwenu ni makubwa zaidi, na mapenzi yao na chuki yao kwa asiye kuwa wewe (ajinabi) ni ndogo, basi waweke katika miongoni mwa watu wao maalumu katika faragha na mahafali mahususi. Kisha (miongoni mwao) wape kipaumbele watu ambao wako wazi zaidi katika kukuambia ukweli mchungu na wasio na msaada katika kukusaidia na kukusindikiza katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu hapendi kwa mawalii Wake; iwe ni kwa matakwa yako au la. Jiunge na watu wachamungu na wakweli, kisha wafundishe kwa namna ambayo hawakusifii (na epuka kubembeleza na kujipendekeza, na pia) wasikusifie kwa maovu ambayo hukuyafanya, kwa sababu sifa nyingi huleta hali ya kujiona  na  kumfanya mtu awe karibu na kiburi na ghururi.


وَلاَ یکونَنَّ الْمُحْسِنُ وَالْمُسِیءُ عِنْدَک بِمَنْزِلَة سَوَاء، فَإِنَّ فِی ذَلِک تَزْهِیداً لاَِهْلِ الْاِحْسَانِ فِی الْاِحْسَانِ، وَتَدْرِیباً لاَِهْلِ الْاِسَاءَةِ عَلَی الْاِسَاءَةِ! وَأَلْزِمْ کلاًّ مِنْهُمْ مَا أَلْزَمَ نَفْسَهُ. وَاعْلَمْ أَنَّهُ لَیسَ شَیءٌ بِأَدْعَی إِلَی حُسْنِ ظَنِّ رَاع بِرَعِیتِهِ مِنْ إِحْسَانِهِ إِلَیهِمْ، وَتَخْفِیفِهِ الْمَئُونَاتِ عَلَیهِمْ، وَتَرْک اسْتِکْرَاهِهِ إِیاهُمْ عَلَی مَا لَیسَ لَهُ قِبَلَهُمْ. فَلْیکنْ مِنْک فِی ذَلِک أَمْرٌ یجْتَمِعُ لَک بِهِ حُسْنُ الظَّنِّ بِرَعِیتِک فَإِنَّ حُسْنَ الظَّنِّ یقْطَعُ عَنْک نَصَباً طَوِیلاً. وَإِنَّ أَحَقَّ مَنْ حَسُنَ ظَنُّک بِهِ لَمَنْ حَسُنَ بَلاَؤُک عِنْدَهُ، وَإِنَّ أَحَقَّ مَنْ سَاءَ ظَنُّک بِهِ لَمَنْ سَاءَ بَلاَؤُک عِنْدَهُ. وَلاَ تَنْقُضْ سُنَّةً صَالِحَةً عَمِلَ بِهَا صُدُورُ هَذِهِ الْاُمَّةِ، وَاجْتَمَعَتْ بِهَا الْاُلْفَةُ، وَصَلَحَتْ عَلَیهَا الرَّعِیةُ. وَلاَ تُحْدِثَنَّ سُنَّةً تَضُرُّ بِشَیء مِنْ مَاضِی تِلْک السُّنَنِ، فَیکونَ الْاَجْرُ لِمَنْ سَنَّهَا، وَالْوِزْرُ عَلَیک بِمَا نَقَضْتَ مِنْهَا. وَأَکْثِرْ مُدَارَسَةَ الْعُلَمَاءِ، وَمُنَاقَشَةَ الْحُکمَاءِ، فِی تَثْبِیتِ مَا صَلَحَ عَلَیهِ أَمْرُ بِلاَدِک، وَإِقَامَةِ مَا اسْتَقَامَ بِهِ النَّاسُ قَبْلَک.


Watu wema na watu wabaya kamwe wasiwe sawa katika maoni na mtazamo wako, kwa sababu hii itawafanya watu wema wasitake kufanya mambo mema na watu wabaya watahimizwa kutenda mabaya; basi mlipe kila mmoja katika hawa kwa yale waliyo jitakia. Taambua kwamba hakuna njia bora ya kupata imani ya gavana kwa (uaminifu) wa raia zaidi ya kuwahurumia na kuwapunguzia gharama na sio kuwalazimisha kufanya yale ambayo hawahusiki nayo, basi jaribu sana kwa njia hii kuwa na matumaini juu ya uaminifu wa watu, kwa sababu matumaini haya yataondoa uchovu mwingi na mateso kutoka kwako na mtu anayestahiki zaidi kuwa na dhana nzuri kwako ni yule ambaye umemtumikia vyema zaidi, na (kinyume chake) yule ambaye umemtendea  ubaya na mtu mstahiki zaidi awe na dhana mbaya na wewe.

Kamwe usivunje mila yenye manufaa na yenye kupendeza- ambayo waanzilishi wa Umma huu waliifuata, na umma wa Kiislamu ukafungamana na kushikamana nayo, na mambo ya raia yakaboreshwa kwayo – na katu usilete jambo ambalo linadhuru ada na mila (nzuri) za kale ambapo tofali lake litakuwa ada kwa mtu ambaye ameliweka na dhambi yake itakuwa yako wewe ambaye umeikiuka, ongea sana na wasomi na jadiliana sana na wanafikra (na mazungumzo na mijadala hii inapaswa kuwa) juu ya mambo ambayo yataboresha mambo ya miji yako na yale ambayo yamechangia maendeleo ya watu kabla yako.


وَاعْلَمْ أَنَّ الرَّعِیةَ طَبَقَاتٌ لایَصْلُحُ بَعْضُهَا إِلاَّ بِبَعْض، وَ لاَ غِنَی بِبَعْضِهَا عَنْ بَعْض

فَمِنْهَا جُنُودُ اللهِ،

وَمِنْهَا کُتَّابُ الْعَامَّةِ وَالْخَاصَّةِ،

وَمِنْهَا قُضَاةُ الْعَدْلِ وَ مِنْهَا عُمَّالُ الْاِنْصَافِ وَالرِّفْقِ،

وَ مِنْهَا أَهْلُ الْجِزْیةِ وَالْخَرَاجِ مِنْ أَهْلِ الذِّمَّةِ وَ مُسْلِمَةِ النَّاسِ،

وَ مِنْهَا التُّجَّارُ وَأَهْلُ الصِّنَاعَاتِ وَ مِنْهَا الطَّبَقَةُ السُّفْلَی مِنْ ذَوِی الْحَاجَةِ وَالْمَسْکنَةِ، وَکلٌّ قَدْ سَمَّی اللهُ لَهُ سَهْمَهُ، وَوَضَعَ عَلَی حَدِّهِ فَرِیضَةً فِی کتَابِهِ أَوْ سُنَّةِ نَبِیهِ(صلی الله علیه وآله) عَهْداً مِنْهُ عِنْدَنَا مَحْفُوظاً.

(Ewe Malik) tambua kwamba watu wa nchi wamo katika makundi kadhaa, ambayo kila moja haliwezi kuboreshwa au kukamilishwa isipokuwa kwa njia ya jingine, na hakuna miongoni mwao lisilohitaji jingine.

Kundi moja ni la askari wa Mungu (wanaohakikisha usalama na utaratibu wa jamii na kuilinda kutokana na madhara ya maadui).

Kundi jingine ni la waandishi wa umma na binafsi (ambao mpango wao ni kuweka hesabu za fedha za serikali, kurekebisha bajeti, kusajili nyaraka na kuelimisha watu).

Kundi jingine ni mahakimu wa haki (wanaoshughulikia na kutatua hasama na kuhakikisha haki inapatikana).

Wengine ni mawakala wa haki na uvumilivu (na mawakala wa serikali).

Na tabaka jingine ni la watu wa jizia na kodi kutoka kwa  wasiokuwa Waislamu wanaoishi chini ya hifadhi ya serikali ya Kiislamu (na kulipa kodi kwa serikali ya Kiislamu kwa ajili ya kulindwa maisha na mali zao) na kundi la Waislamu (wanalima ardhi ya kukodisha na kulipa kodi yake).

Kundi jingine ni wafanyabiashara na watu wa viwanda, na kundi jingine ni tabaka la chini la jamii, masikini na wasiojiweza (na walemavu na wazee na wasiojiweza, wasioweza kufanya lolote). Mwenyezi Mungu ameweka fungu kwa kila kundi katika makundi haya na katika Kitabu Chake au Sunna ya Mtume (saww) ametuainishia jukumu na wadhifa tofauti kwa sura ya ahadi kutoka kwake ambaye tumeihifadhi.


فَالْجُنُودُ، بِإِذْنِ اللهِ، حُصُونُ الرَّعِیةِ، وَزَینُ الْوُلاَةِ، وَعِزُّ الدِّینِ، وَسُبُلُ الْاَمْنِ وَلَیسَ تَقُومُ الرَّعِیةُ إِلاَّ بِهِمْ. ثُمَّ لاقِوَامَ لِلْجُنُودِ إِلاَّ بِمَا یخْرِجُ اللهُ لَهُمْ مِنَ الْخَرَاجِ الَّذِی یقْوَوْنَ بِهِ عَلَی جِهَادِ عَدُوِّهِمْ، وَیعْتَمِدُونَ عَلَیهِ فِیمَا یصْلِحُهُمْ وَیکونُ مِنْ وَرَاءِ حَاجَتِهِمْ. ثُمَّ لاقِوَامَ لِهَذَینِ الصِّنْفَینِ إِلاَّ بِالصِّنْفِ الثَّالِثِ مِنَ الْقُضَاةِ وَالْعُمَّالِ وَالْکتَّابِ، لِمَا یحْکمُونَ مِنَ الْمَعَاقِدِ، وَیجْمَعُونَ مِنَ الْمَنَافِعِ، وَیؤْتَمَنُونَ عَلَیهِ مِنْ خَوَاصِّ الْاُمُورِ وَعَوَامِّهَا. وَلاَ قِوَامَ لَهُمْ جَمِیعاً إِلاَّ بِالتُّجَّارِ وَذَوِی الصِّنَاعَاتِ، فِیمَا یجْتَمِعُونَ عَلَیهِ مِنْ مَرَافِقِهِمْ، وَیقِیمُونَهُ مِنْ أَسْوَاقِهِمْ وَیکْفُونَهُمْ مِنَ التَّرَفُّقِ بِأَیدِیهِمْ مَا لایبْلُغُهُ رِفْقُ غَیرِهِمْ. ثُمَّ الطَّبَقَةُ السُّفْلَی مِنْ أَهْلِ الْحَاجَةِ وَالْمَسْکنَةِ الَّذِینَ یحِقُّ رِفْدُهُمْ وَمَعُونَتُهُمْ. وَفِی اللهِ لِکلّ سَعَةٌ، وَلِکلّ عَلَی الْوَالِی حَقٌّ بِقَدْرِ مَا یصْلِحُهُ، وَلَیسَ یخْرُجُ الْوَالِی مِنْ حَقِیقَةِ مَا أَلْزَمَهُ اللهُ مِنْ ذَلِک إِلاَّ بِالاِهْتِمَامِ وَالاِسْتِعَانَةِ بِاللهِ، وَتَوْطِینِ نَفْسِهِ عَلَی لُزُومِ الْحَقِّ، وَالصَّبْرِ عَلَیهِ فِیمَا خَفَّ عَلَیهِ أَوْ ثَقُلَ.

Lakini askari ni walinzi wa ngome na makazi ya raia, pambo la watawala, heshima ya dini, na njia za usalama, na utulivu wa watu hauwezekani isipokuwa kupitia kwao. Kisha uthabiti na uimara wa askari hauwezekani isipokuwa kwa kulipa kodi, jambo lile lile ambalo wanaimarishwa nalo kwa ajili ya Jihad na adui, na wanalitegemea hilo ili kujiboresha na kukidhi haja zao nalo.

Makundi haya mawili (askari na walipa kodi) halifikii uthabiti isipokuwa kwa kundi la tatu la mahakimu na viongozi wa serikali na makatibu na wahasibu, kwa sababu wanaimarisha mikataba na kukusanya kodi na wanaaminika katika kuandika mambo ya kibinafsi na ya umma.

Makundi yote haya hayawezi kuboreka bila wafanyabiashara na wenye viwanda/mashirika (kwa sababu) wao (wafanyabiashara na wenye mashirika) wanakusanya suhula za kuishi na kuzitoa sokoni, na (kundi miongoni mwao) linatengeneza zana na suhula kwa mikono yao wenyewe. Kisha kuna tabaka la chini, wahitaji na walemavu, wanaohitaji kusaidiwa.

Katika uumbaji Wake, Mungu ameweka upeo kwa kila tabaka hizi, na kila moja yao ina haki kwa gavana kwa kiwango cha kusahihisha kazi yao. Gavana kamwe hatoweza kutimiza yale ambayo Mwenyezi Mungu amemlazimu kuyafanya, isipokuwa kwa kujitahidi na kuomba msaada kwa Mwenyezi Mungu na kujiweka tayari kuitumikia haki na kuwa na subira na kusimama kidete dhidi yake, likiwa ni jambo jepesi au zito.


فَوَلِّ مِنْ جُنُودِک أَنْصَحَهُمْ فِی نَفْسِک لِلَّهِ وَلِرَسُولِهِ وَلاِِمَامِک، وَأَنْقَاهُمْ جَیباً، وَأَفْضَلَهُمْ حِلْماً، مِمَّنْ یبْطِئُ عَنِ الْغَضَبِ، وَیسْتَرِیحُ إِلَی الْعُذْرِ، وَیرْأَفُ بِالضُّعَفَاءِ، وَینْبُو عَلَی الْاَقْوِیاءِ، وَمِمَّنْ لایثِیرُهُ الْعُنْفُ، وَلاَ یقْعُدُ بِهِ الضَّعْفُ. ثُمَّ الْصَقْ بِذَوِی الْمُرُوءَاتِ وَالْاَحْسَابِ، وَأَهْلِ الْبُیوتَاتِ الصَّالِحَةِ، وَالسَّوَابِقِ الْحَسَنَةِ، ثُمَّ أَهْلِ النَّجْدَةِ وَالشَّجَاعَةِ، وَالسَّخَاءِ وَالسَّمَاحَةِ; فَإِنَّهُمْ جِمَاعٌ مِنَ الْکرَمِ، وَشُعَبٌ مِنَ الْعُرْفِ. ثُمَّ تَفَقَّدْ مِنْ أُمُورِهِمْ مَا یتَفَقَّدُ الْوَالِدَانِ مِنْ وَلَدِهِمَا، وَلاَ یتَفَاقَمَنَّ فِی نَفْسِک شَیءٌ قَوَّیتَهُمْ بِهِ، وَلاَ تَحْقِرَنَّ لُطْفاً تَعَاهَدْتَهُمْ بِهِ وَإِنْ قَلَّ; فَإِنَّهُ دَاعِیةٌ لَهُمْ إِلَی بَذْلِ النَّصِیحَةِ لَک، وَحُسْنِ الظَّنِّ بِک. وَلاَ تَدَعْ تَفَقُّدَ لَطِیفِ أُمُورِهِمُ اتِّکالاً عَلَی جَسِیمِهَا، فَإِنَّ لِلْیسِیرِ مِنْ لُطْفِک مَوْضِعاً ینْتَفِعُونَ بِهِ، وَلِلْجَسِیمِ مَوْقِعاً لایسْتَغْنُونَ عَنْهُ.

Wateue makamanda wa jeshi lako wale walio wema zaidi kwa Mwenyezi Mungu, Mtume, na Uimamu machoni pako, na wasafi wa mioyo na wenye hekima kuliko wale ambao ni wepesi wa hasira na wepesi wa kukubali udhuru.

Anapaswa kuwa mtu mpole na mwema kwa wanyonge na hodari mbele ya wenye nguvu, mtu ambaye hatayumbishwa na matatizo na hatapigishwa magoti na udhaifu.

Kisha nenda kwa wale ambao wana shakhsia na asili ya kifamilia kutoka katika familia za wachamungu na zilizoimarishwa vizuri na wana neema na ujasiri na ukarimu na wema, kwa sababu wao ndio kitovu cha utu na matawi ya wema na ustahiki.

Kisha kaguua kazi zao (na matatizo na mahitaji) kama baba na mama wanavyokagua na kumfariji mtoto wao. Kamwe usifikirie kuwa ulichowatia nguvu nacho ni kikubwa machoni pako, wala usidharau wema na upendo unaowaonyesha, hata ukiwa mdogo. Hii itawafanya kujisikia vizuri juu yako (na kuimarisha mafungano ya kihisia).

Kamwe usiache kuangalia na kukagua kurekebisha mambo yao madogo kwa sababu ya kutegemea kurekebisha mambo yao ya jumla; kwa sababu kukidhi mahitaji madogo kuna nafasi ambayo watafaidika nayo, kama ambavyo kukidhi  mahitaji muhimu kuna nafasi ambayo hakuwezi kuwafanya wasiwe wahitaji.


وَلْیکنْ آثَرُ رُءُوسِ جُنْدِک عِنْدَک مَنْ وَاسَاهُمْ فِی مَعُونَتِهِ، وَأَفْضَلَ عَلَیهِمْ مِنْ جِدَتِهِ، بِمَا یسَعُهُمْ وَیسَعُ مَنْ وَرَاءَهُمْ مِنْ خُلُوفِ أَهْلِیهِمْ، حَتَّی یکونَ هَمُّهُمْ هَمّاً وَاحِداً فِی جِهَادِ الْعَدُوِّ; فَإِنَّ عَطْفَک عَلَیهِمْ یعْطِفُ قُلُوبَهُمْ عَلَیک، وَإِنَّ أَفْضَلَ قُرَّةِ عَینِ الْوُلاَةِ اسْتِقَامَةُ الْعَدْلِ فِی الْبِلاَدِ، وَظُهُورُ مَوَدَّةِ الرَّعِیةِ. وإِنَّهُ لاتَظْهَرُ مَوَدَّتُهُمْ إِلاَّ بِسَلاَمَةِ صُدُورِهِمْ، وَلاَ تَصِحُّ نَصِیحَتُهُمْ إِلاَّ بِحِیطَتِهِمْ عَلَی وُلاَةِ الْاُمُورِ، وَقِلَّةِ اسْتِثْقَالِ دُوَلِهِمْ، خوش بین شوی، زیرا این خوش بینی، خستگی و رنج فراوانی را از تو دور می‌سازد و سزاوارترین کسی که می‌تواند مورد حسن ظن تو قرار گیرد آن کس است که تو بهتر به او خدمت کرده‌ای و (به عکس) آن کس که مورد بدرفتاری تو واقع شده است سزاوارترین کسی است که باید به او بدبین باشی. فَافْسَحْ فِی آمَالِهِمْ، وَوَاصِلْ فِی حُسْنِ الثَّنَاءِ عَلَیهِمْ، وَتَعْدِیدِ مَا أَبْلَی ذَوُو الْبَلاَءِ مِنْهُمْ; فَإِنَّ کثْرَةَ الذِّکْرِ لِحُسْنِ أَفْعَالِهِمْ تَهُزُّ الشُّجَاعَ، وَتُحَرِّضُ النَّاکلَ، إِنْ شَاءَ اللهُ. ثُمَّ اعْرِفْ لِکلِّ امْرِئ مِنْهُمْ مَا أَبْلَی، وَلاَ تَضُمَّنَّ بَلاَءَ امْرِئ إِلَی غَیرِهِ، وَلاَ تُقَصِّرَنَّ بِهِ دُونَ غَایةِ بَلاَئِهِ، وَلاَ یدْعُوَنَّک شَرَفُ امْرِئ إِلَی أَنْ تُعْظِمَ مِنْ بَلاَئِهِ مَا کانَ صَغِیراً، وَلاَ ضَعَةُ امْرِئ إِلَی أَنْ تَسْتَصْغِرَ مِنْ بَلاَئِهِ مَا کانَ عَظِیماً.

Makamanda bora wa jeshi machoni pako wanapaswa kuwa wale wanaosaidia askari zaidi na kuwasaidia zaidi ya uwezo wao, kwa kiwango ambacho askari na wale walio chini ya uangalizi wao wanasimamiwa vizuri; kwa namna ambayo wote wanafikiri juu ya jambo moja, nalo ni Jihadi dhidi ya adui, kwa sababu mapenzi yako na wema wako kwao vitaelekeza nyoyo zao kwako.

(tambua) jambo bora zaidi linalofanya macho ya magavana kung’aa ni kusimamisha uadilifu katika miji yote na kudhihirika kwa huba na mapenzi ya watu juu yao, na upendo na mapenzi ya watu kwao hayadhihirishwi isipokuwa kwa usafi wa nyoyo zao (na kuondoshwa kwa dhana yoyote kwa viongozi). Na ihsani zao huwa na manufaa kabisa ikiwa watakusanyika kwa hiari karibu na watawala na utawala wao usiwe mzito juu yao na wasisubiri mwisho wa utawala wao.

Kwa muktadha huo, panua uwanja wa unayoyatamani (ya maisha) mbele ya jeshi lako (na wape mahitaji yao katika jambo hili) wahimize kila mara na uhesabu matendo muhimu waliyoyafanya watu miongoni mwao, kwa sababu kukumbuka mema yao kutawakumbusha watu wao majasiri na hilo kuhimiza shughuli zaidi na hilo linahimiza wasio na bidii kufanya kazi. Inshallah.

Kisha unapaswa kujua thamani ya jitihada za kila mtu kwa makini na kamwe usihusishe kazi nzuri ya mtu mwingine na usifikirie thamani ya huduma yao chini ya jinsi ilivyo. Usiruhusu tabia ya mtu ikufanye uifikirie kazi yake ndogo kuwa kubwa, au udogo wa hadhi ya mtu ikufanye ufikirie huduma muhimu kuwa ndogo.


وَارْدُدْ إِلَی اللهِ وَرَسُولِهِ مَا یضْلِعُک مِنَ الْخُطُوبِ، وَیشْتَبِهُ عَلَیک مِنَ الْاُمُورِ فَقَدْ قَالَ اللهُ تَعَالَی لِقَوْم أَحَبَّ إِرْشَادَهُمْ: (یا أَیهَا الَّذِینَ آمَنُوا أَطِیعُوا اللهَ وَأَطِیعُوا الرَّسُولَ وَأُولِی الْاَمْرِ مِنْکمْ فَإِنْ تَنازَعْتُمْ فِی شَیء فَرُدُّوهُ إِلَی اللهِ وَالرَّسُولِ) فَالرَّدُّ إِلَی اللهِ الْاَخْذُ بِمُحْکمِ کتَابِهِ، وَالرَّدُّ إِلَی الرَّسُولِ الْاَخْذُ بِسُنَّتِهِ الْجَامِعَةِ غَیرِ الْمُفَرِّقَةِ.


Rejesha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume mambo muhimu yenye uzito kwako na yenye shaka na utata katika kazi mbalimbali (na taka msaada kutoka katika  maneno yao kwa ajili ya kuguundua hukumu). Mwenyezi Mungu aliliambia kundi ambalo linapendwa kuongozwa naye: Enyi mlio amini! Mt´iini Mwenyezi Mungu, na mt´iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume. Kurejesha kwa Mwenyezi Mungu maana yake ni kushikamana na Qur'ani Tukufu na kuchukua maelekezo kutoka katika aya zake Muhkamat, na kurejesha kwa Mtume maana yake ni kushikamana na Sunna ya uhakika na thabiti ya Mtume huyo, ambayo watu wameafikiana na ndani yake hakuna hitilafu.

ثُمَّ اخْتَرْ لِلْحُکْمِ بَینَ النَّاسِ أَفْضَلَ رَعِیتِک فِی نَفْسِک، مِمَّنْ لاتَضِیقُ بِهِ الْاُمُورُ، وَلاَ تُمَحِّکهُ الْخُصُومُ، وَلاَ یتَمَادَی فِی الزَّلَّةِ، وَلاَ یحْصَرُ مِنَ الْفَیءِ إِلَی الْحَقِّ إِذَا عَرَفَهُ، وَلاَ تُشْرِفُ نَفْسُهُ عَلَی طَمَع، وَلاَ یکْتَفِی بِأَدْنَی فَهْم دُونَ أَقْصَاهُ; وَأَوْقَفَهُمْ فِی الشُّبُهَاتِ، وَآخَذَهُمْ بِالْحُجَجِ، وَأَقَلَّهُمْ تَبَرُّماً بِمُرَاجَعَةِ الْخَصْمِ، وَأَصْبَرَهُمْ عَلَی تَکشُّفِ الْاُمُورِ، وَأَصْرَمَهُمْ عِنْدَ اتِّضَاحِ الْحُکْمِ، مِمَّنْ لایزْدَهِیهِ إِطْرَاءٌ. وَلاَ یسْتَمِیلُهُ إِغْرَاءٌ وَأُولَئِک قَلِیلٌ، ثُمَّ أَکْثِرْ تَعَاهُدَ قَضَائِهِ، وَافْسَحْ لَهُ فِی الْبَذْلِ مَا یزِیلُ عِلَّتَهُ، وَتَقِلُّ مَعَهُ حَاجَتُهُ إِلَی النَّاسِ. وَأَعْطِهِ مِنَ الْمَنْزِلَةِ لَدَیک مَا لایطْمَعُ فِیهِ غَیرُهُ مِنْ خَاصَّتِک، لِیأْمَنَ بِذَلِک اغْتِیالَ الرِّجَالِ لَهُ عِنْدَک. فَانْظُرْ فِی ذَلِک نَظَراً بَلِیغاً، فَإِنَّ هَذَا الدِّینَ قَدْ کانَ أَسِیراً فِی أَیدِی الْاَشْرَارِ، یعْمَلُ فِیهِ بِالْهَوَی، وَتُطْلَبُ بِهِ الدُّنْیا.

Kisha chagua mtu bora zaidi kati ya raia wako kwa ajili ya kuhukumu miongoni mwa watu. Yule asiyeweka mambo yake mbalimbali katika matatizo na makabiliano ya wapinzani wake na uadui wa maadui zake baina yake na wao kwa wao haumkasirishi na kuwa mkaidi, haendelei katika kuteleza na makosa yake, na inapodhihiri kosa lake kwake, si vigumu kwake kurudi kwenye haki ambaye nafsi yake haielekeo kwenye tamaa, katika kuelewa mambo, hapaswi kuridhika na utafiti mdogo na bali aendelee hadi mwisho, na kuwa mwangalifu zaidi katika utata (shubha), kusisitiza zaidi kuliko wengine katika kushikamana na ushahidi (hoja) na mwenye kusisitiza kuliko wote juu ya dalili na hoja, na mwenye kuchoka kidogo kwa kumrejea mara kwa mara wagomvi; kuwa na subira zaidi katika kugundua ukweli wa mambo na inapodhihirika haki awe madhubuti na imara kuliko wote katika kutoa hukumu. Asipate kiburi kwa kusifiwa sana (asihadaike) sifa na kusifiwa sana kusimfanye aelekee upande wa anayemsifia, ingawa watu wa aina hii ni wachache.

Kisha zichunguze hukumu zake kwa uzito uwezavyo na usambaze ukarimu wako kwake katika kumpa haki zake ili akidhi haja na mahitaji yake na asifikia hatua aone haja yake iko kwa watu (Mungu apishe mbali asichafuliwe kwa rushwa) na kwa mujibu wa hadhi yake nyanyua nafasi na daraja yake ili asiwepo miongoni mwa masahaba wako wa karibu atakayekuwa na pupa ya ushawishi ndani yake.

Na kwa njia hii uwe salama kutokana na njama na madhara ya watu kama hao mbele ya macho yako. Kisha yatazame kwa makini niliyoyasema (na utekeleze maamrisho yote haya kwa usahihi) kwa sababu dini hii ilitekwa na mikono ya waovu kwa hawaa na matamanio ya nafsi, kupitia kwayo walidai ulimwengu (kwa upande mmoja, kuabudu matamanio na kwa upande mwingine, kuabudu dunia kulikuwa umetikisa nguzo zote za dini).


ثُمَّ انْظُرْ فِی أُمُورِ عُمَّالِک فَاسْتَعْمِلْهُمُ اخْتِبَاراً، وَلاَ تُوَلِّهِمْ مُحَابَاةً وَأَثَرَةً، فَإِنَّهُمَا جِمَاعٌ مِنْ شُعَبِ الْجَوْرِ وَالْخِیانَةِ. وَتَوَخَّ مِنْهُمْ أَهْلَ التَّجْرِبَةِ وَالْحَیاءِ، مِنْ أَهْلِ الْبُیوتَاتِ الصَّالِحَةِ، وَالْقَدَمِ فِی الْاِسْلاَمِ الْمُتَقَدِّمَةِ، فَإِنَّهُمْ أَکْرَمُ أَخْلاَقاً وَأَصَحُّ أَعْرَاضاً، وَأَقَلُّ فِی الْمَطَامِعِ إِشْرَاقاً، وَأَبْلَغُ فِی عَوَاقِبِ الْاُمُورِ نَظَراً. ثُمَّ أَسْبِغْ عَلَیهِمُ الْاَرْزَاقَ، فَإِنَّ ذَلِک قُوَّةٌ لَهُمْ عَلَی اسْتِصْلاَحِ أَنْفُسِهِمْ، وَغِنًی لَهُمْ عَنْ تَنَاوُلِ مَا تَحْتَ أَیدِیهِمْ، وَحُجَّةٌ عَلَیهِمْ إِنْ خَالَفُوا أَمْرَک أَوْ ثَلَمُوا أَمَانَتَک. ثُمَّ تَفَقَّدْ أَعْمَالَهُمْ، وَابْعَثِ الْعُیونَ مِنْ أَهْلِ الصِّدْقِ وَالْوَفَاءِ عَلَیهِمْ، فَإِنَّ تَعَاهُدَک فِی السِّرِّ لاُِمُورِهِمْ حَدْوَةٌ لَهُمْ عَلَی اسْتِعْمَالِ الْاَمَانَةِ، وَالرِّفْقِ بِالرَّعِیةِ. وَتَحَفَّظْ مِنَ الْاَعْوَانِ; فَإِنْ أَحَدٌ مِنْهُمْ بَسَطَ یدَهُ إِلَی خِیانَة اجْتَمَعَتْ بِهَا عَلَیهِ عِنْدَک أَخْبَارُ عُیونِک، اکْتَفَیتَ بِذَلِک شَاهِداً، فَبَسَطْتَ عَلَیهِ الْعُقُوبَةَ فِی بَدَنِهِ، وَأَخَذْتَهُ بِمَا أَصَابَ مِنْ عَمَلِهِ، ثُمَّ نَصَبْتَهُ بِمَقَامِ الْمَذَلَّةِ، وَوَسَمْتَهُ بِالْخِیانَةِ، وَقَلَّدْتَهُ عَارَ التُّهَمَةِ.

Kisha, kuwa mwangalifu katika mambo yanayohusiana na mawakala wako na uwatumie kwa mtihani na kuwapima na sio kwa kuzingatia "mielekeo ya kibinafsi" na "ubabe na maoni ya kibinafsi", kwa sababu vitovu hivi viwili ni katika matawi ya dhulma na usaliti, chagua miongoni mwao watu ambao wana uzoefu na usafi wa roho kutoka kwa familia za wachamungu na waliotangulia katika Uislamu, kwa sababu maadili yao ni masafi zaidi na familia zao ni safi zaidi na uzingatiaji wao wa tamaa ni mdogo na makini zaidi katika kupima matokeo ya matendo. Kisha wape riziki nyingi (na uwape mishahara ya kutosha) kwa sababu hii itawatia nguvu katika kujirekebisha na itawafanya wasiwe wahitaji na kutolazimika kuisaliti mali iliyo chini ya udhibiti wao, na pamoja na hayo, itakuwa ni dalili na hoja dhidi yao ikiwa watakengeuka na kuasi amri zako au kusaliti amana yako.

Kisha ufuatilie kazi yao kwa kutuma mawakala wa siri wakweli na waaminifu, kwa sababu ukaguzi wa siri wa mara kwa mara utawahimiza kuwa waaminifu na wastahimilivu kwa wasaidizi wao na kuwatunza wasaidizi wao. Na ikiwa mmoja wao (maajenti wako) atafikia kufanya uhaini na w maajenti wako wa siri kwa pamoja wakakuripotia dhidi yake, tosheka na kiasi hiki kwa anuani ya ushahidi na shahidi, na uruhusu adhabu ya kimwili dhidi yake, na umuadhibu kwa kiwango ambacho amefanya khiana katika kazi yake, kisha (muadhibu kisaikolojia na) muweke katika hali ya udhalili na uchungu wa usaliti na sio kumtupia tuhuma ya kashfa shingoni mwake (na mtambulisheni kwa namna ambayo iwe funzo kwa wengine).

وَتَفَقَّدْ أَمْرَ الْخَرَاجِ بِمَا یصْلِحُ أَهْلَهُ، فَإِنَّ فِی صَلاَحِهِ وَصَلاَحِهِمْ صَلاَحاً لِمَنْ سِوَاهُمْ، وَلاَ صَلاَحَ لِمَنْ سِوَاهُمْ إِلاَّ بِهِمْ، لاَِنَّ النَّاسَ کلَّهُمْ عِیالٌ عَلَی الْخَرَاجِ وَأَهْلِهِ. وَلْیکنْ نَظَرُک فِی عِمَارَةِ الْاَرْضِ أَبْلَغَ مِنْ نَظَرِک فِی اسْتِجْلاَبِ الْخَرَاجِ، لاَِنَّ ذَلِک لایدْرَک إِلاَّ بِالْعِمَارَةِ; وَمَنْ طَلَبَ الْخَرَاجَ بِغَیرِ عِمَارَة أَخْرَبَ الْبِلاَدَ، وَأَهْلَک الْعِبَادَ، وَلَمْ یسْتَقِمْ أَمْرُهُ إِلاَّ قَلِیلاً. فَإِنْ شَکوْا ثِقَلاً أَوْ عِلَّةً، أَوِ انْقِطَاعَ شِرْب أَوْ بَالَّة، أَوْ إِحَالَةَ أَرْض اغْتَمَرَهَا غَرَقٌ، أَوْ أَجْحَفَ بِهَا عَطَشٌ، خَفَّفْتَ عَنْهُمْ بِمَا تَرْجُو أَنْ یصْلُحَ بِهِ أَمْرُهُمْ; وَلاَ یثْقُلَنَّ عَلَیک شَیءٌ خَفَّفْتَ بِهِ الْمَؤُونَةَ عَنْهُمْ، فَإِنَّهُ ذُخْرٌ یعُودُونَ بِهِ عَلَیک فِی عِمَارَةِ بِلاَدِک، وَتَزْیینِ وِلاَیتِک، مَعَ اسْتِجْلاَبِک حُسْنَ ثَنَائِهِمْ، وَتَبَجُّحِک بِاسْتِفَاضَةِ الْعَدْلِ فِیهِمْ، مُعْتَمِداً فَضْلَ قُوَّتِهِمْ، بِمَا ذَخَرْتَ عِنْدَهُمْ مِنْ إِجْمَامِک لَهُمْ، وَالثِّقَةَ مِنْهُمْ بِمَا عَوَّدْتَهُمْ مِنْ عَدْلِک عَلَیهِمْ وَرِفْقِک بِهِمْ، فَرُبَّمَا حَدَثَ مِنَ الْاُمُورِ مَا إِذَا عَوَّلْتَ فِیهِ عَلَیهِمْ مِنْ بَعْدُ احْتَمَلُوهُ طَیبَةً أَنْفُسُهُمْ بِهِ; فَإِنَّ الْعُمْرَانَ مُحْتَمِلٌ مَا حَمَّلْتَهُ، وَإِنَّمَا یؤْتَی خَرَابُ الْاَرْضِ مِنْ إِعْوَازِ أَهْلِهَا، وَإِنَّمَا یعْوِزُ أَهْلُهَا لاِِشْرَافِ أَنْفُسِ الْوُلاَةِ عَلَی الْجَمْعِ، وَسُوءِ ظَنِّهِمْ بِالْبَقَاءِ، وَقِلَّةِ انْتِفَاعِهِمْ بِالْعِبَرِ.

Angalia kwa karibu suala la ushuru na kodi, kwa njia ambayo ni nzuri kwa walipaji kodi, kwa sababu uboreshaji wa hali ya ushuru na uboreshaji wa hali ya walipaji ushuru itasababisha uboreshaji wa hali ya wengine (na matabaka mengine ya jamii ya Kiislamu) na wengineo kamwe hawatapata mema isipokuwa kama watozaji ushuru watakuwa wema, kwa sababu watu wote wanategemea walipaji kodi na ushuru, na inakupasa kuzingatia zaidi ujenzi na uboreshaji wa ardhi kuliko kuzingatia kwako kukusanya kodi, kwa sababu ushuru hauwezi kupatikana isipokuwa kwa maendeleo, na anayetaka kudai ushuru bila maendeleo na ujenzi ataharibu miji na kuwaangamiza waja wa Mungu , na misingi ya utawala wake itatikisika, kiasi kwamba, hautadumu zaidi ya kitambo kidogo.

Basi ikiwa watu wanakulalamikia juu ya uzito wa kodi, maradhi, au kukauka kwa maji katika chemchemi, au mvua kidogo, au mabadiliko ya ardhi kwa mafuriko (na kuharibika kwa mbegu) au kiu kali ya kilimo (na kisha ukosefu wa mazao), kodi zao punguza kiasi kwa matumaini ya kuboresha kazi zao.

Kamwe usiruhusu punguzo la gharama unazowapa kuwa ghali kwako, kwa sababu itakuwa akiba ambayo itarudishwa kwako kupitia maendeleo ya nchi yako, na itapamba serikali yako, na zaidi ya hayo, watakukumbuka vizuri, na kwa sababu ya kuenea uadilifu baina yao kutoka kwako utakuwa radhi nao (na kuridhika kwao na utawala wako). Hii ni pamoja na kwamba unaweza kuwafanya wajisikie raha kwa kuwaimarisha kupitia akiba uliyoweka kwaona kuwa na uhakika nao kwa sababu ya uadilifu na wema uliowazoesha.

Na itatokea sana huko mbeleni utakumbana na matatizo ambayo ukitegemea watu waondoe shida hizo, watakubali kwa wema (na kukusaidia katika kutatua tatizo).

Uharibifu wa ardhi unapatikana tu kutokana na umasikini wa wamiliki wake, na umasikini wao unatokana tu na uzingatiaji wa watawala katika kujilimbikizia mali na utajiri, na dhana mbaya kuhusu kuendelea kuwepo kwa serikali yao na kutopata ibra na funzo (kutoka hatima ya watawala waliotangulia).

ثُمَّ انْظُرْ فِی حَالِ کتَّابِک فَوَلِّ عَلَی أُمُورِک خَیرَهُمْ، وَاخْصُصْ رَسَائِلَک الَّتِی تُدْخِلُ فِیهَا مَکایدَک وَأَسْرَارَک بِأَجْمَعِهِمْ لِوُجُوهِ صَالِحِ الْاَخْلاَقِ مِمَّنْ لاتُبْطِرُهُ الْکرَامَةُ، فَیجْتَرِئَ بِهَا عَلَیک فِی خِلاَف لَک بِحَضْرَةِ مَلاَ وَلاَ تَقْصُرُ بِهِ الْغَفْلَةُ عَنْ إِیرَادِ مُکاتَبَاتِ عُمِّالِک عَلَیک، وَإِصْدَارِ جَوَابَاتِهَا عَلَی الصَّوَابِ عَنْک، فِیمَا یأْخُذُ لَک وَیعْطِی مِنْک، وَلاَ یضْعِفُ عَقْداً اعْتَقَدَهُ لَک، وَلاَ یعْجِزُ عَنْ إِطْلاَقِ مَا عُقِدَ عَلَیک، وَلاَ یجْهَلُ مَبْلَغَ قَدْرِ نَفْسِهِ فِی الْاُمُورِ، فَإِنَّ الْجَاهِلَ بِقَدْرِ نَفْسِهِ یکونُ بِقَدْرِ غَیرِهِ أَجْهَلَ. ثُمَّ لایکنِ اخْتِیارُک إِیاهُمْ عَلَی فِرَاسَتِک وَاسْتِنَامَتِک وَحُسْنِ الظَّنِّ مِنْک، فَإِنَّ الرِّجَالَ یتَعَرَّضُونَ لِفِرَاسَاتِ الْوُلاَةِ بِتَصَنُّعِهِمْ وَحُسْنِ خِدْمَتِهِمْ، وَلَیسَ وَرَاءَ ذَلِک مِنَ النَّصِیحَةِ وَالْاَمَانَةِ شَیءٌ. وَلَکنِ اخْتَبِرْهُمْ بِمَا وُلُّوا لِلصَّالِحِینَ قَبْلَک، فَاعْمِدْ لاَِحْسَنِهِمْ کانَ فِی الْعَامَّةِ أَثَراً، وَأَعْرَفِهِمْ بِالْاَمَانَةِ وَجْهاً، فَإِنَّ ذَلِک دَلِیلٌ عَلَی نَصِیحَتِک لِلَّهِ وَلِمَنْ وُلِّیتَ أَمْرَهُ. وَاجْعَلْ لِرَأْسِ کلِّ أَمْر مِنْ أُمُورِک رَأْساً مِنْهُمْ، لایقْهَرُهُ کبِیرُهَا وَلاَ یتَشَتَّتُ عَلَیهِ کثِیرُهَا، وَمَهْمَا کانَ فِی کتَّابِک مِنْ عَیب فَتَغَابَیتَ عَنْهُ أُلْزِمْتَه.

Kisha zingatia hali ya makatibu wako na uwakabidhi kazi yako kwa walio bora zaidi miongoni mwao. Toa na kabidhi barua zako za siri, ambazo zina mipango ya siri kwa mtu ambaye ana maadili mazuri zaidi. Awe miongoni mwa wale ambao cheo na wadhifa havimleweshi na kuwa na kiburi, na hivyo kuthubutu kupingana na wewe mbele ya shakhsia wakubwa (wazee) na wakuu wa watu.

Mtu ambaye haghafiliki katika kukuletea barua za mawakala wako na kupata majibu yao sahihi, iwe ni juu ya mambo anayopokea kwako au anayokukabidhi. Anapaswa kuwa mtu ambaye kila anapokuwekea kandarasi hatalegea na inapotokea kufungwa mkataba dhidi yako hatashindwa kuupatia ufumbuzi. Yule ambaye anatambua thamani na hadhi yake katika mambo mbalimbali, kwa sababu mtu asiyejua thamani na utu wake atakuwa hajui zaidi thamani na utu wa wengine.

Kisha, katika kuchagua makatibu hawa, kamwe usiridhike na mtazamo wako wa mbele imani yako binafsi na dhana nzuri, kwa sababu watu (wenye kutafuta fursa) hujionyesha na hutumikia vyema ili kuvutia watawala, katika hali ambayo, nyuma kujionyesha huko ambako kidhahiri kunavutia, hakuna kabisa utakaji kheri na utunzaji amana.

Wajaribu kupitia kwa mamlaka waliyokuwa nayo watawala wema kabla yako na waaminini wale walioacha wema bora miongoni mwa watu na wanajulikana zaidi kwa uaminifu. Ukifanya hivyo, huu ni uthibitisho wa ukarimu wako na utiifu wako kwa Mola, pamoja na utiifu kwa yule ambaye umekubali Wilayah (uongozi) kutoka kwake (yaani Imamu na kiongozi wako).

Kwa kila sehemu ya kazi yako, chagua kiongozi na msimamizi kutoka miongoni mwao; mtu ambaye haumfanyi kuzidiwa na kukosa msaada katika kazi yake muhimu, na asikengeushwe na wingi wa kazi, na (unapaswa kujua) kosa lolote linalopatikana kwa makatibu wako maalumu ambalo hulijui, utawajibika kwa hilo.

ثُمَّ اسْتَوْصِ بِالتُّجَّارِ وَذَوِی الصِّنَاعَاتِ، وَأَوْصِ بِهِمْ خَیراً: الْمُقِیمِ مِنْهُمْ وَالْمُضْطَرِبِ بِمَالِهِ، وَالْمُتَرَفِّقِ بِبَدَنِهِ، فَإِنَّهُمْ مَوَادُّ الْمَنَافِعِ، وَأَسْبَابُ الْمَرَافِقِ وَجُلاَّبُهَا مِنَ الْمَبَاعِدِ وَالْمَطَارِحِ، فِی بَرِّک وَبَحْرِک، وَسَهْلِک وَجَبَلِک، وَحَیثُ لایلْتَئِمُ النَّاسُ لِمَوَاضِعِهَا، وَلاَ یجْتَرِءُونَ عَلَیهَا، فَإِنَّهُمْ سِلْمٌ لاتُخَافُ بَائِقَتُهُ، وَصُلْحٌ لاتُخْشَی غَائِلَتُهُ. وَتَفَقَّدْ أُمُورَهُمْ بِحَضْرَتِک وَفِی حَوَاشِی بِلاَدِک. وَاعْلَمْ مَعَ ذَلِک أَنَّ فِی کثِیر مِنْهُمْ ضِیقاً فَاحِشاً، وَشُحّاً قَبِیحاً، وَاحْتِکاراً لِلْمَنَافِعِ، وَتَحَکماً فِی الْبِیاعَاتِ، وَذَلِک بَابُ مَضَرَّة لِلْعَامَّةِ، وَعَیبٌ عَلَی الْوُلاَةِ، فَامْنَعْ مِنَ الاِحْتِکارِ، فَإِنَّ رَسُولَ اللهِ صلی الله علیه وآله وسلم مَنَعَ مِنْهُ. وَلْیکنِ الْبَیعُ بَیعاً سَمْحاً: بِمَوَازِینِ عَدْل وَأَسْعَار لاتُجْحِفُ بِالْفَرِیقَینِ مِنَ الْبَائِعِ وَالْمُبْتَاعِ. فَمَنْ قَارَفَ حُکْرَةً بَعْدَ نَهْیک إِیاهُ فَنَکلْ بِهِ، وَعَاقِبْهُ فِی غَیرِ إِسْرَاف.


Kisha, kwanza jinasihi kuhusu wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda (kutunza kuhifadhi na kuimarisha) na pia uwaamuru wengine nao kufanya mema.

(Katika kunasihi huku) usitofautishe kati ya wafanyabiashara wanaoishi katika vituo vya biashara au wale wanaotembea na wanaozunguka, pamoja na watu wa viwanda na wafanyakazi (vibarua) wanaofanya kazi kwa nguvu zao za mwili, kwa sababu ndio vyanzo kuu vya manufaa (ya watu) na sababu ya utulivu (wa jamii) na utajiri wa biashara muhimu kutoka ardhi za mbali, kutoka jangwani na baharini na ardhi laini na mbaya ya mahali pa utawala wako na kutoka kwa maeneo ambayo umma kwa ujumla haujihusishi nayo.

Na (hata) hawana ujasiri wa kwenda huko, wanakusanyika, kwa sababu wao (wafanyabiashara na watengeneza vifaa) ni watu wenye afya nzuri ambao hawaogopi madhara na marafiki wa amani ambao hawana hofu ya usaliti na hila. Fuatilia na upange kazi zao, iwe ni walioko mbele yako (na kitovu cha ugavana wako) na wale wanaoishi katika pembe za nchi yako.

Na ujue! pamoja na hayo yote niliyosema, kuna idadi kubwa ya watu miongoni mwao wenye fikra finyu na ubakhili, wanalanguzi (wanaoficha bidhaa ili waje kuziuza kwa bei) suhula na vitu zinazohitajika na watu, na wasio na haki katika kuainisha bei, na hawa ndio sababu ya hasara kwa watu, aibu na fedheha kwa watawala.

Jiepusheni na ulanguzi (kuficha bidhaa) kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amekataza, na miamala ifanywe katika mazingira rahisi: Kwa vigezo uadilifu na kwa bei ambazo hazimdhuru muuzaji wala mnunuzi, na kila mtu ambaye atafanya ulanguzi baada ya wewe kukataza, muadhibu; lakini (kamwe) usichupe mipaka katika adhabu.


ثُمَّ اللهَ اللهَ فِی الطَّبَقَةِ السُّفْلَی مِنَ الَّذِینَ لاحِیلَةَ لَهُمْ، مِنَ الْمَسَاکینِ وَالْمُحْتَاجِینَ وَأَهْلِ الْبُؤْسَی وَالزَّمْنَی، فَإِنَّ فِی هَذِهِ الطَّبَقَةِ قَانِعاً وَمُعْتَرّاً، وَاحْفَظِ لِلَّهِ مَا اسْتَحْفَظَک مِنْ حَقِّهِ فِیهِمْ، وَاجْعَلْ لَهُمْ قِسْماً مِنْ بَیتِ مَالِک، وَقِسْماً مِنْ غَلاَّتِ صَوَافِی الْاِسْلاَمِ فِی کلِّ بَلَد، فَإِنَّ لِلْاَقْصَی مِنْهُمْ مِثْلَ الَّذِی لِلْاَدْنَی، وَکلٌّ قَدِ اسْتُرْعِیتَ حَقَّهُ; وَلاَ یشْغَلَنَّک عَنْهُمْ بَطَرٌ، فَإِنَّک لاتُعْذَرُ بِتَضْییعِک التَّافِهَ لاِِحْکامِک الْکثِیرَ الْمُهِمَّ. فَلاَ تُشْخِصْ هَمَّک عَنْهُمْ، وَلاَ تُصَعِّرْ خَدَّک لَهُمْ، وَتَفَقَّدْ أُمُورَ مَنْ لایصِلُ إِلَیک مِنْهُمْ مِمَّنْ تَقْتَحِمُهُ الْعُیونُ، وَتَحْقِرُهُ الرِّجَالُ; فَفَرِّغْ لاُِولَئِک ثِقَتَک مِنْ أَهْلِ الْخَشْیةِ وَالتَّوَاضُعِ، فَلْیرْفَعْ إِلَیک أُمُورَهُمْ، ثُمَّ اعْمَلْ فِیهِمْ بِالْاِعْذَارِ إِلَی اللهِ یوْمَ تَلْقَاهُ، فَإِنَّ هَؤُلاَءِ مِنْ بَینِ الرَّعِیةِ أَحْوَجُ إِلَی الْاِنْصَافِ مِنْ غَیرِهِمْ. وَکلٌّ فَأَعْذِرْ إِلَی اللهِ فِی تَأْدِیةِ حَقِّهِ إِلَیهِ. وَتَعَهَّدْ أَهْلَ الْیتْمِ وَذَوِی الرِّقَّةِ فِی السِّنِّ مِمَّنْ لاحِیلَةَ لَهُ وَلاَ ینْصِبُ لِلْمَسْأَلَةِ نَفْسَهُ، وَذَلِک عَلَی الْوُلاَةِ ثَقِیلٌ، وَالْحَقُّ کلُّهُ ثَقِیلٌ; وَقَدْ یخَفِّفُهُ اللهُ عَلَی أَقْوَام طَلَبُوا الْعَاقِبَةَ فَصَبَّرُوا أَنْفُسَهُمْ، وَوَثِقُوا بِصِدْقِ مَوْعُودِ اللهِ لَهُمْ.

Kisha (Imam (as) akasema:) Mtangulize Mwenyezi Mungu, mtangulize Mwenyezi Mungu kuhusu tabaka la chini la jamii; Wale ambao hawana suluhisho (hata kwa riziki rahisi). Hao ni masikini, mafakiri na wasiojiweza, na (tambua kwamba) katika tabaka hili, kundi moja linaridhika (na wanaridhika na walichopewa) na kundi jingine ni wale wanaohoji (na wakati mwingine kupinga dhidi ya msaada wanao pewa) (wanao) chunga kile ambacho Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuhusu haki yake kwao.

Watengee sehemu ya hazina ya Waislamu na sehemu ya nafaka ya falme za Kiislamu katika kila mji (na vitongoji) kwa sababu walio mbali wana fungu sawa na walio karibu, na wewe ndiye ambaye unawajibika kuheshimu haki za wote. Kamwe usiruhusu kiburi na ulevi wa uongozi wako kukufanya uwe na shughuli nyingi (na usikuzuie kuhudhuria kazi zao) kwa sababu hautasamehewa kuacha huduma ndogo kwa kisingizio cha mambo mengi na muhimu unayofanya.

Hupaswi kujitenga nao na kujiepusha nao (na kuwapuuza) na kulinganisha na matendo ya wale wasioweza kukufikia na watu wanawaangalia kwa jicho la dharau, (hata) watawala nao wanawaona kuwa ni wadogo (kwa uangalifu). Angalia na kwa hili, chagua mtu wa kuaminika (au watu) wanaomcha Mungu na mnyenyekevu ili kuripoti hali yao kwako.

Basi litendee kundi hili kwa namna ambayo Mola atakapokutana nawe (Siku ya Kiyama) atakubali udhuru wako, kwa sababu miongoni mwa watu, kundi hili linahitaji uadilifu zaidi, na kila mmoja wao lazima atoe udhuru na sababu mbele za Mungu kwa namna ambayo hata haki ya mtu mmoja isipotee.

Tunza kazi ya yatima na wazee wasiojiweza na hawawezi kunyoosha mikono yao kuomba msaada kwa watu, licha ya kuwa kufanya hili (kuhusiana na tabaka lisilojiweza na lenye kuhitaji) ni zito kwa watawala, lakini kutekeleza haki kwa hakika kote ni kuzito, na wakati mwengine Mwenyezi Mungu anaifanya kaumu kuwa jambo jepesi kuvumilia haki (kutokuwa zito jambo). Watu wanaotafuta hatima njema na wamezoea kusimama kidete na kushikamana na subira na wana uhakika katika ukweli wa ahadi za Mungu.


وَاجْعَلْ لِذَوِی الْحَاجَاتِ مِنْک قِسْماً تُفَرِّغُ لَهُمْ فِیهِ شَخْصَک، وَتَجْلِسُ لَهُمْ مَجْلِساً عَامّاً فَتَتَوَاضَعُ فِیهِ لِلَّهِ الَّذِی خَلَقَک، وَتُقْعِدُ عَنْهُمْ جُنْدَک وَأَعْوَانَک مِنْ أَحْرَاسِک وَشُرَطِک; حَتَّی یکلِّمَک مُتَکلِّمُهُمْ غَیرَ مُتَتَعْتِع، فَإِنِّی سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلی الله علیه و آله و سلم یقُولُ فِی غَیرِ مَوْطِن، لَنْ تُقَدَّسَ أُمَّةٌ لایؤْخَذُ لِلضَّعِیفِ فِیهَا حَقُّهُ مِنَ الْقَوِی غَیرَ مُتَتَعْتِع. ثُمَّ احْتَمِلِ الْخُرْقَ مِنْهُمْ وَالْعِی، وَنَحِّ عَنْهُمُ الضِّیقَ وَالْاَنَفَ یبْسُطِ اللهُ عَلَیک بِذَلِک أَکْنَافَ رَحْمَتِهِ، وَیوجِبْ لَک ثَوَابَ طَاعَتِهِ. وَأَعْطِ مَا أَعْطَیتَ هَنِیئاً، وَامْنَعْ فِی إِجْمَال وَإِعْذَار.


Kwa wale wanaokuhitaji, panga wakati kushughulikia mahitaji yao binafsi (na uso kwa uso) na kuwaandalia mkutano wa hadhara (na kuketi na kutatua matatizo yao) katika mkusanyiko huo kwa ajili ya Mungu aliyekuumba, uwe mnyenyekevu na waweke askari na wasaidizi wako wako mbali nao, wakiwemo walinzi na polisi, ili yeyote anayetaka kuzungumza nawe kwa uwazi na bila woga wala kigugumizi basi aweze kufanya hivyo, kwa sababu nimesikia kutoka kwa Mtume (saww) mara nyingi akisema hivi:

"Taifa ambalo haki ya wanyonge haijachukuliwa waziwazi kutoka kwa wenye nguvu haitauona kamwe uso wa utakatifu na usafi (na amani itatoweka kutoka kwao). Kisha wavumilie jeuri yao, hali yao ya kusuasua, na kutokuwa na uwezo wa kusema, na uondoe vikwazo vyovyote, mawazo finyu, na kiburi kwao (ili waweze kusema yaliyo mioyoni mwao).

Kwa kufanya hivi, Mungu atakunyooshea huruma yake na kukulipa kwa utii wake. Samehe kile unachosamehe kwa namna ambayo ni ya kupendeza (na bila majuto) na unapokataa kusamehe (kwa sababu yoyote), fanya hivyo ukiambatanisha na kauli ya huba na kuomba radhi.

ثُمَّ أُمُورٌ مِنْ أُمُورِک لابُدَّ لَک مِنْ مُبَاشَرَتِهَا: مِنْهَا إِجَابَةُ عُمَّالِک بِمَا یعْیا عَنْهُ کتَّابُک، وَمِنْهَا إِصْدَارُ حَاجَاتِ النَّاسِ یوْمَ وُرُودِهَا عَلَیک بِمَا تَحْرَجُ بِهِ صُدُورُ أَعْوَانِک. وَأَمْضِ لِکلِّ یوْم عَمَلَهُ، فَإِنَّ لِکلِّ یوْم مَا فِیهِ. وَاجْعَلْ لِنَفْسِک فِیمَا بَینَک وَبَینَ اللهِ أَفْضَلَ تِلْک الْمَوَاقِیتِ، وَأَجْزَلَ تِلْک الْاَقْسَامِ، وَإِنْ کانَتْ کلُّهَا لِلَّهِ إِذَا صَلَحَتْ فِیهَا النِّیةُ، وَسَلِمَتْ مِنْهَا الرَّعِیةُ.

Kisha (fahamu) kuna sehemu ya kazi yako ambayo wewe binafsi unatakiwa kuishughulikia (na hupaswi kuwaachia wengine), ikiwa ni pamoja na kuwajibu watendaji wa serikali pale ambapo makatibu hawawezi kuijibu, na nyingine ni kukidhi mahitaji ya watu katika Siku ile ile ambayo mahitaji na matakwa yao yanaripotiwa kwako na wasaidizi wako wana matatizo katika kuyashughulikia.

(Kuwa na akili) Fanya kazi za kila siku katika siku ile ile (na ufikirie kuhusu kesho) kwa sababu kila siku ina kazi yake (na ikiwa kazi ya siku nyingine itaongezwa kwake, itakuwa shida).

Na unapaswa kutenga nyakati bora na sehemu bora za maisha yako kwa ajili ya kunong’ona na Mungu, ingawa kazi yako yote ni ya Mungu ikiwa una nia safi na wahusika wanaishi kwa afya na amani kwa sababu hiyo.


وَلْیکنْ فِی خَاصَّةِ مَا تُخْلِصُ بِهِ لِلَّهِ دِینَک: إِقَامَةُ فَرَائِضِهِ الَّتِی هِی لَهُ خَاصَّةً، فَأَعْطِ اللهَ مِنْ بَدَنِک فِی لَیلِک وَنَهَارِک، وَوَفِّ مَا تَقَرَّبْتَ بِهِ إِلَی اللهِ مِنْ ذَلِک کامِلاً غَیرَ مَثْلُوم وَلاَ مَنْقُوص، بَالِغاً مِنْ بَدَنِک مَا بَلَغَ. وَإِذَا قُمْتَ فِی صَلاَتِک لِلنَّاسِ، فَلاَ تَکونَنَّ مُنَفِّراً وَلاَ مُضَیعاً، فَإِنَّ فِی النَّاسِ مَنْ بِهِ الْعِلَّةُ وَلَهُ الْحَاجَةُ. وَقَدْ سَأَلْتُ رَسُولَ اللهِ(صلی الله علیه وآله)حِینَ وَجَّهَنِی إِلَی الْیمَنِ کیفَ أُصَلِّی بِهِمْ؟ فَقَالَ: صَلِّ بِهِمْ کصَلاَةِ أَضْعَفِهِمْ وَکنْ بِالْمُؤْمِنِینَ رَحِیماً.

Moja ya mambo unayopaswa kuyafanya kwa ajili ya ikhlasi ya dini yako kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kutekeleza ibada ambazo ni makhsusi kwa dhati yake safi, basi ziache nguvu zako za kimwili kwa Mwenyezi Mungu mchana na usiku na fanya yale yanayokukurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Fanya kwa ukamilifu na bila mapungufu, hata kama hilo litasababisha uchovu mwingi wa mwili, na unaposimama kwa ajili ya kuwaswalisha watu Sala ya Jamaa (isiwe ndefu) kiasi cha kuwafanya watu waichukie, na isiwe (ya haraka) kiasi cha kufanya ivunje faradhi za Swala (nguzo za wajibu katika Sala), kwa sababu miongoni mwa watu (wanaosimama na wewe katika Sala) kuna wagonjwa au wenye mahitaji ya dharura. Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliponituma Yemen: Je, nisali nao vipi? Akasema: Sali pamoja nao Sala iliyo kama ya walio dhaifu miongoni mwao, na kuwa na huruma kwa Waumini.

وَأَمَّا بَعْدُ فَلاَ تُطَوِّلَنَّ احْتِجَابَک عَنْ رَعِیتِک، فَإِنَّ احْتِجَابَ الْوُلاَةِ عَنِ الرَّعِیةِ شُعْبَةٌ مِنَ الضِّیقِ، وَقِلَّةُ عِلْم بِالْاُمُورِ; وَالاِحْتِجَابُ مِنْهُمْ یقْطَعُ عَنْهُمْ عِلْمَ مَا احْتَجَبُوا دُونَهُ فَیصْغُرُ عِنْدَهُمُ الْکبِیرُ، وَیعْظُمُ الصَّغِیرُ، وَیقْبُحُ الْحَسَنُ، وَیحْسُنُ الْقَبِیحُ وَیشَابُ الْحَقُّ بِالْبَاطِلِ. وَإِنَّمَا الْوَالِی بَشَرٌ لایعْرِفُ مَا تَوَارَی عَنْهُ النَّاسُ بِهِ مِنَ الْاُمُورِ، وَلَیسَتْ عَلَی الْحَقِّ سِمَاتٌ تُعْرَفُ بِهَا ضُرُوبُ الصِّدْقِ مِنَ الْکذِبِ، وَإِنَّمَا أَنْتَ أَحَدُ رَجُلَینِ: إِمَّا امْرُؤٌ سَخَتْ نَفْسُک بِالْبَذْلِ فِی الْحَقِّ، فَفِیمَ احْتِجَابُک مِنْ وَاجِبِ حَقّ تُعْطِیهِ، أَوْ فِعْل کرِیم تُسْدِیهِ! أَوْ مُبْتَلًی بِالْمَنْعِ، فَمَا أَسْرَعَ کفَّ النَّاسِ عَنْ مَسْأَلَتِک إِذَا أَیسُوا مِنْ بَذْلِک! مَعَ أَنَّ أَکْثَرَ حَاجَاتِ النَّاسِ إِلَیک مِمَّا لامَئُونَةَ فِیهِ عَلَیک، مِنْ شَکاةِ مَظْلِمَة، أَوْ طَلَبِ إِنْصَاف فِی مُعَامَلَة.


Na baada ya (amri hii), kamwe usijifiche kwa raia kwa muda mrefu, kwa sababu watawala kukaa siri machoni pa raia husababisha aina fulani ya ukosefu wa elimu juu ya mambo (ya watu na nchi) na huwafanya kutofahamu yale ambayo wamejificha kwayo, matokeo yake, masuala makubwa huwa madogo machoni mwao na mambo madogo huwa makubwa machoni mwao, kazi nzuri hunekana kuwa mbaya na kazi mbaya huonekana kuwa nzuri; na haki na batili huchanganyikana. (Na kwa hakika mpango muhimu wa mambo ya nchi hauwezekani katika hali kama hiyo) kwa sababu mkuu wa gavana ni binadamu tu, hajui mambo ambayo watu wanamficha, na haki sio kila wakati ina ishara ya wazi, na si mara zote inawezekana kuona "uaminifu" katika nyuso tofauti za "Uongo" na wakati huo wewe hautakuuwa nje ya hali mbili: Ama wewe ni mtu ambaye uko tayari kuwa mkarimu na  na kutoa katika njia ya haki, kwa hivyo hakuna sababu ya wewe kujificha na kukataa kutoa haki ya faradhi, na kuacha kitendo cha ukarimu unachopaswa kufanya, au wewe ni mtu bahili na mwenye fikra finyu uko hivi (watu wakikuona na kutambua sifa hii ndani yako) watakatishwa tamaa na ukarimu wako. Fauka ya hayo, matamanio mengi ya watu hayakugharimu chochote; kama vile kulalamikia uonevu au kuomba haki katika mabadalishano ya kibiashara.

ثُمَّ إِنَّ لِلْوَالِی خَاصَّةً وَبِطَانَةً، فِیهِمُ اسْتِئْثَارٌ وَتَطَاوُلٌ، وَقِلَّةُ إِنْصَاف فِی مُعَامَلَة، فَاحْسِمْ مَادَّةَ أُولَئِک بِقَطْعِ أَسْبَابِ تِلْک الْاَحْوَالِ. وَلاَ تُقْطِعَنَّ لاَِحَد مِنْ حَاشِیتِک وَحَامَّتِک قَطِیعَةً، وَلاَ یطْمَعَنَّ مِنْک فِی اعْتِقَادِ عُقْدَة، تَضُرُّ بِمَنْ یلِیهَا مِنَ النَّاسِ، فِی شِرْب أَوْ عَمَل مُشْتَرَک، یحْمِلُونَ مَؤُونَتَهُ عَلَی غَیرِهِمْ، فَیکونَ مَهْنَأُ ذَلِک لَهُمْ دُونَک، وَعَیبُهُ عَلَیک فِی الدُّنْیا وَالآْخِرَةِ. وَأَلْزِمِ الْحَقَّ مَنْ لَزِمَهُ مِنَ الْقَرِیبِ وَالْبَعِیدِ، وَکنْ فِی ذَلِک صَابِرا مُحْتَسِباً، وَاقِعاً ذَلِک مِنْ قَرَابَتِک وَخَاصَّتِک حَیثُ وَقَعَ، وَابْتَغِ عَاقِبَتَهُ بِمَا یثْقُلُ عَلَیک مِنْهُ، فَإِنَّ مَغَبَّةَ ذَلِک مَحْمُودَةٌ. وَإِنْ ظَنَّتِ الرَّعِیةُ بِک حَیفاً فَأَصْحِرْ لَهُمْ بِعُذْرِک، وَاعْدِلْ عَنْک ظُنُونَهُمْ بِإِصْحَارِک، فَإِنَّ فِی ذَلِک رِیاضَةً مِنْک لِنَفْسِک، وَرِفْقاً بِرَعِیتِک، وَإِعْذَاراً تَبْلُغُ بِهِ حَاجَتَک مِنْ تَقْوِیمِهِمْ عَلَی الْحَقِّ.

(Pamoja na hayo) mtawala ana watu maalum na wenye siri (na watu wa karibu na wanaowazunguka) wenye ubinafsi na wanaotafuta ubora na wasiozingatia uadilifu na usawa katika kuamiliana na watu. Ng'oa mzizi wa dhulma yao kwa kuikata njia yake, na kamwe usimpe rafiki yako na wafuasi wako ardhi kutoka katika ardhi za Waislamu, na wasiwe na pupa ya kuingia mkataba kwa manufaa yao ambao utasababisha madhara kwa majirani wa ardhi hiyo; iwe katika umwagiliaji au kazi nyingine ya pamoja. Kwa namna ambayo wanawawekea wengine gharama zake, na matokeo yake faida yake ni kwao tu, na kasoro zake na fedheha yake duniani na Akhera ni yako. Iwapo ni kutoka kwa jamaa zako au la, subiri juu yake na uiweke katika hisabu ya Mwenyezi Mungu (na umuombe ujira wake), ijapokuwa hilo litaleta shinikizo kwa jamaa zako na marafiki zako wa karibu, kubali uzito wa kazi hii, kwa sababu mwisho wake ni wa kupendeza, na kila inapotokea raia wana dhana ya wewe kutofanya uadilifu (rekebisha kile kilichopelekea dhana mbaya) kwa sababu kwa upande mmoja, hii itapelekea malezi ya maadili (akhlaq) yako, na kwa upande mwingine, ni urafiki na wema kwa raia, na itakufanya ueleze udhuru wako kwa madhumuni yako, ambayo ni kuwalazimisha kufanya jambo la haki.


وَلاَ تَدْفَعَنَّ صُلْحاً دَعَاک إِلَیهِ عَدُوُّک وَلِلَّهِ فِیهِ رِضًی فَإِنَّ فِی الصُّلْحِ دَعَةً لِجُنُودِک، وَرَاحَةً مِنْ هُمُومِک، وَأَمْناً لِبِلاَدِک، وَلَکنِ الْحَذَرَ کلَّ الْحَذَرِ مِنْ عَدُوِّک بَعْدَ صُلْحِهِ، فَإِنَّ الْعَدُوَّ رُبَّمَا قَارَبَ لِیتَغَفَّلَ فَخُذْ بِالْحَزْمِ، وَاتَّهِمْ فِی ذَلِک حُسْنَ الظَّنِّ. وَإِنْ عَقَدْتَ بَینَک وَبَینَ عَدُوِّک عُقْدَةً، أَوْ أَلْبَسْتَهُ مِنْک ذِمَّةً، فَحُطْ عَهْدَک بِالْوَفَاءِ، وَارْعَ ذِمَّتَک بِالْاَمَانَةِ، وَاجْعَلْ نَفْسَک جُنَّةً دُونَ مَا أَعْطَیتَ، فَإِنَّهُ لَیسَ مِنْ فَرَائِضِ اللهِ شَیءٌ النَّاسُ أَشَدُّ عَلَیهِ اجْتِمَاعاً، مَعَ تَفَرُّقِ أَهْوَائِهِمْ، وَتَشَتُّتِ آرَائِهِمْ، مِنْ تَعْظِیمِ الْوَفَاءِ بِالْعُهُودِ. وَقَدْ لَزِمَ ذَلِک الْمُشْرِکونَ فِیمَا بَینَهُمْ دُونَ الْمُسْلِمِینَ لِمَا اسْتَوْبَلُوا مِنْ عَوَاقِبِ الْغَدْرِ; فَلاَ تَغْدِرَنَّ بِذِمَّتِک، وَلاَ تَخِیسَنَّ بِعَهْدِک، وَلاَ تَخْتِلَنَّ عَدُوَّک، فَإِنَّهُ لایجْتَرِئُ عَلَی اللهِ إِلاَّ جَاهِلٌ شَقِی. وَقَدْ جَعَلَ اللهُ عَهْدَهُ وَذِمَّتَهُ أَمْناً أَفْضَاهُ بَینَ الْعِبَادِ بِرَحْمَتِهِ، وَحَرِیماً یسْکنُونَ إِلَی مَنَعَتِهِ، وَیسْتَفِیضُونَ إِلَی جِوَارِهِ، فَلاَ إِدْغَالَ وَلاَ مُدَالَسَةَ وَلاَ خِدَاعَ فِیهِ، وَلاَ تَعْقِدْ عَقْداً تُجَوِّزُ فِیهِ الْعِلَلَ، وَلاَ تُعَوِّلَنَّ عَلَی لَحْنِ قَوْل بَعْدَ التأکید وَالتَّوْثِقَةِ وَلاَ یدْعُوَنَّک ضِیقُ أَمْر، لَزِمَک فِیهِ عَهْدُ اللهِ، إِلَی طَلَبِ انْفِسَاخِهِ بِغَیرِ الْحَقِّ، فَإِنَّ صَبْرَک عَلَی ضِیقِ أَمْر تَرْجُو انْفِرَاجَهُ وَفَضْلَ عَاقِبَتِهِ، خَیرٌ مِنْ غَدْر تَخَافُ تَبِعَتَهُ، وَأَنْ تُحِیطَ بِک مِنَ اللهِ فِیهِ طِلْبَةٌ، لاتَسْتَقْبِلُ فِیهَا دُنْیاک وَلاَ آخِرَتَک.

Kamwe usikatae sulhu (mapatano) inayopendekezwa na adui na radhi ya Mungu iko ndani yake, kwa sababu katika sulhu kunaliletea utulivu jeshi lako (na sababu ya kujadidisha nguvu/kujikusanya na kujiimarisha tena) na kwako mwenyewe ni chanzo cha utulivu kutoka katika ghamu na huzuni na kuuiletea usalama nchi yako; akini jihadhari sana na adui yako baada ya kufanya mapatano ya amani naye, kwa sababu adui wakati mwingine anakaribia ili kukushtukiza, kwa hivyo kuwa mtazamo wa wa upeo wa mbali na uweke kando mtazamo mzuri katika kesi hii.

Na ikiwa umefanya mapatano baina yako na adui yako, au ukamfunika nguo ya usalama (na ukampa hifadhi), basi timiza ahadi yako na uheshimu mkataba wako, na ulinde maisha yake dhidi ya ahadi zako, kwa sababu hakuna wajibu wa Mwenyezi Mungu kama kuheshimu "kutekeleza ahadi" na watu wa ulimwengu licha ya tofauti zao zote za maoni, lakini wanakubaliana juu yake. Hata washirikina wa zama za ujahilia waliitunza na kuiheshimu kwa Waislamu, kwa sababu walikuwa wamepatwa na matokeo machungu ya kuvunja ahadi. Kwa hiyo, kamwe usivunje ahadi (agano) na usifanye khiyana agano lako na ukamdanganya adui yako, kwa sababu hakuna yeyote isipokuwa mtu mjinga na muovu kabisa anayefanya hilo mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mungu, kwa rehema Zake, amefanya agano lililofungwa kwa jina lake kuwa ni faraja kwa waja wake na mahali pa usalama pa kukimbilia na kuitumia kufanya kazi yao, kwa hiyo haikubaliki uharibifu, udanganyifu wala hila katika ahadi na mapatano.

(Mbali na haya) kamwe usiingie mapatano ambamo ndani yake kuna ibara zina nafasi ya matatizo (na utumiaji mbaya wa adui), (kama ambavyo katika hati ya makubaliano haipasi kuweko ibara  ambazo adui atazitumia vibayaa), wewe pia baada ya msisitizo na masharti yenye nguvu ya agano, usiegemee katika baadhi ya ibara dhaifu na zilizo hatarini kuvunja agano, na kamwe kuwa katika shida na mbinyo kutokana na matakwa ya agano la Kimungu kusikulazimishe kuvuunja mkataba kwa njia isiyo ya haki, kwa sababu subira yako katika dhiki ya mapatano, ambayo (kwa rehema ya Mwenyezi Mungu) ina matumaini ya kufungua na kushinda mwisho wake, ni bora kuliko kuvunja mapatano na kufanya khiyana ambayo kwayo unaiogopa adhabu. Uvunjaji huo huo wa mkataba unasababisha uwajibikaji wa ki-Mungu ambao huwezi kuwajibika (kutoa majibu) si hapa duniani wala kesho akhera.


إِیاک وَ الدِّمَاءَ وَسَفْکهَا بِغَیرِ حِلِّهَا، فَإِنَّهُ لَیسَ شَیءٌ أَدْنَی لِنِقْمَة، وَلاَ أَعْظَمَ لِتَبِعَة، وَ لاَأَحْرَی بِزَوَالِ نِعْمَة، وَانْقِطَاعِ مُدَّة، مِنْ سَفْک الدِّمَاءِ بِغَیرِ حَقِّهَا. وَاللهُ سُبْحَانَهُ مُبْتَدِئٌ بِالْحُکْمِ بَینَ الْعِبَادِ، فِیمَا تَسَافَکوا مِنَ الدِّمَاءِ یوْمَ الْقِیامَةِ; فَلاَ تُقَوِّینَّ سُلْطَانَک بِسَفْک دَم حَرَام، فَإِنَّ ذَلِک مِمَّا یضْعِفُهُ وَیوهِنُهُ، بَلْ یزِیلُهُ وَینْقُلُهُ. وَلاَ عُذْرَ لَک عِنْدَ اللهِ وَلاَ عِنْدِی فِی قَتْلِ الْعَمْدِ، لاَِنَّ فِیهِ قَوَدَ الْبَدَنِ. وَإِنِ ابْتُلِیتَ بِخَطَإ وَأَفْرَطَ عَلَیک سَوْطُک أَوْ سَیفُک أَوْ یدُک بِالْعُقُوبَةِ; فَإِنَّ فِی الْوَکْزَةِ فَمَا فَوْقَهَا مَقْتَلَةً، فَلاَ تَطْمَحَنَّ بِک نَخْوَةُ سُلْطَانِک عَنْ أَنْ تُؤَدِّی إِلَی أَوْلِیاءِ الْمَقْتُولِ حَقَّهُمْ.

Epuka kabisa kumwaga damu kwa njia isiyo ya haki, kwa sababu hakuna kitu kinachokaribia kusababisha kisasi cha kimungu na adhabu kali zaidi, kuharakisha kupungua kwa baraka na kukomesha serikali, kama kumwaga damu kwa njia isiyo ya haki. Katika mahakama ya Siku ya Kiyama, Mungu Mwenyezi kwanza atahukumu kati ya waja wake kuhusu damu iliyomwagika, hivyo kamwe usiimarishe serikali na uongozi wako kwa kumwaga damu iliyoharamishwa kumwagwa, kwa sababu kitendo hiki kinadhoofisha misingi ya serikali au huihamisha kwa wengine, na hakuna kisingizio chochote kinachokubaliwa na Mungu au mimi kwa mauaji ya kukusudia. Na adhabu ya hilo ni kisasi, na ikiwa umehusika katika kuua bila haki na ukamuadhibu mtu kwa mjeledi au upanga wako au (hata) mkono wako, kwa sababu inawezekana kumuua mtu hata kwa ngumi moja au zaidi, basi usiruhusu kiburi cha uongozi wako kikuzuie kutekeleza haki ya ndugu aliyeuawa (na kupata ridhaa kutoka kwao).


وَإِیاک وَالْاِعْجَابَ بِنَفْسِک، وَالثِّقَةَ بِمَا یعْجِبُک مِنْهَا، وَحُبَّ الْاِطْرَاءِ، فَإِنَّ ذَلِک مِنْ أَوْثَقِ فُرَصِ الشَّیطَانِ فِی نَفْسِهِ لِیمْحَقَ مَا یکونُ مِنْ إِحْسَانِ الْمُحْسِنِینَ. وَإِیاک وَالْمَنَّ عَلَی رَعِیتِک بِإِحْسَانِک، أَوِ التَّزَیدَ فِیمَا کانَ مِنْ فِعْلِک، أَوْ أَنْ تَعِدَهُمْ فَتُتْبِعَ مَوْعِدَک بِخُلْفِک، فَإِنَّ الْمَنَّ یبْطِلُ الْاِحْسَانَ، وَالتَّزَیدَ یذْهَبُ بِنُورِ الْحَقِّ، وَالْخُلْفَ یوجِبُ الْمَقْتَ عِنْدَ اللهِ وَالنَّاسِ. قَالَ اللهُ تَعَالَی: (کبُرَ مَقْتاً عِنْدَ اللهِ أَنْ تَقُولُوا ما لاتَفْعَلُونَ). وَإِیاک وَالْعَجَلَةَ بِالْاُمُورِ قَبْلَ أَوَانِهَا، أَوِ التَّسَقُّطَ فِیهَا عِنْدَ إِمْکانِهَا، أَوِ اللَّجَاجَةَ فِیهَا إِذَا تَنَکرَتْ، أَوِ الْوَهْنَ عَنْهَا إِذَا اسْتَوْضَحَتْ، فَضَعْ کلَّ أَمْر مَوْضِعَهُ، وَأَوْقِعْ کلَّ أَمْر مَوْقِعَهُ.

Jiepusheni na kujiona, kutegemea nguvu zako, na kupenda kuzidisha sifa zako (kutia chumvi), kwani sifa hizo ni miongoni mwa fursa za uhakika za shetani kufuta na kuharibu na kuangamiza amali za watu wema.

Epuka kufanyia masimbulizi (masimango) raia wako wakati wa wema, na (pia) jizuie kuhesabu zaidi ya uliyoyafanya, na pia jihadhari na kuwatolea ahadi kisha kuzivunja, kwa sababu masimbulizi yanabatilisha wema, kukuza neema kunaondoa nuru ya haki,  kuvunja ahadi husababisha hasira ya Mungu na watu; Mwenyezi Mungu anasema: "Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda", epuka kufanya haraka katika mambo ambayo bado hayajatokea, na epuka kulegeza kamba katika mambo ambayo nazingira yake yya kufanyika yamejitokeza, jiepusha kufanya ukaidi (kutoambilika) katika mambo yasiyofahamika na jihadhari kuwa dhhaifu waakati yatakapofahamika. (Ndiyo) Fanya kila kitu kwa mahali pake na kila kitu kwa wakati wake.


وَإِیاک وَالاِسْتِئْثَارَ بِمَا النَّاسُ فِیهِ أُسْوَةٌ، وَالتَّغَابِی عَمَّا تُعْنَی بِهِ مِمَّا قَدْ وَضَحَ لِلْعُیونِ، فَإِنَّهُ مَأْخُوذٌ مِنْک لِغَیرِک. وَعَمَّا قَلِیل تَنْکشِفُ عَنْک أَغْطِیةُ الْاُمُورِ، وَینْتَصَفُ مِنْک لِلْمَظْلُومِ امْلِکْ حَمِیةَ أَنْفِک، وَسَوْرَةَ حَدِّک، وَسَطْوَةَ یدِک وَغَرْبَ لِسَانِک، وَاحْتَرِسْ مِنْ کلِّ ذَلِک بِکفِّ الْبَادِرَةِ، وَتأخیر السَّطْوَةِ حَتَّی یسْکنَ غَضَبُک فَتَمْلِک الاِخْتِیارَ: وَلَنْ تَحْکمَ ذَلِک مِنْ نَفْسِک حَتَّی تُکْثِرَ هُمُومَک بِذِکْرِ الْمَعَادِ إِلَی رَبِّک.

Epuka kujitafutia upendeleo katika yale ambayo watu wako sawa, na jihadhari na uzembe katika kufanya yale yanayokuhusu na yako wazi mbele ya macho ya watu, kwa sababu kwa vyovyote vile unawajibika mbele ya watu kwa hilo na hivi karibuni pazia la kazi zako litafunuliwa na kisasi cha mdhulumiwa kitalipizwa kwako. Wakati wa hasira, jizuie na upunguze ukali wako, nguvu ya mkono wako, na jeuri ya ulimi wako, na ili kuepuka mambo haya ya kufanya vitendo vya haraka na maneno yasiyofikiriwa na kuchukua adhabu, kuwa mwangalifu, ili hasira yako ipungue na wewe mwenyewe hutaweza kuwa mtawala katika uwanja huu isipokuwa ukikumbuka Kiyama na kurudi kwa Mungu wako.


وَالْوَاجِبُ عَلَیک أَنْ تَتَذَکرَ مَا مَضَی لِمَنْ تَقَدَّمَک مِنْ حُکومَة عَادِلَة، أَوْ سُنَّة فَاضِلَة، أَوْ أَثَر عَنْ نَبِینَا صَلَّی اللهِ عَلَیهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ أَوْ فَرِیضَة فِی کتَابِ اللهِ، فَتَقْتَدِی بِمَا شَاهَدْتَ مِمَّا عَمِلْنَا بِهِ فِیهَا، وَتَجْتَهِدَ لِنَفْسِک فِی اتِّبَاعِ مَا عَهِدْتُ إِلَیک فِی عَهْدِی هَذَا، وَاسْتَوْثَقْتُ بِهِ مِنَ الْحُجَّةِ لِنَفْسِی عَلَیک، لِکیلاَ تَکونَ لَک عِلَّةٌ عِنْدَ تَسَرُّعِ نَفْسِک إِلَی هَوَاهَا. وَأَنَا أَسْأَلُ اللهَ بِسَعَةِ رَحْمَتِهِ، وَعَظِیمِ قُدْرَتِهِ عَلَی إِعْطَاءِ کلِّ رَغْبَة، أَنْ یوَفِّقَنِی وَإِیاک لِمَا فِیهِ رِضَاهُ مِنَ الْاِقَامَةِ عَلَی الْعُذْرِ الْوَاضِحِ إِلَیهِ وَإِلَی خَلْقِهِ، مَعَ حُسْنِ الثَّنَاءِ فِی الْعِبَادِ، وَجَمِیلِ الْاَثَرِ فِی الْبِلاَدِ، وَتَمَامِ النِّعْمَةِ وَتَضْعِیفِ الْکرَامَةِ، وَأَنْ یخْتِمَ لِی وَلَک بِالسَّعَادَةِ وَالشَّهَادَةِ، إِنّا إِلَیهِ راجِعُونَ. وَالسَّلاَمُ عَلَی رَسُولِ اللهِ صَلَّی اللهِ عَلَیهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ الطَّیبِینَ الطَّاهِرِینَ، وَسَلَّمَ تَسْلِیماً کثِیراً، وَالسَّلاَمُ.

Ni wajibu kwako daima kuzikumbuka serikali za uadilifu zilizokuwa kabla yako, pamoja na mila au matendo mema yaliyoshuka kutoka kwa Mtume (saww). Zingatia wajibu uliotajwa katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na ufuate yale uliyoyaona katika vitendo vyetu katika serikali, na pia ni wajibu kwako kufanya kila uwezalo katika kufuata yaliyomo. Nimekunasihi ufuate yaliyomo katika barua hii, na nimetimiza hoja yangu kwako ili nafsi yako ya uasi ishindwe, hautakuwa na udhuru mbele yangu. Ninamuomba Mwenyezi Mungu, kwa rehema hiyo kubwa na uwezo mkubwa anao tupa kila analotaka, atufanikishe mimi na wewe, ili tuweze kupata radhi Zake kwa kufanya mambo yanayotupa udhuru kutoka kwake na kwa viumbe vyake, sambamba na sifa na jina zuri miongoni mwa waja na matendo mema katika miji yote na (pia naomba) atimize baraka zake (juu yangu na wewe) na azidishie utukufu wake.

Na ninamuomba (Mwenyezi mwenye adhama) aufikishe mwisho uhai wangu na wako kwa furaha na kufa shahidi, ambaye Kwake sote tutarejea na Swala za Mwenyezi Mungu zimshukie Mtume Wake pamoja na Maimamu watoharifuu katika Aali zake na salamu kamili nyingi mno.