Barua ya Imam Ali kwa Sahl bin Hunaif

Barua ya Imam Ali kwa Sahl bin Hunaif (Kiarabu: رسالة الإمام علي إلى سهل بن حنيف) Barua ya Imam Ali kwa Sahl bin Hunaif ni miongoni mwa barua zake mashuhuri kwa watu mbali mbali. Barua hii aliiandika ili kumliwaza Hunaif baada ya baadhi ya wafuasi wa Sahl bin Hunaif kumwacha mkono Imamu Ali (a.s) na kujiunga na Mu’awiya. [1] Hii barua ya Imam Ali (a.s) ya kwa ajili ya Sahl, aliyekuwa gavana wake katika mji wa Madina, alaiyoiandika akimhimiza Sahl kutohuzunika kutokana na kuondoka kwa baadhi ya watu wa Madina kwenda kuungana na Mu’awiyah. Alibainisha kuwa watu hao hawakujiunga na Mu’awiya kwa sababu ya kutafuta uadilifu au haki, bali walivutwa na tamaa ya mali mapambo ya kidunia na hatimae wakapotea na kutumbukia katika upotovu. [2]
Sahl bin Hunaif alikuwa ni miongoni mwa Masahaba wa Mtume (s.a.w.w), na alikuwa ni mmoja wa magavana wa Imamu Ali (a.s), aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo huko Madina. [3] Aidha, alihesabiwa kuwa mmoja wa Shurtat al-Khamis, kikundi cha wapiganaji waaminifu wa Imam Ali (a.s), waliokuwa pamoja na Imamu Ali (a.s) katika uongozi wake. [4]
Barua hii ni miongoni mwa nyaraka zilizotatwa tajwa katika vyanzo mbalimbali vya Kiislamu vya madhehebu ya Shia pamoja na Sunni. Hata hivyo, matini iliyotolewa na Sayyid Radhiyy katika kitabu Nahju Al-Balagha, inatofautiana kidogo na ile iliyosimuliwa na Baladhuri, ambaye ni mwana historia wa karne ya tatu Hijria, aliye nukuu matini hiyo katika chake Ansab al-Ashraf. [5] Na pia matini hiyo iliomo katika Nahju Al-Balagha, kwa kiasi fulani inatofautiana na ile ya Ya’qubi ilioko katika Tareekh Ya’qubi. Katika toleo la Ibnu Maitham, barua hii inashika nafasi 69, [6] miongoni mwa barua zilizoorotheshwa kitabuni humo, wakati katika matoleo ya Ibn Abi al-Hadid, [7] Allama Majlisi, [8] Muhammad Abduh, [9] Subhi Saleh na Faidh al-Islam, [10] imeorodheshwa kama ni barua namba 70 miongoni mwa barua zake (a.s). [11]
Matini ya Barua kwa Kiarabu na Tafsiri ya Kiswahili
من كتاب له ع إلى سهل بن حنيف الأنصاری و هو عامله على المدينة فی معنى قوم من أهلها لحقوا بمعاوية
أَمَّا بَعْدُ فَقَدْ بَلَغَنِي أَنَّ رِجَالًا مِمَّنْ قِبَلَكَ يَتَسَلَّلُونَ إِلَى مُعَاوِيَةَ فَلَا تَأْسَفْ عَلَى مَا يَفُوتُكَ مِنْ عَدَدِهِمْ وَ يَذْهَبُ عَنْكَ مِنْ مَدَدِهِمْ.
فَكَفَى لَهُمْ غَيّاً وَ لَكَ مِنْهُمْ شَافِياً فِرَارُهُمْ مِنَ الْهُدَى وَ الْحَقِّ وَ إِيضَاعُهُمْ إِلَى الْعَمَى وَ الْجَهْلِ فَإِنَّمَا هُمْ أَهْلُ دُنْيَا مُقْبِلُونَ عَلَيْهَا وَ مُهْطِعُونَ إِلَيْهَا.
وَ قَدْ عَرَفُوا الْعَدْلَ وَ رَأَوْهُ وَ سَمِعُوهُ وَ وَعَوْهُ وَ عَلِمُوا أَنَّ النَّاسَ عِنْدَنَا فِي الْحَقِّ أُسْوَةٌ فَهَرَبُوا إِلَى الْأَثَرَةِ فَبُعْداً لَهُمْ وَ سُحْقاً إِنَّهُمْ وَ اللَّهِ لَمْ [يَفِرُّوا] يَنْفِرُوا مِنْ جَوْرٍ وَ لَمْ يَلْحَقُوا بِعَدْلٍ.
وَ إِنَّا لَنَطْمَعُ فِي هَذَا الْأَمْرِ أَنْ يُذَلِّلَ اللَّهُ لَنَا صَعْبَهُ وَ يُسَهِّلَ لَنَا حَزْنَهُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ وَ السَّلَام
Mingoni mwa Barua za Imam Ali (a.s) kwa Sahl bin Hunaif Al-Ansari, aliyekuwa gavana wake wa Madina, aliyoiandika kuhusiana na baadhi ya watu wa Madina walioungana na Mu’awiya.
Amma baad (ama baada ya hayo), kwa kweli nimepata habari kwama; baadhi ya watu walioko upande wako wanatoroka kutoka kwako kwa siri na kuungana Mu’awiah. Basi, usihuzunike kwa kupoteza idadi yao wala kwa kukosa msaada wao.
Basi yawatosha wao kupotea, na kule kukimbia kwao kutoka kwenye uongofu na ukweli na kuelekea kwao upofu na ujinga ni faraja kwako wewe, hii ni kwa sababu wao ni watu wa kidunia wanaokimbilia (dunia hiyo) na kuitafuta kwa hamu kubwa.
Na hakika wameujua uadilifu (uko wapi), wameuona, wameusikia, na wameuelewa, na wamejua fika kwamba; sisi katika suala la haki, huwaangali watu wote kwa jicho la sawa (bila ubaguzi). Basi wao (baada ya yote hayo) wakaamua kukimbilia kwenye ubinafsi. Basi watokomea mtokomeo ulioje, na waingia kwenye upotevu! Naapa kwa Mungu, kwamba wao hawakukimbia udhalimu, wala hawakuandamana na uadilifu.
Na hakika, tunatarajia katika jambo hili kwamba; Inshalla Mwenye Ezi Mungu atatuwepesishia ugumu wake na kuturahisisha masumbuko yetu kutokana huzuni zilizosababishwa na jambon hili, amani.