Nenda kwa yaliyomo

Balagha Al-ulaa Bikamaalihi

Kutoka wikishia

Balagha Al-‘ulaa Bikamaalihi (Kiarabu: بَلَغَ العُلیٰ بِکَمالِه) ni shairi maarufu lililoandikwa na mwanamshairi mashuhuri wa Kifarsi, Sa’adi Shirazi, linalomsifu kwa dhati Mtume Muhammad (s.a.w.w.w). Shairi hili la kipekee, limeandikwa kwa lugha ya Kiarabu, na linapatikana katika utangulizi wa kitabu chake maarufu, Gulistan (Golestan au Golastan), ambacho ni hazina maaruu ya hekima na mafunzo ya maisha. Katika ubeti wa kwanza, Saadi anamwelezea Mtume Muhammad (s.a.w.w.w) kama ni kiumbe aliyefikia ukamilifu wa hali ya juu zaidi, na kwa nuru yake, amelitakasa na kulifuta giza lote ulimwenguni. Hili linaashiria uwezo wa kipekee wa bwana Mtume (s.a.w.w.w) katika kuleta mwanga wa ukweli na uadilifu katika dunia iliyokuwa imegubikwa na giza la ujinga na dhulma. Katika ubeti wa pili, Sa’adi anaendelea kumsifu bwana Mtume (s.a.w.w.w) kwa ufasaha alio nao, akisisitiza kuwa sifa zote nzuri na kamilifu zinapatikana kwake yeye. Hatimae Anahitimisha ushairi wake kwa kumwombea Mtume Muhammad (s.a.w.w.w) na familia yake tukufu rehema na baraka za Mwenye Ezi Mungu, akionyesha heshima na upendo wake kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.w) na familia yake, na nafasi yake ya kipekee katika jamii za Kiislamu na ulimwengu mzima. Shairi hili ni dogo mno, ila ni shairi linaloelezea kwa kina hadhi na sifa za Mtume Muhammad (s.a.w.w.w), nalo ni miongoni mwa mashairi yanayo tumika mara kwa mara katika muktadha wa kuonyesha mapenzi na heshima kwa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w.w). Golestan ni kielelezo cha juu cha urithi wa fasihi karika lugha ya Kiajemi, na ni miomngoni mwa vitabu vipendwavo mno mbele ya jamii zitumiazo lugha ya Kifarsi.

Shairi la (بلغ العلی بکماله) linajulikana na kutambuliwa kama ni moja ya tungo bora za Saadi Shirazi. Watafiti wa fasihi wamebaini kwamba, katika shairi hili pamoja na mashairi mengine ya Sa’adi, kuna dalili za wazi za kumbukumbu na heshima kwa Ahlul-Bait (a.s), jambo ambalo linaonesha mwelekeo wake wa Kishia. Kwa Sa’adi, shairi hili hawakilishi tu mapenzi yake kwa bwana Mtume (s.a.w.w.w), bali pia linadhihirisha msimamo wake wa kidini na mwelekeo wake wa kimadhehebu.

Shairi hili limeacha alama isiyofutika katika ulimwengu wa fasihi na sanaa, likiwa na athari kubwa kwenye maandiko ya nathari na mashairi yaliyofuata baadae. Waandishi wengi wamelitumia jina la shairi hili kama funguo ya maandishi ya vitabu vyao, wakitambua umuhimu na uzito wa ujumbe uliomo ndani yake. Aidha, shairi hili limepata nafasi ya kipekee katika kazi za sanaa, kama vile uchoraji, uandishi wa maandishi ya nakshi, na hata usanifu wa vitambaa. Umaarufu wa shairi hili umevuka mipaka kwa fasihi yake pekee, na sasa linatumika sana katika sherehe mbalimbali za Waislamu, likiwa ni alama ya heshima na upendo kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na familia yake. Waislamu wengi wamelikumbatia shairi hili, na hulitumia mara kwa mara katika hafla na maadhimisho yao ya kidini, likiendelea kuvutia na kuhamasisha vizazi vya leo na vijavyo.

Utambulisho


کَشَفَ الدُّجیٰ بِجَمالِهِ * بَلَغَ العُلیٰ بِکَمالِهِ
حَسُنَت جَمیعُ خِصالِهِ * صَلُّوا عَلَیهِ وَ آلِهِ [1]


Tafsiri: Mtume Muhammad (s.a.w.w) amefikia viwango vya juu kabisa vya ukamilifu, Kaliondoa giza kwa nuru ya uzuri wake wa kipekee, zimepambika sifa zake zote kwa mapambo mema. Basi msalieni Yeye pamoja na Ahlul-Bait zake. [2]


Shairi la (بلغ العلی بکماله) lililoandikwa na Sa’adi Shirazi, ni shairi maalumuu linapatikana katika utangulizi wa kitabu chake maarufu Gulistan. [3] Katika baadhi ya nakala za Gulistan, shairi hili limekuja kwa mfumo beti moja, ambapo mstari wa kwanza unachukuliwa kuwa ni mshororo wa kwanza wa shairi, na mstari wa pili unakuwa ni mshororo wa pili wa shairi hili. [4]

Ingawa shairi hili limeandikwa kwa lugha ya Kiarabu, ila ni wazi kwamba; haikuwa jambo geni kwa watu wanaozungumza Kifarsi wa kutunga mashairi kwa lugha ya Kiarabu, [5] na jambo hili kwao wao ilikuwa sehemu ya urithi wa kitamaduni katika uwanja wa kifasihi. Neno (دُجیٰ), katika shairi hili, linalomaanisha giza [6] au viza vingi, [7] limechukua nafasi muhimu katika ubeti wa pili wa shairi hili maarufu. Dehkhoda, msomi mashuhuri wa lugha na fasihi ya Kifarsi, alitafsiri mstari huu kwa maana ya kuelezea nuru ya uzuri wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.w) ilivyoondoa giza la ulimwengu mzima. [8] Hata hivyo, kuna tafsiri nyingine zilizo tolewa kuhusiana na maana ya neno hilo, ambapo baadhi ya wataalamu wameelezea kwamba; neno (دُجیٰ) lina maana ya pazia, ikimaanisha kwamba; pazia la uzuri wa nuru ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.w) limefunguliwa. [9] Tafsiri hizi tofauti zinaonyesha utajiri wa maana na taswira zilizomo ndani ya shairi hili, na jinsi ushairi wa Sa’adi Shirazi unavyoendelea kuvutia na kuchochea tafakuri miongoni mwa wasomaji na wataalamu wa fasihi hadi leo.

Mshairi

Makala asili: Sa’adi

Shairi la (بلغ العلی) limepata umaarufu mkubwa kama mojawapo ya mashairi ya kuvutia ya Sa’adi Shirazi, [10] nala linahesabiwa kuwa ni ishara ya mapenzi yake ya dhati kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). [11] Watafiti wengine wameeleza kwamba; beti hizi mbili ni miongoni mwa mashairi bora zaidi duniani yaliyo tungwa ajili ya kumsifu Mtume Muhammad (s.a.w.w). [12] Utafiti wa kina unaonyesha kwamba; Saadi, kwa kutumia Aya za Qur'ani pamoja na Hadithi za Mtume (s.a.w.w), ameweza kumuelezea na kumsifu bwana Mtume (s.a.w.w), kwa njia bora zaidi kupitia maneno mafupi yenye uzito ndani ya shairi hili. [13] Mwishoni mwa shairi lake, Sa’adi anawataja Ahlul-Bait, jambo ambalo pia linaonekana katika mashairi mengine ya Sa’adi. [14] Hii imetafsiriwa na baadhi ya wataalamu kama ni ishara ya mwelekeo wake wa Kishia, ingawa maoni haya bado yanajadiliwa na watafiti mbali mbali. [15]

Nafasi Yake na Jinsi Lilivyo Pokewa

Shairi la (بلغ العلی) lililoandikwa na Sa’adi Shirazi limekuwa na athari kubwa katika nyanja mbalimbali za kazi andishi, sanaa, na fasihi ya umma, kama ifuatavyo:

Katika Kazi Andishi

Shairi hili limetumika sana katika kazi za washairi na waandishi wa Kiarani na wa kigeni. Kwa mfano, waandishi maarufu kama Reihanullah Nakha'i Golpayegani (aliyeishi kati ya mwaka 1318 na 1412 Hijiria) [16] na Mohammad Taghi Kermani (aliye fariki mwaka 1215 Hijiria) [17] wameonekana kujumuisha shairi hili katika maandiko yao, likiwa ni ishara ya heshima kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Vilevile, waandishi wa kigeni kama vile Zafar Ali Khan kutoka Pakistan (aliye ishi kati ya mwaka 1873 na 1956 CE), pai nao wameiga na kufaidika na shairi hili, wakiliongeza beti za shiri hili kwenye mashairi yao. [18] Pia, kuna wengine kadhaa waliojaribu kuiga mtindo wa Sa’adi kwa kuandika mashairi yanayofanana na (بلغ العلی) kwa lengo la kumsifu bwana Mtume (s.a.w.w). [19] [20] Shairi hili pia limetumika katika maandiko ya nathari zenye kutoa kusiana na bwana Mtume [21] pamoja na Maimamu (a.s). [22] Hata baadhi ya kazi za ushairi zimepewa jina la (بلغ العلی بکماله) kama alama ya ushawishi na kuvutia mashairi hiyo. [23]

Katika Sanaa

Shairi la (بلغ العلی) limegeuka kuwa chanzo cha msukumo katika sanaa mbalimbali. Wachoraji na waandishi wa kaligrafia akiwemo Mirza Mohammad Ridha Kalhur na Ismail Jalayer wameunda kazi maridadi za kaligrafia zenye msingi wa shairi hili, kazi ambazo zilitolewa mnamo mwaka 1298 Hijiria. [24] [25] Pia shairi hili limeandikwa kwa mtindo wa kaligrafia kwa hati (font) za Nastaliq. Mara nyingi shairi hili utalikuta limefumwa kwenye mikeka katika mashindano mbali mbali ya fasihi. [26] Zaidi ya hayo, pia mistari ya shairi hili utaikuta imechongwa kwenye kuta za baadhi ya majengo ya kihistoria. [27]

Katika Fasihi ya Umma

Shairi la (بلغ العلی) limekuwa ni maarufu mno katika fasihi ya umma, [28] likitumika mara kwa mara katika sherehe za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) [29] na hata katika maombolezo ya siku za Muharram. [30] Shairi hili husomwa katika maeneo mbalimbali duniani. Mbali na watu wa kawaida, hata madaruweshi pia nao hulitumia shairi hili la Sa’adi kwa namna maalum kabisa. [31] Athari ya shairi hili imevuka mipaka ya Iran na kuenea kote duniani, kiasi ya kwamba imeelezwa kuwa; shairi hili limekuwa ni maarufu miongoni mwa watu wa Kashmir ambalo huimbwa kwa sauti ya juu misikitini mwao. [32]

Maudhui Zinazo Husiana

Rejea

Vyanzo