Aya ya al-Naba

Kutoka wikishia

Aya ya al-Naba’ (Surat al-Hujurat Aya ya 6) katika Usul al-Fiq’h inachunguzwa kwa anuani ya hoja ya Khabar Wahed (hadithi ambayo kutokana na idadi ya wapokezi wake hakuna uhakika kama imetoka kwa Maasumu). Akthari ya wafasiri wa Qur’an wanasema kuwa, Aya hii ilishuka kuhusiana na taarifa na habari ya Walid bin Uqbah kuhusiana na kukataa kabila la Bani Mustaliq kutoa Zaka. Baada ya kuenea habari ya tukio hili Aya ya al-Naba’ ikashuka na Waislamu wakafanya uhakiki kuhusiana na habari na taarifa ya Walid na wakafahamu kutokuwa kwake sahihi. Katika elimu ya Usulul-Fiq’h na katika kuchunguza hoja ya Khabar Wahed (hadithi ambayo kutokana na idadi ya wapokezi wake hakuna uhakika kama imetoka kwa Maasumu) Aya hii hujadiliwa.

Andiko na tajumi ya Aya

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ

Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyoyatenda.Maandishi ya kooze

Sababu ya kushuka Aya hii

Wafasiri wa Qur’ani wametaja matukio mawili kuhusiana na sababu ya kushuka Aya hii: Akthari yao wameandika kuwa, Aya hii ilishuka kwa Walid bin Uqbah ambapo Mtume (s.a.w.w) alimtuma kwa kabila la Bani Mustaliq ili akakusanye Zaka. [1] Kwa mujibu wa Fadhl bin Hassan Tabarsi katika Maj’maa al-Bayan ni kuwa, wakati kabila la Bani Mustaliq lilipopata habari kwamba, mjumbe wa Mtume (s.a.w.w) anakuja kwao walikwenda kumpokea; hata hivyo, Walid bin Uqbah kutokana na uadui aliokuwa nao kwao katika zama za Ujahilia, akadhani kwamba, wamekusudia kumuua. Kwa msingi huo alirejea kwa Mtume (s.a.w.w) na kumjulisha kwamba, watu wa kabila hilo wamekataa kutoa Zaka. Mtume akachukua uamuzi wa kutaka kupigana nao vita na ndipo Aya hii iliposhuka ambapo iliwaambia Waislamu kwamba, akikujieni mpotovu na khabari yoyote, kwanza ichunguzeni. [2] Baadhi pia wamesema kwamba, Aya hii ilishuka kuhusiana na tukio la tuhuma dhidi ya Mariyya al-Qibtiyyah mke wa Mtume (s.a.w.w). Katika kisa hiki, Imam Ali (as) ambaye alipewa jukumu la kumuadhibu mkosa, alimuuliza Mtume je anaweza kutoamiani uvumi na kuachana nao endapo uchunguzi wake utakuwa kinyume na maneno ya watu wengine? Mtume (s.a.w.w) akampa idhini ya hilo. Hatimaye ikafahamika kwamba, hakuna tendo la dhambi lililofanyika na kwamba, uvumi ule ulikuwa uongo mtupu. [3].

Aya ya al-Naba’ na hoja ya khabar wahed

Katika elimu ya Usulul-Fiq’h aya ya al-Naba’ imechunguzwa na kujadiliwa kwa ajili ya kuthibitisha Khabar Wahed (hadithi ambayo kutokana na idadi ya wapokezi wake hakuna uhakika kama imetoka kwa Maasumu). Hata hivyo Usuliyuun katika kuthibitisha kuwa hoja khabar wahed kwa kutumia Aya hii hawana kauli na mtazamo mmoja. Kwa mfano Muhammad Hussein Naini amesema kuwa, ni sahihi kutumia Aya hii kama hoja ya kuthibitisha kuwa hoja khabar wahed; [4] lakini Shekhe Murtadha al-Ansari yeye anaamini kwamba, Aya hii haionyeshi na kuthibitisha kuwa khabr wajed ni hoja. [5]