Aya ya Anfalu

Kutoka wikishia

Aya ya Anfalu: Ni Aya ya Kwanza ya Suratu al-Anfalu. Aya hii kiuhalisia inakusudia kutoa tangazo la wazi ya kwamba; Mwenye Ezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w) ndio wamiliki wenye haki kamili juu ya mali zote zisizomilikiwa na watu fulani zikiwemo ngawira zinazokusanywa kutoka vitani.

Mwanazuoni maarufu aitwaye Tabatabai pamoja na Makarim Shirazi, wote wawili wakiwa ni wafasiri wa Qur’ani, wameihisabu mali ya ngawira kuwa ni miongoni mwa mali za anfali. Ila Mola Fat'hullahi Kashani, ameihisabu mali ya ngawira kuwa ndio mali pekee ya anfali iliyo kusudiwa kuashiriwa katika Aya hii.

Dhana na nadharia mashuhuri kuhusiana na sababu ya kushushwa kwa Aya aya Anfalu, inasema kwamba; Katika zama za kushuka kwa Aya hiyo, kulikuwa na kunda la watu kutoka kwa Wahajirina na Ansari walio khitalifiana katika mali ya ngawira iliokusanywa kutoka katika vita vya Badri. Khitilafu zao hizo zilipelekea wao kurudi kwa bwana Mtume (s.a.w.w) ili kutafuta suluhu za khitilafu zao juu mgao wa ngawira hizo, na Mwenye Ezi Mungu akashusha Aya hii ili kutoa tiba ya khitilafu zao hizo. Kuna kundi dogo la wafasiri miongoni mwa waislamu akiwemo Mujahid bin Jabru, wanao amini juu ya kufutwa kwa Aya ya Anfalu kupitia Aya iliyokuja kuzungumzia hukumu za khumsi. Hata hivyo wafasiri wengi wa Kisunni na Kishia ni wenye kupingana na madai ya kufutwa kwa Aya hiyo. Hii ni kwa sababu ya kwamba wao wanaamini ya kuwa hakuna dalili ya za kukinaisha juu ya madai hayo. Matini na Tafsiri ya Aya Aya ya kwanz ya Suratu al-Anfalu inajulikana kwa jina la Aya ya Anfalu [1] ﴿يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنْفَالِ قُلِ الْأَنْفَالُ لِلَّهِ وَالرَّسُولِ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ ١﴾ [انفال:1] (Kwa jina la Mwenye Ezi Mungu Mrehemevu Mwingi wa rehema. [Awe Mtume] Wanakuuliza kuhusiana na anfalu (ngawira), waambie anfalu ni za Mwenye Ezi Mungu na Mtume, basi mcheni Mola wenu na patanisheni juu ya khitilafu zenu, na mcheni Allah na Mjumbe wake ikiwa kweli nyinyi ni waumini.) Suratu al-Anlaf, Aya ya kwanza.

Muktadha wa Kushuka kwa Aya ya Anfalu

Kuna mitazamo miwili tofauti katika tafsiri za Kishia Kuhusiana na muktadha wa kushuka kwa Aya ya Anfalu. Tafsiri nnyingi za Kishia zinaswma kuwa; sababu ya kushuka kwa Aya hiyo ni tukio la khitilafu lilizojitokeza miongoni mwa baadhi ya Waislamu kuhusiana na suala la mgao wa ngawira, ambapo kila mmoja alidhani kuwa na haki ya kupata resheni kubwa zaidi kiliko wengine. Na kwa upande wa pili kuna mtazamo mwengine tofauti na huo, nao ni mtazawo unaoshiliwa na tafsiri chache miongoni mwa tafsiri za Kishia. Mtazamo huu unasema kwamba; Sababu ya kushuka kwake ni hamu ya baadhi ya Wahajirina (wahamiaji) ya kutolipa khumsi inayo husiana na mali zao. Yaaani wao walipenda kuona wanpata msamaha wa kuto daiwa khumsi kutokana na mali walizonazo. • Kulingana na tafsiri ya Majma’ al-Bayan iliyoandikwa na Fadhl ibn Hasan Tabarsi, Al-Tibyan iliyoandikwa na Sheikh Tusi, Tafsir Minhaj al-Sadiqin iliyoandikwa na Mulla Fat’hullah Kashani, na Tafsiri Nemuuneh iliyoandikwa na Makarem Shirazi, ni kwamba Aya hii ilishuka kuhusiana na ghanima (ngawira) za vita vya Badri, na iliteremshwa baada ya kundi la Waislamu wa Kihajirini na Ansar kutofautiana juu ya mgawanyo wa ghanima hizo, kila mmoja akitaka sehemu kubwa zaidi kuliko mwengine, ambapo hatimae walikwenda kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya kutatua suala hilo. [2] • Kulingana na maelezo amabo yanapatikana katika vitabu viwili vya Majma’ al-Bayan la Tabarsi na Al-Tibyan la Sheikh Tusi tu, ni kwamba; Aya ya Anfalu iliteremshwa baada ya baadhi ya Wahajirina kutotaka kulipa sehemu moja ya tano (Khums) ya mali zao. [3] Dhana ya Aya Allama Tabatabai na Makarem Shirazi, ambao ni wafasiri wa Kishia, wanaamini kwamba; Anfalu inajumuisha mali zote ambazo hazina mmiliki binafsi, na kwamba katika hiyo mmiliki wake huwa ni Mwenye Ezi Mungu, Mtume, na warithi wake (yaani warithi wa Mtume) (s.a.w.w). [4] Kwa msingi huu, ngawira zote za vitani zinachukuliwa kama ni sehemu ya Anfalu. [5] Mulla Fathullah Kashani, mfasiri wa Kishia wa karne ya kumi Hijria aliyeishi katika kipindi cha utawala wa Safawiyyah, katika tafsiri yake ya Manhaj al-Saadiqina, anaelezea dhana ya Anfalu, kwa maana ngawira za kivita, na anazichukulia ngawira hizo kama ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa ajili ya wapiganaji. [6] Neno “anfalu” katika lugha ya Kiarabu, ni wingi wa neno “nafal” lenye maana ya ziada juu ya kitu fulani; hivyo chochote kile kinacho onekana kuwa ni ziada juu ya asili ya kitu fulani, huinaitwa nafal au naafilah, kwa mfano, sala zinazoswaliwa kabla au baada ya sala za wajibu zinaitwa sala za naafilah kwa sababu sala hizo ni za ziada juu ya sala asili za wajibu. [7]

Kufutwa au Kutofutwa kwa Aya ya Anfalu Kupitia Aya ya Khumsi

Kulingana na alichoripoti Sheikh Tusi katika tafsiri yake ya Tibyanu, ni kwamba; Baadhi ya wafasiri wa Sunni, akiwemo Mujahid bin Jabru (aliyeishi kati ya mwaka 21 n a104 Hijiria), ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Ibnu Abbas katika tafsiri ya Qur’an, na Abu Ali Juba’i (aliye ishi kati ya mwaka 235 na 303 Hijiria), ambaye mwanatheolojia wa Muutazila (Mu’tazilite), waliamini kwamba Aya ya kwanza ya Suratu Al-Anfali imefutwa kupitia Aya ya Khumsi. [8] Hata hivyo, wafasiri wengine wa Shia na Sunni wamekataa kauli hiyo inayodai kuwa Aya ya Khumsi imekuja kufuta Aya ya Anfalu. [9]

Sheikh Tusi hakukubali kufutwa kwa Aya ya Al-Anfalu, kwani anaamini kwamba; Kukubali kufuta kwa Aya hii kunahitaji ushahidi na ithibati kamili, na zaidi ya hayo, hakuna mgongano au kuto owana kati ya Aya ya Al-Anfalu na Aya ya Khumsi, kiasi ya kwamba kuwepo haja ya kuamini kwamba ya imefutwa. [10] Baadhi ya wafasiri kama vile; Fadhl ibnu Hassan Tabarsi, Nasir Makarem Shirazi, na Sayyid Mohammad Hussein Tabatabai pia hawakukubaliani na dhana ya kuwepo kwa mgongano kati ya Aya mbili hizo. [11] Allamah Tabatabai anaamini kwamba Aya ya 41 ya sura ya Anfal, ambayo inajulikana kama Aya ya Khums, ni Aya iliyo kuja kuchambua na kutoa tafsiri ya Aya ya kwanza ya Suratu al-Anfal; kwa sababu katika Aya ya kwanza, tata zote kuhusiana na umiliki wa Anfalu zimetatuliwa ndani yake. Na tayari kupia Aya hiyo ya kwanza ya Suratu al-Anfalu, ilikwisha eleweka ya kwamba; hakuna mtu anayemiliki Anfalu, ambayo miongoni mwake ni ngawira za vita, ambayo kupitia Aya hiyo imehisabiwa kuwa mali ya Mwenye Ezi Mungu na Mtume wake. Ila katika Aya ya 41, Waislamu wamepewa ruhusa ya kutumia theluthi nne kutoka katika theluthi zote tano za ngawira hizo, na ni theluthi moja kati ya tano hizo inayo ingia na kumilikiwa na Mungu pamoja na Mtume wake. [12] Kulingana na maoni ya Tabatabai, aina hii ya tafsiri, haioneshi kuwepo kwa mgongano wala utata unao weza kujitokeza kuhusiana na maudhui ya Aya mbili hizi, kiasia ya kwamba iweze kujengeka imani kwa Aya hiyo ya kwanza ya Suratu al-Anfal. [13] Wengine pia wanaamini kwamba mali zote hizi hizo zinazoingia kwenye kichwa cha habazi cha Anfalu, ziko chini ya udhibiti wa mtawala wa Kiislamu, naye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa theluthi nne za ngwaira hizo na kuwagawia wapiganaji jihadi. [14]