Nenda kwa yaliyomo

Aya ya Jald

Kutoka wikishia

Aya ya Jald au Aya ya hukumu ya Uzinzi (Kiarabu: آيَة الجَلد أو آيَة الزِّنا Ni Aya ya pili ya Surat Al-Nur, nayo ni Aya inayo elezea adhabu ya kisheria kwa mwanamke na mwanamme mzinifu. Adhabu ya uzinzi kulingana na Aya hii, ni viboko mia moja, adhabu ambayo inapaswa kutekelezwa mbele ya kundi la waumini. Pia, imekatazwa kuwahurumia wazinifu hao katika kuwatimizia adhabu hii. Kwa mujibu wa maoni ya mafakihi, Aya hii inahusiana na wazinifu walio huru ambao si watumwa, na sio مُحْصِن Muhsin. Neno “Muhsin” lina maana ya mtu mwenye uwezo wa kuwa na mahusiano ya ndoa kihalali. Kwa maoni ya baadhi ya wafasiri, Aya hii imekuja kufuta Aya ya 15 ya Surat Al-Nisaa inayohusiana na wanawake wazinifu.

Umuhimu wa Aya ya Adhabu ya Kupiga Viboko

Aya ya 2 ya Surat Al-Nur ni ijulikanayo kwa jina la Aya ya Kupiga Viboko au Aya ya Uzinzi. [1] Aya hii ni moja ya Aya za hukumu za kisheria, ambayo mafakihi huitumia Aya hii kwa ajili ya kueleza na kuthibitisha adhabu ya wazinifu. [2] Aya hii imeelezea hukumu hiyo kama ifuatavyo: (الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ وَلَا تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ) ; Mpigeni kila mmoja kati ya mzinifu wa kike na wa kiume bakora mia moja. Na ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenye Ezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi katu msiwe na huruma juu yao katika kutekeleza sheria ya dini ya Mwenye Ezi Mungu. Na adhabu yao ishuhudiwe na kundi la waumini. (Nur: 2)

Kwa mujibu wa baadhi ya wafasiri, Aya hii inaashiria mambo matatu yafuatayo:

  1. Kuthibitisha hukumu ya bakora mia moja kama ni adhabu halisi ya wazinifu.
  2. Kukataza suala la kuwa na huruma katika kuwatekelezea wazinifu haki yao hiyo.
  3. Amri ya kuwepo kwa kundi la waumini wakati wa kutekeleza adhabu hiyo, ili iwe ni fundisho kwa wengine. [3]

Matumizi ya Kifiqhi

Ibara za kitabu kiitwacho Sharai'u al-Islam, zinasema kwamba; Adhabu ya bakora mia moja ni kwa ajili ya wazinifu ambao sio مُحصِن Muhsin (mtu asiye na uwezo wa kuwa na mahusiano ya ndoa kihalali). Ama adhabu ya mzinifu amabaye ni مُحصِن Muhsin ni رجم rajmu, yani ni kupigwa mawe. [4]

Allama Hilli katika kitabu Tahrir al-Ahkam, anaamini kuwa; Mzinifu mwanamme anapaswa kupigwa bakora ahli akiwa uchi; ila kichwa, uso na sehemu za siri zinapaswa kulindwa dhidi ya bakora hizo. Akitegemea Aya inayosema: (Arabic ; Wala msishikwe na huruma katika kutekeleza adhabu ya Mwenye Ezi Mungu), amesema kwamba, bakora hizo zinapaswa kuwa ni bakora kali. [5]

Sheikh Tusi naye akitegemea Aya isemayo: (وَلْيَشْهَدْ عَذٰابَهُمٰا طٰائِفَةٌ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ; Na adhabu yao ishuhudiwe na kundi la waumini), anasema kuwa kiongozi anapaswa kuwapasha watu habari, ili waweze kuhudhuria wakati wa kutekelezwa kwa adhabu hiyo dhidi ya wazinifu, ili watu hao wawe na hadhari na waepuke kutenda dhambi kama hiyo. [6] Na ni vyema wale wanaoshuhudia adhabu hiyo wawe ni miongoni mwa watu wema. [7] Kwa mujibu wa Tafsiri ya Majma' al-Bayan iliyoandikwa na Tabarsi, ni kwamba; wafasiri wamesema kwamba neno طائفة (kundi) lililoko kwenye kweye Aya hii, linaweza kumaanisha mtu mmoja, wawili, watatu au zaidi. [8]

Pia, imesemwa kuwa Aya hii ya 2 ya Surat Al-Nur, imekuja kufuta Aya ya adhabu ya uzinzi iliyopo katika Suratu Al-Nisaa, ambayo ni Aya ya 15 ya Sura hiyo. Kwa mujibu wa maoni ya Sayyid Muhammad Hussein Tabataba'i, mwandishi wa Tafsiri ya al-Mizan, ni kwamba; Aya ya adhabu ya kupiga bakora, imefuta Aya ya 15 ya Surat Al-Nisaa, isemayo: "Ikiwa wanawake wenu watatenda uzinzi, basi wafungeni nyumbani mpaka watakapo kufa au Mwenye Ezi Mungu awape (awajaalie) njia nyingine". [9] Tabataba'i anasema kwamba ibara isemayo: (أَوْ یجْعَلَ اللَّهُ لَهُنَّ سَبیلا ; Au Mwenye Ezi Mungu awajaalie wanawake hao njia fulani), yaonesha kuwa Aya hii itakuja kufutwa baadae. [10]

Nukta za Kitafsiri

Tabrasi, mmoja wa wafasiri wa Kishia, ameichambua Aya hii, kwa kuzingatia nukta kadhaa ndani yake, nukta hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Aya hii inahusiana na wanawamke na wanaume huru غیرمُحْصِنِ (wasiokuwa Muhsin). Kwa hiyo kama mzinifu huyo atakuwa ni mtumwa wa wakike (mjakazi) au ni mtumwa wa kiaume, adabu yake itakuwa ni kupigwa nusu ya bakora mia moja, hii ni kwa mujibu wa Aya ya 25 ya surat Al-Nisaa. [11] Mwenye Ezi Mungu katika Aya hiyo anasema: "Basi (wajakazi) wanapoolewa, ikiwa watatenda uzinzi, wao adhabu yao itakuwa nusu ya adhabu ya wanawake walio huru". [12]
  2. Aya hii imeelekezwa kwa Maimamu (a.s) na wale waliowekwa na Maimamu hao; kwa sababu hakuna mtu mwingine isipokuwa Imamu na wawakilishi wao tu, ndio wenye haki na mamlaka ya kutekeleza adhabu za kisheria. [13]
  3. Neno الزّانیة (Mzinifu wa kike) katika Aya hii, limetangulia kabla ya neno الزّانی (Mzinifu wa kike). Mfasiri wa Qur’ani wa Kishia aitwaye Tabarsi, ametoa sababu kadhaa kuhusiana na sababu za kutangulia kwa neno hili, miongoni mwazo ni kama ifuatavyo:
  • Sifa ya uzinzi kwa wanawake ni sifa ya aibu zaidi. [14]
  • Shauku na nguvu za shahawa kwa wanawake ni kubwa zaidi. [15]
  • Uzinzi unaleta madhara zaidi kwa wanawake kwa sababu ya uwezekano wa kupata mimba. [16]

Mada Zinazo Husiana