As’wad bin Qutbah

Kutoka wikishia

Isichukuliwe kimakosa na As’wad bin Qutbah Tamimi

As’wad bin Qutbah alikuwa mmoja wa masahaba wa Imamu Ali (as) na kamanda wa jeshi lake katika eneo la Hulwan. [2] Kuna barua ya Imamu Ali (as) aliyoiandika akimhutubu As’wad bin Qutbah na andiko lake linapatikana katika Nahajul-Balagha. [3] katika barua hii, Imamu anamuagiza As’wad kwamba, ajitenge na suala la kufuata hawaa na matamanio ya nafsi na dhulma, awafanyie watu uadilifu na atumuie fursa ya kuwahudumia. [4] Barua ya Imamu Ali kwa As’wad bin Qutbah imenukuliwa kwa Nun katika tukio la Siffin ambapo madhumuni yake yanafanana na barua ya 59 katika kitabu cha Nahajul-Balagha. [5]

Ali Ahmad Miyanji (aliaga dunia: 1379 Hijria Shamsia) anasema katika kitabu cha Makatib al-Aimah kwamba, waandishi na wafafanuzi wa Nahajul-Balagha wametofautiana kuhusiana na jina la baba wa As’wad kwamba, ni Qutbah au Qutnah au Qatayna. [6]

Katika sherh ya Ibn Maytham Bahrani, imesajiliwa lafudhi ya Qatayna. [7] Ibn Abil Hadid, mmoja wa wafafanuzi wa Nahajul-Balagha katika karne ya 7 Hijria anaelekea upande wa mtazamo wa kitabu cha Aal-Isti’ab kuhusiana na nasaba ya As’wad ambapo anasema, yeye ni As’wad bin Zayd bin Qutbah bin Ghanam al-Ansari. [8] Baadhi wanaamini kwamba, As’wad bin Qutbah alishiriki katika vita vya Badr. [9] Sayyid Murtadha al-Askari (aliyefariki: 2007), mwanahistoria wa Kishia, amemtambua As’wad bin Qutbah kuwa mlengwa wa barua ya Imam Ali katika Nahaj al-Balagha kuwa ni Sabai Qahtani na si As’wad bin Qutbah Tamimi. [10] Kwa mtazamo wake ni kuwa, As’wad Tamimi ni shaksia ya kubuni katika historia ya Uislamu ambayo haikuweko. [11]

Tarjumi ya barua ya 59 katika Nahajul-Balagha

Ama baad, kwa hakika iwapo maoni na mawazo ya mtawala yatabadilika, yatamzuia kutekeleza haki. Kwa hivyo, kazi ya watu inapaswa kuwa sawa katika mtazamo wako wa kile ambacho ni haki, kwa sababu hakuna bei ya haki katika udhalimu. Jiepushe na yale usiyoyapenda kuwafanyia wengine na jilazimishe kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu amewajibisha juu yako huku ukitaraji malipo ya Mwenyezi Mungu na kuogopa adhabu yake. Tambua kwamba, dunia ni nyumba ya mtihani, na mja mwenye kuabudu dunia hatabakia humo hata saa moja isipokuwa atajuta Siku ya Kiyama, na katu hakuna kitakachokufanya usiwe mhitaji haki. Na ni haki kwako kuilinda nafsi yako na kufanya kazi kwa bidii uwezavyo katika mambo ya raia, kwa sababu unachopata katika njia hii ni bora kuliko kile unachopoteza katika nguvu zako za mwili. Wassalaam. [1]