Nenda kwa yaliyomo

Amina binti Shurayd

Kutoka wikishia

Amina binti Shurayd (Kiarabu: آمنة بنت شريد)alikuwa mke wa Amr bin Hamiq al-Khuzai (aliyefariki 50 Hijiria) na alifungwa jela kwa amri ya Muawiya ibn Abi Sufyan na mkasa huu ndio uliopelekea apate umashuhuri.

Amina binti Shurayd ni miongoni mwa wanawake waliokuwa na ufasaha (katika kuzungumza) wa mji wa Kufa na alikuwa mke wa Amr bin Hamiq al-Khuzai [2] na miongoni mwa Mashia na wafuasi wa Imam Ali ibn Abi Talib (a.s). [3] Ibn Tayfur, mwanahistoria wa Waislamu wa Ahlu-Sunna (204-280) amenukuu katika kitabu chake cha Balaghat al-Nisaa maneno ya Amina binti Shurayd kwa Muawiya ibn Abi Sufyan. [4] Katika kitabu cha A’yan al-Shia[5] na A’lam al-Nisaa al-Mu’minat [6] pia kumenukuliwa habari hizi za Ibn Tayfur.

Zirikli, mwandishi wa historia wa karne ya 14 Hijiria anasema, sababu ya umashuhuri wa Amina ni tukio la kufungwa kwake jela na maneno yake kwa Muawiya. [7] Baada ya kuuawa shahidi Imamu Ali Ibn Abi Talib (a.s), baadhi ya Mashia akiwemo Amr ibn Hamiq al-Khuzai walianza kusakwa na kufuatiliwa na Muawiya. Amr alikimbia na kujificha, hivyo Muawiya akatoa amri ya kutiwa mbaroni mkewe na akafungwa jela kwa miaka miwili huko Damascus. [8] Baada ya kufa shahidi Amr ibn Hamiq al-Khuzai mwaka 50 Hijiria, kwa amri ya Muawiya kichwa chake kilichukuliwa na kupelekwa Damascus na kupelekwa gerezani mbele ya Amin binti Shurayd, hata hivyo Amina alisimama na kutoa wasifu kwa mumewe na kumlaani Muawiya. [9] Baada ya hapo aliachiliwa huru na kupelekwa katika mji wa Kufa. Amina aliaga dunia mwaka 50 Hijiria kwa ugonjwa wa tauni akiwa njiani katika mji wa Homs, Syria. [10]

Rejea

Vyanzo

  • Amīn, al-Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Taʿāruf, 1403 AH.
  • Ḥasūn, Muḥammad. Mashkūr, Umm ʿAlī. Aʿlām al-nisāʾ al-muʾmināt. Tehran: Uswa, 1421 AH.
  • Ṭayfūr Aḥmad, Ibn Abī Ṭāhir. Balāghāt al-nisāʿ. Beirut: 1972 CE.
  • Ziriklī, Khayr al-Dīn al-. Al-Aʿlām. Beirut: Dār al-ʿIlm li-l-Malāyyīn, 1989 CE.