Nenda kwa yaliyomo

Al-Tafsiru wa al-Mufassiruna fi Thaubihi al-Qashibi (Kitabu)

Kutoka wikishia

Tafsiru wa al-Mufassiruna fi Thaubihi al-Qashibi (Kiarabu: التَفسیر وَ المُفَسِّرون فی ثَوبِه القَشیب): Ni kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na Muhammad Hadi Ma'rifat (1385 AH). Kitabu hichi kiliandikwa kwa lengo la kutetea misingi na kanuni za tafsiri katika madhehebu ya Kishia na ni jibu la kitabu cha Muhammad Hussein Dhahabi, msomi kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar, nchini Misri, ambacho kilipewa jina la Tafsiru wa al-Mufassiruna.

Kitabu hichi kimeandikwa katika mfumo wa juzuu mbili. Juzuu ya kwanza baada ya kutoa utangulizi na kuelezea tafauti za tafsiri, ta-awil (ukengeushi wa maana dhahiri), aina mbalimbali za tafsiri, mwandishi ameendelea kuelezea mabadiliko ya katika historia ya tafsiri ya Qur'ani Tukufu kuanzia; enzi za bwana Mtume (s.a.w.w), Masahaba, hadi zama za Tabi'ina. Pia, kitubu hichi kimetoa maelezo muhimu na ya ndani juu ya mchango wa Ahlul-Bayt katika tafsiri ya Qur'ani. Sehemu nyingine ya juzuu hii inahusiana na kuwatambulisha wafasiri maarufu waliokuja baada ya zama za Tabi'ina. Juzuu ya pili ya kitabu hichi imejikita zaidi katika masuala ya tafsiri athari (tafsiri kupitia Hadithi), pia inachambua masuala ya Hadithi za uongo (israiliyati) katika tafsiri hizo. Pia juzuu hii inatoa ufafanuzi wa kina juu ya kazi mbali mbali zilizofanywa na wafsiri wa Kishia na Kisunni.

Watafiti wamekisifu kitabu cha "al-Tafsiru wa al-Mufassiruna" kwa sifa kadhaa, zikiwemo; utetezi wa misingi na kanuni za tafsiri za Kishia, matumizi ya vyanzo vingi na vya kuaminika, umakini katika kushughulikia masuala ya Hadithi bandia (israiliyati) pamoja na ubunifu wa kielimu. Hata hivyo, kitabu hichi pia kimekosolewa kwa kutozingatia ipasavyo na kuto jumuisha madhehebu na mifumo ya tafsiri inayopatikana katika nchi za Misri na Yemen.

Mwandishi

Makala Asili: Muhammad Hadi Ma'rifat

Muhammad Hadi Ma'rifat (aliye ishi kati ya mwaka 1309 na 1385 Hijiria Shamsia), alikuwa miongoni mwa wanazuoni maarufu wa Kishia, akiwa na umahiri mkubwa katika taaluma za Hadithi, fiqhi, pamoja na tafsiri ya Qur'ani Tukufu. [1] Hakuwa maarufu kwa kuwa ni faqihi mahiri, bali pia kama mfasiri mashuhuri wa Qur'ani tukufu. Hadi Ma'rifat alitoa mchango mkubwa katika kuendeleza welewa wa taaluma za Qur'ani na fiqhi miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Shia. Moja ya kazi zake mashuhuri ni kitabu chake "al-Tafsiru wa al-Mufassiruna", ambacho kinachambua kwa kina mbinu mbalimbali za tafsiri ya Qur'ani pamoja na sifa za wafasiri waliotangulia. Mbali na kitabu hichi, Ma'rifat aliandika vitabu vyengine vingi muhimu vinavyoangazia masuala mbali mbali ya Qur'ani, kama vile; "al-Tamhidu fi Ulumi al-Qur’ani",[2] ambacho ni kazi ya kipekee inayochunguza sayansi mbalimbali za Qur'ani, al-Tafsiu al-Athariyyu al-Jaami’I [3] ambayo ni tafsiri fafanuzi ya Qur'ani tukufu inayozingatia Riwaya za Mtume na Maimamu wa Ahlul-Bait, Shubuhatu wa Rududu Haula al-Qur’ani, [4] kinachojadili na kujibu shaka kuhusiana na Qur'ani na Siyanatu al-Qur’ani Mina al-Tahrifi, [5] kitabu ambacho kinathibitisha usahihi na utakatifu wa maandiko ya Qur'ani dhidi ya madai ya upotoshwaji wa Qur’ani tukufu. [6]

Mfumo wa Kitabu na Muktadha Wake

«Tafsiru wa al-Mufassiruna fi Thaubihi al-Qashibi» (Tafsiri na Wfasiri katika Vazi Jipya): ni kitabu kinachozungumzia elimu na fani zinazo husiana na Qur'ani (ulumu al-Qur’ani) nacho kimechapishwa katika mfumo wa juzuu mbili. Sura tatu za mwanzo za kitabu hichi zimeanza kwa utangulizi unaoeleza sababu za kuandikwa kwake pamoja na sifa zake maalum. [7] Kwa mujibu wa maelezo ya Muhammad Hadi Ma'rifat, kitabu hichi kiliandikwa kama majibu dhidi vitabu viwili; «al-Tafsiru wa al-Mufassiruna», kilichoandikwa na Muhammad Hussein Dhahabi (1333-1397 Hijiria) aliyekuwa mwalimu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na «Madhahibu al-Tafsiru al-Islamiyyu», cha Abdul Halim Najjar. Ma'rifat anasema kwamba; vitabu hivyo vimekuja na madai yasiyo sahihi na yanayopingana na misingi ya Ushia na Uislamu kwa jumla, hivyo basi, yeye alihisi kuwa kuna haja ya kuyajibu madai hayo kupitia kitabu chake hicho maridadi. [8]

Juzuu ya kwanza ya kitabu hichi inajumuisha sura sata ndani yake, sura tatu za mwanzoni zina zungumzia utangulizi na ufafanuzi, masharti ya tafsiri, na aina za tafsiri. Pia, inajadili ndani yake uhusiano kati ya tafsiri na ta'wil (tafsiri kengeushi, au ya maana mbadala), pamoja na mbinu za uwasilishaji wa maana za Qur'ani Tukufu. [9] Sura nyingine tatu za zinazo fuata, zinahusiana na uchambuzi juu ya mwenendo wa kihistoria wa tafsiri ya Qur'ani, kuanzia enzi za bwana Mtume (s.a.w.w), Masahaba na Tabi'ina, pia kumetolewa maelezo ya ndani yake kuhusiana na nafasi ya Ahlul-Bayt (a.s) katika fani ya tafsiri ya Qur'ani. [10] Hatimae, sura ya saba ya juzuu ya kwanza inajadili wafasiri maarufu katika kipindi baada ya Tabi'in, [11] ingawa sehemu ya mwisho ya ukamilisho wa sura hii, imeendelezwa mwanzoni mwa juzuu ya pili ya kitabu hichi. [12]

Juzuu ya pili ya kitabu "al-Tafsiru wa al-Mufassiruna", inajumuisha sehemu mbili kuu ndani yake. [13] Sehemu ya kwanza inajadili tafsiri athari au tafsiri zitegemeazo Hadithi, ambapo Muhammad Hadi Ma'rifat katika sehemu hii, anakusudia kuonyesha udhaifu na matatizo yanayohusiana na Hadithi bandia (israiliyat) katika tafsiri zitegemeazo Hadithi. Aidha, amearifisha tafsiri muhimu za upande wa Kishia na Kisunni kutoka karne ya tatu Hijiria zitegemeazo Hadithi mbali mbali. [14] Sehemu ya Pili ya juzuu hii, inahusiana na mbinu za tafsiri ya kiijtihadi, ya fiqhi, ya kisayansi, ya kifasihi, ya lugha, tafsiri kulingana na mpangilio Sura, mada, kijamii na tafsiri ya Kisufi. Sehemu hii inatoa mchango wa kina katika kuelewa na kutofautisha mbinu na aina mbalimbali za tafsiri zinazotumika katika uwanja wa elimu wa Qur'ani. [15]

Sifa za Kitabu na Mapungufu Yake

Kitabu "al-Tafsiru wa al-Mufassiruna" kimepata sifa kadhaa za kipekee, katika uwanja wa tafsiri. Hata hivyo, kitabu hichi pia kimekosolewa kwa kutozingatia ipasavyo madhehebu ya tafsiri katika maeneo tofauti, na pia kutoakisi juhudi na shughuli za tafsiri kutoka kwa Maimamu (a.s) huko Madina. Baadhi ya sifa na faida za kitabu hichi ni kama ifuatavyo:

  • Matumizi ya Vyanzo Vingi na vya Kuaminika: Ayatullah Ma'rifat ametumia zaidi ya vyanzo 500, ikiwa ni pamoja na vyanzo vya elimu ya Qur'ani, historia, na ensaiklopidia, katika kuandika kitabu hichi. [16]
  • Ubunifu na Uwasilishaji wa Maoni Mapya: Kitabu hichi kimezalisha nadharia mpya [17] na kuchambua vya kutosha juu ya fani ya tafsiri pamoja na kueleza kanuni zake. Pia mwandishi amejitahidi kuonesha nafasi ya la Ahlul-Bayt (a.s) katika tafsiri ya Qur'ani, na kugawanya mbinu za tafsiri katika nyanja mbili kuu; tafsiri ya ijtihadi na tafsiri ya kutegemea Hadithi (Tafsiru bi al-Maathuri). [18]
  • Umuhimu wa Kukabiliana na Hadithi bandia: Kitabu hichi kinazungumzia moja ya changamoto kubwa zinazoathiri tafsiri zitegemeazo Hadithi za Kishia pamoja na Kisunni. [19]
  • Kazi ya Kwanza Huru ya Kishia: Kitabu al-Tafsiru wa al-Mufassiruna kinachukuliwa kuwa ndiyo kazi ya kwanza huru ya Kishia inayohusiana na tafsiri pamoja na elimu ya Qur'ani, kwani kabla ya hapo, mada hizi zilikuwa zimewasilishwa kwa njia isiyojikita na isiyo jitawala kama fani binafsi. Hapo mwanzo muktadha wa mada hii ulikuwa ukijadiliwa kwa mparaganyiko kwenye vitabu mbli mbali. [20]
  • Utetezi wa Madhehebu ya Kishia: Mojawapo ya sifa kuu za kitabu hichi ni utetezi wa madhehebu ya Kishia. Muhammad Hadi Ma'rifat aliandika kitabu hichi kama ni jibu la kitabu al-Tafsiru wa al-Mufassiruna cha Muhammad Hussein Dhahabi, [21] ambaye alikosoa misingi ya tafsiri za Kishia pamoja na kuonesha dharau dhidi ya kadhaa zikiwemo tafsiri maarufu kama vile; Mir-aat al-Anwaar, Majma'u al-Bayan, Al-Safi fi al-Qur'an na tafsiri ya Imamu Hassan al-Askari (a.s). baadhi ya watafiti wamemkosowa Dhahabi kutokana na kuwa na mitazamo ya upendeleo na isiyo ya haki dhidi ya wengine. [22]

Baadhi ya ukosoaji dhidi ya kitabu hichi ni pamoja na:

  • Kuto orodhesha madhebu yote ya Tafsiri: Katika kuwasilisha madhehebu ya tafsiri, Muhammad Hadi Ma'rifat ametaja wafasir wa kutoka Makka, Madina, Kufa, Sham na Basra peke yao, na hakutaja chochote kuhusiana na madhehebu ya tafsiri yalioko huko Misri na Yemen. [23]
  • Ukosefu wa Uwasilishaji wa Uwepo wa Ahlul-Bait (a.s) Huko mjini Madina: Kitabu al-Tafsiru wa al-Mufassiruna hakikutoa ripoti yoyote ile kuhusiana na uwepo wa athari za Ahlul-Bayt (a.s) huko Madina au jinsi walivyoshughulikia masuala ya Qur'ani mjini humo. [24]

Chapisho na Tafsiri ya Kifarsi

Kitabu «al-Tafsiru wa al-Mufassiruna» kilichoandikwa na Ayatullahi Ma'rifat, kilichapishwa na Ofisi ya Uchapishaji ya Chuo Kikuu cha Sayansi za Kiislamu cha Radhawi huko Mashhad. Pia, tafsiri ya Kifarsi ya kitabu hiki, pamoja na nyongeza zake, ilichapishwa katika juzuu mbili chini ya jina la «Tafsir wa Mufasirane», na «Muasasa al-Tamhid». Kazi ya kufasiri kitabu hicho kwa lugha ya Kifarsi ilifanywa na Ali Nasiri akishirikiana na Ali Khayyat mnamo mwaka 1380 SH (2001 AD). [25]

Mada Zinazo Husiana

Rejea

Vyanzo