Nenda kwa yaliyomo

Al-Nadhafatu Mina Al-Iman

Kutoka wikishia

Al-Nadhafatu Mina Al-Iman "Usafi ni sehemu ya imani" (Kiarabu: النَّظَافَةُ مِنَ الْإِيمَانِ): Ni usemi maalumu unaoaminika kuwa ni Hadithi, Hadithi ambayo inahusishwa moja kwa moja na bwana Mtume (s.a.w.w). Hadihi inakusudia kusema kwamba; usafi ni ishara ya imani. Hadithi hii inapitikana katika kitabu kiitwacho "Tib al-Nabi (s.a.w.w)", kilichotungwa na Abu al-Abbas al-Mustaghfiri (aliyefariki mnamo mwaka 422 Hijria). [1] Kitabu cha "Tib al-Nabi" ni miongoni mwa vyanzo vilivyotegemewa katika uandishi wa kitabu "Bihar al-Anwar" kilichoandikwa na Allama Majlisi. Hadithi  imenukuliwa kwa ukamilifu ndani ya kitabu hichi. [2] Ibara hii isemayo: "Usafi ni sehemu ya imani" inahusishwa moja kwa moja na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na ni sehemu ya Hadithi refu izungumziayo maudhui ya usafi. Hadithi hii imekuja kama ifuatavyo; «تَخَلَّلُوا فَإِنَّهُ مِنَ النَّظَافَةِ وَ النَّظَافَةُ مِنَ الْإِيمَانِ وَ الْإِيمَانُ مَعَ صَاحِبِهِ فِي الْجَنَّة؛ "Safishenii meno yenu (kwa kijiti) kwa sababu jambo hilo ni sehemu ya usafi na usafi ni sehemu ya imani na imani huwa sambamba na mwenywe imani hiyo huko Peponi". [3]


Hadithi Kuhusu Usafi na Afya

Hadithi zote zilizomo katika kitabu cha "Tib al-Nabi (s.a.w.w)" zinazohusiana na muktadha wa usafi na matibabu, na zinazotokana na Mtume Muhammad (s.a.w.w), zimeandikwa bila ya kutaja nukuu inayohusiana na wapokezi wa Hadithi hizo. [4] Jambo hili liimepelekea kuibuka kwa mijadala na dadisi mbali mbali miongoni mwa watafiti kuhusiana na uhalali wa Hadithi hizo. [5]

Hata hivyo, maudhui ya hadithi hii imeridhiwa na kukubalika mbele ya watafiti wa kidini kwa sababu zifuatazo: [6]

1.     Msisitizo wa Qurani: Kuna Aya kadhaa ndani ya Qurani zinazohimiza suala la usafi na kuepukana na aina mbali mbali za uchafu, ikiwemo Aya ya 33 ya Suratu Al-Ahzab na Aya ya 125 ya Sura Al-Baqara. [7]

2.     Uwepo wa Hadithi Kuhusiana na Usafi na Afya: Kuna Hadithi nyingi mno zinaosisitiza umuhimu wa usafi na afya kwa jumla. Miongoni mwazi ni; Hadithi isemayo usafi ni nusu ya imani [8], Hadithi itoayo ushauri wa kusafisha nguo [9], Hadithi itoayo ushauri wa kusafisha nyumba [10], na Hadithi inayosisitiza kuepuka mambo yanayohatarisha hali za kiafya, kama vile kutosafisha vyombo na kutoifagia nyumba. [11]

3.     Hadithi Kutoka Vyanzo vya Kale vya Sunni: Kuana Hadithi chungu nzima katika vyanzo vya kale vya Kisunni zilizo nukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusina maudhui hii, ambazo zinafanana kwa kiwango kikubwa na Hadithi hii. Miongomi mwazo ni ile Hadithi isemayo:

«تَخَلَّلُوا، فَإِنَّهُ نظافةٌ، وَالنَّظَافَةُ تَدْعُو إِلَى الْإِيمَانِ، وَالْإِيمَانُ مَعَ صَاحِبِهِ فِي الْجَنَّةِ؛ "Safisheni Mabaki ya chakula menoni mwenu (kwa kijiti au uzi) kwa sababu kufanya hivyo ni sehemu ya usafi, na usafi unapelekea imani, na imani huwa sambamba na mwenye imani huko Peponi". [12]

Allama Muhammad Baqir Majlisi alikihusisha kitabu cha Tibb al-Nabi (s.a.w.w) na mwandishi ajulikanaye kwa jina la al-Mustaghfiri. [13] Pamoja na kwamba yeye alionyesha tahadhari fulani kuhusiana na chanzo au mwandishi wa kitabu hichi, ila yeye ameonesha kuridhiswa kwake na Hadithi hii, alizinukuu Hadithi zote zilizomo kitabuni humo kikamilifu katika kitabu chake maarufu kiitwacho, Bihar al-Anwar. [14] Pia Hadithi hii inaonekena kukubalika na kupewa uzito maalumu mbele ya mwanahadithi mashuhuri Nur al-Din al-Tabarsi, ambaye aliinukuu Hadithi hii ndani ya kwenye kitabu chake kiitwacho, Mustadrak al-Wasail. [15]

Kwa karne nyingi, Hadithi ya "al-nadhafatu min al-iman" (usafi ni sehemu ya imani) imekuwa ni msingi muhimu katika mafunzo ya Kiislamu yanayolenga kuhamasisha usafi wa kimwili na kiroho. Katika maandishi ya fasihi za Kiislamu, kuna kazi kadhaa andishi kuhusiana na Hadithi hii, ambapo mara nyengine imeonekana kuambatanishwa na mada maalumu kavile fiqhi na mara nyingi kuandikwa katika mada huru mbali mbali. Mara kwa mara utakuta Hadithi ndiyo wa kusisitiza usafi ndani ya jamii katika muktadha wa fiqhi, usafi wa mazingira, pamoja na usafi katika maadili ya kijamii. [16].

Aidha, katika nchi za Kiislamu, hadithi hii imekuwa ikitumiwa sana kama chombo cha mawasiliano ya umma katika usisitizaji wa usafi. Ili kufikisha mbiu ya usafi ndani ya jamii, wahusika wa masuala ya usafi huisambaza ibara hii kwa ktumia mabango, maandishi ya ukutani, pamoja na kuiandika juu ya vifaa vya elimu kwa malengo ya kuimarisha maadili ya usafi ndani ya jamii. [17]