Nenda kwa yaliyomo

Abdul-qaadir Aliy Mwayaa

Kutoka wikishia
Sheikh Abdul-qaadir Aliy Mwayaa

Sheikh Abdul-qaadir Aliy Mwayaa (Kifarsi: عبدالقادر علی موایا)(1950-2014 A.D) alikuwa ni kiongozi wa mashia na mudiir wa taasisi ya Ahlul-baiti (a.s) katika nchi ya Uganda, mtu ambae alifanya juhudi na khidma nyingi sana kwa ajili ya kueneza na kutangaza Madhehebu ya ushia na maarifa ya Ahlul-baiti (a.s) katika nchi hii, kiasi kwamba ameweza kujenga misikiti zaidi ya sabini, madrasa na vituo vingi vya kidini katika nchi hii na kwa sababu ya harakati zake za ujenzi katika eneo hili akaitwa kwa jina mashuhuri la (chui wa maendeleo Uganda).

Sheikh Mwayaa amezaliwa mnamo mwaka 1950 A.D katika kijiji cha Kawwale katika eneo la Mayoge Uganda katika familia fukara na yenye watu wengi. Mama yake anatokana na familia ya wanazuoni wakubwa na mashuhuri wa Ahlu-sunnah. Alianza na kupata masomo yake ya primary akiwa kwa mjomba wake Sheikh Ibrahim Said Luwumba na kuendelea na masomo yake mwanzaoni mwa miaka ya 60 A.D katika shule na Namakoko. Kwa hakika sheikh huyu kutokana na kuathirika kwake na mapinduzi ya kiislaam ya Iran aliamua kujiunga na madhehebu ya kishia na kuhamia Iran na kuishi pembezoni mwa haram tukufu ya Kariime Ahlul-baiti (a.s) katika mji mtukufu wa Qom na kujishughulisha na masomo ya kidini katika mji huo.

Kuvutiwa Kwake na Imamu Khomeini na Ayatullah Khamenei

Shahidi Abdul-qaadir amesema kuhusiana na Imamu Khomeiniy: (Mimi nilikuwa nikivutiwa na shakhsiya ya Imamu Khomeiniy (r.h) na bado navutiawa na shakhsiya hiyo). Vivyo hivyo alikuwa na mapenzi makubwa kwa Walii na kiongoni wa mambo ya waislaam duniani mheshimiwa Ayatullahil-udhmaa Khomenei na alipokutana na mkuu wa kitengo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislaam katika nchi ya Uganda alisema na kumwambia maneno yafuatayo: (Kwa hakika mimi nina matarajio ya kukutana na kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislaam, lakini kwa bahati mbaya sijapata tawfiqi hiyo na katika kikao hiki ninatoa ombi langu kwako kwamba nifikishie sala zangu kwake).

Harakati za Kitamaduni na Kitablighi Uganda

Sheikh Abdul-qaadir baada ya kuhitimu masomo yake katika Hawzah ya Qom alirejea Afrika, kwa bahati mbaya hali ya kisiasa ya Uganda, kama vile mauaji ya halaiki katika mji wa Kampala, yalimlazimisha kuishi na kumaliza muda wake mwingi na mrefu katika nchi ya Kenya. Katika kipindi hiki alipata na kupokea cheti chake cha P.H.D mnamo mwaka 1364sh katika nchi ya Kenya na baada ya hali ya kisiasa ya Uganda kutulia aliamua kurudi Uganda na kusimamia harakati nyingi sana zenye malengo ya kutangaza na kueneza maktab ya Ahlul-baiti (a.s) na maarifa safi ya kiislaam. na baadhi ya harakati zake muhimu katika nchi ya Uganda ni kama zifuatazo:

  • Tarjama ya kitabu Jihadi Akbar cha Imamu Khomeiniy (r.h) Kwa lugha ya Luganda.
  • Kuasisi na kuanzisha Hospitali katika eneo la Imbali, Buwariya na Maayugoo huko Uganda.
  • Kuasisi na kuanzisha taasisi ya kiislaam ya Ahlul-baiti (a.s) katika nchi ya Uganda: Taasisi hii hadi sasa imeasisi na kujenga misikiti 24 na madrasa 20. Vivyo hivyo inasimamia mafunzo na malezi ya watoto na vijana. Na miongoni mwa harakati zingine za taasisi hii ni kusambaza umeme, kuchimba visima vya maji zaidi ya 40 na utandikaji wa mabomba ya maji ya majumbani, kutoa huduma za matibabu ya bure na kutoa ajira kwa watu mbalimbali.
  • Kuasisi na kuanzisha msikiti na Huseiniyah ya Al-mahdi.
  • Ujenzi wa shule ya msingi ya Tawhid mnamo mwaka 1358 sh.

Kufariki Kwake Shahidi

Mwishowe mwazuoni huyu, baada ya umri alio utumia katika jihadi ya kielimu na harakati za kitamaduni na uenezaji wa Maktaba ya Ahlul-baiti (a.s) na kuvumilia mambo mengi na mitihani migumu katika njia hii, aliuwawa katika usiku wa siku ya Al-khamisi tarehe 26 mwaka 2014 A.D, wakati alipokuwa akirudi kutoka kwenye ibada ya dua ya Kumail, katika eneo la Mayugi Iganga, katika shambulizi la kiterorism, kwani alikuwa ni lengo la ufyatuaji risasi la kikundi cha ukufurishaji cha kiwahabi na hatimae kufa shahidi katika shambulio hilo. Mwili wake ulisafirishwa hadi kwenye mji wa Kampala mji mkuu wa Uganda na baada ya hapo kuhamishiwa kwenye mji wa Buniya na shughuli ya usindikizaji jeneza na mazishi yake kufanyika katika eneo hili mazishi ambayo yalifanyika na yalihudhuriwa na halaiki kubwa ya watu wa eneo hilo.

Shughuli hii ilihudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa kijeshi na kiserikali, na miongoni mwao akiwa waziri wa mambo ya nje wa Uganda, viongozi wa usalam, mkuu wa jeshi la polisi wa eneo hilo na pia maulamaa na wanazuoni pia wanafuzni wa nchi hii, wote hao walihudhuria. Shakhsiya nyingi na taasisi mbalimbali za kisiasa na kidini walipinga na kukemea mauaji ya mwanazuoni huyu na walitoa salam za rambirambi, na kuungana na jamii ya mashia wa Uganda katika msiba huu mkubwa.

Rejea

Vyanzo