Nenda kwa yaliyomo

Aali-Bueih

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka AALI-BUWEIH)
Ramani inayoonesha eneo walipokuwa wanapatikana Aali-Bueih

Aali-Buweih au Buuiyaan (Kifarisi: آل بویه یا بوئیان) ni jina la kundi na ukoo maalumu wa Mashia waliokamata hatamu za uongozi na kutawala maeneo kadhaa ya Iran na Iraq, kuanzia mwaka 322 hadi 448 Hijiria. Mwanzilishi wa kundi hili alikuwa ni Ali Bin Buweihi (aliyefariki mwaka 338 Hijiria) alianzisha kundi hili kupitia himaya na msaada wa ndugu zake, waliojulikana kwa jina la Ahmad na Hassan. Jina la kundi hili linatokana na jina la baba yao, ambaye alikuwa akiitwa Buweihi. Maadhimisho ya maombolezo ya Imam Husein (a.s) ndani ya utawala wa ukoo huu wa Kishia, yalitambulikana rasmi kiserikali. Hivyo basi maadhimisho ya siku ya Ashura pamoja na sherehe za kuzaliwa imamu Ali bin Abi Talib (a.s) zinazotambulikana kwa jina Eid Al-Ghadir, yalipata motisha na kuungwa mkono moja kwa moja na utawala huo. Pia, katika kipindi hicho, ibara isemayo; ‘Hayya 'Alaa Khairi al-Amal’ ilikuwa ni sehemu ya wito wa swala (adhana) iliosikika kila wakati wa swala. Ilikuwa ni jambo la kawaida kabisa na haikuwa karaha kutumia kipande cha udongo wa kusujudia kinachowekwa kwenye kipaji cha uso na wafuasi wa madhehebu ya Kishia pale wanaposujudu katika swala zao. Watawala wa ukoo huu, walijenga na kuimarisha upya makaburi ya maimamu wa Kishia yalioko huko Iraq, na safari za kwenda kuzuru makaburi ya maimamu hao ikashamiri ndani ya zama hizo.

Baadhi ya watafiti, wakinukuu vyanzo vya kihistoria na kutoa ushahidi kadhaa, wamelihisabu kundi la watawala hao kuwa ni kundi la watawala wa Kishia. Hata hivyo, kuna maoni tofauti kuhusu Ushia wao, na kwamba jeو tokea mwanzo walikuwa ni Mashia wanaoamaini Maimamu kumi na mbili, au walikuwa ni wafuasi wa madhehebu ya Zaidiyyah kisha wakabadili madhehebu yao na kufuata Maimamu kumi na mbili. Ruknu Al-Dawlah (aliyetawala kuanzia 323 hadi 338 Hijiria), Muizzu-AlDawlah (aliyetawala kuanzia 325 hadi 356 Hijiria) na Adhdu Al-Dawlah (aliyetawala kuanzia 338 hadi 372 Hijiria), walikuwa ndio watawala maarufu wa ukoo huo. Kuna maandiko kadhaa yaliyoandikwa kuhusiana na Aali Buweih. Moja kati ya vitabu muhimu na maarufu kilichoandikwa kuhusiana na ukoo huu, ni Kitabu cha Ibn Muskaweihi Tajaarubu Al-Umamu (kilichoandikwa katika karne Hijiria).

Nafasi na Umuhimu Wao

Aali-Buweihi ni ukoo wa Kishia uliotawala sehemu za Iran na Iraq kwa zaidi ya miaka 120 (322-448 Hijiria).[1] Wakati wa utawala wao, baadhi ya nembo na mila za Kishia, kama vile maombolezo ya Imam Hussein (a.s) na kuadhimisha sikukuu ya Ghadir, kwa mara ya kwanza kabisa zilitambulika rasmi kiserikali na kufanyika hadharani. Kipindi hiki kinachukuliwa kuwa moja ya vipindi imara vilivyoshamiri zaidi ndani yake ustaarabu wa Kiislamu.[2]

Utawala wa Aali-Buweihi ulianzishwa na Ali, mtoto wa Abu Shujaa, kwa msaada wa ndugu zake Ahmad na Hasan, na ndio maana utawala huo ukapewa jina la Aal-Buweihi au Buuiyaan. Pia wakati mwengine ukoo wa watawala hao hutambulika kwa jina la Diyalmeh[3] au Dilmiyaan.[4]

Madhehebu Yao

Sadiq Sajjadiy, mwandishi wa makala ya Aal-Buweihi katika Ensaiklopidia Kuu ya Kiislamu, anasema kwamba: Haiwezekani kutoa tamko la wazi kabisa kuhusiana na madhehebu halisi ya Aali-Buweihi.[5] Hata hivyo, mwanahistoria wa Kishia Rasul Jafarian[6] (aliyezaliwa mwaka 1343 Shamsia) na baadhi ya waandishi wengine,[7] wakinukuu vyanzo mbali mbali vya kihistoria na kutoa ushahidi wao, wemeuhisabu ukoo wa Aal-Buweihi, kuwa ni ukoo wa madhehebu ya Kishia unaoamini maimamu kumi na mbili. Miongoni mwa dalili muhimu zinazothibitisha Ushia wao, kule kuimarisha kwao kwa mila za Kishia, kuwa na mawaziri wa Kishia serikali, watawala kuwa na majina ya Kishia, pamoja na uhusiano iliopo baina yao na wanachuoni wa Kishia.[8] Pia, mwanahistoria wa Kisunni Ibn Kathir wa Damascus wa karne ya 8 Hijiria, amewahisabu viongozi wa ukoo huo kuwa ni Mashia na Marafidhi.[9] Abdul Jalil Qazvini, mwanazuoni wa Kishia wa karne ya 6 Hijiria, amewatambua viongozi hao kama ni viongozi walishikamana na madhehebu ya Kishia.[10]

Kulingana na historia ya Madhehebu ya Zaidiyyah huko Tabaristan, baadhi ya waandishi pia wamependekeza na kutilia mkazo dhana inayowahisabu watawala wa ukoo wa Aali Buweihi kuwa wafuasi wa madhehebu ya Zaidiyyah.[11] Wao waanaamini ya kwamba watawala wa ukoo wa Aali Buweihi, mwanzo kabisa walikuwa ni wafuasi wa madhehebu ya Zaidiyyah na baadae wakabadili madhehebu yao na kushikamana na madhehebu ya Shia Ithna'ashariyyah.[12] [Maelezo 1] Vilevile Rasul Jafarian, amenukuu kutoka katika kitabu cha Muntakhabu Ad-diin Razi, ambaye ni mwanazuoni wa Kishia wa karne ya sita Hijiria, ambapo kwa mujbu maandiko yake, mwandishi alinukuu kutoka kwa Ibn Shahr Ashob kwamba; Aali Buweihi aliingia kwenye Ushia kupitia mikononi mwa Taj Al-Ruasaa bin Abi Al-Sa'adaa, ambaye ni mmoja wa wanazuoni wa Kishia.[13] Jafarian anatilia shaka na kudhani kuwa kule Aali Buweihi kutoka madhehebu ya Shia Zaidiyyah na kwenda Shia Ithna Ashariyyah, kumetokana na kuwa kama watawala wa Aali Buweihi wangeliendelea kushikamana na madhehebu ya Zaidiyyah, basi wangelilazimika kuikabidhi serikali mikononi mwa wafuasi wa madhehebu ya Alawiyyah, ila wakishikamana na madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah, serikali itaenedela kubaki mikononi mwao.[14]

Ilya Pavlovich Petroshevsky (aliyezaliwa mwaka 1898), ambaye profesa katika chuo kikuu cha Urusi, anaamini kwamba waanzilishi wa serikali ya Aal-Buweihi walikuwa ni Mashia, ila warithi wa ukoo huu waliokuja baadae, ingawa kiundani walikuwa na mwelekeo wa Kishia, ila kwa mtazamo wa nje, rasmi walidhihiri kama ni Masunni.[15] Mwandishi wa makala ya “Aal-Buweihi na jukumu lao katika kusimamisha sherehe na misimu ya Shia Imamiya huko Iraqi” aliizingatia dhana hii kuwa sidhana sahihi. Mwandishi huyu ametia shaka kwamba kule viongozi na watawala wa Aal-Buweihi kuukubali utawala wa Bani Abbas, ndiko kulikopelekea kuzaliwa kwa dhana hiyo.[16] Pia mtaalamu wa masuala ya Mashariki wa Kijerumani, bwana Bertold Spühler (aliyeishi baina ya mwaka 1911na 1990 AD), katika kitabu chake History of Iran in the First Islamic Centuries, anaamini kwamba tokea mwanzo watawala wa ukoo wa Aal-Buweihi walikuwa ni Mashia wa madhehebu ya Ithna Ashariyyah na walidumu na imani hii hadi mwisho.[17]

Maadhimisho ya Mila za Kishia

Utawala wa Aali-Buweihi ulichukua hatua nyeti katika kukuza na kuadhimisha mila mbali mbali za madhehebu ya Shia Imamiyyah, kama vile:

  • Maadhimisho ya maombolezo ya siku ya Ashura: Kupitia amri ya Muizzu Al-Doulah Deilamiy, siku maombolezo ya siku ya Ashura ilitangazwa kuwa ni siku ya huzuni kwa taifa zima, amri hiyo ilitolewa mnamo mwaka 352 Hijiria. Katika kipindi hicho watu walitakiwa kuonyesha huzuni zao kwa kuvaa nguo nyeusi. Kwa mujibu wa maoni ya Ibnu Khalduni, katika siku kama hii, wanawake walikuwa wakitoka majumbani mwao wakiwa na nywele zilizotimuka na nyuso zilizosawijika, huku wakijipiga vichwa na nyuso zao huku wakilia na kuomboleza maombolezo kwa ajili ya Imam Husein (a.s).[18] Pia, kwa mujibu wa riwaya ya mwanahistoria wa Kisunni Ibn Jouzi (aliyefariki mnamo mwaka 597 Hijiria), siku kama hii, biashara zilikuwa zilifungwa na kujengwa mahema sokoni, na harakati za maombolezo zilikuwa zikifanyika kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s).[19] Kamel Shibiy pia anaamini kwamba, makundi ya waombolezaji yalionekana kujitokeza kwa mara ya kwanza kabisa mnamo mwaka 352 Hijiria.[20]
  • Maadhimisho ya siku kuu ya Ghadir: Maadhimisho ya siku ya Ghadir yalitekelezwa kupitia amri ya Muizzu Al-Daulah mnamo mwaka 351 Hijiria. Kupitia amri hiyo shina la maadhimisho hayo likaatikwa mjini Baghdad.[21] Pia viongozi waliokuja baadae wailendeleza maadhimisho hayo.[22]
  • Kuchanua kwa mfumuko wa kuzuru makaburi ya maimamu wa Kishia: Aali Buweihi walichukua hatua muhimu kuhusiana na maimamu waliozikwa katika mji wa Iraq. Miongoni mwa hatua hizo ni kukarabati makaburi hayo, kujenga minara na kuimarisha majengo ya makaburi hayo,[23] kutoa wakfu na kutenga posho maalumu kwa ajili ya makaburi hayo, kurahisisha na kuhimiza watu kuzuru makaburi hayo pamoja kuwataka watu kujenga na kufanya ujirani na makaburi hayo, kutenga posho maalumu pamoja na zawadi maalumu kwa ajili ya kuwasaidia majirani wa makabri hayo.[24]
  • Kusoma adhana: Kuanzia mwaka wa 356 Hijria, kusema Hayya alaa khairil amal katika adhana ikawa ni desturi kila adhana, na hali hiyo iliendelea hadi mwanzoni mwa utawala wa Kiseljuki.[25]
  • Kueneza fikra matumizi ya kidonge cha udongo wa Imam Husein: Katika kipindi cha Aali-Buweihi, watu waliandaa tasbihi zilizoundwa kupitia udongo wa ardhi ya Karbala, au udongo wa kaburi la Imamu Husein (a.s). Pia walitengeneza vidonge maalumu kupiti audongo huo, kwa ajili ya kusujudu juu yake wakati wa swala na kuwapa watu.[26]

Baadhi ya wnadishi wamenukuu habari za kutumika aina maalumu ya sarafu katika zama za utawala wa Aali Buweihi, sarafu ambazo zilikuwa zimechorwa maandiko yaliyosomeka; Laa Ilaha Illa Llahu, Muhammadu Rasusulu Llahi, Aliyyun Waliyyu Llahi.[27]

Viongozi Kashuhuri

Baadhi ya viongozi mashuhuri wa utawala wa aali buweihi ni:

  • Ali bin Buweihi, aliyepewa lakabu ya Imadu Al-Dawlah Deylami, alikuwa mtoto wa Abu Shujaa Deylami na mwanzilishi wa serikali ya Aali-Buweihi huko mji wa Fars.
  • Hassan bin Buweihi, aliyepewa jina lakabu ya Ruknu Al-Dawlah, ambaye ni mtoto wa Abu Shuja Deilmi na mtawala wa meneo ya Milimani. Yeye alipigana vita vingi ili kupanua eneo la utawala wa Aali Buweihi katika mikoa ya Ray, milimani, Tabaristan na Gorgan.
  • Ahmed bin Buweihi, aliyepewa lakabu ya Mu'izzu Al-Daulah Deilmi, ambaye ni kaka wa Ali na Hassan bin Buweihi, ambaye aliiteka Baghdad mwaka wa 334 Hijiria. Yeye ndiye aliamuru kufanyika kwa maadhimisho ya maombolezo ya siku ya Ashura[28] na sherehe za Eid Al-Ghadir[29] huko Baghdad.
  • Adhdu Al-Dawlah Deilmi aliyekuwa mtoto wa Hassan bin Buweihi, ambaye alimrithi ami yake huko Fars baada ya ami yake Imadu Al-Dawlah kufariki dunia. Yeye alikuwa ni mmoja wa viongozi wa Kishia wa Iran wenye nguvu zaidi waliotawala maeneo makubwa ya ardhi za Kiislamu na Iran kwa jumla. Miongoni mwa kazi muhimu ni ukarabati wa magofu ya Baghdad,[30] ujenzi wa hifadhi kubwa za maji huko Fars,[31] ujenzi wa Hospitali ya Azdiy huko Baghdad,[32] ukarabati wa makaburi ya maimamu, ikiwemo na Haram ya Kazmain[33] na Haram ya Askariyyain,[34] pia alijenga uzio uliouzunguka mji wa Madina.[35]

Machipuko yao Kihistoria

Kielelezo cha Sarufi ya Aali-Bueih

Mwanzoni mwa karne ya nne Hijiria, Ukoo wa Deilamian ulianza harakati zake nchini Iran dhidi ya ukhalifa wa Bani Abbas.[36] Maakaan bin Kakiy, Esfarini Shiiruyeh na Mardawij Ziiyari, kila mmoja aliondoka kutoka mji wa Deilam na kikosi cha jeshi. Ali na Hassan, wana wa Abu Shujaa, walijiunga na Makan mfuaasi wa Wasamani (Saamanian). Katika mwaka wa 321 Hijiria, Mardawij Ziiyari alitawala Gorgan na Tabaristan, Ali na Hassan walijiunga na Mardawij kupitia ushawishi wa Maakaan. Yeye Alimteua Ali kuitawala Karaj,[37] Ali akaenda Karaj na kwa kuziteka kwake ngome zilizouzunguka mji wa Karaj, kukukawa ndio chanzo cha kupatikana hofu ndani ya moyo wa Mardawij. Kwanza alikusudia kuiteka Isfahan, lakini alishindwa na jeshi la kaka yake Mardawij, na baada ya muda, aliiteka Arrajan na Nuubandjaan, na kaka yake (Hassan) kupitia amri yake akaiteka Kazeruun.[38] Ali aliiteka Shiraz mnamo mwaka 322 Hijiria, na akaanzisha jimbo la Aali-Buweihi mjini Shirazi baada ya kuuteka mji hou.[39] Hata hivyo, kwa mujibu wa kauli ya Sadiq Sajjadiy, baadhi ya wanahistoria wanamoni ya kwamba; kutekwa kwa mji wa Arjan (321 Hijiria/ sana na 932 Miladia) kulikuwa ndio mwanzo wa msingi wa serikali ya Aali Buweihi.[40] katika kipindi cha miaka 12 baada ya hapo, Hassan na Ahmad waliziteka Ray, Kerman na Iraq, na utawala wa serikali ya Aali Buweihi ukagawanywa katika matawi matatu makubwa na tawi moja dogo lililotawala Kerman na huko Oman.[41]

Kwa mujibu wa kauli ya mhakiki wa kihistoria bwana ali Asghar Faqihiy (aliyefariki mwaka 1382 Shamsia), kitabu Tajaarubu Al-Umam, ndio kitabu asili kilichotegemewa na waandishi wa nyanja za kihistoria kuhusiana na tawala za Aali Buweihi.[42] Kitabu ambacho kimeandikwa na Ibnu Muskawaihi (aliyeishi baina ya mwaka 320 na 420 Hijiria). Mwandishi ambaye aliishi ndani ya zama za tawala za Aali Buweihi.[43]

Vitabu Husika

Pia kuna vitabu na maandiko mengi kuhusiana na Aali-Buweihi, baadhi yake ni:

  • Kitabu cha Historia ya Aali-Buweihi kilichoandikwa na Ali Asghar Faqihi (aliyeishi mnamo mwaka 1296 na1382 Shamsia): Kitabu hichi kimejikita kwenye historia ya Aal-Ziyaar na Aal-Buweihi pamoja na hali na matokeo tofauti ndani ya zama zao. Maandiko ya kitabu hichi yalikusanywa mnamo mwaka 1378 yakatumika kama maandishi ya kozi ya historia katika kiwango cha shahada ya kwanza ya vyuo vikuu vya Irani.[44]
  • Uchunguzi wa uamsho na uzinduzi wa kitamaduni katika enzi za utawala wa Aali Buweihi uliofanyika kupitia kitabu cha (The era of Islamic Renaissance by Joel. L. Crimson). Kitabu hichi kimechunguza ustawi wa kiakili na kiutamaduni wa vituo vya serikali ya Aali Buweihi, haswa serikali yao iliyokuwa na makazi yake huko Baghdad. Kazi hii pia imetafsiriwa kwa Kiajemi.[45]
  • Kitabu Maisha ya Kisayansi Katika Enzi ya Aali Buweihi cha Ghulamridha Fadai, Profesa wa Chuo Kikuu cha Tehran (aliyezaliwa mwaka 1324 Shamsia): Kitabu hichi ni sehemu ya mkusanyo wa Maisha ya Kisayansi katika Enzi ya Serikali za Kishia, ambacho kinatoa wasifu wa maisha ya wanasayansi katika kipindi cha Aali Buweihi.[46]
  • Al-Taji fi Akhbar Al-Dawlah Al-Dilamiyyah cha Ibrahim bin Hilal Sabi (aliyefariki 384 Hijiria), ni mmoja wa waandishi wa historia wa Aali Buweihi, kitabu ambacho kimeshighulikia historia ya nasaba za ukoo wa huu wa Aali Buweihi katika miaka ya utawala wa Azad al-Dawlah. Kitabu hichi kiliandikwa kwa amri ya Azd al-Doulah mji wa Dailamah pamoja na utawala wao. Ibn Muskawaihi amekitumia kitabu katika kuandika kitabu chake Tajaarubu Al-Umam. Nakala ya sehemu ya kitabu hicho imehifadhiwa katika maktaba ya Msikiti Mkuu wa Sana'a. Mohammad Hussein Zubeidiy alikichapisha kitabu hicho kwa jina la Al-Muntza'a Min Kitab Al-Taji mnamo mwaka 1977 huko Baghdad.

Maelezo

  1. Kwa mujibu wa maoni ya Fatimah Jafarnia, watu wa Dilam waliufahamu Uislamu na Ushia kupitia waumini wa madhehebu ya Alawiyyiina, kama vile [Nasser Kabir], Nasser Atroosh na Hassan Bin Qasim. Hassan bin Qasim alikuwa ni mfuasi wa madhehebu ya Zaidiyyah, ila kuna maoni tofauti kuhusiana madhehebu ya Nasser Atrosh. Rejea kitabu cha Jafarnia , Utafiti juu nafasi ya Utawala wa Aali Buweihi na Kusambaza Ushia na Kuimarisha Majengo ya Ibada Mjini Iraq, Uk, 24.

Rejea

  1. Sajjady, «Aali-Bueih», juz. 1, uk. 629.
  2. Golizavareh, «Barresii naqsh daulat Aali-Bueih dar gastrash tashayuu wa amran itbat Iraq», uk. 122.
  3. Tazama Mustawfi, Najhat al-Qalub, uk. 98, 99 na 174.
  4. Golizavareh, «Barresii naqsh daulat Aali-Bueih dar gastrash tashayuu wa amran itbat Iraq», uk. 122.
  5. Sajjad, «Aal-bueih», juz. 1, uk. 640.
  6. Jafarian, Tarikh tashayuu dar Iran, 2007, uk. 375.
  7. Jafarian, Tarikh tashayuu dar Iran, 2007, uk. 376 ; Jafarian, «Siyasatihaye hukumat Aali-Bueih dar jihat tahkim wahdat miyan shia wa ahlu-sunna, uk. 24.»
  8. Jafarian, «Siyasatihaye hukumat Aali-Bueih dar jihat tahkim wahdat miyan shia wa ahlu-sunna, uk. 24.»
  9. Ibn Kathīr, al-Bidāya wa l-nihāya, juz. 11, uk. 307.
  10. Qazwīnī, al-Naqḍ, uk. 42.
  11. Jaʿfarnīya, "Sīyāsat-hā-yi ḥukūmat-i Āl būya dar jahat-i taḥkīm-i waḥdat mīyān-i Shīʿa wa ahl-i sunnat", uk. 24.
  12. Shaybī, al-Ṣila bayn al-taṣawwuf wa l-tashayyuʿ, juz. 2, uk. 39.
  13. Jaʿfarīyān, Tārīkh-i tashayyuʿ dar Irān, uk. 380.
  14. Jaʿfarīyān, Tārīkh-i tashayyuʿ dar Irān, uk. 378.
  15. Pūraḥmadī, "Āal-Bueih wa naqsh-i ānān dar barpāyī-yi marāsim wa mawāsim-i Shīʿa-yi Imāmīyya dar Irāq", uk. 112.
  16. Pūraḥmadī, "Āal-Bueih wa naqsh-i ānān dar barpāyī-yi marāsim wa mawāsim-i Shīʿa-yi Imāmīyya dar Irāq", uk. 112.
  17. Jaʿfarīyān, Tārīkh-i tashayyuʿ dar Irān, uk. 375.
  18. Ibn Khaldūn, Tārīkh Ibn Khaldūn, juz. 3, uk. 425.
  19. Ibn al-Jawzī, al-Muntaẓam, juz. 7, uk. 15.
  20. Shaybī, al-Ṣila bayn al-taṣawwuf wa l-tashayyuʿ, juz. 2, uk. 39.
  21. Ibn Khaldūn, Tārīkh Ibn Khaldūn, juz. 3, uk. 420-425.
  22. Ibn al-Jawzī, al-Muntaẓam, juz. 6, uk. 163.
  23. Dhahabī, al-ʿIbar fī khabar man ghabar, uk. 232.
  24. Khaṭīb Baghdādī, Tārīkh-i Baghdād, juz. 1, uk. 424.
  25. Ibn al-Jawzī, al-Muntaẓam, juz. 8, uk. 164; Ibn Khaldūn, Tārīkh Ibn Khaldūn, juz. 3, uk. 460.
  26. Thaʿālibī, Yatīmat al-dahr, juz. 3, uk. 183.
  27. Jaʿfarīyān, Tārīkh-i tashayyuʿ dar Irān, uk. 380.
  28. Ibn Khaldūn, Tārīkh Ibn Khaldūn, juz. 3, uk. 527.
  29. Ibn al-Athīr al-Jazarī, al-Kāmil fī l-tārīkh, juz. 8, uk. 549.
  30. Abū ʿAlī Miskawayh, Tajārub al-umam, juz. 6, uk. 477 and 478.
  31. Farshād, Tārīkh-i ʿilm dar Irān, juz. 2, uk. 790.
  32. Farshād, Tārīkh-i ʿilm dar Irān, juz. 2, uk. 749-751.
  33. Āl Yāsīn, Tārīkh al-mashhad al-kāẓimī, uk. 24.
  34. Maḥallātī, Maʾthar al-kubrā fī tārīkh Sāmarrāʾ, juz. 1, uk. 321.
  35. Samhudī, Wafāʾ al-wafā, juz. 2, uk. 269-270.
  36. Sajjādī, "Āl Būya", juz. 1, uk. 629.
  37. Ibn al-Athīr al-Jazarī, Al-Kāmil fī l-tārīkh, juz. 8, uk. 267.
  38. Maqrizī, al-Sulūk, juz. 1, uk. 27.
  39. Ibn Taghrī-Birdī, al-Nujūm al-zāhira, juz. 3, uk. 244-245.
  40. Sajjādī, "Āali-Buweih", juz. 1, uk. 629.
  41. Sajjādī, "Āali-Buweih", juz. 1, uk. 629.
  42. Faqīhī, Tārīkh-i Āali-Buweih, uk. 17.
  43. Faqīhī, Tārīkh-i Āali-Buweih, uk. 17.
  44. Faqīhī, Tārīkh-i Aali-Buweihi, uk. 4.
  45. Kramer, Iḥyā-yi farhangī dar ʿahd-i Aali-Buweihi: Insān garāyī dar ʿaṣr-i runisāns-i islāmī.
  46. Fadāʾī ʿIrāqī, Ḥayāt-i ʿilmī dar ʿahd-i Aali-Buweihi, Shabake Jamie Kitabu Gysavam

Vyanzo

  • Abū ʿAlī Miskawayh, Aḥmad b. Muḥammad. Tajārub al-umam. Edited by ĀmadRūz, Cairo: Maṭbaʿat al-shirkat al-tamaddun al-ṣanāʿīyya, 1332 AH.
  • Āl Yāsīn, Muḥammad Ḥasan. Tārīkh al-mashhad al-kāẓimī. Al-ʾAmāna al-ʿāmma li l-ʿatabat al-Kāẓimīyya al-muqaddasa, 2014.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Al-ʿIbar fī khabar man ghabar. Edited by Abū Hājar Muḥammad. Beirut: Dār al-kutub al-ʿarabīyya, 1405 AH.
  • Fadāʾī ʿIrāqī, Ghulāmriḍā. Ḥayāt-i ʿilmī dar ʿahd-i Āl būya. Tehran: Muʾassisa-yi chāp wa intishārāt-i dānishgāh-i Tehran, 1383 SH.
  • Faqīhī, ʿAlī Asghar. Tārīkh-i Āl būya. Tehran: Sāzmān-i Muṭāliʿeh wa Tadwīn-i Kutub-i ʿUlūm-i Insānī Dānishgāh-ha, 1378 Sh.
  • Farshād, Mahdī. Tārīkh-i ʿilm dar Irān. Tehran: Muʾssisa intishārāt Amīr Kabīr, 1366 SH.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, 1399 AH.
  • Gulīzawāra, Ghulāmriḍā. "Barrasī-yi naqsh-i dawlat Āl būya dar gustarish-i tashayyuʿ wa ʿumrān āatabāt-i Irāq". Zīyāra 37, 1397 SH.
  • Ibn al-Jawzī, ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAlī. Al-Muntaẓam fī tārīkh al-umam wa l-mulūk. Hyderabad: Dāʾirat al-Maʿārif al-ʿUthmānīyya, 1358 AH.
  • Ibn Khaldūn, ʿAbd l-Raḥmān b. Muḥammad. Tārīkh Ibn Khaldūn. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1391 AH.
  • Ibn Kathīr al-Dimashqī, Ismāʿīl b. ʿUmar. Al-Bidāya wa l-nihāya. Beirut: Dār al-Fikr, 1407AH-1986.
  • Ibn Taghrī-Birdī, Abū al-Maḥāsin Yūsuf. Al-Nujūm al-zāhira fī mulūk miṣr wa l-qāhira. Cairo: Wizārat al-Thiqāfa wa al-Irshād al-qawmī, Mu'assisat al-Misriyya al-'Amma, 1392/1972.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Tārīkh-i tashayyuʿ dar Irān. Tehran: Nashr-i ʿIlm, 1387 SH.
  • Jaʿfarnīya, Fāṭima. "Sīyāsat-hā-yi ḥukūmat-i Āl būya dar jahat-i taḥkīm-i waḥdat mīyān-i Shīʿa wa ahl-i sunnat". Tārīkhnāma-yi Khwārizmī 22, 1397 SH.
  • Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh-i Baghdād. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1407 AH.
  • Kramer, Joel. Iḥyā-yi farhangī dar ʿahd-i Āl būya: Insān garāyī dar ʿaṣr-i runisāns-i islāmī. Translated by Muḥammad saʿīd Ḥanāyī Kāshānī. Tehran: Markaz-i nashr-i dānishgāhī, 1375 SH.
  • Maḥallātī, Ḍhabīḥ Allāh. Maʾthar al-kubrā fī tārīkh Sāmarrāʾ. Qom: Maktabat al-Ḥaydariyya, 1384 Sh.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Sulūk li maʾrifa dūn al-mulūk. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1420 AH.
  • Mustawfī, Ḥamd Allāh. Nuzhat al-qulūb. Qazwīn: Ḥadīth-i imrūz, 1381 SH.
  • Pūraḥmadī, Ḥusayn. "Āl Būya wa naqsh-i ānān dar barpāyī-yi marāsim wa mawāsim-i Shīʿa-yi Imāmīyya dar Irāq.". Faṣlnāma-yi Shīʿashināsī 3 and 4, 1382 SH.
  • Qazwīnī, ʿAbd al-Jalīl. Al-Naqḍ. Tehran: Anjuman-i Āthār-i Millī, [n.d].
  • Sajjādī, Ṣādiq. "Āl Būya". Dāʾirat al-maʿārif buzurg-i Islāmī. Tehran: Markaz-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Buzurg-i Islāmī, 1369 Sh.
  • Samhudī, ʿAlī b. ʿAbd Allāh. Wafāʾ al-wafā bi akhbār dar al-Muṣṭafā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 2006.
  • Shaybī, Kamil Muṣtafā. Al-Ṣila bayn al-taṣawwuf wa l-tashayyuʿ. Beirut: Dār al-Andulus, 1982.
  • Thaʿālibī, ʿAbd al-Malik b. Muḥammad al-. Yatīmat al-dahr. Beirut: Dār al-kitāb al-ʿarabī, 1352 AH.